Kuanzia usiku wa leo(saa sita usiku kwa saa za Afrika Mashariki),blog maarufu ya Muhidin Issa Michuzi,itabadilisha anuani.Badala ya kupatikana kupitia www.issamichuzi.blogspot.com sasa itapatikana kupitia www.michuzi-blog.com.

Mbali na mabadiliko hayo ya anuani,yupo “mwana” mwingine ambaye naye anazaliwa.Hiyo ni tovuti nyingine chini ya usimamizi wa huyu huyu gwiji wa blog. Tovuti hiyo ambayo inapatikana kupitia www.bongotyube.com ni maalumu kwa habari,burudani,michezo nk kupitia video.

Kama kawaida yetu,tulipopata habari kuhusiana na mabadiliko hayo katika blog hiyo ya jamii pamoja na tovuti mpya inayoanzishwa,tuliona ni heri tumtafute Michuzi mwenyewe ili atupe undani kidogo kuhusu mabadiliko hayo nk.Kwa uungwana kabisa akakubali kufanya nasi mahojiano utakayoyasoma hivi punde ingawa ukweli ni kwamba yuko bize ili kuhakikisha kwamba mabadiliko yaliyotajwa hapo juu yanakwenda salama kabisa.

Lakini pamoja na kuongelea mabadiliko hayo,Issa Michuzi,ametoa mafunzo na changamoto muhimu sana kwa wanablog na pia washika dau mbalimbali katika sekta au fani ya habari na mawasiliano.Je ni changamoto na mafunzo gani?Anawaambia nini “wadau” wakati huu anapojiandaa kuendeleza “libeneke” kwa mapana na marefu zaidi? Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC:Kwa mara nyingine tena naomba nikukaribishe ndani ya BC.Mambo yanakwendaje?

MICHUZI: Asante sana BC. Mambo mswano tu. Ila kwanza naomba nikupongeze kwa kazi nzuri mnayofanya. Kwa kweli ingawa wengi hawakubali kwa kuwa hawajafikiria hilo lakini staili yenu ya kipekee na haina mfano. Ningependa magazeti ya hapa nyumbani yaige mfano huu kwani habari ni watu na matukio sio viongozi pekee. Linalofanyika BC ni mfano wa kuigwa (sio wa ku-copy na ku-paste kama inavyoanza kujitokeza sasa ambapo naona magazeti yameanza kufanya hivyo) na wa kupewa sifa zote. Mie ni mpenzi sana wa BC na lazima nipitie humu kila siku na huwa siangushwi. Kila siku nakuta mahojiano mapya na kama si mahojiano muziki wa enzi hizo na za sasa. Hii inafurahisha sana. Hongera sana sana BC.

BC: Kwanza kabisa hongera kwa kuzindua tovuti yako itakayokwenda kwa www.bongotyube.com na pia kuboresha uwezo wa blog yako maarufu ya Issa Michuzi kwa kuihamishia kwenye www.michuzi-blog.com. Kwa vyovyote vile mabadiliko haya yamefuatia au yanaelekea kwenye mipango fulani.Unaweza kutuambia kidogo kuhusu sababu zilizopelekea mabadiliko haya?

MICHUZI: Asante sana. Sababu ni rahisi sana; nayo ni kupiga hatua moja mbele zaidi. Naona furaha na fahari kwamba hivi sasa fani ya blogu imepiga hatua kubwa kwenda mbele kiasi ya kwamba blogu zimeanza kutambulika kama mojawapo ya vyombo muhimu vya habari. Hivi unavyozungumza hata stesheni zingine za redio zimeanza kupitia blogu kama zifanyavyo magazeti mengine. Nahisi muda si mrefu ujao stesheni za TV nazo zitafuatia kama wafanyavyo wenzetu wa magharibi.

Hivyo, kwa kujibu swali lako ni kwamba hii ni hatua moja kwenda mbele, na kama ilivyokuwa kwenye blogu yetu ya jamii nahisi nitapata wadau wa kufuata nyayo katika nia ya kuendeleza kile ambacho mie napenda kuita libeneke. Uwanja ni mpana sana mie peke yangu ama na watu kama BC hatuwezi kuujaza. Lazima wapatikane wengi wengine kama inavyojitokeza kwenye blogu. Inanifurahisha sana na kunitia moyo kwamba blogu zinakuwa nyingi. Natumai baada ya muda si mrefu bongotyube zingine pia zitaibuka.

