Ni ijumaa nyingine tena.Baada ya mzuka wa kule Dodoma,baraza lile lile la mawaziri nk,ni wakati wa kusonga mbele huku tukitumaini kwamba kesho itakuwa bora kuliko jana. Usipofanya hivyo unaweza kurukwa na akili.Au unasemaje?
Leo tunarudi miaka michache nyuma na kuwakuta Nchinga Sound.Wimbo unaitwa Fadhila Kwa Wazazi. Kibao hiki kilipikwa na Marlone Linje ukiwa utunzi wa Rogert Hega Caterpilla(pichani) ambaye pia ni miongoni mwa waimbaji wa wimbo huu.Anaimba ubeti wa kwanza.Waimbaji wengine ni Muumin Mwinjuma “Kocha wa Dunia”,Roshi Msekela “Sauti ya Maji”, Rashid Mwezingo “Silver Boy”. Kwa upande wa vyombo,bass guitar linacharazwa na Adolph Mbinga “Mtuhumiwa”, Jose Watuguru”Mtaalamu wa Solo” huku kinanda kikiwa chini ya udhibiti wa Deo Mwanambilimbi “Mzee wa Goba”.Kikosi kilikuwa kimetulia hiki,we acha tu.
Wimbo huu ni maalumu kwa wote waliopoteza mzazi au wazazi wakati wowote,popote pale mlipo.Wimbo huu uwe ni faraja kwenu.Ijumaa Njema. Bonyeza player hapo chini uusikie wimbo.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Shukrani Pius Mikongoti kutoka ndani ya Malaysia kwa wimbo huu.
Feedback / Comments
13 Responses to “FADHILA KWA WAZAZI”
Leave a Reply


sending...
Tunashukuru sana kwa wimbo huu kwa faraja kubwa, lakini kuna watu wengine huwa hawana thamani na wazazi wao nao huwafanya wazazi waishi kwa masikitiko sana kwaajili ya watoto wao walio wazaa. Hii inasikitisha sana kwani mtu anatamani kurithi mji wa wazazi wake akiwa na hai. Je watu kama waelimishweje. Na hii tabia imeshamiri sana Mbeya kwa sababu limekuwa jiji watu wanataka utajiri na kutaka kuuwa wazazi wao ili wauze miji. Tunaomba ushauri, je hii ni haki.
Ijumaa ipo paleeeee palee…duu bonge la wimbo.
Wimbo unaujumbe mzito sana.
Hakika hii ni kweli kuna kipindi inatokea,mtu unakuwa una mikakati ya kuwafanyia bonge la “saprize” au kufanya jambo lolote jema kwa wale uwapendao na waliochangia mafanikio yako lakini ghafla mola anawapenda zaidi na kuwatwa.
Ndio kazi yake Mungu.Jina lake lihimidiwe.Amina
Lakini ikitokea hivyo sio mwisho,vema jitahidi kuendeleza yale mema waliyokuwa wanafanya na kuishi kuendana na matarajio yao kwako,hiyo pia itakuwa njia njema ya kuwaenzi.
Ijumaa njema wazalendo.
Tutafika tu.
Kama kuna wimbo Mchinga sound waliimba ni huu, hauchuji,hauchoshi, una mafunzo mazuri, ingawa pia ni wa masikitiko.
Rogati Hegga hapa hakika ulifanya mambo.
Asante BC kwa wimbo huu
Big up Caterpillar mtu wa watu, Prince, Silver boy na wengine katika Mchinga band.
Ndugu zangu nyote mna vipaji vya nguvu Mola na awabariki nanyi mzidi kujibidisha kupitia vipaji vyenu kwa maendeleo yenu na Taifa kwa ujumla.
Nimekumbuka siku ile tukiwa wote pale Maisha Club mlipokuja na rafiki yangu Prince kazi yenu si haba. Muumin nasubiri kusikia mapya kutoka bendi yako mpya uliyohamia baada ya kutoka TOT.
Rafiki yenu wa Uholanzi (Dr.)
Shukrani kwa aliyeleta wimbo huu! Walio na mzazi/wazazi hai, muwathamini jamani, uchungu ni mkubwa wanapotangulia kwa mwenyezi Mungu, hasa pale unapodhani wangekuwepo pengine kwa namna fulani wangekusaidia!! kwa sasa hivi unaweza usilione hilo, lakini once wanapoondoka ndo utatambua ninalozungumzia. Inauma sana pale ninapowaona watu wana-enjoy maisha, kwa starehe zilizozidi kiwango, wakati wazazi hawana hili wala lile… Ahsate tena mdau uliyeleta hii nyimbo!!!
Kwa kweli umenikumbusha mbali. Wimbo una maudhui mazuri sana. Hongers sana bwana Roggati Hegga. I hope next time tutapat wimbo wa neema toka wana kibandi nkoi wa enzi za silent Inn. I remember those good days known as faculty day!
Ninachoweza kusema ni kuwa Rogert Hega “hana bahati” ila ni mtunzi mzuri sana jamaa, Namuamini sana hasa akiwa na Rasheed Mwezingo “Silver Boy”
Asante sana. Naupenda sana wimbo huu.
huwa unanikumbusha marehemu baba yangu. Amenisomesha nimemaliza shule, naanza tu kazi Baba yangu anafariki, natamani angekuwa hai nimnunulie hata shati alivae na mimi nijisikie raha. lakini sikubahatika.
Kwa wale mlio na wazazi wenu hai plzz, fadhila ni jambo kubwa sana tusiwasahau wazi wetu. Mzazi hata ukimpa kitu kidogo tu huwa anafurahi sana na unapata baraka
Big up Robert This is the great song
BC thanx kwa wimbo,mimi naona umenigusa haswa maana nakumbuka nlikuwa natoka mzika mama angu Musoma 1999 na selection ya form 5 imetoka, sasa nawahi shule, tuko basi la Falcon,Mwanza-Nairobi-Dar hii kanda iliimba njia nzima. Alieiweka hakujua km kuna mtu inamgusa mno
Dr. Uholanzi uko eneo gani? Niko Rotterdam, for all the time I’ve been here wabongo niwajuao hapa ni 2 tu.
nyimbo imetulia hata mimi inanikumbusha wazazi wangu wote wawili wamefariki hata sijawatunza
TUWAOMBEE WAZAZI WETU NI KWELI KABISA PIGO ZITO UNAPOONDOKEWA NA WAZAZI MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA PEPONI AMIN.LAKINI HOME BOY MWINJUMA MBONA SIMSIKII MICHUZI TUPE HABARI ZAKE MBALI NA MUSIC NAMFAHAM TOKA KULE MBEGANI HADI KIJIJI CHA PANDE BAGAMOYO ALIMUIMBA ALIE KUWA MKE WAKE,PIA AKAWAIMBA WAZAZI WAKE JAMAA HUYO WALIOKUWA WANAGOMBEA MPAKA WA SHAMBA SI MBAYA NI MAFUNDISHO BIG UP BONGO MUSIC
CHAFOSA CHAI GODA
Safi kabisa na kazi njema, mbona nyimbo baadhi zinacheza vipande hazikamiliki?
kama Fadhila unacheza kwa sekunde kadhaa unakatika namna gani?
Asante
Eee Mwenyezi Mungu warehemu wazazi wangu wapenzi!!!!!!