Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini (Bongofleva), Khalid Mohamed maarufu kama T.I.D leo amehukumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kupatikana na hatia ya kushambulia na kujeruhi.

T.I.D mwenye miaka 26 alisomewa adhabu yake hiyo na Hakimu Hamisa Kalombola wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne walioletwa mahakamani na upande wa mashitaka.

Baada ya kusikiliza ushahidi huo, ndipo Hakimu Kalombola alisema ushahidi uliotolewa na mashahidi hao wanne ulithibitisha mtuhumiwa kufanya kosa hilo na hivyo Mahakama inamtia hatiani kwa kosa hilo. Kwa habari zaidi bonyeza hapa.

Feedback / Comments

59 Responses to “TID AHUKUMIWA KWENDA JELA MWAKA MMOJA”

  1. Comment by any on July 23rd, 2008 2:12 pm

    POLE MWENZETU! mwaka mmoja si mbali utamaliza tu! ukirudi jichimbie maskani uchape zako kazi.
    Huyu kaka ni mzuri! anafanana na basketballer mmoja Francis alikuwaga ROCKET na kina Yao Ming! ni mzuri kwa mtazamo wangu. wengine wanaweza mwona sivyo!

  2. Comment by michelle on July 23rd, 2008 2:25 pm

    Kwa kweli ni kijana mwenye uwezo mzuri ktk fani hii ya muziki, sasa sijui nisemeje, basi akitoka huko itabidi asinywe tena na hasa kama ana kichwa cha kuku. Pole TID

  3. Comment by Angeline on July 23rd, 2008 3:47 pm

    NO!

  4. Comment by warda on July 23rd, 2008 4:19 pm

    kila la heri mungu atakusaidia kikubwa fanya ibada 2.

  5. Comment by Dunda Galden on July 23rd, 2008 4:21 pm

    Nimeshutushwa na habari hii ni mwezi mmoja toka tuongee kwenye simu kwa kazi za musiki na maisha najua ana kesi lakini hakuna alietegemea itakuwa hivi pole sana T.I.D pole sana bi mkubwa
    ,,,ndio hivyo sheria haina jinsi nakuombea mungu na niwakati wa kujipanga ukiwa uko wala si wakati mawazo mengi hilo limepangwa na mungu.na amini kipaji kitapanda zaidi
    Chai goda

  6. Comment by Ed on July 23rd, 2008 5:05 pm

    Being celebrity doesn’t means your immune to rule of law. However, the punishment seems to be rediculous and unfair. It is my believe that TID had the super attorney like Maira in his portfolio.

    Vingenevyo, that should be example kwa so called Bongo celebrity kwamba jela is always an option for stupid people who decides to bend the law for their own political correctness.

  7. Comment by hombiz on July 23rd, 2008 6:45 pm

    Mafisadi nao watafungwa!? Ama segelea {magereza} ni ya wenzangu na mie tu!?. Sheria za Bongo sitaziita msumeno mpaka nione mafisadi nao wanakwenda gerezani. La sivyo sheria za BONGO nitaziita ni-”nusu meno!”

  8. Comment by E-The Great on July 24th, 2008 1:55 am

    Its lyk Do or Die!,Ur Thug Man!,utamaliza mtu wetu then Street kama kawa

  9. Comment by hash on July 24th, 2008 1:58 am

    du! mwana mungu awe nawe. ukitoka, toka na mawe yako sasa.

  10. Comment by Chris on July 24th, 2008 2:34 am

    Ndo uzuri wa sheria, ni msumeno na haingalii uwezo wa mtu, social status, kama ni celebrity etc…. though kama alivyosema hombiz mafisadi nao inabidi siku ya siku wafungwe! I am sorry for the fella! Japo ni funzo kwa celebrities wengine who may misbahave kwa sababu ya u-spoon walio kuwa nao mitaani!

    Mwaka mmoja hauwezi zima ndoto zako TID. Always aim high and head up!

