Jina lake kamili ni Robert Gathecha Mongi.Wengi hivi leo tunamtambua kama Bobby.Bila shaka kabisa,Bobby ni miongoni mwa wasimamizi mahiri wa shughuli(MC),watangazaji wa radio na televisheni ambao Tanzania ya leo inaweza kujivunia.Awe anasimamia shughuli,radioni au kwenye televisheni ukimsikiliza utagundua jambo moja;anaipenda kazi yake na anaifanya kwa umakini na utulivu wa hali ya juu.Pengine utulivu huo ndio uliomfanya awe ni mtangazaji wa kutegemewa katika vituo mbalimbali vya radio nchini Tanzania na pia msimamizi wa shughuli zenye hadhi za kimataifa.
Pamoja na mafanikio na “soko” ambalo tayari alikuwa ameshajitengenezea,hivi karibuni alifanya uamuzi mgumu wa kuamua kurudi shuleni ili kunoa zaidi kipaji alichonacho.Hivi sasa anasoma katika Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini.Mbali na kuamua kurudi shule,Bobby ndio kwanza alikuwa “amepata jiko” kabla ya kuwa baba mapema baadaye.Mchanganyiko huo wa mambo ndio unaotufanya tuuite uamuzi wake wa kurudi shule kuwa mgumu!How is he handling all these?
Hivi karibuni tulipata nafasi ya kuzungumza naye machache kuhusiana na maisha yake,shule,ndoto zake na mengineyo mengi.Je anasemaje kuhusu Afrika Kusini anaposomea hivi sasa?Anasomea nini?Nini ushauri wake kwa vijana wanaoota kila siku kwenda “bondeni”?Anazungumziaje maendeleo ya muziki na filamu ya Tanzania akilinganisha na Afrika Kusini? Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;
BC: Bobby,karibu sana ndani ya BC.Tunafurahi kupata fursa hii ya kufanya nawe mahojiano.
BOBBY: Niwashukuru nyie BC kwa kunipatia mimi fursa hii ya kipekee.
BC: Kwanza kabisa hongera sana kwa mambo kadhaa uliyofanikisha hivi karibuni.Tunajua umeoa hivi karibuni,umepata mtoto na sasa umerudi tena shuleni.Mambo yanakwendaje katika maeneo yote hayo matatu?Unasomea nini hivi sasa?
BOBBY: Namshukuru Mungu kwa kunijalia mwenza anayenifaa na pia mtoto wa kiume mwenye afya njema aitwaye Ethan Patrick. Kwa sasa ninasoma katika Chuo Kikuu cha Cape Town nchini South Africa, ninachukua BA in Film and Media Production.

Bobby pamoja na mkewe Helena Mkonyi(now Mrs.R.G.Mongi) siku ya harusi yao.
BC: Ilikuwaje ukaingia kwenye fani ya utangazaji na mambo yote ambayo umekuwa ukiyafanya hususani upande wa burudani?
BOBBY: Kwa upande wa burudani hili ni jambo ambalo lilikuwa likinifurahisha tangu utotoni. Nilianza kutambua kipaji changu nilipokuwa Umbwe High School( I think you remember the Mawenzi concert…you did a Bob Marley Song….) that is when I first realised what I want to do later on life, if not personally be the one entertaining then at least be part of the whole entertaining process.

Proud Father.
BC: Ni kwanini umeamua kurudi tena darasani hata baada ya kuwa umeshajitokeza kama mmojawapo miongoni mwa Djs na MCs mahiri kabisa nchini Tanzania?Je ulikuwa uamuzi mgumu sana kufikia?
BOBBY: Ukweli ni kwamba kipaji peke yake hakitoshi haswa kama ni mtu mwenye falsafa za kiharakati za kuleta mabadiliko katika maisha ya mtanzania kama mwafrika. Fani ya media nchini imekuwa kwa kasi sana lakini taaluma yenyewe bado haijafikia viwango vya kiushindani.Wapo wadau wachache mno wenye uwezo wa kufanya kazi zitakazoweza kushindana kimataifa lakini sio wengi kama inavyotakiwa na ndio maana nikaamua kurudi masomoni. Kingine ni kwamba sikupata bahati ya kufahamu chuo kinachotoa elimu katika fani ya filamu hapa nchini, kama vipo haviingii ndani zaidi kitaaluma ndio maana nikachagua kuja kusoma South Africa.
