MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Pichani ni Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete(kushoto) akimwapisha Waziri mpya wa Wizara ya Miundombinu,Dr. Shukuru J.Kawambwa anayechukua nafasi iliyoachwa wazi na Andrew Chenge aliyejiuzulu hivi karibuni kufuatia kashfa ambayo hivi leo inafahamika miongoni mwa wengi kama “kashfa ya vijisenti”.

Picha kwa hisani ya Mroki Mroki

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

31 Responses to “KAWAMBWA AMRITHI CHENGE”

  1. Comment by Kamanzi on May 13th, 2008 5:07 am

    Nasikia wewe ni ndugu kabisa na JK. Wanadai eti JK ni mjomba wako wa damu kabisaaa. Hivi unajisikiaje nchi yetu ikigeuzwa mali ya familia ndugu Kawambwa? Huoni hata kaaibu kidogo na kuwaachia wenye uwezo waiendeshe nchi? Ama kweli Tanzania kichwa cha mwendawazimu. Hivi lini wataruhusu dual citizenship niombe uraia na nchi nyingine yenye akili? Nimechoka na Tanzania maana haibebeki.

    Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Walaani Mafisadi

  2. Comment by Gervas on May 13th, 2008 7:44 am

    Nafikiri imefikia wakati Viongozi/mawziri wasiwe wanakaa muda mrefu ktk ofisi moja kwani inachochea ufisadi. Kuna watu eti tokea enzi za Mwinyi bado mawaziri tu mpaka leo. wasimalize miaka 6. Kusudi ziwepo na nafasi za ajira kwa wengine.

  3. Comment by iii on May 13th, 2008 7:56 am

    kawambwa na muungwana sio ndugu wa damu,ukaribu wao wote ni wenyeji wa bagamoyo,na skul mates.

  4. Comment by pound on May 13th, 2008 8:06 am

    mhhhhh haya bwana yetu macho na masikio

  5. Comment by Chala on May 13th, 2008 8:32 am

    jamani nadhani kwa upeo wangu wizara inatakiwa kuongozwa na mtu angalau awe na ka idea kidogo kuhusu wizara husika , maana tunajua uwaziri hausomewi ila pia lazima tutumie busara kumuweka mtu wizara ya kilimo mf, halafu anakuwa hata hajui zao gani linatumia mbolea gani, au wizara ya miundo mbinu hata hajui chochote anasubiria kuandikiwa na katibu report na ndio chanzo cha kupewa report ya uongo ..mf. mdogo tu mangufuli anazijua barabara za nchi hii ni balaa kwa hiyo hata ni rahisi kumanage ingawa naye amekaa sana ila anajua sana huhusu barabara ,, lakini kama jk angekuwa pia naangalia hilo ingesaidi somehow jamani…

    leo hii barabara jiji hili hazipitiki hasa mvua zikinyesha huyu jamaan leo umwambie aende barabara za kimara zile zinzogawa mitaa ni moja au mbili 2 ndio zipo kwenye hali nzuri na moja wapo ile ya diwani wa kata hiyo ambapo zipo shule zake … mbona manzese siku hizi vijinjia vya mitaa vimetengenezwa vizuri tuu…

    ushauri wangu kwa jk awe makini asimuweke mtu ambaye akiingia kwenye wizara anang’aa macho aangalie kila pahala panapohusu njia vijijini na mijini…. watendaji huko ni hopeless.

  6. Comment by sally on May 13th, 2008 8:44 am

    Mmm jamani haya tuone mambo mapya. Lakini bado tunasubiri HARI MPYA KASI MPYA NA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.

  7. Comment by Dullah on May 13th, 2008 8:52 am

    Jamaa maana ya kiapo wanaiharibu kabisa, kila waziri aliapa kutokula rushwa na kuwa mkweli kwa watanzania, wakimaanisha kinyume. We will see again who will be the next one kula kiapo. We are in the world of ilusion.

  8. Comment by Pearl on May 13th, 2008 9:11 am

    jamani wao kua ndugu si kosa cha msingi awe mchapakazi na asiyependa vijisenti. undugu unakua tabu pale ambapo tena na huyu atakua vijisenti boy.

    ndo hayo tu.

  9. Comment by hombiz on May 13th, 2008 9:57 am

    Hapa ni ufisadi tuu. Hakuna jipya! Ni ngonjela tu kila siku.

  10. Comment by Bablii on May 13th, 2008 10:29 am

    Huo ni “mvinyo mpya kwenye chupa ya zamani…”

  11. Comment by Kekue on May 13th, 2008 10:34 am

    Jk utaapisha viongozi mwaka huu mpaka basi, ndo kazi iliyopo!!! Tanzania nchi yangu nakupenda kwa moyo wote.

  12. Comment by Angeline on May 13th, 2008 11:09 am

    Hivi huyu Shukuru ni kiraka??? Tokea JK ameingia katika uongozi huyu jamaa ameshapewa uongozi wa wizara ngapi? Hivi yawezekana kweli akafanya kazi kama inavyotakiwa kwa bandika bandua hii?? Napata wasiwasi….

