Kuna jamaa mmoja aliwahi kusema kwamba katika mapenzi,uongo lazima usemwe…japo kidooogo.Sina uhakika kama hilo ni la kweli au la.Utaniambia.Lakini inakuwaje kama huo uongo ukizidi?Yaani ukiwa “too much”?Na je ishakutokea ukaota unadanganywa?Ukiamka unamuelezea mwenzio juu ya ndoto yako au unauchuna tu?

Ukitaka kupata jibu au dalili za jibu,basi msikilize Hayati Mbaraka Mwinshehe katika wimbo wake Mashemeji Wangapi akilalamika jinsi ambavyo idadi ya mashemeji imemzidia.Wamekuwa wengi kiasi kwamba anashanga kwanini mwenzie asifungue tu shule aiite “College ya Mashemeji”.Pata burudani,pata ujumbe.Ijumaa Njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Feedback / Comments

24 Responses to “MASHEMEJI WANGAPI?-MBARAKA MWINSHEHE”

  1. Comment by Mswahilina on March 14th, 2008 3:27 am

    Big up BC, Wengi utatukumbusha wakati wa Ujana wetu. Ninakutakieni Kazi njema.

  2. Comment by Debora kiaka kizuguto on March 14th, 2008 7:56 am

    si utani japo nilikuwa mdogo lakini niliziimba sana enzi hizo muweke vitu kama hivyo siku njema

  3. Comment by Gervas on March 14th, 2008 8:41 am

    Weee Mswahilina, ya kweli hayo? mi mwenyewe kibao hiki kinanikumbusha mkesha wa mwaka mpya 1962 pale morogoro, mara baada ya uhuru tu! tena nakumbuka kibao hiki kilitoka sambamba na kibao “chaupele mpenzi wangu” teh, teh tulikuwa tuna-shake babe, na togwa mkononi.

  4. Comment by simba on March 14th, 2008 9:34 am

    Nakubali unatukumbusha mbali, weka basi NIMEHAMIA MTAA WA SABA, NA TOKA LINI JOGOO LA SHAMBA LIKAWIKA MJINI

  5. Comment by Chris on March 14th, 2008 9:51 am

    Hili songi nimelikubali…. Cheers guys… College ya mashemeji… Tutapata wapi waimbaji km hawa tena…

  6. Comment by Musa on March 14th, 2008 11:05 am

    Asante sana kwa kutuwekea kibao hiki wengine tuok mbali,tunakumbuka nyumbani na mambo mengine mengi,asante sana

  7. Comment by Mswahilina on March 14th, 2008 4:08 pm

    Mwanafunzi wangu wa Kiswahili “Gervas”, Big up.

  8. Comment by Chris on March 14th, 2008 4:38 pm

    Mswahilina na Gervas nani katambulishwa km shemeji…. Ni nani anaota anadanganywa….

  9. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on March 14th, 2008 5:06 pm

    BC. Mie ninawakubali, kwa lugha ya “ulaya” ninasema “Big up”.
    Mie ninapenda sana hizi zilizopendwa wakati huo. Kuna ombi langu nilitoa kwenye mada zilizotangulia:
    “Mtuwekee pia Makassy, Chidumule, Ndekule, Bayankata, n.k.” Lakini kwa Ujumla NINAKUFAGILIENI BC, keep it up.

  10. Comment by Gervas on March 15th, 2008 12:04 am

    Chris, uchokozi huo sasa, hujui unanikumbusha gramaphone yangu iliyoliwa na panya?

  11. Comment by Gervas on March 15th, 2008 12:10 am

    Mswahilina, sasa unaniabisha tena hapa, na nashangaa kama kweli wakipenda kiswahili, sasa “Big Up” ninini? tena hiyo ndo mbaya kabisa kuchanganya lugha, unaharibu tashwishwi nzima ya kiswahili na unastahili bakola tu.

  12. Comment by Mswahilina on March 15th, 2008 4:00 am

    Chris, wewe ndiye uliyetambulishwa kama shemeji….
    Na wewe ndiye unaota kuwa umedanganywa….
    Kuna methali ya Kiswahili inasema hivi:
    “Cha mwenzako kigumu, meza mate ulale”
    ikiwa na maana kuwa:
    “Mambo yasiyokuhusu usiyakodolee macho”
    na nyingine inasema hivi:
    “Dunia mti mkavu kiumbe usiuelemee”
    ikiwa na maana kuwa:
    “Mimi ni nyumba ya Udongo sihimili kishindo”

  13. Comment by Godluck on March 15th, 2008 4:17 am

    kusema ukweli wakubwa zangu mi ni kijana wa miaka 27 tu sema nazikubali sana hizi nyimbo na hii moja ya nyimbo zinazoniacha na raha mustarehe,kweli wakubwa zangu mlifaidi sana

  14. Comment by mkwanja on March 15th, 2008 5:43 am

    Aaaaaaaaaaiiiiiiiiiiiiiih Hata Michuzi pia ni shemeji yangu? aaaaah siwezi mwenzio zarau! Hata Bangusilo naye ni shemeji yangu? Matonya pia ? Hata huyu muuza mikeka mtaa wa pili? Aaaaaaaaaaaaaaaah Basi bora ufungue College ya Mashemeji. Michuzi bado hatujapata Mbaraka Mwinshehe mwingine ndugu yangu!Endelea kuweka mavituuuuuuuz kila wikiendi.