MC: Kama DJ,MC,TV personality nk ndani ya Tanzania utakuwa umekuwa ukifuatilia maendeleo ya sanaa na maonyesho kama vile kwenye muziki,filamu nk.Unaweza kuyaongelea vipi mabadiliko mbalimbali ambayo umekuwa ukiyashuhudia?Na sasa ukilinganisha kidogo na Afrika Kusini ulipo,unadhani tupo wapi katika medani za kimataifa?
BOBBY: Fani ya muziki ni fani ambayo naweza nikasema ndio inayopeperusha bendera ya Tanzania kisanaa. Vijana wanafanya kazi kama vile hawataamka kesho.Guys are working very hard and have created a trade mark for Tanzania as the Hip Hop/Rap Hub of East Africa.
Kwenye sanaa ya filamu, hatua za mchakamchaka ndio zinaanza kuchanganya, licha ya kwamba kuna mengi ya kuboreshwa najivunia kusema ya kwamba sasa hivi watanzania sio waoga kujaribu vitu vipya japo kuwa wakati mwingine unaweza ukahisi wadau wa fani hii wanataka kuiga mtindo wa Nigeria. Ushauri wangu ni kwamba, tusitizame ushindani wa Nigeria tu, tujiandae kushindana na watengeneza filamu wa duniani kote, haswa nikizungumzia lugha na ubora wa picha na sauti zinazotumiwa kwenye filamu zetu. Mifano yakutizama na kushindana nayo iwe Bollywood na Hollywood.Tukiweza wafikia hao then mwendo utakuwa ni wa mbio za kasi na sio mchakamchaka kama sasa. Mfano mzuri ni music videos za Bongo mbona quality inafaa hata kimataifa?
Kiujumla lakini, hatua na mwendo uliopo ndio wenyewe. Ndio kwanza tumeanza, dunia inapaswa kuogopa kwani Bongo ndio inapanda sasa. Inapendeza kuona pia ya kwamba hivi sasa wameanza kutoa tuzo kwa ajili ya filamu za kitanzania, hii itakuwa changamoto kubwa kwa sanaa hii huko tunakoenda.Ila ufisadi na uswahili usiingizwe humu tu!
BC: Ni wanamuziki gani wa barani Afrika wanaokuvutia?Una sababu zozote?
BOBBY: Wapo wengi sana ila ningependa kuwataja kwa mtiririko huu, Uganda, Kenya, Tanzania na South Africa. Hawa ni Bebe Cool, Nameless, Profesa J na HHP. Sababu zangu kuu ni kwa sababu kazi zao siku zote haziyumbi bali huboreshwa siku hadi siku.Wametoka mbali mno mpaka wamefika walipo, wamejitunzia heshima zao na wanaheshimu walipotoka. Kwa ufupi” these are hustlaz who made it big and are still humble!”
BC: Ni jambo gani ambalo unaweza kusema huwa unalihofia zaidi unapokuwa unasimamia shughuli au kwa maneno ya kigeni unapokuwa Master of Ceremony?
BOBBY: Kwangu mimi kuna sheria moja tu, uoga ni neno ambalo halipo kwenye kamusi yangu. Ila kama ushauri, ni muhimu mtu kuwa na utulivu kwanza, kujua utakachokisema na kwa mtirirko upi.Kuwa na mbinu mbadala endapo hitilafu yeyote itatokea ukiwa jukwaani na kama ni muoga wa halaiki basi usiwatazame usoni bali uwa tazame vitosi vyao haswa vile vya waliosimama nyuma kuliko wote.Kwa kufanya hivi utakuwa hauwatizami machoni lakini utaonekana kuwa unajiamini na kuwatazama wao.

Bobby(kushoto) akiwa na MC mwenzake Jokate Mwegelo katika usimamizi wa shughuli.As he puts it,confidence matters.
BC: Ni jambo gani unalolihofia zaidi maishani mwako?
