
Kama kuna mambo ambayo yalikuwa mazuri wakati wa mkutano wa Sullivan uliomalizika hivi karibuni huko Arusha Tanzania,basi mojawapo ya mambo hayo ilikuwa ni fursa kwa watu mbalimbali kukutana,kupata fursa ya kupiga picha,kubadilishana anuani nk.Lakini pia kulikuwepo na kivutio kingine.Watu wengi walionekana kutaka kupiga picha na Hasheem Thabeet kwa minajili ya “kupima urefu” kwani kijana huyo amekwenda hewani vilivyo.Pichani ni mwanamuziki Nakaaya akiwa na Hasheem Thabeet wakati wa mkutano huo.
Photo/Bernard Rwebangira
Page 1 of 3 | Next page