Popote alipo huwa yupo kamili ili kuendeleza libeneke.

BC: Ni miaka kadhaa sasa imepita tangu uanze kublog.Kwa mtu asiyehusika moja kwa moja na mambo ya blogs, anaweza kudhani kwamba pengine ku-blog hakuna changamoto tena hususani akizingatia uzoefu ambao unao.Unakubaliana na mtazamo kama huo? Kama jibu ni hapana,je ni changamoto gani unazokabiliana nazo hivi sasa tofauti na pale ulipoanza kublog?

MICHUZI: Kwangu mimi kwa sasa changamoto kubwa zaidi sio za kiutendaji bali za kuhamasisha wadau wengi wafungue blogu na kuendeleza libeneke. Kama nilivyosema, sie tulio katika fani peke yetu hatutoshelezi. Ukiangalia blogu za wenzetu nje utakuta zina mambo tofauti tofauti na sio ya aina moja tu kama ilivyo sasa blogu zetu za hapa Tanzania. Nashangaa kukuta kwamba magazeti hayana blogu. Wenzetu wa ughaibuni wana blogu kwa kila mada kwenye habari zao, mfano michezo ina blogu yake. Hii inasaidia kufanya wasomaji wachangie na kujisikia wanahusika na hilo gazeti. Wakati umepita kwa wenye magazeti kuandika peke yao na kutegemea wasomaji waishie kusoma tu. Kwa taarifa yako kuna uchunguzi umefanyika mwanzoni mwa mwaka na kugunduliwa kuwa wasomaji hivi sasa ndio wanaoandika sana kuliko waandishi wenyewe kwenye hizo blogu, na kwamba blogu kwenye tovuti ya gazeti husaidia pia kuvuta wasomaji wengi, kwani mijadala inayoendelea huwa burudani na elimu tosha.

Hivyo changamoto niliyonayo ni kujaribu kuiweka ndoto yangu katika hali halisi. Nataka magazeti na stesheni za redion na TV zifungue blogu kwa kila mada kwenye kurasa ama vipindi vyao. Pia kuhamasisha wadau wafungue blogu kwa kufuata fani zao. Mfano wachonga vinyago wawe na blogu zao watuonyeshe kazi zao pamoja na vinyago vyao, nasi tupate fursa ya kuvijadili. Wanamitindo, wanamuziki, hata madereva teksi. Unaonaje tukimpata mtu kama dereva wa daladala ambaye atakuwa na blogu inayoelezea shughuli zake za siku hadi siku. Pamoja na kufaidika kwa kujua kinachoendelea pia hii ni njia rahisi na ya haraka ya kupashana habari.

BC: Mara kwa mara tumekuwa tukishuhudia blogs mbalimbali za watanzania zikianzishwa.Hata hivyo,nyingi miongoni mwa blogs hizo huwa hazidumu.Unakuta blog inaanza leo na keshokutwa inakuwa ishakufa.Kwa uzoefu wako,nini huwa kinasababisha hali hiyo na unatoa ushauri gani kwa wanablog wapya au hata wale wa zamani ambao tunaweza kusema wamezitelekeza blogs zao?

MICHUZI: Mie nachelea kuwalaumu sana wadau wote wa aina hiyo. Wengi huwa ni sababu ya kukosa nyenzo ama muda wa kutosha kuendesha blogu. Wengi wengine ni kuishiwa cha kuweka kwenye blogu, sababu kubwa ni kutaka kuiga ya blogu iliyofanikiwa bila kujua kwamba mwenye nayo huwa ameamua kuwa bloga kwa hali na mali. Hivyo inyeshe ama liwake ni lazima aweke mambo kwenye blogu.

