MEJA JENERALI ZAWADI MADAWILI

Pichani ni Meja Jenerali, Zawadi Madawili (pichani) ambaye ndio mwanamke mwenye cheo cha juu kupita wote nchini Tanzania. Takwimu ambazo bado hazina uhakika kamili zinasema kwamba Meja Jenerali Madawili inawezekana ndio pia mwanamke mwenye cheo cha juu kupita wote kusini mwa jangwa la Sahara.

Meja Jenerali Madawili alizaliwa mwaka 1953 na alijiunga na jeshi mwaka 1972.Hivi sasa ndiye mkuu wa Tawi la Mgambo jeshini.Ukitaka kujua habari kuhusu wanawake wengine duniani ambao wameandika historia kwa kuwa “wa kwanza” katika mambo mbalimbali hususani kiutendaji, bonyeza hapa.

Page 1 of 3 | Next page