Natumaini kwamba u-mzima na tayari kabisa kuukabili mwisho wa wiki.Kwa upande wetu sisi hapa BC,tupo tayari kabisa hususani baada ya kushuhudia historia mpya kwa mtu mweusi Barack Obama kuchaguliwa rasmi kuwa mgombea wa Chama cha Democrat nchini Marekani.Yawezekana Obama asije kuwa chochote wala lolote jipya kwa Afrika au ulimwengu lakini kwa namna yoyote ile,if you are black you gotta be proud of him and actually give him the credits he deserves.Zaidi ya hapo utaonekana mpika “majungu”.Au?
Turudi kwenye shughuli yetu ya Ijumaa.Burudani.Hivi dawa ya mapenzi ni nini?Swali hili,hata baada ya miaka chungu nzima ya wajuzi kujaribu kulipatia majibu,bado linaendelea kuulizwa mpaka leo.Sababu?Mapenzi yangalipo na yataendelea kuwepo.Bado mapenzi yanaua,yanatesa,yanafurahisha,yanatia wazimu na wengine wanasema ndio chanzo cha kila vita iliyopo duniani.Sina uhakika na hilo.Nasikia tu.
Lakini je,unaweza kukubali kwamba kwa “karumanzila” kunaweza kupatikana dawa ya mapenzi?Si ushawahi kusikia hadithi za “limbwata” nk?Inawezekana kweli ukalipata penzi chini ya mkeka?Msikilize Hayati Mbaraka Mwinshehe akiimba kuhusu Dawa ya Mapenzi katika wimbo huu.Wikiendi Njema.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Pichani ni Mbaraka Mwinshehe na mkewe Amney Shadad siku ya ndoa yao tarehe 17/3/1972 huko mjini Morogoro.
Feedback / Comments
34 Responses to “DAWA YA MAPENZI-MBARAKA MWINSHEHE”
Leave a Reply


sending...
Sure, dawa ya mapenzi ni Limbwata tu, unakula wewe na mpenzi wako basi, no divorce, no separation no ngumi. Hebu jaribuni muone!!
Hakuna dawa ya mapenzi wandugu zaidi ni kujaaaliana na kuheshimiana,hayo ya kwenda kwa kalumanzila ni uongo mtupu na kuharibiana akili manake ukimwendea mwenzio kwa kalumanzila utapewa dawa ya kumpumbaza na wala si kumuongezea akupende. kama mtu hakupendi ni hakupendi tu.
Jamani obama ni mmarekani ndo mana karuhusiwa kugombea urais,wabongo tuache uzembe na kuanza eti atatusaidiaje weusi! that is primitive thinking let us work hard and stop depending on aids and grants from developed countries.
Gervas mzima wewe?
Matty mfumo unasemaje?
mama wa kichanga na wengine wote..
Swaiba Debra upo?
nawatakia ijumaa njema na mwisho mzuri wa wiki huku tukisema yote yanawezeka…na ni CHANGES
OBAMA
Hongera Obama!
Hakuna kitu kinachoitwa dawa ya mapenzi!!!!
Mapenzi ni KUAMINIANA,KUHESHIMIANA,KUPENDANA,NA KUJALIAANA hayo masuala ya limbwata ni uzushi tu…..
Hivi hushtukizii ukienda kwa mganga waambiwa upeleke KUKU,MCHELE na NAZI kisha wapewa makaa sijui yalosagwa waabiwa dawa hujijui umempa mwenzio chakula hapo wali wa nazi kwa supu ya kuku hehehehe! na bado unalipa na vijisenti juu khaaaaa!!!!Kweli hizi imani nyingine mbovu kabisa…..
hahaha unaona limbwata lilivyo baya??
gppmie Says: August, 29, 2008 at 9:55 am nadhani tayari kishalishwa angalia vitu anavyoongea sasa
Prove tunayo hapahapa!! hahaha
hakuna dawa ya mapenzi!!! What is important is knowing and understanding your partner. naona siku hizi haya mambo ya kalumanzila yapo juu sana. nashangaa…..!
Nipo Endwin Ndaki mfumo ni ule ule tutafika tu!
Obama juu juu zaidi!!
