MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

 

Wiki chache zilizopita ilielekea kwamba suala la “mpasuko” wa kisiasa visiwani Zanzibar lilikuwa limepatiwa ufumbuzi.Mambo yanaelekea kuwa yamebadilika kufuatia kikao cha CCM huko Butiama hivi majuzi. Ni nini kimetokea?Demokrasia au kitendawili?Kama hujui nini kinaongelewa bonyeza hapa na hapa na hapa kwa undani wa kilichotokea huko Butiama na tathmini nzima ya suala la muafaka.Wakati huo huo soma habari kuhusu Katibu Mkuu wa CUF,Seif S.Hamad kutimkia Ulaya kuwashitaki CCM kwenye Jumuiya ya Madola kwa kubonyeza hapa.

Pichani ni Katibu Mkuu wa CCM,Yusuph Makamba.Picha kwa hisani ya Global Publishers.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

24 Responses to “MUAFAKA ZANZIBAR;DEMOKRASIA AU KITENDAWILI?”

  1. Comment by Majita on April 2nd, 2008 11:28 pm

    CUF si mchezo.Mara hii tu wameshamtoa mzee wa watu “NAKOZI” hapo kwenye paji la uso.Du!!! kumbe ndo maana CCM waliktaa muafaka ni kulipiza kipondo hicho alichopata Makamba

  2. Comment by Komba .H on April 3rd, 2008 1:49 am

    Kilichofanyika Butiama ni kitu kibaya ambacho huenda kikasabisha vurugu kule Zanzibar.Watanzania wengi tulifikiri ccm watatupa mambo mazuri ya kuondoa mpasuko kumbe wao ndio wameongeza mpasuko zaidi.Sasa tunasikia kuwa Maalim Seif anaenda kuishitaki serikali yaani ccm kwa wafadhili picha inaonyesha bakola zitakuja kwa wananchi watanzania na si kwa ccm maana wao wanamaisha mazuri familia zao ziko na hali nzuri watakaoteseka ni watu wenye kipato cha chini .Shida tulizo kuwanazo hatujaziweza kuzitatua kama vile EPA,Ricmond,Umeme,BOT ,Ajira na maisha bora kwa kila mtanzania hatujaweza kutatua sasa linakuja lingine la mpasuko zanzibar sijui hii nchi Raisi Kikwete anaipeleka wapi.

  3. Comment by Mzalendo on April 3rd, 2008 2:36 am

    Nimesoma haraka hotuba ya raisi kupitia Michuzi sinior blog. Nilichoelewa rais amesema CCM imeamua makubaliano yapelekwe kuamuliwa na wananchi.

    Kwa maoni yangu nafikiri CCM chini ya rais Kikwete wamechemsha. Kwa upeo wangu mdogo nikiwa mzawa wa bongo, sina ushahidi wowote kushirikishwa kwenye mambo muhimu mfano suala la muungano n.k. Hata wazazi wangu ambao ni wakereketwa wa CCM nafikiri walisimamia kwenye kauli mbiu “zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM” Nimekuwa nikisikia tunawawakilishi bungeni lakini sio kweli yanayopitishwa huko ni uamuzi wa wengi wape au ni kutetea matakwa ya tabaka la wachache.

    Rais wetu ameheshimika kusaidia muafaka wa jirani zetu Kenya. Swali ninajiuliza, mbona huko Kenya hawakutaka maamuzi yapelekwe kwa wananchi?

    Mheshimiwa rais alikuwa na uwezo na ushawishi wa kufanya kama kule Kenya, inawezekana amekutana na upinzani mkali ndani ya chama. Kama kweli wapo wanaopingana na busara, je wana maono ya kulitakia mema taifa?

    Nafikiri ni vema busara ikatumika kuepusha nchi changa na maskini kama Tz kujiingiza kwenye machafuko yasiyo ya lazima. Machafuko yanapotokea wanaoathirika ni watu wa chini na sio wanasiasa wenye mazingira ya uhakika kimaisha.

    Mimi sikutegemea suala la vikao vya muafaka kuchukua muda mrefu badala ya kujadili mikakati ya kuinua uchumi. Ninafikia kukubaliana na usemi kuwa waTz tumejaliwa mazungumzo bila vitendo.

