
Kwa wapenzi wa filamu za Bongo ni jambo la faraja kuona kwamba hatimaye,kwa mara ya kwanza,mwaka huu kutatolewa Tuzo kwa sekta hiyo ambayo inazidi kukua siku baada ya siku.Tuzo hizo zimeitwa Tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania au Tanzania Vinara Film Awards.
Kama ambavyo mmekuwa mkifuatilia kupitia vyombo mbalimbali vya habari,kampuni ya One Game Promotions ndio waandaaji wakuu wa Tuzo hizi.Baada ya mchakato mzima wa kuwasaka vinara hao wa filamu,majina rasmi ya walioingia hatua ya mwisho ya kuwania tuzo hizo yametangazwa.Here are the nominees;
TUZO ZA VINARA WA FILAMU TANZANIA (TANZANIA FILM VINARA AWARDS) 2007 – 2008
Muigizaji Chipukizi wa Kike (Up coming actress)
Irene James – Miss Bongo II
Irene Uwoya – Diversion Of Love
Fatuma Makame – Karibu Paradiso
Jennifer Mwaipaja – Silent Killer
Grace Michael – Malipo ya Usaliti
Muigizaji Mwandamizi wa Kike (Best Actress in a Supporting Role)
Irene Uwoya – Diversion Of Love
Mama Frank – Yolanda
Irene James – Miss Bongo II
Susan Lewis – Behind the Scene
Tecla Mjata – Macho Mekundu
Muigizaji Bora wa Kike (Best Actress)
Lucy Komba – Diversion Of Love
Grace Michael – Malipo ya Usaliti
Halima Yahya – The Stranger
Elizabeth Chijumba – Copy
Riyama Ally – Fungu la Kukosa
Muongozaji Bora wa Filamu (Best Film Director)
Gervas Kasiga – Fake Pastors
Jimmy Mponda – Misukosuko II
Kulwa Kikumba – Macho Mekundu
Haji Adam – The Stranger
Halfan Ahmed – Copy
Mtunza Sauti Bora (Best Soundman of The Year)
Adam Wazir – Fungu la Kukosa
Cleophance Ng’atingwa – Kolelo
David Sagala – Copy
Camillius Kanuli – Fake Pastors
Swalehe Juma – Fungu la Kukosa
Mpiga picha Bora wa Filamu ( Best Cameraperson of The Year)
Mbalikwe Kasekwa – Misukosuko II
Sylon Malalo – Kolelo
Rashid Mrutu – Copy
Nicholaus Mtengwa – Kilio moyoni
Sylon Malalo – Simu ya Kifo
Adui Bora wa Filamu (Best Film Villain)
Mohamed Aziz – The Body Guard
Irene Uwoya – Diversion Of Love
Sebastian Mwanangulo – Misukosuko II
Ahmed Ulotu – Silent Killer
Elizabeth Chijumba – Copy
Mhariri Bora wa Filamu (Best Film Editor)
Moses Mwanyilu – Misukosuko II
John Kalage – Miss Bongo I
Rashid Mrutu – Copy
Hassan Mbangwe – Malipo ya Usaliti
Sylon Malalo – Kolelo
Mwandishi Bora wa Filamu (Best Script Writer)
Seleman Mkangara – Malipo ya Usaliti
Hammie Rajab – Kolelo
Kulwa Kikumba – Diversion Of Love
Lucy Komba – Utata
Elizabeth Chijumba – Copy
Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kiume (Best Actor in a Supporting Role)
Aliko Tshmwala – Segito
Single Mtambalike – The Stranger
Adam Kuambiana – Fake Pastors
Halfan Ahmed – Copy
Emmanuel Muyamba – Fake Pastors
Muigizaji Chipukizi Bora wa Kiume (Best New And Upcoming Actor)
Emmanuel Muyamba – Fake Pastors
Laurent Anthony – Karibu Paradiso
Hassan Nguleni – Body Guard
Yussuf Mlela – Diversion Of Love
Uswege – Malipo ya Usaliti
Muigizaji Bora wa Kiume (Best Actor)
Single Mtambalike – Agano la Urithi
Nurdin Mohamed – Utata
Jacob Steven – Copy
Haji Adam – Miss Bongo
Yussuf Mlela – Diversion Of Love
Mapambo na Maleba Bora (Best Costume And Makeup of The Year)
Misukosuko II
Macho Mekundu
Kolelo
Utata
Copy
Mtunzi Bora wa Filamu (Best Creater of The Year)
Lucy Komba – Utata
Nicholaus Mtitu – Diversion Of Love
Single Mtambalike – The Stranger
Halfan Ahmed – Copy
Hammie Rajab – Kolelo
Filamu Bora ya Mwaka (Best Movie of The Year)
Behind the Scene
The Stranger
Diversion Of Love
Macho Mekundu
Misukosuko II
Simu ya Kifo
Copy
My Sister
Silent Killer
Miss Bongo I
Agano la Urithi
Malipo ya Usaliti
Utata
Kilio Moyoni (Crying Silently)
Fake Pastors.
Ungependa kuona nani anashinda?BC inawatakia kila la kheri all the nominees.
Feedback / Comments
19 Responses to “AND THE NOMINEES ARE…”
Leave a Reply


sending...
Mhmh hii kali mbona waigizaji tunaowajua sisi, kama kna kanumba na kin aRay hawamo.. mhmh sijui kazi kwelikweli.. na hii award ni za movies zote zilizotoka ama ni za wmaka jana?
Jamani wana kama nitakuwa nimekoea naomba mnirekebishe.
Hilo jina la “Tanzania Film Vinara awards” mie naona kama haileti maana “in a professional level” kwanini wamechanganya kiswahili na kingereza/english?? kwanini wasinge andika ktk “lugha” moja kiswahili au kingereza?
but nikitu kizuri kwa Tz!
