Bendi ya kitanzania,The Ngoma Africa Band,yenye makazi yake nchini Ujerumani hivi karibuni imetoa single yake mpya inayokwenda kwa jina Apache Wacha Pombe.Single hii tayari inatamba katika vituo mbalimbali vya radio huko Ulaya na pia Afrika Mashariki.Upo katika mahadhi unayoweza kuyaita Bongo Dance.
Kama kawaida yao,The Ngoma Africa Band,wamekuja tena na wimbo mwingine wenye kuchezeka vizuri lakini wakati huo huo kubeba ujumbe muhimu kwa wanajamii.Pombe,pombe,pombe.Apache anaambiwa aache pombe ili apate uwezo wa kuwekeza kwenye elimu ya watoto au familia.
Katika wimbo huu,Ras Makunja(kiongozi wa The Ngoma Africa Band) anaimba na Christian Bakotessa a.k.a Chris B.Usikilize wimbo Apacha Wacha Pombe kwa kubonyeza player hapa chini.Bab Kubwa The Ngoma Africa Band,endeleeni kupeperusha bendera yetu huko mlipo.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Page 1 of 3 | Next page