Irene Sanga(kushoto) akiwa jukwaani na Elidadi Msangi.

Kama ikitokea ukawa umechoshwa na kusikiliza nyimbo au miziki inayoelemea upande mmoja tu(mara nyingi upande wa mapenzi) basi hutojutia kubadilisha frequency na kusikiliza wimbo uitwao Salamu Zangu ukiwa ni utunzi mahiri wa msanii Irene Sanga ambaye ameuimba wimbo huo kwa kuwashirikisha msanii maarufu wa mashairi,Mrisho Mpoto na Elidadi Msangi. Salamu Zangu ni mojawapo ya vibao ambavyo vilitokea kupendwa sana nchini Tanzania na kimebakia kuwa gumzo mpaka hivi leo.

Akiongea na BC hivi karibuni, Irene Sanga,alisema aliamua kutunga au kuandika mashairi kama unavyoweza kuyasikia katika wimbo huu,baada ya kukerwa na jinsi ambavyo wasanii wengi wa muziki wanavyokuwa wameegemea zaidi upande wa nyimbo za kimapenzi peke yake na hivyo kusahau kabisa pande zingine za maisha ya jamii kwa mfano umasikini,uonevu nk.Kwake yeye,anasema, muziki au sanaa sio chombo cha kuburudisha tu bali kuonya,kukosoa,kukumbusha nk.

Mshairi Mrisho Mpoto akituma Salamu zake kwa mjomba.

Wimbo huu umo ndani ya albamu iitwayo “Utandawazi” ambayo Irene anasema bado hajaamua kuitoa rasmi sokoni kutokana na sababu mbalimbali.Nyimbo zingine ndani ya albamu hiyo ni kama vile Utandawazi(inayobeba jina la albamu), Pangisheni,Maureen,Usivunje,Ndoto,Afrika Yote na huu Salamu Zangu/Salamu kwa Mjomba.Albamu hiyo imetengenezwa ndani ya Mawingu Studio jijini Dar-es-salaam.

Wimbo huu ambao leo ndio unatupa burudani ya wiki ni ombi rasmi kutoka kwa Pius Mikongoti.Pata Burudani.Wikiendi Njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Picha zote na Bob Sankofa.

Be Sociable, Share!

Feedback / Comments

39 Responses to “SALAMU ZANGU-IRENE SANGA ft MRISHO MPOTO na ELIDADI MSANGI”

 1. Comment by any on July 24th, 2008 9:20 pm

  EEh, haya bwana, personal decision nyingine, haya wee.

 2. Comment by Salamu zangu kwako Mjomba « Spoti na Starehe on July 25th, 2008 12:11 am

  […] Blog ya Bongo Celebrity kama kawaida ijumaa hukupatia wimbo mmoja kwa ajili ya kukupoza na mchakamchaka wa weekend nzima, weekend hii wamekuja na kibao Salamu Zangu tokakwake Irene Sanga akimshirikisha Mrisho mpoto na Elidadi Msangi ikiwa ni ombi langu rasmi, Bofya hapa […]

 3. Comment by Pearl on July 25th, 2008 2:24 am

  mashavu ya MPOTO tu ndo huwa yananiacha nimechoka.

 4. Comment by Edwin Ndaki on July 25th, 2008 4:07 am

  Hapa sasa leo kwa mara nyingi mutima wangu umeburudika sana.

  Kuna kipindi wimbo ulileta utata kwamba nani mtunzi wa songi.Ila kwa tuliojua ukweli tuliendelea kuamini kuwa mashairikatunga Irine.

  ´Gervas na Matty yaani kwenye wimbo huu napenda pale “pa shoka hapaingii kisu”

  Any,Michelle,Angelina,Dinah,Warda,Dunda Galden,Ed Hombizi,Hans …nyie nawapa hii..”mkifunga mkanda matanga yataisha upesi”.

  Chris,Pearl,mtoto mzuri,mama wa kichaga,kekue,Lina…”pepo haina maana pasipokuwepo jehanamu…”

  Debra swahiba..najua tumetanganishwa na ukuta..lakini pokea salamu zangu…

  BC nanyie..vibwaya..mviweke hadharani tucheze ngoma zetu wanazosema ni za kishenzi…a aaaa

  Dinah..”visima vya kale havifukiwi” umeidaka hiyo…

  hizo ni salaama zangu kwa wadau wote wa BC..

  maneno mengi haya jengi ghorofa.

  salaaaaam zangu kwanu eee heeeee..ijumaa tamu watu wangu.

  tutafika tu..nawapenda sana

 5. Comment by Mkwaya on July 25th, 2008 4:36 am

  Mi namkubali sana Irene na Mrisho.. wamekaa na kufikiri sio kama wasanii wettu wa ubongo wa fleva…
  Mkipta za Maembe tafadhali mziweke maana hawa vijana wamekaa chini wakafikiri…

 6. Comment by Matty on July 25th, 2008 5:02 am

  Any, haya mambo ni kama Ngonjera kimtindo ..ila huyu dada ni black byute!!!!

