Pichani ni bondia Francis Cheka(kushoto) na Mbwana Matumla(aliyeipa mgongo kamera) walipokuwa wakipambana mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar-es-salaam.

Bondia Francis Cheka alimshinda Matumla kwa knock-out katika raundi ya kumi na hivyo kufanikiwa kutwaa ubingwa wa UBO(Universal Boxing Association) kanda ya Afrika.Kwa ushindi huo Cheka hivi sasa anahesabika kuwa “mbabe” wa familia ya kina Matumla kwani aliwahi pia kumtwanga bondia maarufu kutoka familia hiyo,Rashid Matumla.

Photo credits:Global Publishers

Feedback / Comments

5 Responses to “NI KICHEKO TU KWA FRANCIS CHEKA”

  1. Comment by David Douglas on March 3rd, 2008 5:47 pm

    Hahahaaaaaaa Cheka cheka sana kaka akina matumla wamekwisha tena hao, walilewa misifa haooooooooooooo. kwisha habari yao
    Asante Cheka Francis wa Moro kasoro bahari.

  2. Comment by David Douglas on March 3rd, 2008 5:49 pm

    Je Cheka unaweza kumpiga Amir Khan kijana mdogo? , kama waweza njoo mi ntakudhamini hehehe

  3. Comment by Nyau on March 4th, 2008 4:01 am

    Haha ha! Rashidi jana alikua anahojiwa anasingizia Cheka anatumia uchawi?! duh wabongo bwana hawakubali kushindwa! ingekua hivyo Tyson angekua mnageria. Haha! nilishuhudia papmbano nafikiri mazoezi ni muhimu, hata kama si mtu wa Cheka Jabu zake mwanangu UTACHEKA hahaha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  4. Comment by jomaeli on March 4th, 2008 4:36 am

    mnapigana bila sababu za msingi

  5. Comment by festo on March 4th, 2008 8:58 am

    Siri ya mafanikio ni kuongeza juhudi na kujifunza makosa kwa waliyoshindwa,cheka yupo taiti zaidi,sasa kina matumla wamlete ndugu yao mwengine.

Leave a Reply