Huwezi kuzungumzia historia ya disco nchini Tanzania na kuacha kumtaja DJ Bonny Luv (pichani). Ukifanya hivyo,wanaoielewa historia, ladha na utamu wa disco, enzi hizo lilipokuwa disco haswa, watakuona una lako jambo.
Huyu ni miongoni mwa DJs wachache ambao, miaka nenda miaka rudi,wamekuwa wakijizolea sifa za kipekee katika kuhakikisha kwamba mashabiki wa muziki sio tu kwamba hawabanduki stejini pindi akiingia mitamboni bali pia wanapata “raha kamili”. Hali hiyo ndio imesababisha watu wengine wathubutu hata kusema kwamba ikiwa hujawahi kuhudhuria disco au shughuli nyingine yeyote yenye burudani za miziki huku udhibiti wa kule inakotokea burudani ukiwa chini ya DJ Bonny Luv, basi huenda ukawa hujapata bado hiyo “raha kamili”. Hata hivyo habari njema ni kwamba hujachelewa kwani Bonny Luv alikuwepo, bado yupo na ataendelea kuwepo.
Sasa kwa wale ambao mnakumbuka enzi zile mlipokuwa hamkosi viwanja au enzi zile mlipokuwa hambanduki stejini kutokana na kunogewa na miziki, basi mwaka huu mnayo nafasi ya pekee kukumbuka enzi hizo sio kupitia kwenye njozi bali uhalisia.Kivipi?
Katika tukio la nadra, tarehe 5 mwezi wa saba(5th July 2008) ndani ya jiji la Columbus katika jimbo la Ohio(Columbus,Ohio) nchini Marekani, DJ Bonny Luv kwa kushirikiana na wakali wengine kama DJ Mix Master Luke kutoka Washington DC na TNT Jackson wanatarajia kutoa burudani ya aina yake. Waandaji wameliita tukio hilo(au ukipenda liite Party) Old School Party of The Century. Ukikosa,usije kumlaumu mtu na kusema hukuambiwa.Habari ndio hiyo.
Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya mahojiano na DJ Bonny Luv kuhusiana na mambo mbalimbali kuhusu muziki na burudani na pia kuhusu ujio wake kwenye party hii ya aina yake ya Columbus,Ohio. Kwa mengi zaidi fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC: Bonny Luv,karibu sana ndani ya BC.Tunafurahi kufanya mahojiano haya na wewe.Mambo vipi?
BL: Mambo powa kaka!
BC: Kwa faida ya wale ambao wapo nje ya nchi kwa muda sasa kiasi kwamba hawajui siku hizi unafanya kazi gani,unapiga disco lipi na mambo kama hayo;unaweza kuwapa update kidogo kuhusu unachokifanya hivi sasa?
BL: Bado nimo ndani ya Muziki (Music). Kama unavyofahamu wigo wake ni mpana sana na kwa hivi sasa najishughulisha sana na Production inayohusika na studio recording nikimaanisha uandaaji wa muziki mathalan Bongflava,Zouk,Taarab,Ngoma za Asili,Kwaya (Choir)-Vipindi vya Radio,Matangazo ya Radio,Matangazo ya TV na kadhalika.

Mtu na fani yake.Kila alipo Bonny Luv huwa amezungukwa na vifaa.Hapa ni mwaka jana alipokuwa nchini Ubelgiji(Belgium) wakati wa Tamasha maarufu la Couler Cafe Belgium.
BC: Mara nyingi kazi au fani kama yako ya u-DJ huwa inaanza kwa mhusika kuwa kushawishiwa au kuvutiwa na utendaji wa mtu au watu fulani. Kwa upande wako nani au nini kilikushawishi mpaka ukaingia kwenye mambo ya U-DJ?
BL : Nadhani ni mtiririko mrefu sana uliopelekea mimi kuingia kwenye u DJ mpaka hapa nilipofikia. Lakini kwa ujumla ni mazingira niliyopitia nikimaanisha sehemu nilizokulia,watu waliokuwa wananizunguka,matukio niliyo husika nayo na mengine mengi.