  11. Comment by Pearl on July 24th, 2008 2:36 am

    namuunga mkono hombiz,TID amemjeruhi mtanzania mmoja na kapewa adhabu hiyo ili iwe fundisho,je hao ambao wanaiba pesa za watanania wote kweli wao hawastahili hukumu kwa vile ni waheshimiwa!!!!?????
    Kweli inasikitisha sana hakuna haki kabisa hapa tunapotezeana muda,yale makubwa yanayofanywa na vigogo wanayanyamazia lakini yanayofanywa na hawa kajambanani ndo wanajua kua kuna sheria.
    mi nasikitika sana.

  12. Comment by kekue on July 24th, 2008 2:41 am

    Maskini dah!! pole sn mkubwa, hiyo yote ni madhara ya pombe; pombe sio chai jamani, waacheni kina masele ndo fani zao ss wewe ukijiingiza kichwa kichwa ndo hayo ss…… lkn am sure ukirudi lzm utakuwa na single nyingi sn maisha ya huko yalivyo so ni sawa na unaenda kutafuta jinsi nyengine ya kutoka. Pole sn…..

  13. Comment by zedu on July 24th, 2008 3:38 am

    Huyu mtoto kazi yake nzuri.ila hili ni fundisho kwa wengine wenye nyodo kama yeye.Aisee amini usiamini labda kama hujawahi kuchanganyika naye huyu jamaa ana Nyodo ni balaa Swala kama hili angeweza kulimaliza ata kifamilia tu;watch out

  14. Comment by juma mhando on July 24th, 2008 4:10 am

    siamini kama umeungana na familia ya babu seya! Inauma sana kusikia unaenda selo.

    Naomba wanamuziki tujifunze tusije ishia wote gerezani.

    Tuache nyodo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    haya kila la heri kwa mapumziko yakujitakia ndugu yangu!!!!!!!

  15. Comment by debra on July 24th, 2008 5:12 am

    Mhhhh letz bounce jamani!!
    Pole sana….
    Siku hazigandi katunge mashairi na kina babu seya na papiii….
    Daaah….mtu wangu pole sana…
    One love,pamoJAH!

  16. Comment by mambo on July 24th, 2008 5:45 am

    Nampongeza hakimu aliyekuhumu maana hajaangalia sura kwani wasanii wa bongo mkipata mafanikio kidogo mnajiona kama mpo juu ya sheria.Ningekuwa mimi ndio hakimu ninge hakikisha nakuchapa mvua za kutosha ili uwe mfano na fundisho kwa wenzio kama ni pombe watu wangapi tunakunywa pombe hatufanyi vurugu au hiyo unatokunywa wewe ikoje?

  17. Comment by majidai on July 24th, 2008 5:47 am

    waswahili wanasema ,siku unayopanda kwenye gari na shing mia ndo siku ambayo konda anakwambia nauli ni shing 150.mi nahisi labda jamaa ana mikosi, mbona akina kalapina na dudubaya kila siku wanapiga watu lakini hawapati matatizo kama hayo.

  18. Comment by Matty on July 24th, 2008 6:44 am

    My God!….pole sana Kijana sina haja ya kuhukumu hapa ila Mungu atakusaidia na kama nchi hii inafata haki basi wakamatwe kwanza wazee wa vijisenti ndipo kieleweke!!!

  19. Comment by MICKEY JOHN AMOS - DENMARK on July 24th, 2008 6:54 am

    I am against any sort of Violence, and It`s right for the JUSTICE to take it`s cause for the sake of Law & Order for our youths in the society.

    At the same time, we have to accept as human beings once in a while we do unexpected wrong doings and regret when it`s too late.

    In this case of TID as one of the very few entertainer who succesfully achieve A TANZANIAN DREAM as Supper Star, expected to be a good example for our New Generation rather than create a non-mercy Violence to the public.

    In my utmost advise to the “System of Law” is to give TID a second chance and not to be put away for such long time, it might be not a good solution.

