NIMENG’ATUKA + UZINDUZI WA ALUTA CONTINUA!

 

Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu,hatimaye wakati umewadia.Tunaongelea uzinduzi rasmi wa albamu mpya kutoka kwa mwanamuziki mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule almaarufu kama Professor Jay(pichani).Albamu hiyo inayokwenda kwa jina la Aluta Continua inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho,tarehe 4 Aprili ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee,uliopo maeneo ya Upanga jijini Dar-es-salaam.

 

Aluta Continua itabeba nyimbo 10 ambazo kwa mujibu wa Prof.mwenyewe na kwa mujibu wa single chache kutoka ndani ya albamu kama vile Hapo Vipi,Ndivyo Sivyo na hivi karibuni Nang’atuka,ni wazi kwamba Aluta Continua ni moto wa kuotea mbali.

 

Katika uzinduzi huo ambao utakuwa wa kwanza kabla hajaelekea mikoani kuzindua pia albamu hiyo kwa mashabiki wa huko,Prof.Jay anatarajiwa kusindikizwa na wasanii mbalimbali maarufu kutoka Bongo na Afrika Mashariki kama vile Jose Chameleon(Uganda),Jua Kali(Kenya),Blue 3(Uganda) ,Ambwene Yessayah ‘AY’, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’, Besta na Rehema Chalamila ‘Ray C’. Wengine ni Feruzi Mrisho ‘Ferooz’, Issa Shaaban ‘Matonya’, Lawrence Malima ‘Marlow’,Mandojo na Domo Kaya, Nakaaya,Nonini and P-Unit pamoja na wengineo wengi.

 

Baada ya hapo uzinduzi utaelekea mikoani ambapo mikoa kama vile Mbeya, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar, Tanga, Iringa, Morogoro na Mara ndio ambayo inatarajiwa kupata burudani hiyo.

 

Albamu hii ni ya kimataifa zaidi kwani imetengenezwa katika studio mbalimbali kama vile 41 Records(Dar-es-salaam),MJ Records(Dar-es-salaam), Mo Records(Mwanza) Ketebull Records(Kenya),No End Entertainment(Uganda) Contact Studio( Kigali-Rwanda) na Jam Works(South Africa).

 

Kiingilio katika uzinduzi huo wa kesho ni Tshs 7000.Wasambazaji wakuu wa albamu hiyo ni GMC Wasanii.Usikose kesho ndani ya Diamond Jubilee.

 

Wakati huo huo,Prof.Jay hivi majuzi ametoa single yake ya Nimeng’atuka ambayo pia imo ndani ya Aluta Continua.Isikilize kwa kubonyeza player hapo chini.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Page 1 of 3 | Next page