    Nilitegemea suala lilitokea Kenya litakuwa darasa zuri kwetu lakini naona tunapuuzia. Nafikiri siasa za maneno matupu zimepitwa na wakati ikiwa tumekusudia kuendana na mabadiliko kimaendeleo.

  4. Comment by Salim K on April 3rd, 2008 2:39 am

    Hiyo ni danganya toto ya CCM, wanapitisha muda mpaka 2010
    Lakini binadamu si mawe iko siku watu watachoka.

  5. Comment by changalamacho on April 3rd, 2008 6:29 am

    Suala kama hilihili la Muafaka huko Kenya Rais Kikwete alikwenda kwa ridhaa yake mwenyewe na kuwa shahidi wa Maafikiano yaliyotiwa saini na Kibaki na Raila kwa niaba ya vyama vyao vya siasa, PNU kwa Kibaki na ODM kwa Raila, kuhusu kuwepo kwa serikali ya mseto,mabadiliko ya Katiba pamoja na mengineyo.Yote haya yalihitimishwa na Viongozi wa Vyama , Raila na Kibaki kwa niaba ya vyama vyao.Halikurudishwa suala hilo kwa wananchi tena ili wakapige kura ya maoni eti kwa sababu yalikuwa masuala nyeti sana na yalihusu mabadiliko makubwa katika mfumo wa serikali!Kwa Kikwete huu ulikuwa ni uamuzi wa busara sana kufanya kwa lengo la kudumisha amani na umoja wa kitaifa nchini Kenya.Fine.Tena mbele ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan akimwakilisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.Fine.Leo hii, suala la Muafaka wa Zanzibar baina ya CCM na CUF ambalo maudhui yake ni yale yale kama muafaka uliotiliwa saini Nairobi Kenya baina ya ya PNU na ODM hivi karibuni tu, Kikwete huyo huyo kabadilika badala ya makubaliano hayo kutiwa saini na pande zote mbili sasa yamerejeshwa yakaanze upya kwa kura ya maoni toka kwa wananchi eti kwa sababu ni masuala mazito na nyeti sana yatakayo sababisha pengine marekeisho ya Katiba na mabadiliko katika Mfumo wa Serikali ya Zanzibar na pengine katika Muungano(?).Huu tuuite nini, UNAFIKI AU KITU GANI?Kumbukeni katika kila hatua ya makubaliano kila upande ulirejea katika chama chake na kupata ridhaa ya kile kilicho jadiliwa na kama kuna pingamizi zilirekebishwa ndipo hatua iliyo fuata ya majadiliano ilipoendelea.Vivyo hivyo hadi hatua ya mwisho ya maafikiano.Lingeibuka suala la kupata KURA YA MAONI ya Wazanzibari wenyewe mazungumzo hayo yasingefikia hatua hiyo iliyofikiwa,yangesitishwa mapema ili wananchi wapewe fursa ya kutoa kura ya maoni.Hilo halikufanyika kwasababu umuhimu huo haukuwepo.Hivi CCM inaipeleka nchi hii wapi?Mzizi wa Fitna tumesha utambua.Fumbo mfumbie mjinga.Mwerevu atalitegua! Sisi yetu macho.Ukipanda Bamia utavuna Bamia!Inshallah.

  6. Comment by ISMA KABENGO on April 3rd, 2008 8:45 am

    MIMI BINAFSI MAWAZO YANGU NI KUWA IMEFIKA WAKATI ZANZIBAR WAENDELEE KIVYAO MUUNGANO HAUNA M,AANA YOYOTE KWA WATANZANIA,SISI BARA TUENDELEE KUITWA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ,NA ZANZIBAR WAITWE JAMHURI YA ZANZIBAR,IMEMEGUKA URUSI TUTAKUWA SISI????

  7. Comment by Mswahilina on April 3rd, 2008 9:06 am

    CCM – Zanzibar kuna Wahafidhina wengi.

  8. Comment by changalamacho on April 3rd, 2008 10:32 am

    Bara ndiyo TOO MUCH tena wanatoka mkoa fulani, niutaje?Tukiwachekea hawa watatuharibia nchi nakwambia Mswahilina.

