Ni Ijumaa tena.Baada ya mapumziko ya sikukuu ni wakati mwingine tena wa kutafakari na kupanga mikakati.Maisha ndivyo yalivyo,hakuna kusimama wala kungoja.Kila siku ni mchakamchaka.Raha na karaha ndio mtindo.
Zipo nyimbo ambazo zikipigwa,kwa njia moja au nyingine,ni lazima zikukumbushe jambo au mambo fulani.Kama hukumbuki enzi zile za mchana mwema chini ya utawala wa RTD peke yake basi unaweza kukumbuka kuyaruka majoka huku noti nyekundu zikiwa na thamani.Ili mradi tu,kwamba hivi leo kila kukicha kheri ya jana!Yaani kwamba dunia ile ilikuwa nzuri kuliko tuliyonayo hivi sasa.Najua kwamba hoja hii inaweza kuwa pana.Lakini leo sio wakati wake.Ijumaa ni wakati wa kubwaga manyanga chini na kupumzisha akili.Majirani zetu(kule ulipo Mlima mrefu!!!) wao siku hizi wanasema ni wakati wa “kubanjuka”.
Leo tunao Bima Lee Orchestra.Wimbo ni Mesenja.Naam,mesenja yule yule aliyeleta balaa.Za nyumbani akapeleka ofisini na za ofisini akapeleka nyumbani.Nyumba unaweza kuiona ndogo ukifanya masihara.Bonyeza player hapo chini upate burudani.Ijumaa Njema.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Page 1 of 3 | Next page