Sasa utakuta mtu akiishiwa cha kuweka kutokana na kutokuwa na aidha ubunifu wa kuendeleza libeneke, hukata tamaa. Lingine kubwa ni kukosa wasomaji ambako wengine hudhani kwamba wingi ama uchache wa maoni ni kupata ama kukosa wasomaji. Hilo ni kosa kubwa. Wadau kutokutoa maoni haimaanishi hawasomi blogu yako. Kwa mfano mimi blogu yetu ya jamii inaonesha kwamba wasomaji wasiotoa maoni ni wengi zadi kuliko wale wanaotoa maoni. Hilo ni funzo ambalo limenipa moyo sana kwani idadi ya wadau inaongezeka hata pale ambapo maoni yanakuwa haba. Tatizo lingine ni kukosekana kwa msisimko kwenye blogu zingine. Utakuta mtu anaposti mambo anayoyataka ama anayoyapenda yeye tu. Hapa pia mfano mwingine ni wa mimi kuchanganya mambo kwenye blogu ya jamii ikiwa ni pamoja na kukaribisha picha, habari na mawazo ama hata mada toka kwa wadau wengine. Hii ni moja ya siri za mafanikio ya blogu ya jamii ambayo kwa sasa siyo yangu tena kwani kila mdau anahisi ni yake pia na ana uhuru nayo kama kwamba ni yeye anayeiendesha. Hivyo ushauri wangu kwa wadau wasome na watafakari kwa makini niliyonena hapo juu, matokeo wataona pale watapoanza kuyatekeleza.

Muonekano wa www.bongotyube.com

BC: Leo hii unapohamia kwenye makazi mapya na pia kuongeza “mwana” mwingine,una ujumbe gani kwa watembeleaji,wachangiaji wa blog yako au wadau kama ambavyo unapenda kuwaita?Watarajie nini?

MICHUZI: Kwanza kabisa naomba hili la kuhamia makazi mengine niliweke sawa. Mie sihami, na blogu itabakia na mtazamo ule ule wa siku zote. Kinachobadilika hapa ni jina la anuani tu. Endapo kama ulikuwa unaipata blogu ya jamii kupitia issamichuzi.blogspot.com sasa utaweza kufanya hivyo kwa kufungua ama kutafuta kwenye google na injini zingine za kusachi kwa kutumia www.michuzi-blog.com. Itapofunguka utakutana na sura ile ile ya blogu ya buluu na kila kitu kinabaki kama kilivyo.

Kinachobadilika katika hiyo ni anuani tu. Pia kwa vile nafasi ya kuweka vitu zaidi kwenye blospot.com ni finyu, nimeamua kuinunulia blogu ya jamii nafasi ama space kubwa sana ambayo itaniwezesha kuweka mapicha na hata video kwa wingi na bila kuwa na wasiwasi wa kujaza space. Na hapa ningependa kuwatonya wana-blogu wote kwamba nafasi ama space kwenye blogu zao zina mwisho na kama mdau atataka aendeleze libeneke bila matatizo anunue space hiyo, vinginevyo itafikiwa wakati atakuta neno ‘you have exceeded your quota, your post cannot be published’. Mie yamenikuta hayo toka mwanzoni mwa mwaka huu na nikanunua nafasi ingine ambayo nayo baada ya kukaribia kujaa nimeona heri ninunue itakayodumu kwa miaka kama mitatu ama minne. Huko mbele ya safari tutajua kifanyike nini endapo kama itajaa tena.

Wadau watarajie mambo mengi zaidi kwa kila tukio, pamoja na video za aina mbalimbali. Mfano hapa BC haya mahojiano wadau wangekuwa wananiona na kunisikia badala ya kusoma maandishi peke yake. Kubwa la wadau kutarajia ni kuendelea kwa libeneke kama kawaida na kwa mapana zaidi. Vile vile watoa mada, habari na maoni wategemee uwanja mpana zaidi kwani space ni ya kutosha kuanzia leo Jumatano saa sita usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Kwenye hiyo www.bongotyube.com wadau watarajie kile walichokuwa hawana kwa muda wote wa historia ya blogu na tovuti za Bongo. Yaani sasa wadau wenye video ambazo wangependa kushea na wengine wajue kwamba mkombozi wao amefika na watajisajili na kuanza ku-posti video za matukio mbalimbali hapo. Hakuna kiingilio wala gharama yoyote, ni bure tu. Hivyo kazi kwao.