Ila ninaweza kusema kitu kimoja ya kwamba wapo watu walionipa changamoto kubwa sana baada ya kuwa ndani ya fani kwa hali na mali. Mmoja wa wahusika wakubwa ni Joseph Kusaga ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group.
BC : Watu wengi wanaokujua au ambao wameshawahi kucheza disko lako wanajua kwamba wewe na Mawingu Entertainment ni kama chanda na pete. Ulijiunga lini rasmi la Mawingu Entertainment?Ilikuwaje?
BL : Ni muda mrefu sana kaka sikumbuki tarehe wala mwezi lakini niliaza mahusiano ya kikazi mnamo mwaka 1987 kama sijakosea. Kabla ya kujiunga na Clouds tayari nilikuwa nimeshaanza shughuli za u- DJ na nilikuwa nikifanya kazi zangu na rafiki yangu wa zamani sana anayeitwa Everist Mashiba na Dj Pio Pouse.
BC : Nchini Tanzania pameshakuwa na DJs wengi sana, wengine bado wapo, wengine wameshafariki na wengine wameachana na muziki nk. Lakini tunapotaja majina ya DJs nchini Tanzania jina lako mara nyingi huwa namba moja.Unadhani nini kinakutofautisha wewe na DJs wengine?
BL : Ukiachilia mbali juhudi,bidii,kujituma,kuwezeshwa na mengineyo nadhani ni BAHATI kaka. Nasema hivyo kwa sababu sidhani kama unaweza kumlazimisha mtu akupende au kupenda unachofanya.Lakini cha msingi zaidi ni nidhamu ya kazi kwa unaowafanyia kazi kwa ujumla iwe ni tajiri yako au wateja wako.
BC : Kwa wengi kizazi hiki cha sasa sio tena cha disco.Badala yake chenyewe ni cha matamasha (concerts) zaidi. Pamoja na hayo, bado tunaweza kusema madisco yapo ingawa labda hayavumi sana kama ya enzi zile kutokana na nyakati zenyewe.Sasa wewe kama mdau wa siku nyingi wa disco tuna hakika unafuatilia mabadiliko haya.Unaonaje disco la leo ukilinganisha na la enzi hizo ulipoanza kazi ya U-dj?
BL : Nadhani kilichobadilika ni teknologia tu.Si unaelewa mambo ya utandawazi?Kwa sababu gani nasema hivyo, mimi mwenyewe nimeshuhudia mabadiliko kutoka kwenye kaseti na rekodi kwenda kwenye CD na Minidisc ukiachilia mbali DAT Tape na sasa tuko kwenye kizazi kingine kabisa. Hivi sasa tunazungumzia kinakilishi (Computer) na mzao wake nikimaanisha Mp 3 na Mp 4,Flash Disc na Harddrive na mengineyo mengi yanayokuja.
Lakini kikubwa ni kwamba burudani bado ni ile ile.Labda Mwenyezi akitujalia uhai miaka kumi au kumi na tano ijayo tuwaulize hawa wa sasa wanayaonaje mazingira ya wakati huo na wakati huu! Hapo ndipo utakapogundua kuwa hadithi ni moja.

Dj Bonny Luv(katikati) akiwa na Light Engineers wakati wa Tamasha la Couler Cafe Belgium.Huyo jamaa wa kushoto ndio alikuwa Light Engineer wa kundi maarufu la muziki wa Reggae la UB40.Je unajua kwamba Bonny Luv amesomea Sound Engineering huko Liberty Hall nchini Uingereza?
BC : Wakati unaanza shughuli zako za U-DJ, muziki wa Bongo Flava haukuwapo kwenye ramani ya muziki. Lini ilikuwa mara yako ya kwanza kupiga muziki wa Bongo Flava katika disco? Unaweza kukumbuka ulicheza kibao gani na watu waliupokeaje?
