
Bila shaka ushawahi kuusikia ule msemo wa “kulala masikini kuamka tajiri”.Nia au kiini cha msemo ule huwa ni kuzungumzia jinsi ambavyo maisha huweza kubadilika ghafla,bila hodi wala karibu.Hii ndio hali halisi kwa mke wa Waziri Mkuu(Mizengo Pinda),Tunu Pinda(pichani) ambaye miezi michache tu iliyopita sio watu wengi sana walikuwa wakimjua.Leo hii mambo sio hivyo tena.Bi Tunu keshaanza kulikwea jukwaa la wananchi maarufu.Wanapoketi wake wa “vigogo” wa nchi,huwezi kumkosa au kumuacha pembeni.That’s life!
Feedback / Comments
36 Responses to “BI.TUNU PINDA”
Leave a Reply


sending...
ni kweli kabisa, BC you are absolutely right!
Yaani kwa wale wanaoamini kuwepo Mungu, Mungu hufanya miujiza. Ndo maana kila mtu naamini yuko yunique na huwezi jua kamwe Mungu alikupangia nini!
Hongera bi. Tunu na Mungu akubariki wewe na familia yako.
Mzee Mizengo Pinda hapa asifiwe vile vile chombo anacho tena kinangara ( you can`t ask for more)
Hongera sana zali la mentali hilo Mama Pinda.
Hongera sana dada, MUNGU yupo pamoja nanyi, endeleeni kumtegemea siku zote za maisha yenu.
oh! black beauty, sasa mama Pinda uwe karibu na mzee asije akapinda mambo! halafu kaa mbali na mkorogo, hiyo rangi yako ni nzuri mno! naogopa usije ukaikoroga! Chonde chonde! mwombe mzee pinda anyooshe kuwashughulikia mafiswadi wa RICH-MONDULI!
Hongera!
hongera mama
Nilishaandika siku moja kwenye huu mtandao kuwa: Kama Mungu muumba wa Mbingu na nchi amekuandikia YES, basi maisha yako yatakuwa Yes tu.
Mheshimiwa Pinda ana takribani miaka 60, Wazazi wake wote (Baba na Mama) wapo hai “wanadunda”.
Mungu pia kampa Mke mwema kama huyu.
Hongereni sana Mama Pinda na Mumeo; Jitahidini msimuache au kumsahau Mungu.
Mungu awalinde msipatwe na janga lolote baya kutoka kwa Shetani au maajenti wake hapa Ulimwenguni. Amen
Safiiiiiiiiiii safu\iii sanaaaaaaaaaaaa ila mama usisahau ulikotokA
wanyonge utukumbuke kwenye ufalme wako
nakutakia kila la kheri ktk maishahaya mapya
usianzishe mifuko ya kifisadi kama ya akina esther sumaye, mama anna mkapa ,na regina lowassa itakuponza mama mpenzi
nakuomba usali rozari maratu usomapo maoni yangu mimi fukara ili watakao kufuata na kuomba urafiki kwa njia isiyo njema mungu akuonyeshe
kila la kheri mama ]
fukara
BC! kauli yako ya kulala masikini kuamka tajiri na mashaka nayo, ina maana mpaka leo na baada yazonge yote ya kina Lowasa bado tunaamini ukipewa shavu kwenye serikali yetu lazima utoke? that;s y siasa zetu lazima utoe rushwa ili uwemo miongoni mwa mafisadi…kudadadek…Mungu ibariki TZ Mungu ibariki Afrique
sasa huyu na mumewe hizo sura zao watoto wametokaje??hebu tutaftie picha za watoto tafadhali bc!
Masahihisho Bc,….Ameingia kwenye Selebrities sio “UTAJILI”
Kweli kiswahili kigumu kueleweka.Nyie mnaosema BC kakosea kakosea,hebu someni vizuri jamani.Hamuelewi nini hapo kwamba BC hakumaanisha habari za utajiri bali kuzungumzia jinsi maisha yanavyobadilika?
Halafu na wewe Gervas, sio utajili…ni utajiri.Mmesoma shule gani nyie?
I think it is time to start thinking of migrating to either Sumbawanga or Bagamoyo or Pemba to be successful! I don’t find anything interesting here in Monduli!
Hongera sana ndugu Tumbwike kwa kumsahihisha huyu ndugu Gervas aliyeandika UTAJILI badala ya UTAJIRI.
