Kwa wengi siku hizi anajulikana kama Binamu.Lakini alipoingia rasmi kwenye ulimwengu wa muziki aliitwa MwanaFalsafa.Jina lake kamili ni Hamisi Mwinjuma(pichani).Ni mshindi wa tuzo maarufu za Kili.
Tangu aingie kwenye fani ya muziki,sifa moja ambayo amekuwa nayo ni kuwa na mashairi au lyrics kali. Ilikuwa ni lazima uwe na uelewa mzuri wa lugha ya Kiswahili ili upate maana halisi ya nyimbo zake.Uwezo wake wa kwenda sambamba na mapigo (beats) za kimuziki huku akighani ipasavyo mashairi yake ni jambo linguine lililomfanya awe mmoja miongoni mwa wanamuziki wa B Flava wenye mashabiki lukuki..
Hivi karibuni MwanaFA amezindua tovuti yake rasmi.BC tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na ujio wa tovuti hiyo,muziki wake,mipango yake ya baadaye na mengineyo mengi.Kwanini ameiita tovuti yake binamu13.com? Ana mipango gani katika miaka mitano ijayo? Anasemaje kuhusu ujio wa mwanamuziki 50 Cent nchini Tanzania hivi karibuni?Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
BC: Kwanza hongera sana kwa kuzindua tovuti yako rasmi hivi karibuni. Pia pongezi nyingi kwa mafanikio ambayo umeyapata tangu uanze kazi za muziki.Mambo yanakwendaje?
MwanaFA:Thanx a lot cuz…Mungu anasaidia sana juhudi zangu zinatoa mwanga wa mafanikio!Nazingatia sana nguvu zake kwenye kila ninachofanya.Najua kila kitu kilishapangwa naye hata kabla sijazaliwa na ninachofanya ni kufumbua mafumbo aliyoniwekea kupata niliyopangiwa kuyapata humu kunako dunia yake.
Mambo kama kawa ndugu yangu…
Labda kabla hatujaenda mbele sana naomba nimpe pongezi na shukrani zangu za dhati my boy Ahmed Babajide kwa kuweza kufanikisha kuwepo kwa tovuti hii.Mungu ataifanya kazi yako yenye thamani siku za karibuni Ahmed.Thanx a lot.
BC: Jambo la kwanza ambalo tumeliona pindi tulipopata habari kuhusu ujio wa tovuti yako rasmi ni kwamba tovuti yako umeiita binamu13.com.Wengi tunafahamu kuhusu jina Binamu lakini hatujui kuhusu namba 13.Unaweza kutuambia namba 13 inamaanisha nini?
MwanaFA: 13 is my birthdate..March 13th!I am a Pieces,like Osama,MethodMan and many others…hahahaha..and I’ve been using the name binamu 13 sehemu kadhaa kwa muda sasa!sikiliza tena intro ya ‘hawajui’ utanifahamu…
BC: Mara nyingi mtu anapoamua kuanzisha tovuti yake anakuwa na malengo fulani maalumu.Kwa msanii kama wewe lengo mojawapo la wazi ni kutumia tovuti yako kujitangaza na kuwasiliana kirahisi na mashabiki wako wenye uwezo wa kutembelea mtandao.Mbali na lengo kama hilo,unategemea kupata nini zaidi kutokana na kuwa na tovuti yako mwenyewe/rasmi?
MwanaFA: Sababu za wazi kabisa baada ya hizo ulizoziorodhesha awali ni kujaribu kuitumia kutafuta njia za kufanya biashara ipanuke.Kwa ulimwengu tulionao watu wengi zaidi wanaweza kukufikia kupitia mitandao kuliko sehemu nyingi nyingine,hasa walio mbali sana na Africa nilipo.Nikijaribu kuwa realistic,hakuna namna msanii wa uzito wangu ataeleweka bila ya kuwa na tovuti.Muda wa mimi kuwa na tovuti yangu rasmi ulishafika.
BC: Kwa kiasi kikubwa tovuti yako imeandikwa katika lugha ya kiingereza kitu ambacho kwa kiasi fulani kinamnyima mshabiki wako asiyefahamu kiingereza nafasi ya kuitembelea na kuifurahia kama sio kusoma yaliyomo.Unaweza kutuambia kidogo kwanini sehemu kubwa umeiweka katika kiingereza?
MwanaFA: Aaamh…kama nilivyosema katika swali lililopita,nalazimika kuwa karibu wa wapenzi wa kazi zangu,HASA WALIO MBALI NA NILIPO.Wengi wanaofahamu Kiswahili tu na sio kiingereza kilichotumika sana kwenye tovuti yangu wapo nilipo…Africa,na hasa Tanzania ambako wana namna nyingine lukuki za kupata habari za maendeleo ya kazi yangu kirahisi.Simaanishi hawatakuwa na nafasi ya kujua kupitia tovuti,no..kadri tunavyoendelea tutakuwa tukijaribu kumfanya kila mmoja ajisikie nyumbani kuipitia…kila mmoja ni binamu yangu!

Binamu a.k.a MwanaFA akiwapa ladha murua mashabiki wake,mashabiki wa muziki wa kizazi kipya hivi karibuni.
BC: Mashairi au lyrics za nyimbo zako, matumizi ya lugha ya Kiswahili ni mambo ambayo yanavutia sana wapenzi wa muziki kiasi kwamba wengine wamewahi kutania kwamba huenda kila unapokwenda huwa huiachi nyuma kamusi ya Kiswahili.Kuna ukweli wowote katika hilo? Je unadhani lugha ya Kiswahili ina nafasi gani kimataifa kupitia muziki?
MwanaFA: Hahahahahaa…sina hata kamusi yenyewe mpwa!Nalichukulia hilo kama compliment anyway!..ukijaribu kuangalia kazi zangu za karibuni nimejaribu sana kurahisisha Kiswahili ninachokitumia ili kuondoa matatizo ya watu kutafuta kamusi ili waelewe nimesema nini…muziki tunaofanya yafaa uwe wa kumpumzisha mtu na sio kumuongezea mzigo wa mawazo..najua unanielewa kama uliwahi kuwa Africa.
Nafasi ya lugha ya Kiswahili sio kubwa kwenye muziki wa kimataifa kwa kweli.Lakini muziki pia unaweza kutumika kukitangaza Kiswahili chenyewe kama utafanywa katika viwango vya kimataifa.Bado tunajaribu kuutoa huu muziki na Kiswahili kwa wakati mmoja.Hakuna namna tutashindana na kina Jay Z kufanya muziki mzuri kwa lugha yao.,so we better stick to ours!

MwanaFA(kulia) akiwa na mshirika wako wa karibu,nyota mwingine wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesaya au AY.Kwa pamoja hivi karibuni walitoka na kitu,Habari Ndiyo Hiyo.
BC: Tanzania hivi karibuni imekuwa ikipata bahati ya kutembelewa na wanamuziki mashuhuri kutoka nje na hususani Marekani. Hivi karibuni mwanamuziki 50 Cent na kundi lake la G-Unit walikuwepo nchini Tanzania na wewe ulikuwa mmojawapo miongoni mwa wahudhuriaji.Unadhani ziara kama zile zinawasaidia ninyi wanamuziki wa kizazi kipya kwa namna yoyote ile?Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuna mambo yoyote ya msingi ambayo mnajifunza kutoka kwao?
Page 1 of 4 | Next page