Raisi Jakaya Mrisho Kikwete,akisoma hotuba wakati wa uzinduzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) leo mchana jijini Dar-es-salaam.TBC imezinduliwa upya rasmi leo pamoja na nembo/logo mpya ya shirika hilo.Kuanzia sasa, iliyokuwa Televisheni ya Taifa (TVT) itaitwa TBC-One na iliyokuwa Radio (PRT) itaitwa TBC-FM na pia kutakuwepo na External Service itakayoitwa TBC International.

Wengine pichani (kulia kwa JK) ni First Lady,Mama Salma Kikwete na Tido Mhando ambaye ndio Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo.Kabla ya kurudi Tanzania kushika wadhifa huo mpya,Tido Mhando alikuwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza(BBC)

 

Nembo mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC).Nembo ina kauli mbiu ya Ukweli na Uhakika. Ni matumaini yetu kwamba hivyo ndivyo itakavyokuwa na si vinginevyo.Picha zote na Ahmad Michuzi.

Feedback / Comments

22 Responses to “JK AZINDUA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TANZANIA”

  1. Comment by Dinah on March 26th, 2008 10:54 am

    Bomba-bomba, ukweli na uhakika bila kulindana….kila la kheri.

    By the path, Kighana Mama Salma na Huyo m-baba(Mhando) wanaowakilisha ujumbe kuwa ni mume na mke au pea/couple kwa vile wamevaa sare. Tufanje research za mavazi kabla hatujavaa na kuruhusu picha kwenda kimataifa kwani inaweza kusababisha misunderstanding. :-)

  2. Comment by Kimori on March 27th, 2008 3:39 am

    Kuna kitu mimi nashindwa kuelewa watanzania wenzangu labda mnieleweshe. Hivi kweli rais wa nchi hana shughuli zingine nyeti za kufanya mpaka awe tu mara kwa mara anazindua TBC, Mlimani City, nk, kazi ambayo hata waziri angeweza kuifanya? Si mara ya kwanza kusikia kuwa rais anazindua “upuuzi” mwingi tu nchini au imekuwa ni fashion kumualika rais hata mpaka kwenye birthday?

  3. Comment by Mconel on March 27th, 2008 6:22 am

    Mimi ninachoshangaa, logo ina TBC ni abbreviation ya kiingereza then kauli mbiu ni kiwsahili, kwani nini wasieke kiingereza pia? kwa sababu nadhani TVT ilikuwa ya kiswahili na wamefanya mabadiliko nusu,Mmechemsha.

  4. Comment by Chris on March 27th, 2008 7:54 am

    BC mbona hamko hewani? Mmetekwa nyara? Au mmeamua kujiunga na hiyo TBC? Nasikia inavipindi vizuri sana hiyo TBC?

  5. Comment by Matty on March 27th, 2008 8:55 am

    Haya jamani tujulisheni na wengine hivyo vitenge vinapatikana wapi na sie tukanunue tushone na tuweke shuka begani wamama oyeeeee!!!!Any uko wapi leo!

  6. Comment by Simon Kitururu on March 27th, 2008 9:40 am

    Najiuliza tu!Kwanini hili shirika kila naposoma linasisitiziwa kwa kiingereza yaani; TBC kuliko SUT aka Shirika La Utangazaji Tanzania? Nazinguka kidogo nionapo TBC halafu msemo chini yake uko kwa kiswahili;Ukweli na Uhakika.

  7. Comment by Gervas on March 27th, 2008 9:54 am

    BC vipi? mbona kimya? au ndo na wewe walishaku-Jambo Forum? maana jana JK nimesikia anakoromea the abuse of the freedom of speech, amewambia owners mtajuta, Kipanya sijui amemwelewa? waachieni wamarekani bwana wenye pure democracy, nchi zetu bado ubabe mwingi, ukifungua mdomo tu rungu….ngoja nijinywee the ulanzi wangu hapa.

  8. Comment by binto on March 27th, 2008 7:34 pm

    na viongozi wanaotumia madaraka vibaya waondolewe haraka sana, haswa wale walio nje ya nchi, ambao hata kazi za maana hawafanyi.

