MwanaFA UNAOA LINI…?

Kwa mila na taratibu za jamii nyingi,hususani zetu za kiafrika,kijana akifikia umri fulani huwa anategemewa kuoa.Ikitokea ukafikia umri ambao kila mwanajamii anakutegemea “kujipatia jiko” na ukawa hujafanya hivyo, hapo lazima ujiandae na swali;unaoa lini?Ukikutana na shangazi swali ni hilo hilo.Ukikutana na mjomba naye anasimamia hilo hilo.Jamii nzima inauliza,unaoa lini?

Sasa je ukiulizwa swali hilo huwa unajibu nini?Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya,Hamis Mwinjuma a.k.a MwanaFA a.k.a Binamu anakupa msaada wa majibu katika single yako mpya inayokwenda kwa jina Bado Nipo Nipo huku akiwa amemshirikisha Miss Universe Tanzania 2007,Flaviana Matata.

Bado Nipo Nipo imepikwa na producer Harmy B.Pia MwanaFA anapewa tough na vichwa vingine kama vile Ambwene Yesaya(AY),Alan,Jabiri,Shehe na mwanadada aitwaye Anna.

Usikilize wimbo Bado Nipo Nipo kwa kubonyeza player hapo chini.Ningependa sana kusikia majibu kutoka kwa kinadada walio single, ni kweli anayoyasema MwanaFA?

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

 1. pandu, 01 July, 2008

  Bado nipo nipo mama…..ukiitwa boyfriend usidhani upo peke yako, sura za utoto lkn wanaifadhi wazee wako, sijui ni tamaa, dhiki au wanaanika njaa tu
  Ukimegemwa dem wako nawe mtafute mnyonge ummegee, aipunguzi maumivu ila inadhihilisha ukidume.
  FA ni nyoko mwana…nimekukubali

 2. P. S. Nalitolela, 01 July, 2008

  nimesikiliza an uncorrupted version from binamu13.com, and I must say, it’s like Binamu is talking to me!! Totally feel what he’s saying, nimeikubali!!

 3. H. Dignified., 01 July, 2008

  Hii ngoma nimeikubali. Ni bonge la song na linatisha si uongo. Mzee uko juu sana tu. Ata “mimi bado nipo nipo kwanza”. Na mademu wenyewe hawa wa siku hizi yaani “Nipo nipo sana tu”.

 4. neema, 01 July, 2008

  upo juuu mwana

 5. hans, 01 July, 2008

  eeh bwana unatisha si utani, wewe ni mzee wa vina kila unachosema ni kweli tupu. hii hata wakisikia ndugu zangu wanaonikomalia nioe wenyewe watazima story. asante sana BINAMU F.A

 6. DUNDA GALDEN, 01 July, 2008

  Bado niko niko kwanza…….
  alilala na bibi harusi wakati si bwana harusi
  nimeupenda huu ujumbe lakin si kwa wanawake wazuri
  msela yeye ndio wazo lake poa mwana uchune ipo siku
  uakutana na mabinti wazuri hapo utachagua kama mimi
  msela wako nilivyochagua baada ya NIPO NIPO YA KIPINDI
  KILICHOPITA
  Chai goda

 7. hombiz, 01 July, 2008

  vicheche wengi sana siku hizi. Sio BONGO tu hata nchi za watu wapo. Cha muhimu ni kumuomba mungu akusaidie kupata mwanamke anayekufaa. La sivyo utazeeka bila kuoa.

 8. baker, 01 July, 2008

  Ebwana FA nimekubali yani toka nianze kusikiliza music wa bongo, ndio leo nasikia hii tune yako na ninavyoona ndio nyimbo ambayo iko na full maujumbe yaliko kwenye maisha yetu haya ya kiswahili. Ebwana FA umelenga kamanda yani pale pale,penyewe mwana. Duh ebwana I cant wait to get ur album men! its cracking tune.Big up

 9. echo, 02 July, 2008

  ebwana dah! nimekukubali mkubwa uko juu ile mbaya katika tungo, nyimbo yako nimeikubali sana iko inaendana na hali jinsi ilivyo sasa…..! wimbo umenigusa sana kwani wazo hilo lipo kichwani mwangu muda mrefu sana nanihawahi kumjibu binti mmoja hvyo hyo kutokana na swali kama hilo…..nlidhani niko peke yangu kumbe tuko kibaaaaoooooooooooooo! BADO NIPO NIPO TU, SAAAAAAAANA TU!!!?