BC: Michuzi,tunakutakia kila la kheri.

MICHUZI: BC nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii.

Feedback / Comments

49 Responses to “ISSA MICHUZI NA HATUA MBILI MBELE”

  1. Comment by Pius on July 2nd, 2008 11:43 am

    Hongera kaka Mbele yako nyuma yetu twafata mfano wako.
    SS

  2. Comment by hombiz on July 2nd, 2008 12:34 pm

    Poa-poa kaka!. Endeleza lee-beneke!

  3. Comment by binti-mzuri on July 2nd, 2008 3:32 pm

    wokeei! wokeei!!

  4. Comment by BATTY JULIUS on July 3rd, 2008 2:59 am

    Misupu God bless you kwa kazi unavyo tupasha kupitia blog michuuuu,ahsante kwa mabadiliko na hongera kuli sukuma gurudumu la maendeleo mzee wa kazi Michuzi,ahsante BC

  5. Comment by Edwin Ndaki on July 3rd, 2008 6:44 am

    Kila la kheri kaka misupu(namtania tu)..aa aa lol

    Kazi zake ni nzuri sana.Inshallah Mungu atakusaidia kuzidi kutufuva kundini(mtandaoni) wadau kwa ujumla.

    Hakuna lisilo wezekana..mara blog, mara bongotyube..kesho na kesho kutwa ..utakuwa utaingia umebia na ze bill kwenye “MAIKROSOFTI na MAYAHUU”.

    Tutafika tu

  6. Comment by Azeez Speezo on July 3rd, 2008 6:53 am

    kaka nadhani unadeserve ma-credit ya kutosha, hiyo ni big step ya kutosha. Wakati mwingine huwa tunadhani hatuwezi but akitokea mtu wa mfano utaona wengine wanaibuka walikofichwa.Lakini amini usiamini aliyetangalia katungulia namii nakupa tano za kutosha kwa kuwa pioneer.BIG UP mtu mzima

  7. Comment by Azeez Speezo on July 3rd, 2008 6:53 am

    kaka nadhani unadeserve ma-credit ya kutosha, hiyo ni big step. Wakati mwingine huwa tunadhani hatuwezi but akitokea mtu wa mfano wako utaona wengine wanaibuka walikofichwa.Lakini amini usiamini aliyetangalia katungulia namii nakupa tano za kutosha kwa kuwa pioneer.BIG UP mtu mzima

  8. Comment by Matty on July 3rd, 2008 7:03 am

    fun with ze fulanazzzzzzzzzzz!

  9. Comment by JBigy on July 3rd, 2008 11:10 am

    Vizuri sana bro michuzi. Fanya makamuz kama kawa kwani sisi tupo pamoja nawe. Ila mbona habari za ndumba bungeni huwa hutwambii na mambo mengine nyeti ya huko?ama bado unayafanyia upembuzi yakinifu?

  10. Comment by Msema on July 3rd, 2008 12:13 pm

    Hii! kaka Michuzi bab kubwa,
    mungu akuzidishie uwezo zaidi na zaidi
    Daima mbele tu

  11. Comment by Ndume on July 3rd, 2008 3:33 pm

    Michu, hiyo Laptop kuiweka karibu na makao makuu nasikia hwa inaharibu network, please!

  12. Comment by P. S. Nalitolela on July 3rd, 2008 11:47 pm

    hongera Nanihii wa tegeta kwa hatua mpya uliyochukua na nakutakia kila la heri katika kuendeleza libeneke.
    Pia nashukuru kwa ushauri wako kwa wanablog wote walianza na kupotea kiaina; ni ushauri mzuri sana na natumai utahamasisha wadau wengi zaidi kuendeleza libeneke.

  13. Comment by ScArEcRoW on July 4th, 2008 1:43 am

    Ze tishet….
    Tangulia na si tunafuata.
    There ain’t a day which passes by without me opening the michu blog na siku ikatokea nimeshindwa basi huwa nakosa raha!

  14. Comment by Leloo on July 4th, 2008 2:35 am

    Michuzi………… “hongera sana ” kwa kuwa mjamii halisi!