Mapenzi hayataki Limbwata wapendwa mimi najua dawa ya mapenzi ni kupendana,kujaliana,kuheshimiana n.k mambo ya kalumanzila ni kudanganyana tu na isitoshe dawa hizo hizo zikiisha nguvu mapenzi utayaona yamechuja bwana hakamatiki bibi nae mhh!
Na kwa nini mtu aende kutafuta mbadala kwa babu??? kwani nikikukuruka tu na utundu wangu jamaa hatanipenda?? aibu mno na ni kumkosea Mungu tu!
Washindwe na walegee wote wanaofanyia wenzao limbwata/ulozi nk.
Mwisho nawatakia wknd njema wote!
Kazi bado kubwa na ndugu yetu Obama kwa upande wa africa tuwe yetu macho hakuna jipya la kutegemea.mafanikio yatatokana na jitihada zetu tusibweteke almujatahada wajjada,
Haya Binti-mzuri wiki nenda inakwendaje?dawa ya mapenzi hakuna utata tuu wengi walijaribu matokeo yake jela na kifo
MAPENZI MATAMU NA MABAYA UNAPOPENDA PASIPO KUPENDWA
WIKI END NJEMA WANA JAVINI WENZANGU CHAI GODA 4 ALL
Edwin, mie swafi tu kamanda….Matty napingana nawewe, kuna mijitu mingine haipendeki ina-cheat tu, hebu jaribu limbwata uone ni kudumisha mila. Mie tumelishana mwaka wa kumi na tatu huu, yaani ukimfumania mkeo wewe ndo unakuwa wa kwanza kumuomba samahani.
Mhh!!Acheni utani wajameni.Dawa ya mapenzi ipo sana.Mimi mke wangu nimefumania mara tatu lakini bado ninampenda tu.Sasa hiyo kama sijapewa limbwata niiteje???
Jamani mimi sishangilii tena kuhusu Obama manake keshashinda.Yaani tukijua huyu mama Palin ni nani hasa na maskendo yake yakoje baasi “Tutafika tu ki Ndaki Ndaki”
Obama oyeeeeee,Kidumu chama cha cha cha nani nani nanii kipi hiki Ndaki hebu malizia….
Baraka Obama, si lolote wala chochote. Sio kila mtu aliye na rangi nyeusi hujivunia rangi hiyo. Wasrilanka na watu wengi Caribean ni weusi. Mtu yeyote anatakiwa ajivunie rangi yake na asili yake atokako. Barack Obama hataki aonekane kuwa ni mtu mweusi na hataki aonekane kuwa ni mwislam.
Barack Obama hakufika katika kumbukumbu ya kuazimisha miaka 40 ya kifo cha Martin Luther King Jr, Condoleeza Rice na watu wengine weusi kibao walifika kuadhimisha kumbukumbu hiyo. Kwa kufanya hivyo, sisi kama wachambuzi wa mambo, tuliona kuwa Obama hakutaka aonekane kuwa anashabikia watu weusi, ili aweze kuzipata kura za Wamarekani weupe wasiowapenda watu weusi. Pia anajitetea kwa kusema kuwa yeye ni mkristo na kuukana uislamu, ili tu aupate Urais wa Marekani.
Sisi waafrika tusitegemee chochote kutoka kwa Barack Obama, na wala sio kuwa tunataka kupata misaada toka USA, bali ni mahusiano ya karibu kati ya nchi zetu za Afrika na Marekani. Mimi siwezi kumpa credit yoyote Barack Obama, kwa vile namwona ni msaliti wa rangi yetu niipendayo na dini yake, japo Mwenyezi Mungu hana dini.
Turudi kwenye mada ya “Dawa Ya Mapenzi”-Mbaraka Mwinshehe. Mjadala wa hapa tusijadili maneno ya wimbo, bali tujadili mchango wa wanamiziki wetu wa Tanzania tangu miaka ya nyuma Mbaraka Mwinshehe akiwa mmoja wa wanamiziki hao.
Hatima ya wanamiziki wetu wa zamani ni TBC wakati ule wakiitwa Radio Tanzania Dar es salaam. Wengi ya wanamiziki wetu walirekodi kazizao hapo,na wale waliokuwa na uwezo kidogo walienda Kenya kutoa santuri zao kama hii tunayoisikiliza ya “Dawa Ya Mapenzi na Mbaraka Mwinshehe.