 10. dadi, 02 July, 2008

  Ndio mkubwa uko juu si kitoto nyimbo nzuri ujumbe bab kubwa………….! mtindo wa sasa ni kumegana tu hakuna mapenzi, ni kama mchezo flani hivi inatakiwa full maujanja uongo c kpole pole…….! hakuna ndoa, ukioa umeolea watu kuna vijamaa flani dem mzuri kwao mpaka awe wa mtu. mabint tamaa zimewazidi. bado nipo nipo tu sana tu, wakuoa ntakuwa mimi, nioe unimegee! Ayaaaaaaaaaaaaaah weeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!? big up fa.

 11. mzee wa vichanchubi, 02 July, 2008

  uko juu mwana ila achana na visungura tope,bado nasubiri cd yangu mwana,misijabisha!!!!!!!!!!Big up

 12. binti-mzuri, 02 July, 2008

  mh we hombiz nawe…mnaonaga wanawake tu…mbona wanaume hawasemwi!?!?who wants to get married to a player!?NOT ME

 13. karen, 03 July, 2008

  Kaka wimbo mzuri sana big up,
  ila kwa nyinyi wasanii ndio mnapenda wanawake wa hi class ndio maana mnakutana na matatizo,jaribu kukaa uchunguze wasani wenzako woote yupi anamsichana wa low class?
  na wanawake wa sikuizi jamani tupendane,manake wanawake nao wamekuwa maadui hata mugabe anaafadhali
  hawajui huyu mume wa mtu au huyu lover wa rafiki yangu hasa hawa wanojiita wasomi,

  tuwe makini la sivyo tutaisha na hiv jamani

 14. Jafa, 03 July, 2008

  binti mzuri..
  naona MwanaFA has made a big point hapa,ila anaongelea upande wake kama mwanamme…lakini it applies for both!…namjua mtu alikuwa anaoa jumamosi na akalala kwa sunguratope mmoja hivi Friday…mtu maarufu tena

 15. sally, 03 July, 2008

  Big up

 16. binti-mzuri, 03 July, 2008

  oke poa jafa! ila mbona unaonesha kushangazwa!?!?..ndio maisha!…’nipe nikupe,raha tupateee’

 17. iAUWDQ, 03 July, 2008

  Huwa simkubali MwanaFA ila sasa nime mkubali maana ule mwimbo wa “Unaoa lini ” yaani yale majibu najiona kama nimeandika mimi ,maana kila kitu ni kama ninacho jibu nikiulizwa swali hilo.

 18. Miss G, 04 July, 2008

  Wewe nae unataka kushangaza uma kwamba huwa humkubali mwana FA, basi unaonekana kichwa chako kigumu kweli, he hehehe
  Big up sana Mwana FA, wimbo umesimama sana kama kawaida yako….hata sisi mabinti bado tupo tupo!!! mapenzi yenyewe haya ya kibongo bongo! umenena ukweli mtupu

 19. mr b, 04 July, 2008

  imenibidi niucjilize huu wimbo baada ya kusoma comments zenu..wimbo ni mkali na binamu huwa hakosei ila tuangalie tusijidanganye coz excuse huwa haziishi…unayosema binamu ni kweli yapo ila tiba sio kuwepowepo..hivi kweli ukitaka kwenda kwenu tanga utasubiri madereva walevi na wavunja sheria za bara2 waishe,hali ya hewa iwe safi ndo usafiri ili usipate ajali? hope jibu unalo,wat u’l do is 2 take precaution nakuanza safari…afterall huwezi kueliminate all problems ndo uoe,uwezo wa mwelevu huonekana kwenye kutatua tatizo litokeapo na si kumbia kwa kuliogopa….young man peter s.n acha kujifaliji oaaaaaaaaaaaaaa……………..