  13. Comment by binti-mzuri on May 13th, 2008 12:13 pm

    Mungu inbariki Tanzania, mungu mbariki Kawambwa katika kazi yake

  14. Comment by DUNDA GALDEN on May 13th, 2008 3:18 pm

    Waungwana hao hawana undugu wala nini hapo ni elimu ndio inayo mpeperusha kwa sifa yeye ni mhandisi kuna ubaya gani kuwepo Miundo mbinu?yeye hana sifa za ufisadi kama wale ndugu na jamaa zetu au kama kuna mapungufu yawe wazi tunayasome?uwezi kukosoa eti kwa vile wanatoka mji mmoja huo ni wivu tuu tena mmbaya sana na hata mmoja kati ya yenu akichaguliwa mlio baki mtasema je kweli tutafika?au kwa vile mjomba ana kashfa ya vijisent hamna budi kuongea.MUNGU IBARIKI TANZANIA MBARIKI DR KAWAMBWA
    Chafosa Darwin Australia

  15. Comment by Andrew on May 14th, 2008 2:34 am

    Kweli Kikwete mwaka huu hana kazi zaidi ya kuapisha viongozi wapya.

  16. Comment by galasa on May 14th, 2008 7:15 am

    Aiiiih jamani,na miye mwenzenu Kikwete atanikumbuka lini Uwaziri? Nina ka Diploma of Something!Rushwa kwangu mwiko.Ninaichukia sipati kusema.Kwanza niko allergic na Rushwa,kumbe je! We hujui?

  17. Comment by Dullah on May 14th, 2008 8:46 am

    Dunda huna haja ya kuandika Australia unless is your last name, ingependeza zaidi kama ungemalizia na jina la nchi yako. Take it easy!!

  18. Comment by Dinah on May 14th, 2008 11:02 am

    Wapya waapishwa na tunawekewa wazi kabisa kwenye media, vipi wale waliachia nyadhifa hizo zinazoapishwa upya wako wapi na hatua gani za nidhamu zimechukuliwa Kserikali na kiCCM?

  19. Comment by Gervas on May 14th, 2008 11:09 am

    Dullah……Dunda hajui kwamba asilimia 95 ya wachangiaji wa room hii ni wabeba mabox?

  20. Comment by Mama wa Kichagga on May 14th, 2008 12:37 pm

    Tunachohitaji WaTZ ni watu safi na hii isijalishe ni mtoto, kaka dada, binamu hata ikiwezekana mashemeji ilimradi mtu ni mtaalamu, msafi kiutendaji na mchapakazi. Vinginevyo patakuwa hapatoshi hapo baadae(baada ya uongozi kwisha).

    Enzi za kugawana madaraka kulingana na kanda/mkoa bila kujali profession eti “Kuweka Usawa (ingawa maji ya bahari yenyewe yalishindwa kuwa flat kutokana na mawimbi)” ndizo zilizotufikisha hapa tulipo. Binafsi mimi siungi mkono ugawaji wa madaraka wa namna hii.

    Kama mtu ni mtaalamu ni mtaalamu tuu. Hivi, unafikiri machifu wetu wa zamani walikuwa wajinga kuwa na “Koo za machifu”!. Hapana, walikuwa magenius sana! Uongozi sio sehemu ya kujifunzia ni sehemu ya kufanya mambo yaende sawa kwa kutumia ujuzi ulionao.

    Kawambwa, tunasubiri kuona chagizo za changamoto yake ndani ya W. ya Miundo mbinu.

  21. Comment by J Bigy on May 14th, 2008 1:42 pm

    Huyu mhishimiwa mpya ni Daktari wa falsafa ila sijui ni katika eneo lipi.Kuna mdau kasema ni katika uhandisi.Sifa hizo mbili-udaktari na uhandisi- ni za msingi mno. Kama pia ana utendaji mzuri sioni tatizo hata kama angekuwa babake ama kakaake Jakaya.Tunachohitaji si kila kabila ama kila mtu awe kiongozi.Cha msingi ni je ana vigezo?
    Utasema nini UDSM kwa hali iliyopo ambapo wahaya wengi ni viongozi na wahadhiri?Utasema ni ukabila?Ukidai hivyo nitaashangaa kwani wahaya wengi(to be honest)wamesoma na wameonesha kustahili nafasi nyingi za kazi pale chuoni.Suala sio kabila.Hili ni soko huria anayefanya vizuri na mwenye vigezo zaidi ndo anayechukuliwa.Mimi ambaye kabila langu ni mKurya siwezidai wawepo wakurya wengi uongozini eti ili kubalance makabila.Nachoangalia ni uwezo wao wa utendajaji, ‘usafi’ wao pamoja na shule. Namalizia kwa kusema kwamba sioni tatizo kama Kikwete hata akimpa Ridhwani(mwanae) uongozi kama kijana anachapa kazi, ni mwadilifu na ana shule ya kutosha(shule anayo kweli).Tatizo ni kama akimpa uongozi wakati ni kibohola,shuleless na ni mwiba vijisentiasiye na huruma na kataifa haka masikini.
    ASENTI

  22. Comment by hombiz on May 14th, 2008 6:22 pm

    kwako jbig, comment #21. Nna swali hili, hivi Kalamagi nae ni msomi?. Na je, ni mhaya ua kabila gani?