Kaka Thido Mhando, usiufurahie Ukurugenzi wa TBC pekee, bado unayo kazi kubwa mbele, kwani tunataka kuwasikia wanamizikialioko kwenye Maktaba zenu za miziki, kama vile John Ondoro Chacha, Juma Nguzos, Dancan Njilima, John Kijiko, Billy Mbwana, John Simon, Zacharia “Tendawema” Daniel na wengine wengi.
This Is Black=Blackmannen
Hapo juu mr Black mannen kaandika vitu vizito navya ukweli kuhusu BarakaObama ambaye katika macho yangu simuoni kama ni muislam kwani ameukana mbele ya kadamnasi ya watu karibu interviews zake zote aliwahi ulizwa swali hilo hilo na jibu lake lilikuwa “mimi sio muumini wa dini ya kiislam”,mimi naona tatizo hapa ni kulelewa na watu tofauti ambao wanawezawakakubadilisha imani uliyozaliwa nayo na kukupa imani wanazo amini wao.Kama sheria ya dini ya kiislam inavyosema mtoto yeyote wa muislam anapo zaliwa huwa ana adhiniwa na mzazi wake mara tu anapozaliwa na hilo haliwezi kubatilishwa na sheria yeyote ya kidunia,Obama ni muislam katika macho yamwenyezi mungu,tusubiri aupate huo uislam tutaona jinsi atakavyo wapinduka Americans ,jamaa yupo katika crisis ya identity,wakati alipo zaliwa aliitwaBaraka na dad wake lakini mara baada ya dad kurudi Kenya wazungu wakaanzakumwita kwa jina la Berry na baadaye katika kutafutaidentity yake alibadilisha majina yote waliyokuwa wakimuita na kufikia hadi kurudi kwao Kenya na kama mlivyoona alifikia mpaka kupiga picha huku kavalishwa nguo za asili za kisomali nasio wasomali pekee ndio wanao vaa namna hiyo hata makabila mengine kule juu yaliyo ya kiislam huvaa namna hiyo,huyu jamaa yuko katika identity crisis ya hali ya juu ni lazima aonekane yuko katika kundi ganikuliko kuwachanganya watu.Tuna mtakiamafanikio mema na wengi tujitayarishe kuona history itakavyo jiandika,Baraka hana mpinzani pale yule mzee ni mchovu wa afya hataakili zake hazifanyi kazi vizuri ni worse zaidi ya Bush,atatuletea tatizo kubwa sana la mambo ya vita na kuvamia nchi zawatu ni mtu hatari sana na sisi weusi hatutokua na nafasi yeyot ile ndani ya US na dunia nzima kwa ujumla,hata sisi waafrika suala litakuwa ni hilo hilo tuu.
wasalaam na Ramadhani njema kwa wote
Willo
hahahahahaha Majita na Gervas ndo mmeua bendi aiseeee khaaaaaaaaa unagombana nae /unamfuma unakuwa wa kwnza kuomba sorry hahahahahahaha! na mimi nasisitiza limbwata ni ushenzi tu kupumbazana akili kusiko na msingi bwana na wanaofanya hivyo wengi wao wameshindikana kitabiaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa ndo wanahisi kufanya hivyo ili kujibaraguza tu!
obama sio mweusi acheni one drope rule hapa mweusi ni wewe na ukoo wako usio kuwa hata chembe ya white blood.mwacheni multiracial wao.hata asipoenda kwenye maadhiisho ya dr. king yeye sio mweusi kama unavyofikiria
Kama Barack Obama amesema yeye sio muislamu, msimlazimishe! Ebo! Na kuhusu mwendo wake wa kisiasa, mimi nampa 5!. Ni kijana mwenye uwezo wa ajabu kisiasa! Ameibuka from no where na kuweza kung`ara kisiasa hatimaye kuweza kuwa mtu mweusi wa kwanza kufikia hatua hiyo aliyoifikia yeye. MWENYEZI MUNGU AMBARIKI, NDOTO YAKE ITIMIE. Swala la utendaji wake, ni mapema sana kumhukumu hivi sasa. Anaweza akafanya vizuri sana au kinyume cha hapo!. Tumpe nafasi tuone. Yetu macho!. Akiendesha nchi vizuri, basi hiyo itaongeza heshima kwake na watu weusi kwa ujumla kwa namna moja ama nyingine. As you know, wazungu wengi huwa hawaamini kitu mpaka washuhudie kwanza. Sasa inawezekana Obama akawashangaza kwa kuwa na karama za uongozi. Of course, raisi wa marekani haongozi peke yake. Huyo Obama washauri wake wengi ni wazungu hao hao. Hata hivyo yeye kama raisi ana power fulani ktk kufanya maamuzi. Kwahiyo kama nilivyosema awali, tusubiri tuone. Yetu macho.