    He should save Probationary out-doors sentance and work “FREE” without salary to our Institutions of Orphans & Street Poor Children in Music and Good Behavior for the goodness of our Future Genaration.

    mickey@mail-online.dk
    COPENHAGEN

  20. Comment by Monica on July 24th, 2008 7:09 am

    Mimi binafsi nimesikitishwa sana na hukumu hiyo kwani kuna watu walioua, majambazi sugu na hata mafisadi wao wanapeta tu mitaani iwe hiyo kujeruhi mtu ambaye bado anapumua!!! Huko ni kukomoana tu kwa nini asingepewa option mbili, ya kufungwa ama kulipa faini! Kosa dogo kama hilo unamfunga mtu mwaka mmoja jela ili akajifunze nini huko? Pole sana TID. Nawaomba wadau wa music wakishirikiana na familia yake watafute wakili na wakate rufaa ili haki itendeke.

  21. Comment by Kisu KIkali on July 24th, 2008 8:38 am

    Hii!habari inanisikitisha sana! na kunitoa machozi,
    Ninachowaomba wasanii ni kwamba muwe waangalifu
    sana! kwani nyinyi ni jicho la jamii
    ukifanya kosa hata liwe dogo basi wenye hasira watatumia
    mkondo wa sheria kama kigezo cha kuwaangamiza……
    Na sheria wanasema ni msumeno …lakini mara nyingine
    utumika kama upepo wa kuzima taa au mshumaa unao
    waka

  22. Comment by Gervas on July 24th, 2008 8:41 am

    Hivi mmesahau kwamba magereza yamejengwa kwa ajili ya masikini na walala hoi. Chunguza popote pale walio gerezani asilimia 90 ni masikini, wenye matatizo ya kisaikolojia, wagonjwa. Siku zote mvunja sheria huwa ni mlala hoi, masikini.

  23. Comment by Edwin NDAKI on July 24th, 2008 9:39 am

    TID pole sana kwa yaliyokusibu.

    Nakumbuka kwenye game achilia mbali “feat” ulizopiga ila kwenye ZEZE hapo walio wengi ndio walianza kukuelewa vema ingawa safari ilianzia mmbali zaidi.

    Akaja TID “sauti ya dhahabu” naona ilifanya vema …Mashabiki walizidi kudata achilia mbali “kazi za nje” mafanikinio makubwa zaidi.

    Kama kuagana hatimaye ukaja na TOP BAND..”Nyota yako” ilizidi kung’aa.Leo hii hatimaye yamatokea maswahiba inabdi uende chuo cha mafunzo-SEGEREA.

    Pole sana kwa ibirisi aliyekuvagaa ukaamua “kumtid” huyo kibosile…si unajua TID nchi ilisha uzwa ungekuwa umemdunda MATTY,GERVAS au EDO ungeweza kulipoza soo ila kwa sasa hao wenye “vijisenti” wanakuwa na nguvu…check wazee wa ufisadi wametuumiza watanzania milioni zaidi ya 36 ..ila bado wapo road wanakula bata tu.

    Pole TID …usijilaumu sana kwa yalitokea tumia muda huo vema ili ukitoka uwashike zaidi kwe game.

    Wengine wajivunze pia kwa hili kuwa hakuna aliye juu ya sheria..tuepuke kuchukua sheria mkononi bora tuzichukue sheria kwenye “begi”
    pole TID..TUTAFIKA TU

  24. Comment by any on July 24th, 2008 9:39 am

    Ivi watu wote wanaopiganaga lazima waishie jela! mbona Dudubaya alimpiga Mr. Nice jukwaani, ivi nae alifungwaga?

  25. Comment by Malenga on July 24th, 2008 12:03 pm

    Kweli sheria ni msumeno,unakata mbele na……

  26. Comment by hombiz on July 24th, 2008 2:17 pm

    Gervas sikubaliani na wewe kuwa sheria popote pale ni kwa wanyoge. Marekani swala kama hilo halipo. Sheria za U.S.A. ni msumeno kwa kila mtu. Mtu akibainika kuwa ni kweli ametenda kosa, basi atahukumiwa kulingana na kosa alilotenda. Magereza ya Marekani yana wauza unga, majambazi, wanyang`anyi, matapeli, watu maarufu kama wacheza sinema(Wesley Snipes-kwa kukwepa kulipa kodi,Paris Hilton-violating her probation), wanamuziki(marehemu 2pac,Lil’ Kim n.k.), na hata wanasiasa wakubwa kabisa kama ma-governor!(George Ryan-for corruption), hata maraisi nao hubanwa na kujiuzuri kwa mfano Richard Nixon.
    Nimeonyesha mifano michache tu hapo juu. Lakini nikisema niwaandike watu maarufu na wanasiasa waliotumia nyadhifa zao vibaya na kuishia kwenye mkondo wa sheria ambayo “NI MSUMENO WA KWELI”- siwezi kuwamaliza hii leo.
    Hivyo basi, sheria za BONGO nazo siwezi kuziheshimu mpaka pale zitakapotumika kama inavyopaswa kwa kila mtanzania bila kujali cheo, mali, sifa, jinsia, dini, wala mjuano! Mpaka hapo hilo litakapotendeka (hasa kwa mafisadi) ndipo nitakapoita sheria za BONGO ni msumeno. Ila kwa sasa bado naziita ni “nusu meno!”