  9. Comment by Gervas on April 3rd, 2008 11:03 am

    power sharing inajumuisha kubadilishwa kwa katiba. katiba haiwezi kisheria kubadilishwa kienyeji tu na mwafuaka wa vyama viwili kwani kuna vyama pia vya siasa vingine vilivoshiriki uchaguzi wa 2005. pili kuna utaratibu wa kuwahusisha wananchi ktk kubadili katiba. wananchi hatumaanishi ccm na cuf pekee. kikwete hajakosea kusema hivo. ni kwamba cuf watulize boli hatua zifuatwe. justice can be delayed but not denied. haya ni mawazo yangu mimi

  10. Comment by Mzalendo on April 3rd, 2008 1:58 pm

    Hakukosea aliyebuni usemi “haiwezekani kesi ya ngedele kula mahindi, kumpelekea nyani atoe uamuzi/hukumu” Ni kwa namna gani utazungumzia haki kwenye mazingira ya kutatanisha kama uchaguzi kenya na zanzibar? Kila mwenye akili timamu including CCM chama tawala wanaelewa kuwa zanzibar kuna tatizo. Sasa nini faida ya kuchelewesha kupitisha maamuzi yaliyokubaliwa kama ilivyofanyika kenya?. Nafikiri ”delayed” inayosemwa hapa iko kusimamia maslahi kitabaka na sio kitaifa.

    Nionavyo mimi Kigezo cha msingi ni amani kwa wote ndio maslahi kitaifa. Palipo na amani shughuli za kimaendeleo zinafanyika na uchumi unainuka kuwawezesha wenye uhitaji. Tuanapoichezea amani kwa siasa za kulindana/mizengwe, matokeo yake yana madhara makubwa sana kitaifa.

  11. Comment by any on April 3rd, 2008 3:49 pm

    ameanza kuzeeka babu wa watu! saa ingine nilikuwa nashindwa kujua wakati gani anatania au yuko serious. funny guy.

  12. Comment by Subby on April 3rd, 2008 4:36 pm

    Sasa waingize CUF kwenye serikali ya mseto huko Unguja na vyama vingine je? Ina maana Zanzibar kuna CCM na CUF tu hakuna vyama vingine?

    Hili suala si la kulifanyia mchezo suala la kuunda serikali ya mseto linahitaji mabadiliko ya katiba, watu wanashindwa kutofautisha ya Kenya na Zanzibar. Muafaka unaotakiwa Zanzibar ni kuwa sio lazima hivyo vyama vya siasa vipate ushindi kiduchu ili kuunda serikali ya mseto hata kama wakishinda kwa asilimia kubwa, basi serikali ya mseto iundwe. Na huwezi kuunda hiyo serikali sasa, muafaka ni maandalizi ya mabadiliko ya katiba. Hao hao wanzanzibari mnaowatetea leo, haweshi kulalamika kuwa hawakushirikishwa kwenye muungano na muungano ulisainiwa na Nyerere na Karume wao hawautambui na wamepeleka kesi mahakami. Tena hao wanaodai wao kama hawakushirikishwa kwenye maamuzi ya muungano ni hao hao ambao sasa hawataki hili suala la muafaka wananchi washirikishwe. Hii ni double standard, wanaogopa nini? Iweje wadai wananchi hawakushirikishwa kwenye muungano hivyo muungano ni batili na inapokuja suala la kusema washirikishwe kwenye muafaka hawataki? Je huo muafaka nao usipokidhi mahitaji yao hawatasema batili kwa kuwa wananchi hawakushirikishwa? Je ikitokea ccm na chama kingine cha siasa huko visiwani vikapata kura zaidi ya CUF watakubali hao wa chama kingine waunde serikali na CCM bila wao? kwani hakuna garantii kuwa cuf au ccm ndio vitakuwa vyama daima dumu.

    Ninashangaa vyama vingine vya upinzani hawaulizi hatma yao itakuwaje baada ya mabadiliko ya katiba, au wanasubiri mabadiliko yatiririke na bara kama maji ya mtoni, kwa kudai mbona unguja kuna mseto! Au hawataki mambo ya seikali ya mseto?

  13. Comment by kingson on April 3rd, 2008 10:24 pm

    Bwana Subby ebu tueleweshe kwa mapana tofauti kati ya suala letu la muafaka na lile la kenya, labda tutapata kuona utofauti kimantiki. Inaonekana hata Kenya nako kulikuwepo vyama vingine pia.

  14. Comment by mwana wa mkulima on April 4th, 2008 6:17 am

    NO WONDER BONGO HATUENDELEI..SASA ANGALI KWELI MTU KAMA MAKAMBA HAPO JUU ANADETERMINE HATMA YA NCHI YETU KWELI…ARE WE REAL? UNAJUA HUYO NI POWERFUL KULIKO HATA WAZIRI YEYOTE?