BOBBY: Ninachokihofia kuliko vyote duniani ni kifo kusema kweli. Sio kuogopa kufa bali kuhofia kifo chenyewe. Nadhani ukiwa na wale uwapendao hupendi utengane nao na hilo wazo tu la kutengana… nalihofia mno!
BC: Umeshakaa Afrika Kusini kwa muda sasa.Miezi michache iliyopita paliibuka vurugu zinazotokana na baadhi ya wa-Afrika Kusini kudai kwamba wageni wanawachukulia kazi zao na nafasi zao za kuendelea.Unadhani hiyo inatokana na nini?
BOBBY: Hili jambo ni la kisiasa mno lakini kwa ufupi ukweli ni kwamba wenzetu walipata taabu sana wakati wa Apartheid na hii iliwaathiri kwa kila namna lakini haswa kitaaluma na kisaikolojia.Haya tunayoyaona ni matunda au madhara ya utawala huo.
BC: Labda kwa mtu ambaye hajawahi kufika Afrika Kusini,unaweza kumuelezea vipi kwa kifupi kuhusu nchi hiyo ambayo katika siku za hivi karibuni imetokea kuwa kimbilio la waafrika wengi katika kutafuta riziki na maslahi?
BOBBY: Ni nchi yenye maendeleo mazuri ukizungumzia infrastructure lakini kama mtu hana shughuli maalum kule sishauri mtu akajitosa kwenda kutafuta riziki kule kwani Bongo kuna mengi yakufanya na riziki imejaa tele. Kama ni biashara ya kihalali sawa, masomo sawa, kuhamia na kufanya kazi endapo utaipata sawa kwa sababu uchumi mzuri sana lakini kujilipua au kuzamia….ohoooo mbona utasota!! Wapo wengi tunaowaona huku.

Bobby(wa pili kutokea kulia) akiwa na marafiki zake,wanafunzi wenzake,U of Cape Town,Afrika Kusini.Kila la kheri Bobby!
BC: Mwisho ungependa kutoa ushauri gani kwa vijana wenzako kuhusiana na suala zima la maisha?
BOBBY: Kusema kweli maisha hayana formula ila binafsi ninayo ya kwangu ambayo ni….. mwogope Mungu, ogopa UKIMWI, chapa kazi / jitume, heshimu watu, tenda mema nenda zako……the rest leave it to God.
BC: Asante kwa muda wako Bobby.Tunakutakia kila la kheri katika masomo yako na pia familia.
BOBBY: Thanks BC.
Feedback / Comments
27 Responses to “SALAMU ZA BOBBY KUTOKA SOUTH AFRICA”
Leave a Reply













Congratulation for your decision,I wish you all the best in your studies.Msisitzo dedicate your love to your family,daima ukifanya hivyo hautaiangusha.
Boby kaka nakuaminia wewe ni mpiganaji na nakutakia kila la kheri…lkn kuvaa hereni sijapenda, haijakaa vema mkubwa…tenda wema nenda zako.
I used to be in the same school with this guy back in the day.
Jamaa ana bidii sana. He’s a very hard worker. Cool composed and focused.
Vipindi vyake hua wanaonesha sana hapa uingereza. Good luck in all ur future endevours kaka.
Nakutakia kila la kheri katika masomo yako huko S. Africa. Nakuomba kuwa makini siku zote, wakumbuke mke na mtoto wako na uwapende siku zote. Best wishes Bobby.
mmmm.. anavutia..yum!
kama hajaoa,mwambie anidipu..namba yangu ile ileee
kila la kheri kijana. Elimu ndio yenyewe!
Personal decision hadi Moshi, bora liende.
Keep it up kaka kwa kuangalia shule.
wakumbuke mke na mwanao! mafisi maji wa kisauzi wasikufanye ukawasahau, na ivi unavutia, usumbufu utakuwa mwingi sana i am sure.
The Daddy..inakuwaje?
Muda mrefu sana mkuu tangu kwenye viunga vya Knyama.