BL: Swali zuri na gumu sana kwa kweli. Unajua maswala ya takwimu yanahitaji utaalamu na mimi kwa kweli takwimu zangu … ah! Unajua tena …. Lakini naweza kukwambia kitu kimoja kwamba nimehusika kwa kiasi kikubwa sana katika kuwashawishi wasanii waimbe ama wa Rap kwa Kiswahili wakati Bongo Flava inaanza na halikuwa jambo rahisi kwao na kwangu maana muda umepita sana na wakati huo mtu aki Rap Kiswahili … yaani ilikuwa haiji (Msemo wa zamani kidogo huo)
BC : Muziki wa kizazi kipya au Bongo Flava hivi sasa unazidi kutamba ingawa wengine wanatabiri kwamba utazimika siku si nyingi. Unadhani nini unaweza kuwa mchango wa DJs aidha kuufanya muziki huu uendelee kutamba au kusaidia kuuzika?
BL : Ndugu yangu kwanza hebu jiulize kitu kimoja … Bongo Flava,kama ulivyo sema inazidi kutamba halafu wakati huo huo watu wanautabiria kifo muziki huu huu wa Bongo Flava. Wewe huoni kuwa kuna walakini hapo?.Mimi nadhani jukumu kubwa la kuufanya muziki huu uendelee ni la wasanii wenyewe na wapenzi wake.Na labda ningependa kuongezea au ku-suggest kwamba fikra za muziki huu kufa zisubiri kidogo maana nadhani bado muziki wenyewe una safari ndefu sana.

DJ Bonny Luv(kushoto) akiwa na Ahmir Khalib Thompson aka QuestLove Drumer kutoka kundi la The Roots.QuestLove ni DJ,Producer,mwandishi wa muziki nk.Miongoni mwa artist maarufu ambao amewahi kuwarekodi ni kama vile Common na D’Angelo. Usisahau kwamba Bonny Luv ni Producer hatari akifanya kazi zake chini ya lebo ya Mawingu Studio.
BC : Tarehe 5 Julai mwaka huu unatarajiwa kuwa ndani ya Columbus,Ohio nchini Marekani tayari kabisa kwa Old School Party. Unawaambia nini wapenzi wa old school watakaohudhuria na wapenzi wengine wa muziki kwa ujumla?
BL: Kwa ujumla nimewatayarishi Safari na Historia ya D.J Boniluv.
BC : Ni DJ gani aliyepo kwenye game hivi sasa nchini Tanzania ambaye unaikubali kazi yake na kumuhesimu? Kwanini?
BL : Dj Peter Moe Kwa sababu katulia na yuko makini.
BC : Bonny,asante sana kwa muda wako. Kila la kheri katika kazi zako.Tuonane Columbus,Ohio.
BL: Shukrani Jeff.
Kwa habari zaidi na maelekezo ya jinsi ya kufika kwenye tukio,bonyeza hapa.BC itakuwa na uwakilishi kamili katika tukio hili.
Feedback / Comments
32 Responses to “DJ BONNY LUV:”NIPO TAYARI KWA COLUMBUS,OHIO””
Leave a Reply


sending...
Kaka Bonny Luv
Big up mtu wangu.Nakumbuka sana enzi za disco la Pool side pale Kilimanjaro hoteli ilikuwa ni moto na nguo kuchanika.Naishi Houston,Tx hivi sasa na lazima nije Columbus hiyo tarehe.Duh..ni noma maanake.
Safi sana waandaaji.Lazima batu bazima tukakumbuke enzi zetu.Nadhani hili litakuwa tukio la mwaka.Planning to be there.Samahani nina swali hivi Bonny Luv ashaoa?Mbona BC hamkumuuliza hilo swali?
uoe sasa nawewe loh
namkubali sana DJ bonny luv,na amechangia sana kuwashawishi wasanii wa hiphop bongo kuimba kwa lugha ya kiswahili hilo halina ubishi na pia haina ubishi kuwa DJ petter moe ndio DJ bora zaidi anayefuata baada ya bonny!
hongera mwaya!unavutia na nakukumbuka wewe pamoja na dj steve B nilikuwa nawaona sana pale maeneo-maeneo!! long tym!