    AMA KWELI AFRIKA NDIVYO TULIVYO..

  15. Comment by mkwanja on April 4th, 2008 6:28 am

    THOUGHT OF THE WEEK-WAZO LA WIKI
    ‘Dont argue with a Fool, people might not notice the difference’.nyingine ni ‘Mjinga wakati wa kwenda, kurudi Mwerevu’.
    Sisi tunacho kizungumzia hapa quite frankly, ni kwamba ‘the cherished reputation of CCM here is at stake.The Credibility of the CCM Political Party as a Point of Reference in Africa has been seriously TARNISHED!
    Wao CUF they have nothing to loose in terms of Credibilty and Political Repute!Watakacho poteza tu hapa ni kulazimishwa Wasubiri.Lakini Haki ya Mtu daima haipotei bali iyacheleweshwa.CCM kama Kongwe ilipaswa kuona mbali zaidi ya ncha ya PUA yake!Kwani 2010 ni mbali?Kwanini uutumie UPUMBAVU wa watu kujineemesha?Hiyo ni dhambi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.Siyo wote wanao tambua madhara ya kushika Biblia mkono wa kushoto na Bunduki mkono wa kulia na huku unahubiri neno la Mungu!Laana haiko majumbani tu.Hata katika Uongozi wa Siasa.Angalia Vioja anavyo fanya Mugabe sasa hivi, ulivitarajia miaka kumi na tano iliyopita?Hapa tunaisikitikia zaidi CCM kuliko CUF kama ulikuwa huelewi.In this episode,by the very ‘unwise decision’ to seek pupolar mandate CCM has LOST and CUF has WON.Tunasema hivi Muafaka basi na Hakuna Kura ya Maoni.CCM na waendelee na serikali yao Visiwani.Uchaguzi Mkuu 2010 utaamua, SIYO MBALI!

  16. Comment by GEORGE on April 4th, 2008 6:55 am

    hii blog ya wahuni nini mbona hamna hata lugha inayoeleweka mnaongea bila mpangilio ni blog ya nani hiii?

  17. Comment by matty on April 4th, 2008 8:21 am

    Wewe George unasemaje???/ sasa ukimjua mwenye blog ili iweje??apange Masharti ya watu wakuingia hapa au umemaanisha nini??
    Wewe kama unaona lugha haieleweki ishia kuangalia kisha kula kona.
    Na unahitaji kuonana na wataalam wa kiswahili wakukalimanie nini kinaongelewa hapa…Mswahilina uko wapi?

  18. Comment by fukara on April 4th, 2008 2:09 pm

    NDUGU ZANGU NASIKITIKA SANA JUU YA USANII HUU UNAO ENDELEZA NA CCM.
    AWALI YA YOTE PESA ZA WALIPA KODI IMETUMIKA KULIPIA VIKAO “FEKI” AMBAVYO NI TAKRIBAN 21 KWA MUJIBU WA SEIF SHARIF’KILA CHAMA WAJUMBE 6/6 KWA MUDA WA MIEZI TAKRIBAN 14.
    YANIN I YOTE HII KAMA KWELI WALIKUWA NA NIA NJEMA WANGEPELEKA KWA WANANCHI WAAMUE WENYE WE .
    VILEVILE KAMA NIA YA CCM NI NJEMA KWANINI WALIACHA MAZUNGUMZO YAENDELLEE KWA GHARAMA ZANGU MYONGE NA BADO HUU MUAFAKA WANAULETEA USANII
    TATU KIKWETE MSANII ALIINGIZA HADI WIZARA YA MUUNGANO NAKULITIA HASARA TAIFA,JE KAMA WADANGANYIKA WA Z’BAR WATAAFIKI MSETO NI DHAHIRI KWAMBA HATA KATIBA ITABADILIKA.
    KIKWETE ANAFANYA MCHEZO NA MAISHA YA WATU TUNAJUA SOTE TUTAKUFA NA HAKI ITOLEWE LA SIVYO ATAVUNA ALICHO PANDA.
    WANASIASA MNAITAFUTIA MATATIZO YA BURE NCHI HII MMESHA HARIBU UCHUMI HELA YA TZ HAINA TENA THAMANI ,BALALI MNAMFICHA USA KWA GHARAMA ZETU.WATANZANIA NAOMBA TUAMKE
    NO CCM 2010 NA HATA IKIWEZEKANA SASA HIVI TUITISHE UCHAGUZI.
    NIMEGUNDUA UKIONA KIONGOZI ANASIFIWA SANA HADI NA MEDIA KIONGOZI HUYO NIBOMU