Kila la kheri kitabu chema…
hongera kwa kurudi shule, nakutakia mafanikio mema kijana soma, elimu ni ufunguo baba
kashaoa na ana familia hereni za nini sasa? aachane na ujana. la sivyo mafisimaji hawatamuacha.
mh! wife nae bomba kwa kweli! ila personal decision yako sikioni sijaipenda maana kwa wenye ufahamu potofu ndo kama vile..
hahahahahah Binti mzuri unaomba akudip? au akubeep?ila nimekuelewa lakini tatizo ni kwamba labda kama hukuona picha ya ndoana hapo juu akiwa na asali wake wa moyo!
We unaejiita binti mzuri hujatulia…we ni fisi maji. Usikimbilie kutoa maoni bila kusoma habari. Boby ameoa na ana mtoto, ukiangalia picha ya juu yupo na mkewe na nyingine kambeba mtoto. Wewe unaombwa akubeep ili iweje??? nyie ndo wadogo usoni mnaihifadhi wazee wetu…sijui ni dhiki au utamaa au mnaanika njaa tu.
Nadhani hii itakuwa mara ya 20 au zaidi nawalaumu BC kuhusu maswali mnayouliza. The question doesn’t tell much.
I am sorry, but hii interview nilikuwa na skip every few line. Muandishi umetunyima utamu kama kawaida.
Ed wewe utakuwa mbeya sana.Ulitaka BC aulize maswali gani zaidi?Sio kila interview inayofanyika lazima iulize kila swali duniani.Unawalaumu unawalaumu…kwanini usianzishe na wewe blog yako ukauliza hayo maswali yako?BC endeleeni hivyo hivyo..mnajua mnachofanya na watu kama Ed wanajua hilo isipokuwa basi tu…watu wengine bwana!
matttyyy sio anibeep…anidipppp…unakua ka huelewi..
nyamihela mi mbona najijua siku nyingi,hahaha. ila si wezi kukwambia kwa bahati mbaya kwanini naomba anidip,coz hayakuhusu
Congrats bwana kaka kwa kufanikisha matukio mbali mbali katika maisha ya binadamu by the way niko curious na huyu jamaa ama nitakuwa namfananisha or something kwa wale wanaomjua watanisaidia nilisoma na mtu kama huyu arusha secondary school o level miaka hio je ni yeye kweli? Kama kuna mtu anamjua pls nisaidieni
hahahahahahahahahaha! yaani watu wengine bwana hata jokes zinachukuliwa serious? sms derively!
Binti -mzuri hadipik huyo shosti kashanyakuliwa!
any #7 inawezekana wewe unaona ana mvuto ila mwingine asione kama wewe.
Bobby piga shule.
Dah i can see u bobby looking fab as ussual, naipenda sauti yako halafu ngeli unaiweza si mchezokumbe uko huko Cape Town University
Hello Mongi!!!
Im totally agree with u what matters in life is professionalis…piga shule mwana nakuamini wewe ni mpiganaji and for that after getting married and being a father u really nid to fight 4 the gud life of u as well as ya family….God bless ya sana and i believe u can make it and gets what ur looking for….Pamoja kaka.
Hello Mongi!!!
Im totally agree with u what matters in life is professionalism …piga shule mwana nakuamini wewe ni mpiganaji and for that after getting married and being a father u really nid to fight 4 the gud life of u as well as ya family….God bless ya sana and i believe u can make it and gets what ur looking for….Pamoja kaka.
Safi sana. Mke mzuriii
Pearl #17, ni kweli mi ananivutia machoni, sijui kwa vile mchaga mwenzangu, maana definition za uzuri kule Moshi ndio kama mnavomwona apo! wengine wasipomwona mzuri nako ni sawa, maana macho tunayo na yanaona na ku judge tofauti! peace Pearl.
matty ndugu yangu,watu si unawajua tenaa… hawatulii mpaka binti-mzuri apayuke payuke aonekane mwehu
nimekupata any,kwahiyo dimpozi kidogo nini basi wasichana na moshi wanajigonga wenyewe.
yeap pearl,. tudimples na kichwa mduara moshi ndio zetu! watu watagongana kukugombania! ila sasa kwa wamarekani wanaume wenye sura hizo wanahusishwa na mambo flani kizenji zenji, if u know what i mean. hahaha
Bobby,mambo vipi?
I real miss your shows here.Kumbe uko South Africa.Thanks BC kwa kutujulisha alipo huyu jamaa.Maliza shule urudi bwana..usije bakia huko SA