  27. Comment by ghsdlfhsd on July 24th, 2008 3:51 pm

    Hivi TID alimdunda yule Ben Mashiba aliyekuwaga body guard wa rais au Mashiba gani??? maana kama ni yule, TID akicheza ataongezewa muda jela. Awaulize wenzie kina babu seya. hIYO sio nchi ya kuishi. Na mimi ndio sirudo ng’o. Bora nikae zangu hukuhuku nioshe vyoo vya wadhungu lakini mwisho wa mwezi nalipwa kuliko mfanya kazi mwenye cheo kikubwa tu serikalini.

  28. Comment by Ignorant on July 24th, 2008 5:29 pm

    Inaelekea TID alitaka kuonyeshana ubabe na huyo victim wake (am afraid, TID has now become the victim). Sawa naamini kujeruhi ni kosa kisheria lakini ukiwa makini na mjanja unaweza kumaliza suala hili nje ya mahakama.

    Kuna fundisho tunapata hapa, aidha TID alidharau kosa alilofanya au alitaka kuendelea kuonyesha ubabe kwa mjeruhiwa. Haingilii akilini kua alikosa mwanasheria mzuri katika hili. Tunapaswa kutambua kua pombe ni kwa ajili ya burudani na wala sio mapigano.

  29. Comment by michelle on July 24th, 2008 5:45 pm

    Wanamuonea wivu tu,dudubaya hukuchukuliwa hatua yoyote, na hao mafisadi wa mali za nchi mbona wao hawafungwi?

  30. Comment by Pearl on July 25th, 2008 2:18 am

    mzee Mandela walimuweka gerezani wakidhani atafia huko badala yake alitoka na akawa ndo rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini.
    TID utatoka tu hivi i vijimambo.

  31. Comment by george on July 25th, 2008 2:22 am

    kwenye hili ninadhani tid alichemsha,ni swala ambalo alitakiwa kulimaliza nje ya mahakama,sasa kutokana na jeuri ya kuoneshana ubabe ndiyo maana imefikia hapa,pole sana kaka,sheria ni msumeno>>>>>>>>>

  32. Comment by Mtanzania on July 25th, 2008 2:42 am

    Mimi si mwanasheria,hivyo upeo wangu wa sheria ni mdogo sana.
    Ninaomba wanasheria wanisaidie kunijibu kwa nini TID hakupewa option ya faini, kama angeshidwa ndio angepelekwa jela huo mwaka mmoja, ukizingatia jela zetu zina msongamano watu waliofungwa kutokana na kesi kama hizi ambazo wanaweza kulipa faini.
    Wapo watu wengi ambao wanakuwa na kesi za namna ya TID lakini wanapewa option ya fine.
    Wanasheria naomba kujifunza,
    Mtanzania.

  33. Comment by trii on July 25th, 2008 3:08 am

    sheria za tz zimegawanyika sehemu 2 wengine wapo juu ya sheria wengine wakina sisi tupo chini ya sheria,fanya kosa uone cha mtema kuni,kufa haufi lakini cha moto utakiona.sijasema TID kafanya vizuri,kweli ni kosa lkn hii sheria upo juu yake tuuu?labda hiki kipengele kilicho muhukum kimetungwa juzi juzi.wengine walipo fanya makosa hakikuwepo?what to say.

