Mwanahawa Ally(pichani) ni miongoni mwa waimbaji Taarabu maarufu nchini Tanzania. Mojawapo ya nyimbo zake ambazo zinajulikana sana ni kama ule wa Viumbe Wazito Part 1 na Part 2. Unaweza kutizama video za nyimbo hizo kwa kubonyeza hapa na hapa. Je Mwanahawa anapoimba kuhusu Viumbe Wazito anamaanisha nini haswa?

Feedback / Comments

14 Responses to “MWANAHAWA ALLY NA VIUMBE WAZITO”

  1. Comment by Gervas on April 5th, 2008 11:11 am

    Sijui..Tembo? enzi nakuwa kulikuwa na ule wimbo wa taarabu unaosema,.. madereva wa mashua kwanini wakae nyumaaaa…mpaka leo sijapata jibu. Eti Matty, tusaidie jamani

  2. Comment by Bablii on April 5th, 2008 11:29 am

    Unapozungumzia modern taarab, basi nimakosa kutokumtaja mwanahawa ally! Ni muimbaji mwenye sauti tamu, anaweza kuimba aina zote za nyimbo za taarab, kuanzia za mipasho (mfano kinyago cha mpapure),za mapenzi (mfano mama shughuli) na za maadili kama hii viumbe wa zito

    Ingawa tafsiri ya wimbo ni bahari , kwa maana tafsir halisi ipo kwa mtunzi au muimbaji mwenyewe, lakini kila mtu anaweza kudadavua kwa upeo wa maarifa yake. Mimi katika wimbo huu wa viumbe wazito, naona hapa amezungumzia kwamba binaadamu hana wema, yaani hata ukitaka uwe mwema vipi kwake basi yeye ataugeuza wema huo kuwa ubaya, kwa maana yeye atakulipa maudhi badala ya shukrani!

  3. Comment by Ali on April 5th, 2008 3:27 pm

    Bi Mwanahawa bado anatamba katika music namkumbuka mama huyu wakati ule mimi ni mtoto mdogo katika miaka ya 70 -80 akiwa jirani nyumba zetu zilikuwa zinatizamana na alikuwa na watoto wawili wa kike ambao naimani sasa watakuwa wanaitwa mama na yeye anitwa bibi mbali na music huyu mama alikuwa moto mungu alimuumba mungu akuzidishie kipaji na maisha ya amani

  4. Comment by DUNDA GALDEN on April 6th, 2008 12:33 pm

    Du huyo ni mama yangu mdogo,mama mkubwa na mdogo na mama yangu mzazi ahsante sana mwana BC wa kule nyumbani Bongo Tza kwa ujumbe wako wa simu na mail mbali na hayo unapozungumza kuh modern taarabu lazima kutakuwa na jina Mwanahawa na sauti yenye kumtoa nyoka pangoni
    MUNGU AKUZIDISHIE MAISHA MAREFU YENYE FURAH NA AMAN MAMA YANGU MWANAO WA (DARWIN AUSTRALIA)
    CHAFOSA CHAI GODA

  5. Comment by matty on April 7th, 2008 3:56 am

    Heee kakayangu Gervas mimi hata siukumbuki huo wimbo maana nilikuwa mdogo sana ila nilikuwa namuona mama amevaa kagauni kafupi na skonkinko a.k.a skuna dizain hivi na nywele amezichana haflo stlye anaenda kurusha roho!
    Huyu mama nae anaimba vizuri mipasho mweee haya mama keep it up!

  6. Comment by zama on April 8th, 2008 4:11 am

    huyo mama ananikuna ile mbaya hasa hapo(sijui niwaweke funguganiii viumbe muesabike)

  7. Comment by Amina on April 8th, 2008 8:08 am

    mi nakwambia hapo..fadhila mfadhili mbuziiiiii mwanadamu ana maudhi kweli hiyo…..

  8. Comment by Daniel Ongera Omoro on June 28th, 2009 12:31 pm

    Heko mamangu mwanahawa Ally kwa hii tungo nadhifu ambayo inaangazia wenye nguvu(matajiri) vile wanavyo wadhulumu akina yahe hata ingawa wanawasaidie namna gani.

    0

  9. Comment by Daniel Ongera Omoro on June 28th, 2009 12:32 pm

    hoko

  10. Comment by Daniel Ongera Omoro on June 28th, 2009 12:32 pm

    heko

  11. Comment by PATRICK MICHAEL OGETO on July 25th, 2009 11:52 am

    wallahi nyimbo zake zanizamisha kwenye bahari ya ki utu. Ananifanya niwe mtu na wala sio kiatu.Mie tangu nianze kuzipenda taarabu, zake ndizo hubaki kama chorus moyoni mwangu. Ni kwli asemavo ‘fadhila mfadhili mbuzi mwanadamu ana maudhi’

    Lakini naomba mnisambazie historia yake na hivi mie niko bara -Nakuru Kenya na naomba nipate kumtazama live anapoimba. Wala sijali gharama na basi ukiwa radhi kunipeleka, nitakukidhi kwenye safari uwe rafiki yangu. contact me on patrickogeto@yahoo.com au newlifekenya@yahoo.com

  12. Comment by rehema kondo on May 26th, 2011 2:49 am

    yaani mimi ananiliwaza sana huyu mama,nikitoka shule kufundisha nimechoka lakini nikisikia sauti yake uchovu wote unaniisha

  13. Comment by Michael Oduor on June 15th, 2011 8:37 pm

    Mwanahawa ni msanii aliyebobea katika nyanja za mziki wa taarabu, kuanzia, classical taarab kama ” usiku wa fadhila” na mordern taarab kama “Kinyago cha mpapure”. Kwa kusema kweli mie ni nyimbo na sauti yake huyu mama ndo ilo nifanya nikawa mpenzi wa nyimbo za taarabu, yaani anapo poromosha vitu vyake huwa nabaki nime duwaa. Basi japo mie mzaliwa wa Bara Nairobi – Kenya huwa najiona nipo visiwani ninapo msikia kipenzi changu Mwanahawa. Lete raha Bi Mwana!

  14. Comment by Michael Oduor on June 15th, 2011 8:42 pm

    Mwanahawa ni msanii aliyebobea katika nyanja za mziki wa taarabu, kuanzia, classical taarab kama ” usiku wa fadhila” na mordern taarab kama “Kinyago cha mpapure”. Kwa kusema kweli mie ni nyimbo na sauti yake huyu mama ndo ilo nifanya nikawa mpenzi wa nyimbo za taarabu, yaani anapo poromosha vitu vyake huwa nabaki nime duwaa.

Leave a Reply