    Ila mimi nimekuwa nawaza au nahisi kuwa the next thing you were going to do is to have a “DATING SITE BONGO”

    Na hasa baada ya kuona kiu ya wadau wengi iliyojitokeza siku za usoni pale kijiweni kwako hadi ikabidi kupiga marufuku.

    Ni ukweli usiopingika kuwa Bongo sasa tunahitaji sana Dating site. maisha yameshakuwa capitalised in such a way hata muda wa watu kutafuta wenza hakuna kwa sababu most of the time wako makazini. Lakini kwa kuwa kazi nyingi hufanyika kwa kutumia computer, ni rahisi kumpata mwenza hapohapo kwenye computer.Sie wengine tuko huku nje lakini tunapenda tuoe nyumbani, tunaporudi tunajikuta hatujui tuanzie wapi.

    Ushauri binafsi:
    Anzisha Dating site ya kulipia, ili kama mtu yuko serious alipie aweze kupata access. na unaweza kufanya kazi na mabenki ili uwe linked kwenye ATM’s kuweza kulipia, na pia Credit cards kwa wale walioko nje. Na mtu lazima alete picha na vielelezo vya kuonesha kuwa yuko serious .
    Nakuhakikishia kuwa hii itakuwa very successful.

  15. Comment by masumbuka on July 9th, 2008 9:38 am

    Hapa Mzee wa Konooooooz unatumia Internet kuvulia samaki au?

  16. Comment by mkandawile on July 10th, 2008 8:53 am

    Michuuz vipi ndugu yangu, Blogu yako imeingiliwa na Popo au vipi? ‘Wakubwa wamechukia nini? Hebu tupashe ukweli wa mambo Mze wa Bongo Celebrity! This is a Family, so we need to know whats up ili ‘Technical Team’ yetu ianze Kazi mara moja.

  17. Comment by Maseri on August 4th, 2008 9:13 am

    Shega, but punguza ubishoooooooooooooooooooooooo

  18. Comment by mimi on August 5th, 2008 10:30 am

    eeeeeeeeeeh baba na we unafikaga maeneo haya?

  19. Comment by AD on August 15th, 2008 8:25 am

    HUONEKANI KAKA? KULIKONI AU NDO MAMBO YA ZAKA AU FUNGU LA KUMI?

  20. Comment by joe on September 14th, 2008 3:14 pm

    kaka naona mambo yako sio mchezo

  21. Comment by silvesta saile on December 18th, 2008 9:43 am

    hongola sana kaka issamichuzi kwaku elimisha wa2

  22. Comment by silvesta saile on December 18th, 2008 9:46 am

    nime fulahi sana kufika kwako magu
    kwe2 ongola sana broo
    fanya kazi kwa mkono
    wamungu broo
    au ww wasemaje

  23. Comment by joe on January 13th, 2009 4:13 pm

    mambo yako ni makubwa ,hongera

  24. Comment by Nadhifa Mshindo on May 25th, 2009 12:14 am

    michuzi mimi mdau wa Australia bado nakupa hongera nyingi sana kwa kutupa habari na mambo yote yanavyokwenda huko home. asante na hongera sana

  25. Comment by febby on May 25th, 2009 9:38 am

    kaka sikuhizi tunachelewa sana kupata habari au ni vekesheni zimezidi?

  26. Comment by kulunge on July 14th, 2009 12:23 pm

    POA KAKA KAZA MSULI ENDELEA KUTUPASHA HAYO NDIO MAMBO YANAYOTAKIWA ACHANA ANAMAFISADI WATAKIONA SIKU YA KIAMA

  27. Comment by Comment by Mzuka Mtanange on September 14th, 2009 12:22 am

    Mambo ni vipi mwana yani mzuka hata huku bundasliga tunakupata kaza buti mwana kazi njema

  28. Comment by BUYAMBA B on January 21st, 2010 12:54 am

    Kaka hongera kwa hatua hiyo.Mara zote mapinduzi ya kweli yanaletwa na jasiri mmoja mwenye moyo wa dhati.

    Tuko pamoja.

  29. Comment by Hellen kiraya on January 22nd, 2010 8:27 am

    Hellow michuzi.yani kaka unatubamba sana mtu wetu, so nivizuri uendelee hivyo hivyo…….Tunaomba undelee kuturusha tu.