 20. ALBERT MBAGO, 05 July, 2008

  Ebwana big up sana BINAMU, track imetulia kinoma umeongea ukweli kuhusu hawa dada zetu, mi mwenyewe bado nipo nipo kwanza tena bado nipo nipo sana, maana life lenyewe limepinda sana bado upate mwanamke wa simu na gari au mkwanja na gari si utakojoa dagaa mwanaume. Bado nipo nipo sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

 21. Frateline, 07 July, 2008

  Hi guys, Mimi kutoka Helsinki- Finland
  Kwa kweli song ni zuri, Lakini wasi wasi wangu huu wimbo umekaa upande mmoja wa shilingi, halafu kwa watu wasio makini unapotosha maana umewaweka wanawake kwenye kundi moja, It is too general, kwani ndiyo wapo wanawake wenye sifa mbaya lakini pia wapo wanawake wenye sifa nzuri ni wengi tu, vivyo hivyo hata sisi wanaumme tupo ambao tabia zetu chafu sana yaani umalaya wa ajabu, na mara nyingi wanaumme wengi ni malaya muno, wengine walevi sana na hawana sifa za kuwa waumme za watu, hivyo sio vizuri kuwanyoshea vidole mabinti wakati wewe mwenyewe na mungu wako unajua ni malaya wa kutupwa, biblia inasema nitakupa wa kufanana naye, wewe malaya halafu unataka bikira itoke wapi, wakati wewe ni mchafuzi na unaharibu mabinti wa watu. Kwanza wanaume wengi wanapenda kudanganya mabinti wa watu kuwa nitakuoa na baada ya kumega anaingia mitini, kwa kweli dada zetu wakati mwingine wanakuwa njia panda hawawezi kujua mkweli nani? Mwisho wanaumme muoe usiutumie huu wimbo kuharalisha tabia chafu ya umalaya, pia dada zangu chonde chonde Mwana FA imewachongea ktk jamii inayotawaliwa na mfumo dume ambapo umalaya ni kwa mwanamke tu, wewe chunguza hata ktk ndoa nyingi wanaume wengi hata mabosi mpaka nyumba ndogo zao zinajulikana, kwani wewe unafikiri mwanamke yeye hana hisia au anamoyop wa chuma hapana lazima atarevenge tu, lakini nawasihi wanawake achana kushindana na wanaume kwani wao ndio wanapata support ya mfumo dume na kuamua nani na lini kuoa, hivyo badilisha tabia tulia,.

 22. karen, 08 July, 2008

  Thanks kaka Frateline
  yani wanaume wote wangekuwa waelewa kama ww basi kungekuwa hamna uhuni wala ukimwi usingeuwepo

 23. Belo, 08 July, 2008

  Binamu una AKILI baba
  Nafikiri ndio msanii wa TZ ambae unafanikiwa kila sekta
  Music
  Shule
  Maisha

 24. linda, 08 July, 2008

  KAZI KWELIKWELI
  Usioe ila unakoelekea ni kufa na ngoma, maana utakuwa unaoa usiku asubuhi uko single!
  hahahahaha ama kweli heri mjinga kuliko mpumbavu.

 25. bona mushi,cosfecaso, 09 July, 2008

  aissseeeeh!!! we AF ni NOMAA,yani ni bonge la dude la ukweliiiii!!.ila ukweli unabaki palepale mwanaume aogopi njaa jitose tuu mzeiiya.

 26. alpha, 09 July, 2008

  linda…hayo aliyoyaimba FA ni kweli kabisa!wat’ss yo problem ma’am??maana kwa jinsi anavyosema,hata ukioa aina ya mabo wanayofanya hao wadada lazima ufe kwa ngoma tu!ona haya kushabikia ukicheche…and stop hating!!

 27. Angel_Eyez, 09 July, 2008

  Wimbo umetulia ila tusisahau kwamba mwisho wa siku unavuna ulichopanda… hakuna mwanadamu anayetaka kuzeeka peke yake lazima upate mwenza wa kukuvua kivuvu (kukutoa upweke).
  Wanaume nao ni waongo pia ktk penzi; tatizo hakuna kuaminiana hivyo inakuwa tabu tu. Unakuta kila mmoja ameshaumizwa zamani na wa ubani wake basi hata akiwa ktk penzi jipya bado anajihami sana hata matokeo yake kupoteza penzi kwa kutokujiamini.