Kuna watu wengi na wazito na wasomi wengi wanaochafua lugha yetu maridhawa ya kiswahili, mfano wengi wanaandika
TAJILI badala ya TAJIRI, MLITHI badala ya MRITHI, ABDARA badala ya ABDALA, ARI badala ya ALI, ALI badala ya ARI, ALOBAINI badala ya AROBAINI, ARUTAKONTINUA badala ya ALUTAKONTINUA, LAMBO badala ya RAMBO, RAMBO badala ya LAMBO. Na mengineyo mengi. Sijui kuna shida gani imetokea mashuleni (hasa shule za msingi) kuanzia awamu ya pili ya utawala wa nchi yetu. Sisi tuliosoma wakati wa mkoloni na Awamu ya kwanza tulikuwa tunafundishwa matamshi na maandishi ya haya maneno vizuri. Kwa bahati mbaya hata waalimu wenyewe wa siku hizi wanaandika na kuzungumza ndivyo sivyo. Inabidi HAKIELIMU washughulikie suala hili pamoja na kuwa wanapigwa vita sana na wasiopenda maendeleo ya lugha ya kiswahili.
HONGERA MAMA,
KATIKA UTAMBULISHO, KAMA ILIVYO KWA AKINA BABA DHAO, BC MUWE PIA MNAWEKA WASIFU WA HAO AKINA MAMA DHAO SIO TU KUSEMA WAMEUKWAA!
Mama Hongera sana, Ama kweli kama umeandikiwa Yes itakuwa Yes tu hata kwa kuchelewa, Mbarikiwa naungana na wewe!!! mh!! wewe xxx !!!!!!!!!
Wewe uliyejiita XXX mpumbavu na huna adabu hata chembe eti sura, sijui watoto wake wanafananaje, hebu weka sura yako kwanza tukuone ndiyo useme, manake inaeleka hata jina lako ni matatizo matupu ndiyo mana umeogopa hata kuliweka. Shame on youe face.
mhhhhhh
Mnisamehe waungwana shule yangu ngubalu, afu miwani yangu iko kwa fundi…!! ila niewakirisha.
Sifa Heshima na Utukufu apewe Mungu kwa kuwa imejulikana kuwa yuko Mungu ndani yao kama kweli wao wanamcha Mungu basi ataendelea kujidhihirisha ndani yao. Wabarikiwe zaidi
Hao wote wawili yeye na mume wake ni choka mbaya tu. Hawa watakachofanya kwanza ni kujinyanyua wawe level na mawaziri wakuu waliotangulia. Alafu huyo mama siku hizi anajaribu kumuiga mke wa kikwete kuvaa huku akirudia rudia baadhi ya nguo. Viongozi waliochoka kama huyo na mumewe tanzania haiwaitaji kwa sasa. Mimi nampa huyu miaka 2 tu kabla hajaingia kwenye tuhuma ya ufisadi. Huyo mama pamoja na ukarimu kubwa aliokua nao bado pesa inaweza kuwafanya wawe dhaifu.
BC viongozi uwe unawaweka baada ya miaka kama 2 hivi madarakani sio mapema hivi. Wake za maraisi wanalipwa mshahara lakini mke wa waziri mkuu halipwi. Mavazi aliyoanza kuonyesha huyu mama inaashiria amesha kwangua akiba yake. Sasa tuone itakuwaje huko mbele. yangu macho.
Hongera mama
Uso wako wa kuvutia unaonyesha wewe cyo fisadi wala mumeo.
Embu fanya makeke utumikie wananchi badala yakuvaa nguo za gharama na kujifungulia miradi jenga kituo kikubwa cha watoto yatima uandike jina lako embu mbona wafadhili wako tuu ili muweke historia niajeeee………..
Alafu wewe xxx umeckia hapa ni ulingo wa urembo ama sirikali na maendeleo?
Muone sura yake kama soli ya sendeu unataka mama pinda ajikoboe na kuweka dhahabu ndiyo utamuona mrembo
songa mbele mamaaaaaaaaaa
Ni kweli jamani :” if iz yes” ni YES TU!!!!! haya mabingwa vifimbo cheza mnisahihishe hapo kwenye iz ila na mimi miwani yangu imevunjika kioo.
KWAKO XXX (tripple x) reception doesn’t matter, tukiangalia sura hatutafika kinachotakiwa ni uwajibikaji ulio makini kwa maslahi ya umma na kutuletea maendeleo siyo kuwa na attractive reception yenye mafumbo ya ufisadi ndani yake lakini huo ni mtizamo wako Mungu akupe ujasiri huo!