  19. Comment by Amina on April 5th, 2008 4:15 am

    We Gorge unasemaje?usituzingue bange unajua?umeamua kututusi ehh sisi wenyewe tunajuana wewe ni mgeni au umeamua kubadili jina kututibua hapa

  20. Comment by Jicky MM on April 5th, 2008 11:07 am

    VYAMA VYOTE VYA AINA YA KIJAMAA VINA MATATIZO YA KUTOKUWA NA MAADILI. NI CHUI NDANI YA NGOZI YA MBUZI, WANATIA KINYAA KWA KWELI KWA SABABU WOTE NI WABINAFSI NA WAPENDA UFISADI NA UONGO NA UKANDAMIZAJI. ILIKUWA HIVYO URUSI MPAKA WARUSI WALIPONG’AMUA, ILIKUWA HIVYO ROMANIA, MPAKA WANANCHI WALIPONG’AMUA, ILIKUWA HIVYO CHEKOSLOVAKIA, POLAND, N.K. BAHATI MBAYA KABISA VYAMA HIVYO HAVINA AIBU KABISA, WALA HAWAJUI HAKI, UTAWALA BORA, NA ETHICS. NDIO WANOLETA UMASKINI, MAGOMVI, NA SHIDA KATIKA BARA LA AFRIKA. JAMANI HAMUWEZI KUBADILIKA NA KUWA WATU WENYE USTAARABU? MBONA INAWEZEKANA KABISA KUWA NA SIASA ZA USTAARABU BILA UWONGO NA ULAGHAI? ANGALIA MUGABE ANAOMBA ASISHTAKIWE, KWA NINI ANAOMBA HILO WAKATI SIKU ZOTE ALIKUWA AKIIMBA KUWA YEYE NI MZALENDO WA KWELI ZIMBABWE. TUMECHOKA NA UONGO WENU CCM na serikali yenu. SISI TUNATAKA SYSTEM SAFI YA SIASA, UCHAGUZI wa kweli, NA DEMOKRASIA YA KWELI; na uongozi bora serikalini. haiwezekani kila siku na kila issue ya kuiutendaji serikalini ikawa bomu, ufisadi, na hasara kwa wananchi. Kwani ni iwe hivyo kila siku, na mpaka lini??.

  21. Comment by Mzalendo on April 5th, 2008 2:38 pm

    USHAHIDI

    Wazanzibari wagawanyika kuhusu mwafaka

    2008-04-05 09:35:31
    Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

    Maamuzi ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), yaliyotolewa Butiama hivi karibuni na kuendelea kufafanuliwa na Mwenyekiti wa chama hicho jijini Dar es Salaam, Rais Jakaya Kikwete, bado yamewagawa Wazanzibari.

    Wananchi wengi wa kawaida waliohojiwa wanasisitiza kuwa kura ya maoni juu ya serikali ya mseto italeta vurumai na kuvuruga umoja wa kitaifa huku wachache wakiona hatua hiyo ni sahihi.

    Nipashe imefanya mahojiano katika maeneo mbali mbali mjini Zanzibar na kugundua kwamba wengi hawakutazamia kama CCM ingekuja na maamuzi hayo na ufafanuzi uliotolewa na CCM bado haujawaingia sawasawa.

    Bw. Abubakar Ali, mkazi wa Amani mjini Unguja alisema suala la kura ya maoni si la msingi, na kwamba jambo la muhimu kutekelezwa ni yale yaliyofikiwa na Kamati ya Pamoja ya Muafaka kwa vile yanalenga kutetea maslahi ya taifa.

    Alisema inashangaa kuona kuwa NEC inataka wananchi waulizwe kuhusu suala hilo la mseto, wakati kuna mambo mazito ya kitaifa yalifanyika bila ya wananchi kuulizwa.

    Alitoa mfano, Rais wa awamu ya pili Zanzibar, Alhaj Aboud Jumbe aliondolewa wadhifa wake bila ya wananchi wa Zanzibar kuhojiwa katika kura ya maoni.