  9. Comment by kijiwe on March 27th, 2008 8:13 pm

    TBC si wameiga BBC?
    upuuzi mtupu!
    i told you guys huyu jamaa msanii kinoma 2010 anachaguliwa tena LOL au copy yake ili imlinde

  10. Comment by amina on March 28th, 2008 2:58 am

    bc mi nataka hicho kitenge nitapata wapi?urafiki kipo au pale mnazi mmoja nitapata

  11. Comment by mtanzania on March 28th, 2008 7:17 am

    hiyo nembo jamani kubwa sana!! inaziba karibu nusu ta screen!! fanyieni editing tafadhari

  12. Comment by Mimi on March 28th, 2008 1:09 pm

    Jamaa Tido kwa sababu alikuwa BBC sasa analeta kasumba za TBC wakati lugha yetu ya taifa ni kiswahili. Kwani wakiliita SUT (SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA TAIFA) kuna ubaya gani?. Nchi zote zilizo makini zinaweka mambo yao kwenye lugha zao, sasa hawa wanaleta ushamba wa kikoloni wakati asilimia kubwa ya wananchi ni waswahili na wanaongea kiswahili. JK naye kila analoambiwa yeye anafuata mkumbo kama bendera bila hata kufikiria maslahi ya wabongo wa kawaida walio wengi ambao ndio wenye mali. Nchi yetu bwana hah!, ovyo kweli.

  13. Comment by binto on March 28th, 2008 2:19 pm

    mama kikwete unavaa vipya kila siku.

  14. Comment by Mswahilina on March 28th, 2008 2:23 pm

    Dinah: umenichekesha kwa kufananisha waliovaa nguo zinazofanana.
    Kimori: TBC, Mlimani City, nk, sio “upuuzi”.
    Mconel: Tanzania tunatumia Kiswahili na Kimombo.
    Gervas: Hongera kwa kuandika kiswahili fasaha.
    Kijiwe: sio upuuzi, pia JK sio Msanii, na ujue kuwa Mungu akimpa uzima ni ‘LAZIMA’ achaguliwe 2010.
    Mtanzania: andika ‘tafadhali’ sio ‘tafadhari’ inavyoeleweka kwa mtanzania halisi anaandika kiswahili (kitanzania) halisi.

    TUKIPENDE KISWAHILI NI LUGHA YA AFRIKA.

  15. Comment by kijiwe on March 29th, 2008 8:09 am

    Mswahilina: awe au asiwe msanii hiyo ni opinion yangu kama wewe unaona siyo msanii poa tu hiyo ni opinion yako na naiheshimu so tafadhali heshimu ya kwangu pia.

    naku quote “na ujue kuwa Mungu akimpa uzima ni ‘LAZIMA’ achaguliwe 2010″

    mbona unajichanganya mwenyewe? kwani mi nimesemaje si nimesema ATACHAGULIWA TENA au?
    soma tena tafadhali.

  16. Comment by kijiwe on March 29th, 2008 8:18 am

    Halafu wewe Mswahilina mbona unapandisha jazba kwa spidi?
    Kimori kaongea point ya maana na ninakubaliana na yeye kuwa hizo kazi za kufingua TBC,Mlimani City n.k hata mawaziri wanaweza kuzifanya.Amezidi kuwa kila kitu kwa hiyo wazalendo hatuna budi kutoa maoni yetu kuhusu usanii kama huu.

  17. Comment by siza on March 31st, 2008 5:36 am

    nikwambieni tbc hawajaiga bbc..nilikua naperuzi kitabu kimoja kilitungwa na mwl nyerere jana nikakuta picha ya zamani miaka ya 60 mwl anaongea na vyombo vya habari moja wapo ya mic imeandikwa tbc..sasa mi ninachhooona wamejaribu kufufufa tena tu hili jina,msiangalie mbele angalieni na nyuma mnauhakika kama wameiga bbc?

  18. Comment by changalamacho on April 1st, 2008 4:16 am

    Nembo au kifupisho cha TBC kinapendeza kukitamka na hakileti ukakasi ulimini.TBC is OK.Chini yake maneno yanasomeka, UKWELI NA UHAKIKA, sawa sina tatizo nalo,yanafaa na maana nzito.Sina uhakika kama kweli CCM au SERIKALI ikiboronga watakuwa na ubavu wa kuikosoa waziwazi bila ya upendeleo wowote.Tusubiri tuone.Wadau wa TBC tutalifuatilia hilo kwa karibu zaidi.Pendekezo langu hapa ni kwamba juu ya kifupisho TBC ni vyema yangekuwepo maneno yasomekayo,SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA TANZANIA, badala ya English Version yake ya Tanzania Broadcasting Corporation, kwa faida ya wote , wanao zungumza Kiswahili na wale wanao zungumza English. TBC ni ya kimataifa .Kwa hiyo mseto huo utakubali vilivyo. Hali kadhalika jitahidini TBC kuboresha ile ‘BACKGROUND SHOWROOM YA USOMAJI WA HABARI’ kama zinavyo onekana za wenzenu.Ukutani kuwepo na DIGITAL SCREEN KUBWA kwa ajili ya matukio,mahojiano,na pazia.Otherwise Tiddo pongezi mabadiliko katika Quality ya Vipindi hususan asubuhi katika JAMBO AFRIKA tumeanza kuyaona.Kila baada ya Nusu Saa pawepo na HABARI KWA UFUPI hata kama ni dakika moja tu.Asubuhi tathmini ya magazeti ifanywe na watu waliobobea katika Fani mbalimbali kama SKYNEWS wanavyofanya au TV Channels nyinginezo.Tangazeni zaidi Mazingira na Vivutio vya Utalii Nchini.Vitawaongezea matangazo zaidi ya Biashara.Kazi njema.