  30. Comment by job on February 4th, 2010 11:42 pm

    Thank you bro, and big up mie ughaibuni nafarijika sana ninapopata habari za home

  31. Comment by alex on April 29th, 2010 10:00 pm

    Mambo yako safi, habari zako zipo shwari na si za majungu hongera sana

  32. Comment by lucy on May 3rd, 2010 6:30 am

    Kaka u’v gone to school! Big up!

  33. Comment by Oscar on May 15 2010 on May 14th, 2010 2:41 am

    Big up Bro, na kaza boot, aim a football fan esp (Arsenal FC)I advise you to up date masuala ya michezo you ‘ll get many viewrs michezo ya Bongo and Ughaibuni.

  34. Comment by Oscar on May 15 2010 on May 14th, 2010 2:59 am

    Big up Bro kwa kazi yako na ikubali. i would like to advise you kuwa unatupa up dates za michezo ya ki Bongo Na Ughaibuni, i think U ‘ll get many viwers.

  35. Comment by issa on June 19th, 2010 10:24 am

    yeah thats good men, wqe realy enjoy it kip it up

  36. Comment by R. Msangi on August 28th, 2010 9:57 am

    Big up men, tunakukubali!

  37. Comment by angel on September 20th, 2010 10:18 am

    weeeeeeeeeeeeeeeeraaaaaaa!kakaaaa big up………mwaaaaaaaa lv u!

  38. Comment by SHABANI KESSY on October 30th, 2010 10:53 am

    tunakubali kazi zako mkubwa

  39. Comment by eddy dembwe on December 16th, 2010 1:44 am

    TUNATAKA WANAHARAKATI KAMA WW BROO.MUNGU AWE PAMOJA NAWE!BIGUP!

  40. Comment by mary D. on January 24th, 2011 10:21 am

    Hongera issa kwa kutupaatia habari nyeti zinazojiri mikoa yote ya TZ kaza buti kaka wengine wavivu kusoma magazeti tunategemea news from you uko juuuuuuuuuuuuuuu?

  41. Comment by mary on April 8th, 2011 5:33 am

    uko juuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!

  42. Comment by ladyjulykitaly on May 9th, 2011 11:31 pm

    mybrohterukojuukamamlima”KILIMANJARO”kaziyakoinakubalikakwapandezote.
    bigupmybother

  43. Comment by ladyjulykitaly on May 9th, 2011 11:35 pm

    WEWEKAKAWAUKWELI,KAZIINAELEWEKA,USHARABAROHAUNAWALANINI,HILONENOBABA………..KUBALITU…

    WA
    UKWELI
    2011

  44. Comment by lucas john on May 12th, 2011 12:25 pm

    kaka mimi nakuliza .hivi kuna habari yoyote kuhusu dawa ya babu loliondo.matokeo yake .tunatafuta sana kujuwa wizara ya afya inasemaje .ni kweri hii dawa inatibu ngomaaa

  45. Comment by EMMANUEL EDWARD on June 3rd, 2011 4:32 am

    mimi ni msanifu majengo(architect) nina penda sana sanaa ya movie kwani ninapopata ugumu katika kazi yangu huwa naangalia movie na pia mimi ni msanii wa movie sasa ninachoomba unisaidie ni kuwa kule marekani kuna wacheza movie kama sisi yaani wa marekani weusi sasa mbona movie zao zina msisimko kuliko za hapa ni wapi tunakosea wabongo?

  46. Comment by JANETH RIDI on July 7th, 2011 4:43 am

    songa mbele tunakupongeza sana na mungu aendelee kukupa afya njema na akulinde na mabaya yote uendelee kutupa habari uko juuuuuuuuuu.

  47. Comment by THOMAS WATELE on November 1st, 2011 4:47 am

    Kaka mambo haya makubwa si mchezo BIG UP MAN.

  48. Comment by Ally A Njiku on November 24th, 2011 11:28 am

    big up kaka,uko juu sana.kila la kheri!

  49. Comment by Beka waukweli on February 7th, 2012 12:29 pm

    Kaza but kaka..wanao bana washindweeeeee…upo juuuuuuuuuu!!!!!

Leave a Reply