  23. Comment by galasa on May 15th, 2008 5:53 am

    ‘Iko veka pilipili gapi dani ya boga? Iko veka Karamaji iko sema yeye miji, kwisa ondoa Balaala bado iko piga kelele, sasa napumjika naweka Kawamba bado iko tikisa kichwa, sasa tajungurusa akili yangu paka lini, iko geusa mimi iko jinga siyo? Ogeja pilipili tano dani ya boga!

  24. Comment by DUNDA GALDEN on May 15th, 2008 6:05 am

    Dullah No 17 poa hamna noma.naandika toka Australia ndiko makazi siko nyumbani Tza lakin kuna ubaya gani?nimezaliwa Tza inshallah nitazikwa Tza Allah akipenda sijui unatatizo gani pindi wasomaji wa BC wanapoandika sehem walipo
    PEACE CHAFOSA.AUSTRALIA DARWIN

  25. Comment by NDLOVU on May 15th, 2008 6:20 am

    WEW GELVAS NAE UNAMUUNGA MKONO DULLAH KWANI SI VIZUR MTU KUANDIKA SEHEM ALIPO?AU MNAOGOPA KWA VILE MAMBO YA KUJILIPUA NA KAMA KUBEBA MABOKS HAYO MAISHA HAINA NOMA AU PONT ZA UFISADI ZIMEWAGUSA WAJAMAN WEW ANDIKA PONT ZAKO BILA MATUSI AU KEBEH
    KILA LA KHER WATANZANIA TAFUTEN MAISHA ILA MSISAHAU KUKUMBUKA NYUMBAN
    AHSANT

  26. Comment by binti-mzuri on May 16th, 2008 8:15 am

    jbigy umeongea point!!

  27. Comment by mkereketwa on May 19th, 2008 10:17 pm

    I’m sure wachangiaji waliowakalia wabeba mabox kama wanavyowaita hata namanga hawajawahi kufika. Badala ya kuchangia mada inayozungumziwa mmeng’ang’ania kuita watu mabeba mabox. Aliyewaambia kuwa kila mtanzania anayeishi nje ni mbeba box nani? Nipo USA for 10 years na sijawahi gusa box! Ndiyo maana bado mko bongo kazi ni kukosoa maisha ya watu. Nani ni bora? si angalau wanaweza hata kuafford kuwa na computers na internet nyumbani na ndiyo maana ni wachangiaji wakubwa wewe mpaka usubiri umeme urudi upande basi kwenda cafe ndiyo maana mkiingia mtandanoni mnatoa hasira zenu badala ya kuchangia mambo ya maana. Hembu watanzania tuwe na respect on each other, iwe mpaa samaki, mbeba box, professor hayakuhusu. Toa hoja zako na urudi nyumbani ukalale. My dear Tanzanians mlioko nje endeleeni kusukuma gurudumu la kujikwamua na hali duni ya maisha hawa waoshavinywa wanatoa frustration zao hapa huwezi jua pengine mtu kanyimwa hata visa ya kuja kutembea sasa anabaki kuita watu wabeba mabox, SO WHAT! KABEBE LAKO BONGO HALAFU UNIAMBIE UMELIPWA KIASI GANI. BEBA BOX WA MAJUU ANAWEZA KUINGIZA MILIONI MOJA YA KITANZANIA KWA WIKI MOJA NA NUSU KAMA AKITAKA, UPO HAPO???????

  28. Comment by binti-mzuri on May 20th, 2008 12:51 pm

    halooo halooo mkereketwaaaa … makofi tafadhaliiiii,nimewaona long tiimee nikamezeaaa tu…dukuduku sasa limenitoka!

  29. Comment by DUNDA GALDEN on May 20th, 2008 3:56 pm

    NDIO MAAANA YA JINA LAKO MKERKETWA,UMELONGA UKWELI MTUPU KAMA BOX SI KAZI MBONA TUNAMBIWA MLIO NJE MCHANGIE NCHI YENU (TZA)UKITUMA SENT KADHAA SI HIYO HIYO INAYOSAIDIA SI YA KIFISADI,27 HAO WAMEZALIWA KUONGEA VINAWAWASHA HATA UKINDIKA MJI ULIPO. MLIO NJE NA BONGO PIGA KAZI.MIM NTAZID KUIPEPELUSHA BC KWA KILA MBONGO WA UGHAIBUN ASIE HIFAM BC
    CHAFOSA CHAI GODA

  30. Comment by Dullah on May 21st, 2008 5:23 am

    Jk tasks
    1. kuunda baraza la mawaziri
    2. kukubali maombi ya kujiuzulu toka kwa mawaziri.
    3. Kuchugua mawaziri wapya
    5. Ziaraaaaaaaaaaaa!

  31. Comment by binti-mzuri on May 26th, 2008 5:27 am

    true that dullah .. JK nae hajafanya lolote la maana, he is the most hopeless president in history!

Leave a Reply