Eti jamani Bonny lov na venture ni ndugu maana nilisikia hawa jamaa ni mtu na kaka yake.
Mdau hapo juu, Boniluv namuona sana siku hizi na maiwaifu wake wa long time toka enzi za miaka ya tisini mwishoni mpaka leo wako pamoja na wanaishi pamoja sasa sijui wameoana au vipi. Ni binti wa mwanza anaitwa sabaha, wa kitambo huyu dada yetu
Halafu mimi sio Jeff wa Bongo Celebrity…. Majina yamefanana tu
Dah mshkaji upo juu aminia mtu wangu nikikumbuka mavitu kama lile songi la Billy Ocean…the going gets tough, the tough get going… huwa unalikung’uta na linanikuna, anyway big up kwa sana.
BC…This is what’s up aisee! this is the old skool party of the century kama alivyosema BC hapo juu don’t miss this opportunity inakuwa once in a lifetime…check it out @www.oldskoolnjoo.com
Hongera kwa kazi nzuri tunakutakia safari njema huko Ohio. Familia ya umaarufu hii, Dj Bonnie love, Dj Venture wa Clouds na Dj Mackay wa EastAfrica
Hahaha we MENDE dah!
Aisee i wish ningekuwa huko OHIO maana vitu vya huyu mchizi navikubali sana yupo juu, kwa wale waliokuwa waudhuriaji wa viwanja kama 7floor, poolside, tazara (MASEBENE) na wale wana wa UD mtakumbuka wazi ma party ya UDASA ilikuwa balaaa kijana yupo juu.
big up Bonny a.k.a MENDE……… Hahahahaha
Duh! Namkumbuka huyu kaka tangu za enzi ya visa vya watoto wa Upanga, shule ya Muhimbili Primary and yote TUITION YA MWALIMU NDOSI! Nilikuwa naye group moja. Unakumbuka viboko vya mwalimu ndosi kuimba table na kusoma vitabu vya kiingereza vya Oxford. Anyway, ninamshukuru sana huyu mwalimu kwani hadi leo hesabu hazinipigi chenga, maana naweza kuzifanya hata bila ya kuandika popote. Wadau wa Muhimbili Primary miaka ya themanini mpo???? Hongera Bonny M. (UNAKUMBUKA HII NICKNAME)? maana sikutaka kuimalizia.
Mkereketwa si ungemalizia tuu hiyo nick name hahahaha Bonny “Matusi”!….alafu tusi lake lilikuwa moja tuu!
Malaika Katende, ni vipi mbona unauliza kama kaoa? U looking to hook up with the brother? ana wake wa ubani huyo. N wewe Amina unaesema “uoe sasa na wewe loh!” unajuaje kama kaoa au hajaoa? jibu umelipata hapo juu. anae mkewe
People, people, people!
We are not here to discuss his marital status, kaoa hajaoa its none of our business, PERIOD!
Waswahili bwana! ndo maana wanatufisadi! tumekalia kufatilia tu maswala binafsi ya watu wengine yetu yanatushinda, ah!
Suala hapa ni OldSkul Party na si nani kaoa nani kaolewa, mwe!
Aminia mwanangu Bonny Luv! Nakukubali kamanda wangu katika masuala ya mixing linapokuja suala la oldies.Nakukumbuka sana wakati ukifanya vitu vyako pale Latarvena karibu na Shoppers Plaza! Unajua hizi nyimbo za oldies jamani mimi zinanikumbusha mbali sana. Kweli kamanda Bonny umenena kwa kumtaja mkali mwingine wa oldies, Dj Peter Moore huyu jamaa mimi pia namkubali hasa kile kipindi chake pale CLOUDS FM cha GROOVE BACK SATURDAY! Jamaa anatest ya muziki! Natamani sana ningejumuika nanyi kwenye hilo libeneke la kufa mtu la oldies hapo Ohio.
