ALIPOTUMBELEA KELLY ROWLAND

Wiki hii Tanzania ilitembelewa na Kelly Rowland,mmoja kati ya wanamuziki waanzilishi wa kundi maarufu la muziki lililojulikana kama Destiny’s Child.Kelly alikuwa nchini Tanzania kama Balozi Maalumu wa Taasisi ya MTV Staying-Alive.Ukitaka kujua mengi kuhusiana na taasisi hiyo,bonyeza hapa.

Alipokuwa nchini Tanzania,Kelly Rowland ambaye aliongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Georgia Arnold, alitembelea sehemu mbalimbali za jiji,alikutana na watu na vikundi mbalimbali kama ambavyo unaweza kuona katika picha hapo chini.

Kelly Rowland (kushoto) akiwa na binti aitwaye Eliza(katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MTV Staying-Alive Foundation,Georgia Arnold(kulia) wakati wa ziara ya Kelly nchini Tanzania .Eliza anaongoza Kikundi kijulikanacho kama Elizabeth Youth Group kinachojishughulisha na miradi mbalimbali ya vijana katika kutoa elimu kuhusu ukimwi na matumizi ya madawa ya kulevya.Eliza mwenyewe ambaye ni muathirika,aliwahi kufanya kazi ya kujiuza kabla hajaamua kubadili maisha yake na kuamua kusaidia wengine.Iangalie documentary kuhusu Uwanja wa Fisi(Hyena Square) na Eliza kwa kubonyeza hapa

Kwa picha zaidi na maelezo zaidi,bonyeza (more) hapo chini;

Kelly Rowland akiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Biafra iliyopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar-es-salaam.Kelly aliitembelea shule hiyo ambapo alipata nafasi ya kuzungumza machache na wanafunzi kuhusiana na suala zima la ugonjwa wa ukimwi na umuhimu wa kupima afya na kujikinga na maambukizi.

Kelly Rowland akimkabidhi Eliza tuzo maalumu ya MTV Staying-Alive kutokana na mchango wake katika kuelimisha vijana kuhusu janga la ukimwi na jinsi ya kujikinga na maradhi hayo nk.

Mojawapo ya maeneo aliyoyatembelea Kelly ni eneo maarufu liitwalo Uwanja wa Fisi.Pichani ni Kelly Rowland akiwa ameongozana na Eliza na watu wengine mbalimbali, huko Uwanja wa Fisi.Eneo hilo ni maarufu kwa pombe,madawa ya kulevya,ngono zembe nk.Inasemekana kwamba hapo Uwanja wa Fisi kuna machangudoa wanaojiuza kwa hata shilingi 200/=Tshs!!

Mkurugenzi Mtendaji wa MTV-Staying-Alive Foundation, Georgia Arnold(kulia), akimkabidhi tuzo Kelly Rowland(kushoto),kutokana na shughuli zake kama balozi wa MTV Staying-Alive.Katikati anayeshuhudia huku akiwa amejawa na tabasamu ni binti Eliza kutoka Elizabeth Youth Group.

Picha ya kwanza juu ni Kelly Rowland akiwa amembeba mtoto ambaye ni muathirika wa ukimwi.

Page 1 of 3 | Next page