  19. Comment by Sebastian Peter on April 19th, 2008 5:54 am

    Ninapenda Kumpongeza sana Mheshimiwa Tido Mhando kwa juhudi zake za kulifanya Taifa letu liwe juu Ki-HABARI. Nchi inaonekana kuwa inakwenda wala si kwamba imesimama sehemu moja kama zamani!!!!

    Hongera Tido, Hongera Serikali Tukufu, Hongereni wafanyakazi woote wa TBC, maana kutoka TBC hapo kale kuja RTD na sasa inarudia tena TBC, Tanganyika Broadcasting Corporation, na sasa Tanzania Broadcasting Corporation) kweli huyu Mheshimiwa Mhando anaijua Historia ya Nchi yetu.

    Ninaomba nijue kama wanaweza kupokea nyimbo kwa njia ya Mtandao, pia sijaona website ya TBC ikiwezekana nijulishwe niweze kuiona.

  20. Comment by chauled on May 12th, 2009 5:27 am

    Hongera shirika la utangazaji Tanzania a.k.a TBC,kiukweli sasa mpo juu,hasamnapotoa tafsiri ya kingereza kwenda kiswahili hii yote ni kuwezesha watanzania kuelewa kile kinachoongelewa ktk taarifa ya habbari,pia kuwa na mahoijano ya moja kwa moja kwa kingereza wanaita LIVE.
    Inaelekea TBC kuna michuzi ya kutosha sasa naona kuna watangazaji kutoka vyombo vya habari binafsi kujiunga na tbc
    La muhimu kupanua studio kuwa kubwa na ya kimataifa ka vile bbc,presstv n.k

  21. Comment by Ray Ephraim Ndewingiya Njau on October 30th, 2009 10:38 am

    Hongera sana ndg Tido na timu kazi yako kwa kujipanga vema katika tasnia ya habari na mawasiliano kwa umma.Kwa kuwa TBC ni mali ya watanzania chini ya uongozi wa watanzania kwa manufaa ya watanzania naomba chumba cha uhariri wa habari kihifadhi rasilimali watu ya wanazuoni wa lugha ya Kiswahili ili usanifu wa lugha uzingatiwe katika matangazo yote ya TBC.TBC iwe kiranja wa idhaa zote za nje zinatangaza kwa lugha ya Kiswahili kwa kuwa mahiri na makini katika matumizi ya lugha ya Kiswahili.Mwisho ndugu Tido na timu kazi yako mtoe elimu kwa watanzania juu ya uwezo wa lugha ya Kiswahili katika zama hizi za sayansi na teknolojia.Ubishi ni mkubwa sana miongoni wa wadau wakibishania kuhusu uwezo wa lugha ya Kiswahili katika asasi za elimu ya juu.Mimi naamini kuwa Kiswahili kina uwezo sawa na lugha zote za kimataifa ila kinachokosekana miongoni mwa wadau ni kuthubutu na uhamasishaji ufaao.
    Wasalaam na shukrani
    Mdau na mtetezi wa lugha ya Kiswahili
    Dar es salaam.

  22. Comment by Ray Ephraim Ndewingiya Njau on October 30th, 2009 10:52 am

    SALAAM NDUGU TIDO MHANDO;
    HONGERA KWA KUTHIBITISHA MSEMO HUU:”UKARIMU HUANZIA NYUMBANI”.KUONDOKA KWAKO LONDON HADI DAR MIKOCHENI NI JAMBO LA PONGENI NA SHUKRANI KAMILI.HONGERA SANA KAKA TIDO.
    UMAHIRI NA UMAKINI WAKO KATI UGA WA HABARI NA UTANGAZAJI NI FAHARI KWA WANAZUONI WOTE WA TAALUMA YAKO.WAKATI HAYO YAKIENDELEA NAKUOMBA UBADILISHE MANDHARI YA STUDIO ZA TBC1 INAPAMBWA KWA MAJENGO KADHAA NA UWEPO MLIMA KILIMANJARO,VISIWA VYA ZANZIBAR NA MBUGA ZA SERENGETI BILA KUSAHAU UJUMBE HUU:”KARIBU TANZANIA KWENYE ARIDHI YA MLIMA KILIMANJARO,VISIWA VYA ZANZIBAR,MBUGA ZA SERENGETI NA DARAJA LA KIBIASHARA KWA NCHI ZA MAZIWA MAKUU.”

Leave a Reply