Kuhusu Afrika kutegemea Barack Obama kusaidia huko, hilo swala limepitwa na wakati. Waafrika tunatakiwa tuamke na kuwa na fikra za kujitegemea wenyewe. Hii tabia ya kuombaomba tunatakiwa kuiacha mara moja kwani inadhalilisha uafrila wetu. Tabia hii ya kuombaomba hovyo kwa nchi za Afrika, imekuwa kama jadi. Mbaya zaidi, hata hiyo misaada inayotolewa, haiwanufaishi walengwa bali MAFISADI wachache walioko madarakani( wana si-hasa).
Njia pekee ya Afrika kujikomboa kwenye umasikini, ujinga, na maradhi, ni kuungana na kufanya kazi kwa pamoja kupambana dhidi changamoto zote za maisha. Viongozi wawe ni viongozi wa kweli na sio vibaraka wa nchi zilizoendelea. Viongozi wasiwe wabinafsi, wasiwe na uchu wa madaraka na wasiwe ma-dikteta. Wananchi nao( waafrika wenzangu) tusibweteka na kutegemea Obama akiwa raisi atakuletea maendeleo Afrika. Nasema “HELL TO THE NO!. Come on people!, tunatakiwa tuamke na kufanya kazi kwa bidii na kujituma. Agalieni Korea na China jinsi wanavyopasua mawimbi hivi sasa. Wanapata maendeleo ya hali ya juu hivi sasa kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa. Hawakutegemea Bush wala Obama bali juhudi zao binafsi za kitaifa. If them, why not us!?
Kwa upande wa mapenzi, mimi binafi naona limbwata haina nafasi. Mapenzi ya kweli yana upendo na heshima kama walivyosema wadau waliotangulia hapo juu. Huwezi kumita mtu mpenzi kama haumpendi. Na kama unampenda, huwezi kumfanyia vitu ambavyo unajua wazi kuwa vitamuudhi au kuvunja moyo wake. Mtu unayempenda kwa dhati, hutapenda kuona anaumia rohoni hasa kutokana na usaliti wako wa penzi. Mtu unayempenda huwezi kumuacha kwa hali yoyote ile hata kama ni kufirisika ama kupata kilema kutokana na ajali ama maradhi. Mpenzi wa kweli huwa karibu nawe wakati wa shida na raha. Hayo ndio mapenzi. Lakini kumpenda mtu kwakuwa ana aidha mali, cheo, sifa, umaarufu, huo ni unafiki tu. Kanye West anaita watu kama hawa ni “GOLD DIGGERZ”. Siku zote wakishakuvuna vya kutosha ama mambo yakikuharibikia, wanakimbia haraka sana. UMASIKINI UKIBISHA HODI MLANGONI NGO! NGO! NGO!, MAPENZI YANATOKEA DIRISHANI!
aisee obama nimekushusha ghafla..kumbeeee!…daah! kweli ng’ombe wa masikini hazai.
Dunda Galden,dawa ya mapenzi ni uaminifu tu ndugu yangu….na ‘ufundi’. naona umechange signature yako from chafosa chai goda to goda 4 all…hongera,umepanda beeii
being a black person living in N. America, I am proud and excited about Obama’s run. As a Tanzanian/African I know there is nothing special that Obama will do for Africa. There is a common misconception amongst some Africans, and particularly Kenyans, that Obama being a son of a Kenyan will try and help out Kenya/Africa in one way or another if he wins the election. The truth is, his loyalty and his responsibility lies with the US first and foremost. Whatever else he may or may not do for Africa (or the rest of the world for that matter) will not be affected by his color or his heritage, rather by the interests of his country. And even if for arguments sake, let’s say Obama had special plans to help out Africa, you have to remember that he will have to go through Congress first; and there’s also a matter of approval rating and re-election in 4 years time to think of. Having said that, I doubt everybody in the US will share the same view of African.
