Jina lake kamili ni Godfrey Tumaini. Kwa wengi anajulikana kama “Dudu Baya”. Ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao waliwahi kutamba na kujipatia umaarufu ingawa mara kwa mara amekuwa akiandamwa na sifa ya ‘ugomvi’ jambo ambalo ni vigumu kulithibitisha bila kusikia pande mbili za shilingi.
Albamu yake ya kwanza aliitoa mwaka 2000 na aliipa jina la Siku ya Kufa Kwangu. Mwaka mmoja baadaye yaani 2001 alitoa albamu nyingine iliyokwenda kwa jina Amri Kumi Za Mungu. Hiyo ilifuatiwa na albamu ya Mpangaji mwaka 2002 kabla ya Papo Kwa Hapo mwaka 2003 na kisha Kiwango mwaka 2005. Mwaka 2006 alifyatua albamu aliyoiita Manundu.
Kwa muda sasa Dudu Baya amekuwa kimya kidogo katika mfufululizo wake wa kufyatua albamu mpya takribani kila mwaka.Miongoni mwa nyimbo zake zinazofahamika zaidi ni ule wa “Nakupenda Tu”. Unaweza kuutizama wimbo huo kwa kubonyeza hapa.
Photo/Global Publishers.
Feedback / Comments
7 Responses to “DUDU BAYA”
Leave a Reply


Huyu Jamaa anaimbaga fresh,naupenda ule wimbo “NAKUPENDA MPENZI USIOPENDA CHAPAAA…HALAAAAA BABYYYYYY” aliomshirikisha Vivian (RIP VIVIAN & COMPLEX) ila sasa anatalent nyingine ambayo ni kuarest wenzake a.k.a mkono mtu!!
mbona hajamjoin TID!
mi sina hata la kusema ila mi namjua zaidi kama mtu mpenda ugomvi.
tentementeeee …. i loveee that song
The dudubaya ni kijana mzuri tu, tena nakumbuka alikuwa Mseminaristi kule Makoko-Musoma. The dudu yeye ana sifa moja bwana mtu akijipendekeza kwake anampa manundu tu basi. He is not a violent guy anyway. Walianza kuimba nakumbuka na bwana Edwin Ndaki enzi hizo…ukwayani.
Ngumi mkononi that why people call dudu baya
ukileta shobo la uzushi chapa ngumi kisawasawa
maana baadhi ya wabongo kuna wengine wanapenda
kujishembendua wanapoona watu
kula tano Tumaini
chaigoda
mi namjua huyu jamaa hakawii kuku chenjia..dar skendo baby hallllaaaa