 7. Comment by mambo on July 25th, 2008 5:03 am

  Nawapa bg up bwana mpoto na irene nyimbo zenu zina nigusa sana hasa ule wa watoto yatima wa njombe nyimbo zenu ni za ki Tanzania sana mnastahili pongezi sana kwa hilo maana wasanii wengi wenye majina makubwa wana copy nyimbo za wamarekani kwa kuzitafsiri kama zilivyo na wengine kuishia kuiba hata mashairi na melody nchi za jirani.Ongezeni ubunifu zaidi tuendelee kupata vitu halisi kutoka kwetu.

 8. Comment by BabyGirl on July 25th, 2008 6:02 am

  Aisee hii nyimbo huwa inanikuna sana Maneno yake
  Hivi kweli viongozi wetu huwa wanasikiliza kweli huu wimbo na kama wanasikiliza halafu hawafuatilii kweli vichwa vyao vimejaa Uwendawazimu.

  Anyway Ndio Bongo yetu hiyo.

 9. Comment by Dunda Galden on July 25th, 2008 6:07 am

  Salam zimefika mjomba BC
  mwimbo mzuri wenye ujumbe unaoendana na nyakati
  Mrisho songa mjomba salam zitawafikia wahusika
  (Taja magogo yote la mbuyu si la mvule)
  ( Lisilo kuwasha haujailmba)
  (Wamulike mapolisi wanaohukumu kwa makofi kabla hakimu hajasoma hukumu)
  Inabidi uwe makini pindi unapisikiliza salam.huu mwimbo utasikilizwa kwa miaka mingi ijayo na utakuwa unamgusa kila mtu,(SIKUFUNDISHI MJOMBA HIZI NI SALAM ZANGU)
  Chafosa mwana wa pangu pakavu

 10. Comment by michelle on July 25th, 2008 12:23 pm

  Hii ndo nyimbo sasa, so mapenzi na viuno tuuuuuuuuu tumechoka bwana

 11. Comment by warda on July 25th, 2008 1:00 pm

  MRISHO MPOTO HAYO MAJASHO NA HIZO RASTA HATARI KWELKWEL.ANY WAY NDIO MAMBO YA BURUDANI HAYO.

 12. Comment by mzee msuya B on July 25th, 2008 9:16 pm

  sikiliza vyombo,halafu mashairi! hawa kweli ni wanamuziki.
  Huu ni muziki hata mimi mzee nausililiza sana.

 13. Comment by GEORGE on July 26th, 2008 3:15 am

  Shem Irene nakupa shavu.Endelea kuwapa somo wajomba.
  Vipi ile sinema yako umekwisha anza kuiuza rasmi.

 14. Comment by Pearl on July 28th, 2008 2:35 am

  Edwin Ndaki salaam zako nimezipata fresh.

 15. Comment by Matty on July 28th, 2008 2:54 am

  E.Ndaki…thanks God wknd ilikuwa njema upande wangu….natumaini ilikuwa njema kwa wana BC wote!! pamoja na BC wenyewe!
  Jamani na mimi nataka kuweka rasta kichwani kuna anayejua niaje kwenye suala la usafi????pls msaada tutani!

 16. Comment by any on July 28th, 2008 9:08 pm

  Wimbo na yeye wanatofauti kubwa sana. Ni mtazamo! Matty hizi salam anapewa nani? Huyo mjomba asiposikia tena basi bwana.

 17. Comment by kekue on July 29th, 2008 4:24 am

  Jamani hizo rasta du!! Matty ni hizo za rasta hapo zimekuvutia mpaka unataka na ww zikutembelee au nini? Nashukuru kwa salam mzee wa tutafika tu.

 18. Comment by Matty on July 29th, 2008 4:56 am

  hahahaahahhaaah Any mjomba asiposikia hata shangazi pia atazipokea kwa niana nadhani hiyo huwaga imo!
  Any sasa mbona hujasema kitu kuhusu rasta???msaada tutani pls au na wewe ni mgeni wa hayo mambo?

 19. Comment by Matty on July 29th, 2008 5:01 am

  heee!! hapo juu ulimi hauna mfupa (niana = niaba)

 20. Comment by Ras Uhuru on July 29th, 2008 7:45 am

  Mashairi yametuliia hasa,kazi nzuri sana Mpoto.
  Ni mashairi ya kuaamsha akili za wananchi.
  Na kuwaonya na kuwakosaa walaji wachache wa taifa letu.
  Enough Respect!