  34. Comment by kingo on July 25th, 2008 4:21 am

    we majidai,kina kalapina na ze dudu wanapiga walalahoi wenzao ndo mana wanapeta.yani aliejeruhiwa hawezi hata kununua karatasi ya kuandikia maelezo achilia mbali kukodi gari la kwenda kumkamatia mtuhumiwa!sasa TID kamdunda mtoto wa “fisadi” we ulitegemea nini?waliahidi kumnyoosha na wameweza.mi namuombea tu amalize kifungo salama aje atuonyeshe walichotunga yeye na papii.

  35. Comment by Mheshimiwa mmoja hivi on July 25th, 2008 6:02 am

    Nimesoma mawazo na michango ya watu mbali mbali na nimeheshimu mawazo yao kwani kila mtu ana uhuru wa kueleza kile anachokiamini nisahihi..mimi nikiwa kama mtanzania nimesikitika kitendo cha TID kufungwa ila lazima tukumbuke sheria ziliwekwa ili kutuongoza tuishi kwa kuheshimiana la sivyo tungeishi kama wanyama.Naomba ikumbukwe hakuna kosa dogo..kosa ni kosa na kama sheria inasema kosa fulani adhabu yake ni jela au faini huo ni uamuzi wa Jaji ila vyote vinakubalika.Tatizo la Watanzania wengi ni kudharau vitu na kuona kila kiti ni kidogo ..kosa la kumpiga na kumjeruhi mtu ni kubwa kwa kuwa unakuwa ummemvunjia mtu haki yake.Tatizo la TID ni kujiona yeye no Bora kuliko wengine ndio mana alidhani anaweza kuvunja sheria na asiguswe..wapo wanaosema mbona Dudu baya na Kalapina..inawezekana wao ni wenye busara mara baada ya kufanya kosa labda hujishusha na kujaribu kutatua tatizo..TId kwa kuwa yeye anajiona bora labda alidharau na hakuona haja ya kumaliza swala hilo kiungwana..Kwa kuwa kukosea ni ubinadamu na vidole havifanani basi labda Khaleed Mohamed (TID) yeye kapata fursa ya kujifunza kupitia njia ngumu(through the hard way).Mwisho kama TID angekuwa ni mtu wa kujifunza angejifunza siku nyingi TId ana kesi nyingi tu..mara kachukua fedha za onyesha Tanga hajatokea..mara kaharibu mali..sasa unapokuwa na kesi za namna hii kuli kukicha hiyo ni dalili kuwa kuna tatizo na unatakiwa ushtuke usingizini ulitatue ukiendelea kudharau mwisho wake ndio huo unajifunza kupitia mazingira magumu.
    Pombe siyo kigezo tena hicho ni kisingizio kisicho faa mana starehe zako binafsi zisiingiliane na uhuru na haki za watu wengine..
    Hivyo TID ajikaze..yatakwisha ingawa Jela siyo sehemu nzuri hata kidogo..baaada ya Miezi 6 atakuwa nje..Maisha ni kama kioo..ukiyachekea nayo yanacheka..people should to respect each other and conduct themselves in any manner which is appropriate regardless of Colour,Gender,Class..
    Thanx

  36. Comment by iryn on July 25th, 2008 6:29 am

    wadau wa TID pliz do something fot this.Ukifatilia kwa makini kuna kitu kimejificha kuamzia kwa ben mashiba mpaka kwa hakimu. kwanza kwa case yake hakupewa option ya fine rather than kupelekwa moja kwa moja selo. kuna kitu kinachoendelea tulichofichwa kuna mkono wa mtu behind all this.kwani kwa ugomvi uliotokea sio wa kumfikisha TID hapo kama ulishuhudia.Pliz do something for TID and wote wanaomtegemea for their daily life.Watanzanie tupendane na Tusigandamizane kwa wivu usio na maana.He realy dont deserve that punshment. pliz kateni rufaa

  37. Comment by vince on July 26th, 2008 4:23 am

    maneno aliyoyatoa kuomba huruma ya mahakama inadhihirisha hakutafuta huduma ya wanasheria,acheni dharau na ubahili.
    Hao wenziwake wawaone mawakili ili waweze ona uwezekano wa kukata rufaa wamtoe huyo jailbird!