Nawe gervas, kwenye hoja #19 maana ya “ila niewakirisha” ni nini? Naomba utafute kamusi ya kiswahili sanifu uwe unaitumia wakati wa kuandika mada zako.
Kweli BC naona wamekosea hii sio kulala maskini kuamka tajiri, hii ni dhamana ya kuongeza nchi na kufanya maamuzi yatakayofaidisha wananchi simply ‘difficult responsibility’ if you wanna call it that. tuachane na ile imani potofu eti ukipanda cheo umeula au umetajirika hii ni kuendekeza rushwa na ubetekaji wa viongozi. He is upgraded to higher responsibilities that will cost him a lot of dedication and time less sleep hours and difficult decision making, etc all these so can move the country forward, lets pray for ‘em
I think umaarufu is a tiny portion of the outcome that they dont even pay attention to compared to the expectation they have to meet
kauli ya kulala maskini kuamka tajiri sioni connection yake hapa isipokuwa kama tunategemea watajilimbikizia mali kutokana na madaraka waliyopewa
We Said Kitu wivu unakukereketa tu huna cha zaidi. Hayo unayoyafikiria kuwa watayafanya nadhani ni mawazo yako wewe, na ungepewa hiyo nafasi wewe ndiyo ungetenda hayo uliyoyasema. MUNGU awabariki sana Bi Tunu na mumewe na awaongoze katika njia njema. WIVU SIYO DAWA hata siku moja.
“Said Kitu” isomeke Said Situ
Saidi Situ uko sayari gani wewe???unataka asivae nguo tofauti??kila siku atinge masuti tu au sijakuelewa?
Suala la yeye kujilinganisha na mama Kikwete ondoa unajuaje kama nguo anazovaa sasa alikuwa nazo toka long time sema tu alikuwa hasikiki wala kuonekana kwenye majority kama sasa pengine waweza kuta anaviwalo heavy sana kuliko yalivyo mawazo yako finyu….ama kweli mswahili ni mtu wa ajabu sana hasa wewe Saidi hivi ungekuwa wewe huyo mama usingeulamba??????????muache apige pamba kwa nafasi yake kwani nini bwana!!!!!!umeniboa sana ninahamu nikuone nikupashe!Eti choka mbaya mweeeeeee wewe uliyesmart una nini???
big up mama tunawatakia uongozi mwema
xxx,said,gervas = washasha LOL
congratulations mrs Pinda
HONGERA SANA MAMA TUMIA BUSARA KUMSAIDIA MZEE PINDA KATIKA SHUGHULI ZAKE ZA KILA SIKU. MUNGU AWABARIKI SANA, AMEN.
yaani huo ndiye mungu wa lslael alinayefanya njia mahali pasipo na njia kwani mungu hawahi wala hachelewi lakini anajibu maombi ndivyo mambo yalikuwa kwa bi Tunu hakutegemea wala kuwaza lakini mungu akitaka kukuketisha pamoja na wakuu anafanya, hongera sana mama usijitie mikorogo mama yangu rangi yako nzuri mno sura imetulia, hongera mshike sana mungu naye atakuwa pamoja na wewe.
hongera sana mama
Hebu acheni majungu…mnaandika nini sasa?kwani what wrong with her mpaka msema zali la mentali mara hakujua wala kuhisi one day atakuwa anaketi na vigogo,mme wake ni waziri mkuu pia mie namzimia kinoma lkn nyie wambea wote…Mbona hammsemi mama kikwete ambaye alikuwa mwalimu primary school?wtf?
Enyi mnaomponda mama Tunu, kumbukeni nanyi mmezaliwa na mwanamke, eti sura. ana ubaya gani huyu mama. na kuhusu kuvaa, huyu kigumegume said, huenda kazoea kumvisha mkewe madira yalochanika. sasa kumbuka huyu ni mke wa kiongozi mkubwa saana. hawezi vaa kama chokest mamaako wala chokest mkeo. Mama vaa wee, kuvaa kwako hakuitikisi pesa ya nchi vaa upendeze baba azidi kukuona chuma, na uiwakilishe tanzania kwa usmart wako. Wanapewa pesa za kununua suti na serikali wanasheria ili wawe smart kuiwakilisha nchi sembuse mama Mwenye heshma zake kama huyu, mwacheni mama ajinome.Na huyo aliyewaambia kua Pinda kabla ya kua Waziri Mkuu alikua kafulia nani? au ndio bongo na uswazi.Mnaongea tu bila utafiti.waache waseme usiku watalala. hongera mama usiyekua na makuu. huu ni wivu wanaadam wote tunao.