Ni Ijumaa Tena.Wakati mwingine wa kupata burudani tayari kwa kuukabili mchana wa siku,jioni au usiku. Si unajua tena mambo ya Ijumaa? Kila mtu yuko “bize”.Ni mwendo wa ujumbe kwenye simu za viganjani(au wewe unaziita za mkononi?).Simu za mezani ofisini na majumbani nazo zinakuwa bize pia.Ukipiga ile ya ofisini usishangae sana ukisikia katibu muhtasi akikujibu bila yale mashamshamu ya kawaida.Ni Ijumaa mchana na anasubiri kwa hamu “kutoka”.Ili mradi tu kila mtu yupo bize kwa namna moja au nyingine. Na ukiwa mwenzangu na mie,ukata umetanda,basi unajidai kuwa na miadi muhimu nyumbani.Unaaga wenzako na kukimbilia nyumbani upesi.Ukifika nyumbani,unajidai uko tena “bize” na mambo ya ofisini.Maisha yanakwenda.Hapo ndio unagundua kwamba kumbe hapa duniani kuna watu wanaishi huku wengine wakiwepo tu.
Kwa upande wa burudani leo tunahama kidogo.Tunaenda kwa jirani zetu Kenya.Pale tunawakuta Gabriel Omollo na mwenzake Omondi Jassor.Wimbo unaitwa Lunch Time.Huu ni mojawapo wa zile nyimbo ambazo hata zipigwe vipi au mara ngapi,bado ukiusikia utakuamsha kama sio kukumbusha jambo,sehemu au mahali fulani.Radio moja maarufu sana jijini Dar ilikuwa inapenda kuupiga kila siku mara majira yanayoitwa mchana au wakati wa lunch(Lunch Time) ukifika.Mimi nikisikia wimbo huu nasikia njaa lakini wakati huo huo napata cha kufanya(kuzuga na window shopping).Pata burudani.Ijumaa Njema.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Page 1 of 3 | Next page