    Bw. Mohammed Seif, mkazi wa Kwaalamsha alisema iwapo kura ya maoni itaitishwa itaamsha na kuongeza matatizo ya kisiasa kutokana na ushindani mkali wa vyama vya CCM na CUF visiwani hapa.

    “Kuitisha kura ya maoni ni kupoteza muda kinachoonekana ni kwamba wenzetu hawapo tayari kutatua matatizo ya kisiasa yanayojitokeza Zanzibar,“ alisema Bw. Seif.

    Mwananchi huyo alisema ni jambo la kushangaza kuona NEC ya CCM inataka maoni ya wananchi kuhusu mseto wakati wadhifa wa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Muungano ulifutwa bila kukusanya maoni ya watu.

    Akizungumzia hatua hiyo, mchambuzi wa masuala ya siasa za Zanzibar Bw. Salum Said, mkaazi wa Malindi alisema tangu mapema hakuwa na imani ya kupatikana muafaka kati ya CCM na CUF kutokana na historia ya miafaka miwili iliyopita.

    Alisema tatizo linalokwamisha muafaka huo ni vyama hivyo kukumbatia siasa za historia za Afro-Shirazi na Hizbu na kuacha maslahi ya wananchi walio wengi.

    Alieleza kuwa hata kama serikali ya mseto ingefikiwa Zanzibar ingepata taabu katika utekelezaji wa majukumu yake kwa vile kuna watu wanahisi wana haki kuliko wengine.

    Kwa upande wake, Bw. Ali Suleiman mkaazi wa Tomondo alisema matokeo ya uchaguzi ya vipindi vitatu katika mfumo wa vyama vingi hapa Zanzibar ni kigezo tosha cha kujua iwapo serikali ya mseto inakuwepo au au kutokuwepo kutokana na tafauti ya kura.

    Hata hivyo, mfanyabiashara Yussuf Khamis wa soko la Samaki Darajani alisema maamuzi yaliyopitishwa na NEC yanapaswa kuungwa mkono na Wazanzibari kwa vile yanalenga kukuza demokrasia.

    “Tupo tayari kupiga kura iwe ya karafuu au nazi muhimu kuondoa shari na kupata muafaka wa maelewano,“ alisema Bw. Khamis.

    Akizungumzia hatua hiyo Bi. Shara Maulid wa Kwamtipura alisema inapopigwa kura ya aina yoyote Zanzibar, hujitokeza vurugu, hivyo kura ya maoni inayokusudiwa kupigwa ni kukaribisha vurugu nyingine na ukinzani wa kisiasa.

    Alisema hali hiyo hutokana na kampeni ziendeshwazo na vyama vya siasa, ambapo kila upande haukubali kushindwa na kuongeza kuwa hali hiyo inaweza kujitokeza katika kura ya maoni.

    Bwana Masoud Othman Said wa maskani ya CCM Wastahamilivu Darajani aliiita hatua ya NEC ya kurejesha suala hilo kwa wananchi kuwa ni uendelezaji wa demokrasia na utawala bora.
    Alisema suala hilo lilipaswa kuzingatiwa mapema katika ajenda za mazungumzo, lakini lilisahaulika kwa sababu za kibinaadamu.

    Kwa baadhi ya wanachama wa CUF Zanzibar maamuzi hayo yamepokelewa kwa kinyogo kwani walijitayarisha kusherekea serikali ya mseto kwa kununua sare na vyakula.

    Wakati huo huo Wazee wa CCM wamempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete kwa maamuzi yaliyofikiwa na NEC huko Butiama wiki iliyopita na ufafanuzi alioutoa wakati alipoongea na wananchi jijini Dar es Salaam.

    SOURCE: Nipashe

  22. Comment by Anonymous on April 5th, 2008 5:23 pm

    Nyie hamuelewi haya mambo ili wapemba waendelee kupata hadhi ya Ukimbizi lazima muafaka ukarogeke. Hivi kukiwa na muafaka kuna mtu ataclaim status ya Ukimbizi wa CUF huko Ughaibuni? Hivi sasa kuna wakimbizi wa CUF Canada, UK na kwingineko, wakati ule wa visa ilikuwa ni kuonyesha kadi yako tu, na sasa wengi wameshapata hata na uraia wa nchi walizokimbilia. Sasa haya mambo ya muafaka bomu, lazima iwe zali tena ili watu wapate kuwa wakimbizi ulaya. Huoni Maalum alivyotimkia majuu kwenda kuweka mambo sawa! Kalaghabaho nyie mnakausha makoo hapa wenzenu wanawapeleka jamaa zao nje kwa tiketi ya ukimbizi. Watu sasa hivi wanaangalia maslahi!