  38. Comment by EDWARD ALEX MKWELELE on July 26th, 2008 11:05 am

    The judge was very right if the evidences shown that he was guilty of the offence he committed, we have to put our record straight that to be a super star, a famous does not warrant somebody to be above the laws, we must reject bad cultures of the music industry and embrace those which are good ones, let us not immitating everythings other people doing across the pond, that is the way they are, not us, let us embrace our modest culture of love and peace, when misunderstanding happens we must strive to reconcile without a bloodshed. He has to pay the price, in other countries that is the end of him even his fan base would have rejected him no matter how good he is that’s it, even now he has already put himself in troubled position, he has criminal record, it will very extremely hard for him to get a visa for any country for his shows, he must forget about the like of USA, UK and most Western countries due to that record(CV) he has got.
    LIWE FUNDISHO KWA WOTE TULIOBAKI.

  39. Comment by MapigoSaba on July 26th, 2008 4:14 pm

    kuna uchaguzi wa adhabu mbili, kufungo na faini. kama TID angejutia kosa lake na kuomba kusamehewa nadhani angehukumiwa kulipa faini.

  40. Comment by Majita on July 26th, 2008 9:44 pm

    Naamini wakati hakimu anasoma hukumu alimalizia kwa maneno yafuatayo “…kuwa unaweza kukata rufaa ndani ya siku 30 kama hukuridhika na huku hiyo…..” So bado TID anawewza kufanya kitu kwa ajili ya plan two.
    Hivi ingekuwa kweli wewe TID amekukong’oli na kukujeruhi ungefanyaje vile?? Zingatia kosa ni “KUJERUHI” na siyo “SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI” au “SHAMBULIO LILETALO MADHARA MWILINI”.Nijuavyo mimi maana ya kujeruhi kisheria ni kitu kizito kidogo so tuwe fair kwa pande zote.
    Otherwise pole sana TID mimi mwenyewe nakuonea huruma na ni mpenzi wa miziki yako japo siku moja ulivulumisha pale Jackies na tukamaliia gemu billyards.Unatakiwa upunguze ubabe kidooogo.

  41. Comment by queen on July 27th, 2008 6:39 pm

    pole kijana, tumikia adhabu yako na ujifunze kutokana na makosa wala huna haja ya kukata rufaa, umekosa kwa wajibu wa sheria kukata rufaa ni kutaka kuleta uzuri au umaarufu wenzio walikata rufaa wakajikuta wanaongezewa adhabu. ridhika na adhabu kwani wewe ni nani hata usifungwe?hakuna kulaumu wala huruma ila kila mtu ajifunze.umetenda kosa , ridhika na adhabu,tumikia adhabu na ukome kurudia kosa.nakutakia kifungo chema, sahahu raha za uraiani na jiunge na maisha mapya yenye kila aina ya ubaya,mateso, uonevu,shida na ukosefu wa uhuru wako mwenyewe.Mungu atakulinda utamaliza kifungo .byeeee!

  42. Comment by Dadi on July 27th, 2008 11:55 pm

    Adhabu aliyaopata bwana mdogo ni haki yake anayostahili maana mbali na kupanda chati ya misic pia alipanda chati ya juu zaidi katika uhuni. Unapotangaza uhuni wako katika maeneo ya starehe ukumbuke kuwa kuna watu wa aina mbalimbali wenye heshima zao, Nadhani ulistahili kufungwa siku nyingi kwa makosa yaliyotangulia “it was just a matter of time”
    Umejitakia mwenyewe, demu uliyetaka mwonyesha kuwa una misuli anaendelea na life yake wakati wewe unajutia huko segerea ………… Mambo ya kijinga saaaanaaa! That’s a proper lesson learnt kwa maflava wengine!
    Ukiwa msanii uelewe maana halisi ya sehemu za starehe na sio uwe mstari wa mbele kubadili maana halisi ya sehemu hizo na kuzigeuza kuwa sehemu za za kuonyesha uhuni wako

    Na wewe Pearl usimfananishe TIJ na Mandela ebo!! Usitushefue hapa. Fikiria kabla a kuandika ujumbe wako