 28. Matty, 10 July, 2008

  Khaaaa!!!!! jamani sikupanga kusema lolote hapa lakini uvumilivu umenishinda hebu kwanza someni Mathayo 7:7 halafu nakuja.

 29. linda, 14 July, 2008

  hahaha matty umenichekesha
  usikimbie we wapige injili hao, vijana wanapaswa kubadilika
  sio sbb mwenzenu kaimba hivyo basi tena mnaiga si kila kitu cha kuiga jamani.
  Mathayo 7:7
  ”Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona, bisheni hodi nanyi mtafunguliwa”
  Sasa watu hawataki kuomba wanataka tambarare tu haya, mtaishia ukicheche tu.

 30. linda, 14 July, 2008

  Alpha
  Endeleeeeeeeeeeaaaaaaaaaaaa

 31. hombiz, 14 July, 2008

  Binti-mzuri, najua kuwa wanaume wazinzi nao wapo. Lakini kiwango chao sio kama cha vicheche!. Vicheche wengi saaana siku hizi!. Hata mimi yalinikuta na nimeshuhudia mengi toka kwa watu ninaowafahamu. I`m talking about super vicheche!
  Kaaaaaaaaaaaaaazi kweli kweli!

 32. Matty, 15 July, 2008

  Linda karibu tusomee uchungaji teh teh tetetetetetetett!

 33. linda, 19 July, 2008

  Asante Matty,
  Kila mtu anapaswa kujua why yuko duniani,
  hahahahaha,
  Umechagua fungu jema.

 34. angel, 31 July, 2008

  it has a good massege.congrats man.it take me more than 4hours simply listen to this true song.angel from IFM.TAKECARE GUYS BOTH GIRS AND BOYS ,MEN AND WOMEN.

 35. peter sigy, 09 September, 2008

  thats good F.A,kupata tunzo hile ilikua haki bro!

 36. FRED MUNGURE a.k.a OG, 11 September, 2008

  {PAMOJA NA KUZALIWA TANGA MAPENZI YALIKO ANZIA BADO NIPO NIPO MAMA} Mwana FA me nakukubali kinoma kwa mashairi,kwani hata mimi bado NIPO NIPO SANA………
  take 5 man

 37. halima, 08 October, 2008

  waswahili tunasema nyani haoni kundule, hata na sisi wanawake bado tupo tupo sana na fikiri tutafika.

 38. Mama wa Kichagga, 31 October, 2008

  Nyimbo ya mfumo dume hii!

  Ungejiimba na wewe kuwa kicheche basi ungevuna sana ila kwa kuwa ktk mrengo wa kushoto na kutuhukumu sisi peke yetu ulikosea sana!

  Hivi huyo demu anajichechea mwenyewe? si kuna ki-mwana FA pembeni?

  NB: Hivi unajua wanawake ni asilimia ngapi TZ au duniani? Kwa kukisia ni sawa na 50%. Huoni hapo kwa kuimba huu wimbo wa kuipotosha jamii unaathiri 50% ya soko la bidhaa zako?

  Think twice & use common sense next time kabla ya kufyatua wimbo na epuka lugha zinazokandamiza jamii fulani. Jua wewe ni kioo hivyo jamii inategemea uimulike kwa haki na sio namna hii hapa! Please bring your school forward au unadesa?

 39. nunku, 05 November, 2008

  FA najua umekomaa kimashairi na haiwezekani kuandika nyimbo yenye ujumbe na hisia nzito kama hii bila kuguswa na kitu au kufikwa na jambo[mfano Jnature ilimuuma sana alipotendwa na cnta] sasa wewe nani kakufilimba mtima wako mpaka ukaamua kutuburudisha namna hiyo mwana? FA kwenye kideo yule binti ananichanganya ni mama yako au ni mama yako mdogo?

 40. Elibahati, 11 December, 2008

  Ebwaba Fa we Noma japo watu wana jib ila waache hawana mistari!

 41. Fifi, 06 January, 2009

  sina la zaidi kwa hayo ndugu yangu Frateline amesema apo ju kidogo ni ukweli kabisa. ungera sana Frateline.

 42. monrasi, 01 February, 2009

  mimi nilihonga simu nikajikuta nimeoa. Lakini sasa nasumbuka kinoma. MAMA HASHIKIKI TENA.

Copyright © Bongo Celebrity