Basi mbali ya Dj Bonny Luv ambaye bado ameweza kuhudumu katika fani ya muziki mpaka sasa je mnawakumbuka hawa wengine kama Young Millionaire, Richie Dillon, Jerry Kotto, Bush Doctor, Eddie Grand, Sure Boy, Choggy Sly, Kalikali, Mr. A wa pale Continental Club Mix, Chris Phabby The Lover. Pia nakumbuka sana huwezi kutaja historia ya disco Tanzania bila kutaja kumbi kama Mbowe Club sasa hivi Club Billicanas, Maggot Ushirika, Rungwe Oceanic, Kilimanjaro Pool Side, Msasani Beach Club, Lan’gata, nk. Huko mikoani kulikuwa na madisco makali kama Magnum Club Mwanza, Uptown Disco, Cave Disco Arusha, Kilimanjaro Disco pale Moshi NK Disco Dodoma. Duh nimemkumbuka marehemu Shaban Satto alikuwa anasimamia madisco ya Space 1900, mungu ailaze roho yake pema peponi na wote ambao walikuwa wadau wa enzi hizo! Hivi jamani nyinyi mnakumbuka makundi ya vijana ya disco kama ILALA FOURWAYS BROTHERS, SWEET CORNER hilo ndilo kundi alilokuwa anachezea disco huyu jamaa anayemiliki sasa hivi studio ya BAUCHA RECORDS, Ally Baucha. Mussa Simba aka Black Moses, Athuman Digadiga, Ommy Sidney walikuwa wakichuana vikali pale Lan’gata Social Hall Kinondoni enzi hizo!
Pamoja na kwamba, sitokuwepo Ohio siku ya siku naomba wadau mtakaokuwepo mumkumbushe Bonny awapigie hizi nyimbo za oldie:
1.HEART & SOUL wa PROJECTION.
2.SKIPS A BEAT wa WARP NINE.
3.LOST YOUR NUMBER wa NUSHUUZ
4.WARM LOVE wa BEATMASTERS.
5.TREAT HER LIKE A LADY wa TEMPTATION.
Jamani the list is endless hizo ni baadhi tu ya kali za enzi hizo. OLD SKOOL WILL ALWAYS REMAIN THE BEST SKOOL!
diblo has a point!
basil unakumbuka Let the beat hit em(rock the house yo!) wa lisa lisa
Mpakakieleweke acha kabisa hilo dude lilikuwa balaa duh!
Huyo mdadaz Lisa Lisa pia alidondosha nondo nyingine mbaya sana ilivuma sana ilikuwa inaitwa TAKE YOU HOME akiwashirikisha FULL FORCE upo kamanda wangu yaani kuna nyimbo ukizisikia mpaka unasisimka mwili. Lakini uzuri wa hizi nyimbo utazifurahia kama ulikuwepo enzi hizo. Je unazikumbuka hizi:
1.DONT U WANT ME – JODY WATLEY.
2.MY ARMS KEEP MISSING U – RICK ASTLEY.
3.HOLD ON – EVELYNE KING .
4.LIVING IN A BOX – LIVING IN A BOX.
5.SOONER LATER – STEVE RICH.
Haya kazi kwenu wadau wa Old Skool mpooooooooz?