  23. Comment by Mzalendo on April 9th, 2008 7:05 pm

    Pamoja na kuwepo michoro au deals kwa mambo mengi ya wanasiasa lakini sisi tunaorizika kuwa waTz tunazo sababu za kimsingi kujadili masuala kama ya muungano n.k.

    Mimi naishi nje na nyumbani na nina watoto sio raia wa bongo lakini ninaona umuhimu wa kuwa na kwetu sehemu ambayo unakuwa huru kupangilia maisha yako. Ninakutana na baadhi ya jamaa “walowezi”maisha wanayoishi ni kama ng’ombe wa kufugwa yaani unaishi kwa maslahi ya tajiri wako.

    Nyumbani tunayo matatizo yetu ndio maana tunatumia fursa kama hii kujadiliana mambo muhimu yanayowezekana kutatuliwa. Sio sahihi kufikiri tuko hapa kukaragabao na kukimbia nchi yako kwenda kufanywa kuwa kama ng’ombe wa kufugwa, ndio jambo la maana kwetu kitaifa. Kama kweli watu kama Seif yuko pale kusaidia jamaa zake kupata maslahi kwa njia ya ukimbizi, hilo ni suala la mslahi ya wachache. Sioni tofauti ya kufanya hivyo na kukubali kutawaliwa yaani kuwa chini ya ukoloni. Kama ni kweli inanifanya nikubaliane na mawazo kuwa Seif alitaka visiwani wajitawale na kuwa chini ya koloni la warabu kama historia ilivyokua.

    Ni upumbavu kuikana ardhi yako kama maliasili na kukimbilia kwa matajiri kupewa uraia na kufanywa kama ng’ombe wa kufugwa. Ebu ndugu zangu tujifunze kwa yanayotokea zimbabwe kwa suala la ardhi kati ya wazawa na waamiaji. Tunachoshindwa kukiona ambacho matajiri wanakikodolea macho, ni ardhi tuliyopewa na Mungu. Hata hao mataifa makubwa matajiri walitokea huko tuliko lakini jitihada na mapinduzi ya viwanda n.k. vimewafikisha walipo leo. Sasa hivi wanajitanua kimataifa kuwa na ardhi ya kutosha kupanua wigo wa unyonyaji. Walipata upinzani kwa waona mbali kama akina nyerere, lakini hivi sasa wanapata upenyo kupitia wachache waliokubali kuishi kama ng’ombe wa kufugwa.

  24. Comment by mvuviwakale on May 13th, 2008 5:04 am

    SIO KWAMBA WANZANZIBARI WANATAMANI KILA KUKUICHA WAGOMBANE, BALI NI UFAKARA NA HALI NGUMU YA MAISHA INAYOWAKABILI KILA UCHAO, UKWELI HALI HII IMESABABISHWA NA UTAPELI NA ULAGHAI WA TANGANYIKA KUIHODHI NA KUINYONYA ZANZIBAR ISIENDELEE KIMAENDELEO, HAPA HAKUNA MUUNGANO BALI NI UBABAISHAJI, NA PICHA NJE KWA WASIOKUWA NA MACHO WALA AKILI YA KUFIKIRI. SISI KIZAZI KIPYA TUNATAKA MABADILIKO NA MASLAHI KWA WANZANZIBARI HATUTAKI PROPAGANDA ZA UAFRO-SHIRAZI NA UHIZIBU HIVYO VIENDELEE KUWA HISTORIA YA MASHULENI NA SIYO ITUMIKE KAMA FIMBO YA KUWATAWALA WALIO WENGI KWA MANUFAA YA WACHACHE.
    KIZAZI KIPYA TUNAHITAJI DIRA MPYA YA SIASA BORA NA SI BORA WANASIASA WABOVU WANAOJALI MATUMBO NA FAMILIA ZAO.
    TUNAHITAJI MUAFAKA UTAKALETA MAENDELEO KWA WANZANIBARI SIO KWA WAJANJA WA MRIMA NA WACHACHE WATAMANIFU…………………..

Leave a Reply