Kwa wale ambao mnaishi ughaibuni au mamtoni kama ambavyo wengine hupenda kupaita,mtakuwa mnatambua kwamba msimu wa majira ya joto(summer) huwa unaambatana na maonyesho mbalimbali ya sanaa,tamaduni nk. Huu ndio huwa wakati mzuri kwa wasanii mbalimbali wa muziki,sanaa za maonyesho nk kutoka sehemu nyingi duniani zikiwemo pia nchi zetu za Kiafrika hupata fursa ya kutembelea nchi mbalimbali ili kuonyesha vipaji vyao.

Miongoni mwa wasanii hao kutoka Tanzania kwa mwaka huu ni Ras Jhikoman(pichani) ambaye kunako tarehe 25 mwezi huu,anatarajiwa kupanda jukwaani huko jijini Helsinki nchini Finland katika tamasha maarufu la sanaa na maonyesho lijulikanalo kama World Village Festival kama inavyoonekana katika tangazo hilo hapo chini.Kila la kheri Jhikoman.Wakilisha.Eti ni kweli kwamba tunaweza kusema Jhikoman ni mfano wa nabii asiyekubalika nyumbani lakini wageni wanamheshimu na kumkubali?Kwa mliopo Helsinki,kazi kwenu.

Shukrani Ras Makunja kwa taarifa hii.Picha ya juu na Bob Sankofa.

Feedback / Comments

9 Responses to “JHIKOMAN NDANI YA WORLD VILLAGE FESTIVAL”

  1. Comment by Edwin Ndaki on May 15th, 2008 5:34 am

    Nilibahatika kuhudhuria moja ya “show” aliyofanya majira ya kiangazi mwaka jana Finland.Hakika Jhikoman anakubalika sana ughaibuni.

    Kazi zake ni nzuri.Mwaka jana aliacha gumzo Finland na kibao kinaitwa kuagana.

    Ni mtunzi,muimbaji na mcharaza gitaa mzuri.

    Kila jema na mafanikio Jhikoman.Naamini siku moja mambo yatakuwa kwenye mstari.

    Tutafika tu

  2. Comment by DUNDA GALDEN on May 15th, 2008 5:51 am

    Safi Jhiko na wengineo.nakumbuka wakati tuko Chuo Bagamoyo huyo jamaa ana kipaji kinoma cha music
    nana nyimbo zenye ujumbe makinif unaokwenda na wakati
    mlio Finland dont try miss that Fest Jhiko ni msanii mzuri
    Mwambie hawaimbie bint ali hicho kibao kikali sana
    VIVA
    CHAFOSA CHAI GODA,DARWIN AUSTRALIA

  3. Comment by binti-mzuri on May 15th, 2008 6:38 am

    mbona simfahamu!

  4. Comment by binti-mzuri on May 15th, 2008 8:08 am

    dunda man, we know you are in australia!

  5. Comment by Amina on May 15th, 2008 9:24 am

    mi namsikia tu ila sijui nyimbo zake zinawekwaga stesheni gani?unajua huku bongo radio wanaweka bongo flava

  6. Comment by baker on May 15th, 2008 10:49 am

    Ebwana kaka nakukubali sana long time! mistari yako si ya kubahatisha, iko level za nyuki sema tu kwa apa kwetu sapoti ndogo ya kuwatoa wasanii kama nyinyi, poa sana kaka kawape good time, Helsink najua one day utalia kivulini kaka.
    Peace and love

  7. Comment by DUNDA GALDEN on May 15th, 2008 2:11 pm

    Sawa bint Mzuri nakuahidi sito andika nilipo
    PEACE

  8. Comment by Amina on May 16th, 2008 2:42 am

    hehehe binti mzuri umenichekesha mimi simo

  9. Comment by kaboka on May 16th, 2008 2:35 pm

    Nimeona tangazo gazeti la leo la Metro,safi sana njoo uwakilishe.Nilimwona Jhikoman mwaka jana hapa Finland,katika mji wa Lahti.

Leave a Reply