  15. Comment by Matty on March 15th, 2008 6:07 am

    Shamooni kakazangu Gervas, Mwalim Mswahilina na Chris maana miaka aliyoongelea Kaka Gervas ya naintini sixte tu sikuwepo kabisa kwenye ramani ya dunia….haya nawatakia weekend njema wote!

  16. Comment by Matty on March 15th, 2008 6:08 am

    Sorry naomba Kujisahihisha mwenyewe kabla Mwalimu hajaona “HAPO MWANZO PASOMEKE SHIKAMOONI”

  17. Comment by Juma Zengwe on March 15th, 2008 9:21 am

    BC,
    Naona kuna watu wengine ni wageni hapa.Tunawakaribisha.Nasema hivyo kwa sababu kuna wengine inaelekea hawajui kwamba kila Ijumaa hapa wenzao huwa tunafaidi na “oldies” za bongo ambazo kikweli ndio muziki haswa.Kwa kuwasaidia,ukienda pale kwenye kalenda juu upande wa kulia na kubonyeza tarehe za ijumaa zilizopita utaweza kusikiliza oldies zote ambazo wameshaziweka.

    Nawafagalia sana BC na nawatakieni kila la kheri.Ijumaa yangu huwa haijakamilika bila kuingia BC na kupata burudani.

  18. Comment by Mswahilina on March 15th, 2008 10:05 am

    Gervas, andika BAKORA sio BAKOLA.

  19. Comment by Chris on March 15th, 2008 2:14 pm

    Marahaba Matty. Weekend yako naamini ni nzuri kabisa, na natumai hata shemeji haulizi kwamba “Yaani Matty hata Chris nae ni shemeji yangu”? Hahahahahaaaa kidding…

    Lakini Gervas inamaana haya maneno “gramaphone na tuna-shake babe” hayana kiswahili chake? Au umeona tu Big up ya Mswahilina?

  20. Comment by Gervas on March 15th, 2008 3:22 pm

    Matty…Marakhabaaa!!! mtoto umejaa heshima!! Asante, …Chris, “Gramaphone na kushake – babe” ukitumia kiswahili tu maana yake haitaeleweka kwa wasomaji. labda niandike gramafoni na kusheki. sasa wewe ungetafuasili vipi?

  21. Comment by Mama wa Kichagga on March 15th, 2008 11:32 pm

    Real song/sound from a real man!

    Kazi ilifanyika na naamini kipaji hiki kimerithishwa kwa mtoto/mjukuu!

    Mbaraka hana mpinzani katika fani hii!

  22. Comment by Malenga on March 16th, 2008 11:59 am

    Mswahilina niuzie hali yako,..Ama bwana Gervas nafurahi sana kuona jitihada zako za kuwa sambamba na marekebisho ya Mswahilina juu ya matumizi na ufasaha wa uandishi wa lugha uwapo kwenye safu hii ya kutoa maoni.Mswahilina wenye hekima wanasena “Koti la mzee halikosi Chawa” hivyo nakuomba hizo chawa zako endelea kuzitoa kwa Bw Gervas na wengine ili hatimaye mambo ya lugha yawe juu ya mstari.Na Bw Gervas vishindo vya Mswahilina visikufanye utishike na pia visikufanye ulale mlango wazi.Ila zingatia tu kuwa,sisi wahenga tunasema “Atangae sana na Jua mwishowe hujua”
    BC Hongera mmeifanya furaha yangu isifikie kifani.

  23. Comment by Malenga on March 16th, 2008 12:01 pm

    …wanasema sio wanasena….BC

  24. Comment by DUNDA GALDEN on April 2nd, 2008 3:01 pm

    DUH WE ACHA ENZI .NIMEMWITA MKE WANGU AJE ASIKILIZE NINI MUSIC NAE KABAKI ANADUAWAA KWA MAANA YA MWIMBO HUO,HIZO ZILIKUWA SI MCHEZO KAKA INGAWA UMRI WANGU ULIKUWA MDOGO NILIKUWA NAMUONA MAREHEM BABA YANGU MDOGO AKIWA KINARA KWENYE HIZO KWANI YEYE PIA ALIWIKA KWENYE BAND MOJA PALE BWAGAMOYO MPKA AKAPATIWA JINA LA KOBRA KWA MAANA YA UKALI WA SAUTI MUNGU AMLAZE MAHALI PEPA PEPONI NA WENGI WENGINEO AMBAO HATUKO NAO HAPA DUNIANI
    DUNDA GALDEN CHAFOSA CHAI GODA NEVER DIE

Leave a Reply