  43. Comment by sally on July 28th, 2008 10:15 am

    Ndo isha tokea kama kahukumiwa kihalali basi maliza kifungo TID

  44. Comment by kindo on July 28th, 2008 10:25 am

    Mtizamo wangu ni kuwa TID alihitaji sana huduma ya wakili ili aweze kumuongoza kuhusu suala hili. Nadhani hata ushahidi wake haukuwa imara sana kwasababu hakuongozwa na wakili. Na bahati mbaya sana hakuwa na shahidi mwingine. Wakili angeweza hata kumshauri awasiliane na mlalamikaji ili walimalize jambo hili nje ya mahakama. muda wa mwaka mmoja ulikuwa unatosha kuweza kufanya mazungumzo na mlalamikaji. Kama ingeshindikana basi ijulikane wazi juhudi zimefanywa lakini mlalamikaji amekataa. lakini Pesa ambayo atapoteza akiwa lupango ingetosha kabisa kuweka Wakili na huenda angeweza kupata huduma hiyo bure kwani mashabiki wake ni wengi na nadhani mawakili hawakosekani.

  45. Comment by doctor on July 28th, 2008 1:50 pm

    mi nilijua iko siku tu huyu dogo atayakanyaga,maana mtoto alishajifanya michael jackson wa kino.maana supastaa yeye bondia yeye mtoto wa mama yeye,milionea yeye almradi taabu tu.alivyompiga jamaa mi nilidhani kidume kahukumiwa anazirai hahaaa poleeee.sasa nenda wakakuwoweee mpk ukome na huko ndo hizo ngumi utapigana vizuri.mahakimu wa kibongo sikuzingine hawakosei,na usikute alimletea nyodo hata huyo hakimu mwenyewe.

  46. Comment by Pearl on July 29th, 2008 2:29 am

    Dadi # 42 TIJ ni nani!!!???? hapo hukufikiri kabla ya kuandika.
    Halafu huna haja ya kujishushia hadhi kwa kuandika comment kutumia maneno makali,learn to address issues in a courtesy way,people will respect you.
    Kingine jifunze kuelewa kitu kwa mapana zaidi,nimemtumia Mandela kama case study,nadhani umeelewa ninaposema case study.

  47. Comment by Matty on July 29th, 2008 5:13 am

    To you Dadi,
    Mbona unahasira namna hiyo???kwani aliyepigwa ni demu?au kaka? au ni mwanao??pls msaada tutani!

  48. Comment by juma mhando on July 29th, 2008 7:33 am

    nakata rufaa ya hukumu ya TID.

    ANASTAHILI MIAKA MITATU HAKIMU KAMPENDELEA.

    ANA NYODO SANA HUYO KIJANA.

    NASUBIRI ARUDI MTAANI NIMFUNGULIEGE KESI!!!!!!!!!!!!

  49. Comment by mimmy on July 29th, 2008 10:31 am

    Ewe Mwenyezimungu naomba umlinde TID na mabaya yote yatokeyayo jela ili aje atoke salama akiwa na afya yake inshAllah!

    TID kafanya kosa la kibinadamu na kapewa adhabu kuuubwa sana, ila kosa limetendeka hukumu imetolewa ilobaki ni kumwomba tu Mungu pamoja na yy mwenyewe.

    fanya ibada TID, Mungu ni tajiri wa kila kitu,

    inaniuma saana kufungwa kwa TID wallah

  50. Comment by Frateline on July 29th, 2008 11:58 am

    Pole kijana, Maisha ni safari, mtegemee mungu ktk kipindi kigumu cha mpito mwaka mmoja sio mwingi hata shida na maadui zako watahaibika siku ya siku, Muombee adui yako aishi siku nyingi ili utakapo barikiwa yeye macho yamtoke, pole sana, nimesikitika sana maana nilikuwa napenda huyu kijana anavyojituma ktk sanaa, pole sana, nimekumbuka Katibu mkuu wa TFF wa zamani Adeni Rage akikaa gerezani na baadaye alikuja shida kesi, usijali kijana kijahidi na tunza maisha yako huko gerezani usiruhusu mtu kukufanyia ushenzi maana nilisoma gazeti kuwa umegombaniwa, nawaomba BC kwa kuonyesha kujali print haya maoni yetu mplekee huko gerezani yampe faraja. TID ni mmoja wa Celebrity wa Bongo.

