Mrembo Amanda Sululu(pichani) jana aliibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Universe Tanzania 2008. Shindano hilo lilifanyikia jana usiku katika ukumbi wa Hoteli ya Movenpick jijini Dar-es-salaam.Kwa maana hiyo Amanda ndiye anarithi taji kutoka kwa Flaviana Matata mrembo ambaye mwaka jana alifanikiwa kuiletea sifa Tanzania baada ya kufanikiwa kuwemo katika tano bora ya mashindano hayo katika ngazi ya dunia yaliyofanyikia nchini Mexico.

Tatu bora-Katikati ni Amanda Sululu,kushoto ni Jamila Nyanga(mshindi wa pili) na kulia ni Eva Babuely(mshindi wa tatu)

Mashindano ya Miss Universe mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tarehe 14 Julai katika ukumbi uitwao Crown Convention Center(Diamond Bay Resort) mjini Nha Trang nchini Vietnam.Zaidi ya washiriki 80 kutoka nchi mbalimbali wanatarajiwa kushiriki.

BC inampa hongera Amanda na kumtakia kila la kheri mbele ya safari.

Feedback / Comments

20 Responses to “MISS UNIVERSE TZ 2008 NI AMANDA”

  1. Comment by DUNDA GALDEN on May 30th, 2008 11:07 am

    Mabint wa kibongo.hawana mchezo wana ng“ara kama wataliano wenye asili ya kimakonde na kizaramo.si rahisi kubainisha sina budi tuseme mashallah,
    chafosa

  2. Comment by DUNDA GALDEN on May 30th, 2008 11:29 am

    BC VIPI LEO WIKI ENDA?

    HAMNA HOME SICK

    MSIALIBU MAMBO TUNATAKA MUSIC AU MAMBO

    YA NET BINT MITAMBO KIDOGO IMELETA SIVYO NDIVYO
    chafosa

  3. Comment by kekue on May 30th, 2008 11:40 am

    Hongera dada, hivi c alikuwa ktka kambi ya mamiss ya kina Richa au nimemfananisha? Hivi umiss una umri wa mwisho mtu kushiriki au hata kama una miaka kama yangu unaweza shiriki??

    Tanzania ni nchi yangu naipenda sana.

  4. Comment by michelle on May 31st, 2008 2:54 am

    Mbona miguu imepauka sana? mamodo wa bongo oyeeeeeeeeeeee.

  5. Comment by trii on May 31st, 2008 4:34 am

    jamilla kajitahidi hakutaka tamaa baada ya kushindwa kwenye kisura.good keep it up,one day u will win.

  6. Comment by matty on May 31st, 2008 5:31 am

    Hongera dada kwa ushindi ..unaonekana unaconfidence plzzzzzzzzzzzusituangushe kule Vietnam…kila la heri!
    Kekuu umenivunja Mbavu umri wako ni upi???au kama wangu?maana mimi najua mwisho ni miaka 24, zaidi ya hapo hiyo sio miss labda ni fashion show nyingine.

  7. Comment by Jennas on May 31st, 2008 6:16 am

    Kekue umiss hauna umri maalum mana hao mamiss wengi wao unakuta ameshasoma na kumaliza vidato vyote na kazi anafanya na wengine wanawatoto wao nyumbani,akiona mwili umekaa kushiriki anaenda kushiriki na kusema anamiaka 18,19,20,21 wachache sana unamsikia nina 22 hapo ujue ni miaka 50 na nusu.
    Samahanini lakini mamiss wenzangu mwenyewe umri miaka 40 ila stejini nasema miaka 11 na nusu olaaaaaaa.

  8. Comment by Amina on May 31st, 2008 7:17 am

    dunda anasumbua bc muwekee basi hiyo nyimbo anaitaka jamani

  9. Comment by kekue on May 31st, 2008 10:42 am

    Matty nishavuka 24 rafiki huko hakunifai tena, Jenas ni kweli kuna warembo wanadanganya umri wao ili mradi umbo linaruhusu, tehe tehe kaaazi kweli kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! hapo utasikia wana miaka 18 kila mmoja mimi sitashangaa kbs.

  10. Comment by kimamy on May 31st, 2008 4:20 pm

    kekue kwani una umri gani? maana hujataja umri wako.lakini jaribu usikate tamaa.

  11. Comment by SANIA on June 2nd, 2008 2:11 am

    Jamila hongera sana umejitahidi mwana wane.

  12. Comment by Pearl on June 2nd, 2008 3:27 am

    hongera amanda,mie nakuombea Mungu ufanye vizuri huko uendako.Haya Jamila vipi tena mamaa,mambo yameshindikana tena na huko!!!!???? usife moyo kuna miss tourism inakuja tena jaribu bahati,halafu kuna miss tz,miss malaika zote jaribu tu.

  13. Comment by polisi on June 2nd, 2008 3:57 am

    Mtoto umependeza sana.wanaohiji miaka yako ni wajinga tu kwani ungekuwa umezidi umri kamati ya shughuli hizo isingekuacha ushiriki.just dont let us down in Vietnam,na uchunge risasi huko kwani kwao ni vita milele.All the best.

  14. Comment by binti-mzuri on June 2nd, 2008 9:18 am

    mwisho wa umiss miaka 24,usiwe na mtoto,hujaolewa wala hujatoa mimba ;) haha..but ni wangapi,wanasema ukweli,that i dont know

  15. Comment by matty on June 3rd, 2008 8:50 am

    hahahahahah binti mzuri you made my day …utamtambuaje ambaye hajatoa mimba?

  16. Comment by maryciana on June 3rd, 2008 11:53 am

    binti-mzuri hiyo ya mimba umeiongezea au?lol

  17. Comment by Jbigy on June 3rd, 2008 8:47 pm

    afazali zis taim ameshinda ‘mzawa’.siku hizi wanashinda wahindi tunasema ni watanzania. wakati mwingine tunaangalia ‘weupe’ na pua za kihindi! Hivi hao ndo wananchi? Miss wa mwaka jana kuiwakilisha TZ sikuona kama ni vema.
    Anyway ni mawazo yangu tu jamani si ‘ubaguzi’.
    Ila kuna siku raisi wa Tanzania atakuwa mhindi kama miss na mbunge wanawezakuwa wahindi!
    DU!

  18. Comment by flora mbuya on June 6th, 2008 2:05 am

    mamiss wengi sio wa kweli kwani wengi ninaowajua wana umri mkubwa lakini akiwa stejini utasikia miaka 18 19 20 wajaribu kuwa wa kweli pia mngekuwa mnaagalia vyeti vya kuzaliwa

  19. Comment by JMbigy on June 6th, 2008 3:19 pm

    Vyeti vya kuzaliwa wanatengenezewa kwa shilingi elfu 20. Hata wewe ukihitaji kinachoonesha una miaka 8 utakipata kaka. Bongo”tambarare”!

  20. Comment by solange on June 7th, 2008 4:42 am

    hivi huyu amanda si alikuwa miss arusha?au nimemfananisha jamani.

Leave a Reply