Why then am I excited about Obama? If you live abroad and see how black people are stereotyped; and how so little of us is expected; it is a nice change for the rest of the races to know that a successful black person doesn’t have to be a pro athlete or an entertainer. We have a number of successful blacks working as Professors, executives, successful businessmen/women even in politics (Condi, Powell), but we are still being judged by the color of our skin and not the content of our character even in this day and age. Having Obama come this far, and possibly win the election in November may probably not change the impression that some redneck from Alabama has of black people, or stop confederate-flag-carrying skin-heads from shouting the N word to me while driving down the road in their pick up trucks; but it will be one step closer to creating a positive image of black folks.
Some may argue that Obama has a white mother so he’s not really black like me. But hey, over here if your skin looks black you face the same judgment and prejudice that all black people face; no matter if you are mixed race or if you were born here or migrated from Africa.
So no, I do not expect any special favors from (hopefully) president Obama, but as a black person I have every reason and the right to be happy.
Blackmannen, what you said about Swnator Obama and MLK’s memorial is simply not true. Here is a video of Obama giving a speech at Ebenezer Baptist Church (Dr. King’s Church) in Jan this year
Anyways, in regards to him running his campaign as a black candidate There are already enough racists who have vowed to not vote for him no matter what. View the following videos after the W. Virginia primary, . Now for him to alienate the neutral voters by identifying his campaign with him being black, that would be political suicide. First of all in terms of numbers, blacks are a minority (12.8%); even if you included other “persons of color” (Hispanics, Asians, multiracials, etc); at 68% whites still are an overwhelming majority; so he can not expect to play the race card and win. When it comes to race Obama is caught in a bit of a paradox; when he stated running he was accused of not being black enough, but if you follow the campaigns, he is now being accused of being too black. Truth is, this is largely a smearing campaign and attempts of Barrack’s oposers playing with people’s emotions and not appealing to their intellect. Unfortunately, I see some African Americans playing right into that trap. For instance did you happen to catch these hecklers ? Listen to Obama’s intelligent response. They (African Americans) expect Obama to have made a fiery response, siding with his black brethren and condemning the (white) powers that be. But do you know how much ammunition that would have given white supremacists?
At the end of the day, whether he holds his fist high like a black-panther rebel or not, it does not change what Obama feels in his heart about being black. If he does not like being black, he could still do all the actions just-for-show so that he could win the black votes; but that would not change the truth of who he is now would it. And he could, for political reasons, appear not so radical, and be able to appeal across different racial groups; win the election and then be able to provide more for the black community. It is a matter of choice for him. Do I run my campaign on a racial basis and lose the election, or do I avoid playing the race card and win the election. If you really wanna know whether Barrack cares or lot, listen to his plans; for example, read his views on affirmative action. For example, if I was running for pres of Tanzania, I can not sell myself as a Chinga. I am a Yao and very proud of it. But unless I am running for president of Mtwara only, I am bound to lose the election.
As intellects, we should not get sucked into the political mumble-jumble and make decisions on issues.
In regards to him being a Muslim; well, he has stated himself that he is not. He was born of a Muslim father, but was not raised as one. It is unfortunate that in recent times, the word Muslim has come to have a negative connotation in the US (and a few other western countries a bit); and now you have some racist and prejudiced people like Glenn Beck using that opportunity to run negative campaigns and smear tactics against Obama. Every person has the right to chose a religion. America is a very hypocritical country; the preach religious tolerance to other countries; yet they are the first to do quite the opposite. Even if Obama was a secretively practicing Muslim, then so what? Should this even be an issue?
Nalitolela! Je maadhimisho ya miaka 40 ya kifo cha Martin Luther King Jr unajua yalikuwa lini?, Je, speech ya Senator Obama katika kanisa la Ebenezer Baptist Church (Dr. King’s Church) januari mwaka huu, ilihusu maadhimisho hayo?