  51. Comment by EDWARD on July 29th, 2008 9:08 pm

    HIZI COMMENTS NI BURUDANI TOSHA NIMESOMA ZOTE NIMECHEKA KARIBU NI-PASS OUT/NIZIMIE.

  52. Comment by Matty on July 30th, 2008 7:28 am

    Juma Mhando, wewe wasema!!
    unasahau kuwa sote ni binadamu na kila mmoja wetu ana mapungufu yake, ana nyodo ni sawa simtetei hata mimi nina nyodo vilevile na wewe unanyodo vile vile sema tu zinatofautiana.
    U guys, muacheni kijana wa watu awe na nyodo asiwe nazo ni yeye kwani ukisema utakata rufaa hakimu amuongezee kifungo who care???au unajifurahisha nafsi yako??? ni wangapi wananyodo hapa chini ya jua na wanaishi??? Tunachozungumzia hapa ni kwamba hakupewa 2choice that is another option kama kulipa faini na kama angeshindwa basi anastahili hicho kifungo!
    Dudu Baya alipompiga Mr. Nice nchi nzima ilijua lakini kwanini hakufungwa??/do u know that Mr. Nice alimfungulia mashtaka mshkaji na soo liliisha???
    Hapa kuna kitu kimejificha chini ya carpet na tunastahili kujua thats all!
    TID uwe ulilewa hukulewa is up to you to learn through mistake!! na mimi nasisitiza maneno ya FRATELINE THAT PRAY TO GOD YR ENEMIES LIVE LONG LIFE SO THAT WEN GOD BLESSED HE/SHE CAN SEE BY HER/HIS EYES!.

  53. Comment by any on July 30th, 2008 11:05 am

    Hamkuwepo kwenye TUKIO so u guys dont know what happened before. The guy isnt crazy hakutoka tu atokako akamrushia mwenzie ash tray! inaama kulikuwa na kutoelewana au aliambiwa kitu ambacho hakuridhika nacho, plus wheat nyingi kwenye bia ilimfanya awe haipa kidogo ndio akajikuta kafanya ambacho hakutakiwa kufanya! acheni kuhukumu wakati hakimu alishafanya kazi yake, khaa. watu wana chuki binafsi ati angestahili kuongezewa miaka! pole yenu mlikuwa wapi wakati wenzenu wanasoma LAW! Nyie mkwepe umande sasa ivi ndio mko busy kumsaidia hakimu kuongeza muda wa kifungo! ndio maana hamjaitwa mahakimu, rudini kwenye fani zenu mkachape kazi, na wenye kubeba box twendeni zetu sie tukawahi box tusikae kupoteza muda apa kumsaidia hakimu kazi yake, chaaa!

  54. Comment by binti-mzuri on July 30th, 2008 11:49 am

    jela noma…namuonea huruma.daaaaaaaah!!!!!

  55. Comment by binti-mzuri on July 30th, 2008 12:11 pm

    pearl no. 46 TIJ = TOP IN JAIL = TID

  56. Comment by side on August 2nd, 2008 10:14 am

    Pole sana,Ila wasanii wengine msome kutoka kwa TID,Kua star sio sababu ya kufanya kitu unachotaka hata kama ni kinyume cha sheria.Jitahidi kufanya ibada na naamini Mungu atakusaidia na kukusamehe.

  57. Comment by polisi on August 6th, 2008 2:50 am

    Hatufanyagi mchezo na sheria kabisa.nilipojiunga humu niliwataarifu kwamba lazima niweke disprini humo. ila jamaa ni mshakaji wangu sana. but he’s ignorant sometimes.let him learn a lesson.
    Pole mwana. itakusmbazia juve ukiwa hukohuko.

    Chias.

  58. Comment by Amina on September 24th, 2008 9:18 am

    huyu mshkaji ananyodo sana saizi yake..naskia mahakamani alikua najibu kizungu hahahhah

  59. Comment by ANNA MTATE on November 12th, 2008 3:30 am

    HATATI YA URUMA MPENI POLE

Leave a Reply