JOTI NA KUBONYEZA KIZENJI

 

Msomaji wetu mmoja ametuandikia na kutuuliza swali ambalo limetuwia gumu kidogo kulijibu.Anasema, hivi karibuni alipokuwa nchini Tanzania(anaishi ughaibuni) alikuwa akisikia sana msemo wa mitaani unaoitwa “kubonyeza kizenji”.Anasema alipojaribu kuuliza wenyeji wake akaambiwa kwamba msemo huo umeanzia au kuanzishwa na Joti,muigizaji maarufu kutoka kundi la Ze Comedy.Miongoni mwa wenyeji wake na jamaa aliowauliza hakuna aliyempatia jibu la kuridhisha au kujitosheleza.Ndio maana akawa hana jinsi bali kutuandikia akitumaini kupata jibu kutoka kwetu.

Kwa bahati mbaya hata sisi hapa BC swali hilo limetupiga chenga.Na kama kawaida,hali hiyo ikitokea huwa hatuna budi kuomba msaada kwako msomaji/mtembeleaji wetu.Kama unafahamu,hebu msaidie huyu msomaji; Kubonyeza kizenji maana yake nini? Chanzo chake nini?

Pichani ni Joti akifanya hiyo mikogo ya “kubonyeza kizenji”

Page 1 of 3 | Next page