Mbona akina Kanumba hawamo, au ndo mmeshaanza mambo yenu ya huko Bongo mpaka uhonge mambo ya kujuana, vinara juu juu zaidi wabongo bwana.
no comments for sure.
jamani hii inakuwaje tena? kuna watu kibao mmewaacha, Ray Kanumba, Mzee kipara na wengine kisha kuna filamu ya shumileta ni nzuri sana mbona haimo? au lazima kitu kiwe kimetoka mwaka huu sielewi kdg jamani!! uigizaji wa hiyo filamu ni mzuri mno.mmh haya….
mi simjui mtu hata mmoja hapo
Duh ebwana wee kweli bongo wameamka sasa! lakini mbona apo kuna kama kuchemsha kidogo? Kiswahili + kingereza???????
kazi ipoooo bongo.
Jamani, mbona majina makubwa kama Kanumba hawaonekani hau ndio stahili za kibongo za kuhongana? Na yule kaka Mtanzania wa Holy-Wood Jonie Mashaka, mbona hayumo? alafu hizi awards zina maana gani kwa sabubu hawa wote ni waganga njaa hapa mjini
Binafsi nina hakika kabisa kuwa One Game wameanza gwaride kwa mguu usio sahihi, labda pengine walikurupuka bila kufanya utafiti wa kina katika tuzo kongwe zitolewazo kwa wenzi wetu waliotangulia katika tasnia hii, kwa sababu wamelipuka tu na kutangaza tuzo bila ya kuweka bayana vigezo vitakavyotumika ima kumfanya muigizaji kuwa mshindi au filamu kuwa na kiwango stahiki; jambo ambalo litachochea ubora wa kazi zetu, kwani kila mmtayarishaji atakuwa akijitahidi kufikia vigezo ili ushindani uwe katikati ya viwango vya ubora. Nimesema wameanza sivyo kwa kuwa kuna kila dalili ya upendeleo na rushwa ya waziwazi katika mchakato mzima mpaka sasa kuna baadhi ya watu wanayo majina ya filamu itakayoshinda na mwigizaji bora wa kike wa kiume n.k. Kwa ujumla lilikuwa ni wazo zuri sana, lakini “hata mawazo mazuri yakifikiwa kwa sababu za kipuuzi huwa ni mawazo ya kipuuzi pia.” Tuombe Mungu wawe na nia njema ili baadae wajirekebishe!
mimi naona kwakuweka majina mapya ni poa sana,sio kila siku hao hao kina kanumba kwani hakuna wengine wanaofanya vitu vizuri mtawafanya wajione kuwa wao tu ndio wanajua pia sifa ziki zidi zitawaharibu watajiona wamemaliza
jamani jamani,tukubari tukatae unapozungumzia filamu za kibongo tanzania na africa mashariki huwezi kuacha kutaja majina haya kanumba,ray,johari na monalisa,vijana hawa ndio wameleta mapinduzi ya film bongo baada ya tasnia hiyo kufa miaka ya nyuma wao wameamsha mpaka sasa,hata sisi wa huku ughaibuni tunawajua wao,hasa kanumba mchango wake unaonekana wazi toka alivyoanza kuigiza na wanaijeria mpaka sinema zako twaziona through dstv,sasa hao waandaaji na majaji wana macho kweli??kueno wa kweli watendeeni haki wasanii wanaostahili nasi kupeana tu,mfano asilimia 60 ya majina yote hapo juu hatuwajui…think…vigezo gani mmetumia?
mi aisha naona rushwa tu hapa au chuki binafsi
kweli hii ni movies star search, hizo ni tuzo za ma-underground pamoja na story butu, poleni Watanzania kwa kurubuniwa na watu wanaotaka umaarufu
aliyetangulia katangulia, kulikoni kushika njia ili hali huna macho ya kuona wakati watu wengine wakiona movements zako? hizo tuzo zina walakini nadhani hata ninyi waandaaji mmeshaanza kuona aibu, coz hao nominees na movies zao ni kama gunia chakavu na pumba za mpunga, siku hizi watu hawaishi kwa kudanganywa kiasi hicho, ninyi ni wasanii wachanga katika industry ya Tz ila mwataka umaarufu ila njia mlioitumia ni ya aibu, hakika mnajimaliza, nendeni mkaziangalie hizo movies upya ndipo mtakapojua kuwa mmechemsha, hata kuna movie moja nilipoiangalia hata nilicheka sana eti mwanamke anamtambulisha rafiki ya kuwa HUYU NI UBAVU WANGU…tangu lini mwanaume akawa ubavu wa mwanamke? but ndo hivyo tena mmeshaliletea aibu Taifa
Inashangaza kuona macho ya majaji ni tofauti na ya waliowengi.Sisemi kwamba mliowateua hawafai ila najiuliza hivi uzoefu hauna nafasi katika masuala ya filamu?Iweje kwa mfano waigizaji kama akina Kanumba,Johari au Ray wote kwa pamoja wasiwemo katika orodha yenu?Ni vigezo gani mlivyotumia kuwapata hao mliowachagua?Ikiwa sisi tunaonunua kazi zao tunazikubali inakuwaje nyie mwone sio nzuri,Je, hata mchango wao kwenye fani hii hauonekani?Ni vema kama mngetuambia kuwa lengo lenu ni kuwa’promot’ ma’underground’ tungewaelewa na tungewasifu vilevile.
HIYO NI TANZANIA RUSHWA AWARD,,NYAMAYAO MBONA HAYUMO,MAMA ABDUL PIA
TANZANIA BWANA
Namjua hapo huyo dada mahiri wa fungu la kukusa, Jacob Steven, hao wengine labla mpaka kidole
tunamtafuta david sagala