 21. Comment by any on July 29th, 2008 2:42 pm

  matty sasa unamwingilia personal decision zake, mi hizo nywele na mashavu are not my cup of tea! ila bado inabakia kuwa personal decision yake! haaa,
  alafu alivopozi apo kwenye picha kama anachungulia, au kama ana usongo fulani! eeeh. wenye kujua luha za picha waje waseme.

 22. Comment by Matty on July 30th, 2008 7:36 am

  Kekuu unajua mimi nywele zangu za asili not reachable kabisa sasa nataka nitest hii staili ya rasta may be nitafanikiwa, maana mambo ya kalikiti na mawiving yamenichosha, ikishindikana basi nitaenda miss universe styl.
  Any huyu kaka anaonekana kama hana mazoezi ndo maana shavu dodo namna hii!

 23. Comment by Dunda Golden on July 30th, 2008 8:10 am

  Edwin Ndaki salam zimefika mjomba
  Lakin majanga yanapozidi roho uwota kutu

 24. Comment by binti-mzuri on July 30th, 2008 11:42 am

  Edwin ndaki nimekupata sawia..ila mie sio mtoto mzuri,ni binti mzuri kaka…nshavunja nanihiii

 25. Comment by any on August 2nd, 2008 12:15 am

  Unene nauhusishaga na uzembe kwenye kila kitu! sasa sijui apa nisemeje! mazoezi basi hata ya kukaza misuli ya mashavu! shavu inamwaika mtoto bado mdogo, khaa.

 26. Comment by trii on August 7th, 2008 2:31 am

  Any-umenifurahisha.kweli yana waka waka,hayo mashavu kwa kufichia nyama ukiiba kwenye sufuria ndo yenyewe.mama hawezi kugundua.

 27. Comment by Amina on September 24th, 2008 8:07 am

  haya kilichowafanya muanze kugombana kuhusu huu wimbo ni nini?

 28. Comment by robert jusatine on March 12th, 2009 3:14 am

  mpoto big up mjomba nyimbo zako zimetulia sasa album yako inaitwaje na nitaipataje mpoto mjomba namba 2 imetulia tunataka kukuchangia nauli uende sasa

 29. Comment by rweza on May 10th, 2009 7:21 am

  shukurani kwa ujumbe huu
  am congolese but i speak swahili
  ningependa pia salam hizi zimufikie mjomba wangu kabila

 30. Comment by KARUNGI on January 21st, 2010 5:23 am

  hongera sana mjomba kwa kuibuka mshindi mwaka 2009 nakutakia kila laheri kwa mwaka2010

 31. Comment by remigius venant on January 22nd, 2010 3:06 am

  hongera mjomba kwa kuamasisha uongoz bora tupe nyimbo ya uchaguz 2010

 32. Comment by J.KIIMBILA . on January 23rd, 2010 4:47 am

  Nawakubali tangu nilipoanza kusikiliza nyimbo zenu . sina shaka salamu zilifika maana kila kitu kiko kwenye wimbo huu . Upungufu ktk uongozi ukome sasa tunaelekea uchaguzi . Palilia ss tofauti utavuna magugu . Kila raheri wajomba na shangazi wote .

 33. Comment by RSWEDI on January 25th, 2010 6:05 am

  MY SELF I RESPECT THE SONG AND THE WAY HEY THINGS ALL THE BEST

 34. Comment by yusam on January 28th, 2010 7:13 am

  nakukubali mkubwa uko juu sana yaaani weni mkali kazi buti mkubwa wala usilegeze waaache mbali kama ulivyoowaacha zidisha juhuudi mkubwa nanakukubali mkuuu mashabiki wako tupo tunasubili vitu vipya.unatisha ilembayaaaaaaaaaa big up mkubwaaaaa

 35. Comment by happy charles on March 2nd, 2010 4:35 am

  yaani mnatisha jamii inawakubali si mchezo kazeni buti, kazi yenu mzuri sana.

 36. Comment by jomba on March 4th, 2010 1:09 pm

  safi sana,maneno ya kweli kabisa

 37. Comment by JK on March 30th, 2010 1:23 am

  kitu kimetulia salaam zimefika hata kama mjomba hataki kuzipokea,wimbo huu hautachuja kwa sababu ndimo tuishimo humo salam ziwafikie

 38. Comment by pamavis1 on April 23rd, 2010 8:55 am

  nakukubali sana ireen sanga, hasa unapokua jukwaani, hiyo sauti yako na makeke yako katika kulitumia jukwaa.ningepennda kujua website yako

 39. Comment by Kioo kwa ccm na jk salaam zako mjomba jk na ccm. on September 25th, 2010 4:41 pm

  […] tunaiweza kuipata kwa lugha nyepesi hapa. http://www.youtube.com/watch?v=FUSnN…eature=related SALAMU ZANGU-IRENE SANGA ft MRISHO MPOTO na ELIDADI MSANGI – BongoCelebrity http://www.youtube.com/watch?v=RpPf2…eature=related Reply With […]

Leave a Reply