Kama kawaida,e-mails na ujumbe kupitia sehemu ya maoni zimetufikia kutoka kwa “wadau’ mbalimbali wakitaka kujua ni kwanini hawaipati blog ya Muhidin Issa Michuzi.Tumewasiliana naye na ametujulisha kwamba blog yake imekumbwa na tatizo la kiufundi ambalo hivi sasa anahangaika kulirekebisha.Tatizo lipo kwa upande wa host wa blog yake(blogger=google).Tatizo wanalijua na wanalishughulikia.Anaangalia pia uwezekano wa kubadilisha host ili mambo yaendelee kuwa mazuri kama ilivyokuwa.
Pia ameomba kuwatoa shaka baadhi ya wasomaji au waulizaji ambao walikuwa wanahisi labda kuna “ufisadi” umefanyika kuiondoa hewani blog yake.Anasema hakuna kitu kama hicho.Wakati huo huo,huku akisubiri mambo yarejee,hivi sasa anaendeleza libeneke kupitia pale kwenye uwanja mpana wa Daily News.Bonyeza hapa ili uone pamoja na mambo mengine,jinsi Watoto wa Jangwani,Yanga, walivyoepushwa na kifungo cha miaka miwili.Haki imetendeka sasa,taratibu zilipindishwa!
Feedback / Comments
7 Responses to “MICHUZI YUPO,ATAREJEA PUNDE”
Leave a Reply


sending...
Akhsanteni BC maana nilishaanza kuumia roho na nusu kukata tamaa ya kuitia machoni blog yangu niipendayo,ninavyompenda michuzi acha kabisa,kabla sijafanya kazi kila asubuhi lazima nimuangalie yeye,siku hizi hata sioni raha tena,anyway mambo ya technology hayo soon things will be ok na atakuwa back on track kama kawa
wish u all the best
Love u Bro Michuzi mungu akuzidishie
Hi Guys kutoka Helsinki-Finland
Vipi michuzi, mbona umekuwa mtu wa kupatikana kwa shida? Vipi kuna mtu anakuhujumu sema wadau tupo wengi tutatoa donation kuiwezesha blog ya jamii ikae hewani, maana hii tabia ya kukatika katika imeaanza kuwa ni sehemu ya blog yako, hii blog ni ya jamii, isipokuwa hewani jamii inapata shida vipi wewe, ninakushauri mzee wa blog tafuta mdau hakusaidie-uza hisa kwa wadau kupitia soko la hisa la DSM- yaani ibinafsishe, wamiliki wawe wengi halafu itoe ajira kwa watu kuiendesha wewe unabaki kama Executive Director wa blog ya jamii
Kila Kheli Michuziiiiiiiiiiiiiiiiiiii
Frateline
BROTHER KULIKONI?KAMA TABU NET ELEZA KUNA UFUMBUZI
DARWIN
yaan michuzi mwenzio nisiposoma blog yanko kwa siku naumwa kabisa kwa nkuna nini kimetokea mwanawani? tunakumiss sana
Mi nilikua napata michuzi kutumia simu yangu thru rss, sasa simpati!
Bro Michu bwana this is becoming serious! Nilikupata over the weekend sasa leo naona ola! I frankly miss our blog we acha tu, yaani nahisi kuna kitu muhimu nimekosa. Anyway sijui tatizo ni nini haswa but whatever it is, kishindwe na kilegee!All the best!
Bro Michu eeeh fanya fanya mambo libeneke liendelezwe kama kawa wadau tumekumiss sana, kama vipi tuambie hata michango tutatoa ili tu “globu” yetu ya jamii irudi hewani