mhhh jamani mi hata sielewi…mi nakumbuka I wanna be down ya brandy,matty unakumbuka?mi hiyo ndo old school
naujua dont u want me wa jody watley, that lady was a ghetto black american na video yake ina matusi kweli. naujua kwasababu wazazi wangu enzi zao walikua mabishoo,wanamkanda walirecodi nyimbo nyingiii saaana basi nilivyokua ndio nikawa naziona. kuuna kaka mmoja anaitwa alexander jamani waooooo,kaka alikua bombaaaaaa na huu mwimbo wa ‘beauty is only skin deep,yeaa yeaaa yeaaa,beauuutyy is only skiiin deeep YEEEAAA YEEAAA’ na ule wa goodlife goodlifee gooodlifee goodlifee,woouu wooouuu wooouuu na back to liiifeee,back tooo realiiityyy EBWANA NDIO WANAMKIZEEE
basil most of hizo nyimbo ninazo nilikuwa nazikusanya tangu 1998(88%) ninazo nyingine kali zilikuwa
nyingine kali zilikuwa
tara kemp – Hold You Tight All Night Extended Mix
soul II soul – A Dream’s A Dream (Club Mix)
Snap – Ooops up
evelyn champagne – Hold On (Extended LP Mix)
D’Bora – Dream About You (E-Smoove Mix)
d.mob – Time To Get Funky
the cool notes – make this a special night
kenny thomas – best of you
adeva – Respect (Extended Mix)
BLACK BOX – FANTASY EXTENDED REMIX
cathy dennis – Just Another Dream
jomanda – Gotta Love For Your Hurley’s House Mix
klymaxx – Good Love (Dub)
karyn white – Secret Rendezvous (After Hours Mix)
kym simms – Too Blind To See (Remix)
list ni ndefu mno nimechoka kutaipu ila zote ninazo in vinyls
yaani ilikuwa balaa pale seven floor na twiga na motel agip
we maryciana mwimbo wa back to life sio wa soul II soul !?!
my name is captin solow he is coming their
Ehhhhhh eheeee! Nilijua tu watarukia wa kurukia wasivyovijua!
Mradi mtu kaingia kwenye blog aonekane na yeye anachangia.
We sijui Binti Mzuri hapo juu hivi ulikuwepo enzi hizo ama ndio nyie mashabiki wa hizi nyimbo zenu za bubble gum? Utamu ukiisha unatema basi! Sasa unadhani huo wimbo Back To Life walipiga akina nani kama sio hao Soul II Soul? Au wewe unazungumzia Back To Life ya vijana wa leo.
Hizi Old Skool kama hukuzicheza ama hukuwepo enzi hizo ni sawa na bure!
Usichangie jambo kama huna uhakika nalo sawa bibie?
Tuachie wadau wenyewe tunaoujua utamu wa hizo nyimbo.
Kachangie nyimbo zenu za akina Matonya, Marlow sijui Chidi Benz!
he makubwa hapa…halafu binti mzuri una damu ya kunguni kila mahala weye wapashwa tu
hahahahahahahahahahahaahaha
Dj Boniluv umeoa?
@Sally
Ndio nimeshaoa
Basil wa mwanza au ? kwani mimi mzee wa sweet corner hahari za masiku naona umenikumbusha mbali saaaaaaaaaana !
Yap! Bonny Luv nakukubali, Napenda sana tusisahau tulikotoka. Nakumbuka enzi hizo watu mnaondoka kwa basi la UDA kwenda posta mapema tu alafu alfu kurudi uswahilini mnachanga na washikaji hela ya taxi, yote hiyo ilikuwa ni upenzi wa music, na ukiwa ndani kukaa kwenye kiti mwiko manake kila wimbo ni kigongo kwahiyo mambo ni kuyaruka mpaka asubuhi.
Tukiongelea Oldie lazima tuwakumbuke ma pioneer kama:-
DJ Say Do
DJ Gerald
DJ Kalikali
DJ John Peter Pantalakis
DJ Choggy Sly
Ma disco hatuwezi sahau ni kama:-
Mbowe
YMCA
Jet set
Msasani beach
Vigongo hatuwezi sahau ni kama:-
Love come down – Evelyn King
Holiday – Madana
My heart is devide – Shannon
Let the music play on – Shannon
I know weekend special – Brenda Fassie
No time to waste – David James
Can’t slow down – L. Richie
Wanna be starting something – M. Jackson
AND THE LIST GOES OOOOOOOOOON!
Paul Onyango – UK