Juhudi za Barack Obama kuingia makanisani ni katika jitihada zake za kuwaonyesha Wamarekani kuwa yeye sio mwislam, bali ni mkristo ili apate kura za hao wabaguzi.
Nalitolile, katika maelezo yako nakuona unajikanganya sana. Umemlaumu Glenn Beck kuwa, anamtupia madongo Obama(…negative campaigns and smear tactics against Obama) kwa kumwita mwislam, na hapo hapo unasema, “Even if Obama was a secretively practicing Muslim, then so what? Should this even be an issue?”.
Mtu mwenye akili yake timamu, hawezi kukataa asili yake na utu wake, eti ili apate kitu anachokihitaji wakati huo, ambacho ni cha muda mfupi, wakati asili na utu wako ni vya maisha yote hadi utakufa navyo! Obama amefanya. Nalitolile, mimi na wengine wanaoniunga mkono kwa haya niyasemayo hapa, hatuko …”get sucked into the political mumble-jumble…”, kama ulivyosema hapo juu, bali ni ukweli unaoonekana.
Je, Amerika, uislam ni kitu “negative?”. Mbona marafiki wa karibu wa Amerika ni nchi za kiislam? Kama vile Saudi Arabia, Kuwait, Jordan, Pakistan, Iraq, Moroko, Egypt n.k. Au urafiki wa Amerika na nchi hizi ni wa kinafiki?
Barack Obama ni sawa na hao dada zetu wanaoikana rangi yao NYEUSI kwa kutumia mikorogo ili wawe weupe. Chao!
This Is Black=Blackmannen
Blackmannen,
Kwanza kuhusu Glenn Beck, na kuhusu comment yangu juu ya “..should it even be an issue”, sijikanyagi. Nachosema mimi, that whether he was a muslim or not, this should not be an issue. However, ukweli halisi wa mambo ni kuwa Americans have chosen to make it an issue ukifuatilia news.
Kwa mantiki hiyo basi, when people like Glenn Beck and others call Obama a Muslim (not because they just think it’s his religion, but rather because they want to link the Muslim issue with terrorism and national security) then inakuwa sasa ni smearing tactics. And to answer your question, yes, to an average American, these days being a Muslim has negative implications, you can’t deny that.
Kuhusu MLK day, I npticed sikuweka link on my earlier post. Here it is http://www.youtube.com/watch?v=Kf0x_TpDris
Hii ndio ya Ebenezer church; ilikuwa tarehe 20 which was a Sunday, ndio maana alikuwa church, unlike unavyoimoly kuwa alikuwa church ili avutie wabaguzi. SIku rasmi ya MLK ilikuwa the following day; January 21st (it’s always on the 3rd Monday in January). Na siku hiyo Obama alitoa speech in S. Carolina video iko hapa: http://www.youtube.com/watch?v=KUsP3EIec4k
January 21 was the S. Carolina primary debate and Senators Obama, Clinton and Edwards were facing off that evening, ndio maana Obama alikuwa S. Carolina, and not anywhere else in the states (such as in Washington at Dr. King’s memorial library). Wala haikuwa sababu ya kutotaka kuhusishwa na kuwa mtu mweusi.
ooohh.. one more thing, kuhusu urafiki na nchi za kiislamu ulizozitaja… you have to understand hizo ni strategic foreign relations. I don’t wanna get into the whole politics of the middle east and all… lakini kumbuka kuwa kuna baadhi ya nchi middle East wamarekani wanaziona kuwa ni adui na wanasupport ugaidi. Hivyo ni lazima awe na marafiki within the area kumsaidia kulinda maslaki yake; kuna baadhi hapo ni suppliers wa mafuta kwa marekani, etc. Hivyo tofautisha urafiki na foreign relation policies ambazo huwa ni symbiotic; nipe nikupe.
Anyways… ukiachana na hayo, serikali ya Marekani na wananchi wake wengi tu wanaweza kuwa waelewa na wasione uislamu ni tatizo kwa njia yoyote. Ila kwa wapiga kura wengi hawana uelewa huo. Na comment yangu ilikuwa inawalenga hawa wapiga kura, sio serikali ya Marekani. Americans are very xenophobic people in general; na since the events of Sept 11, kwa Mmarekani wa kawaida mtaani fikra zao ni kuwa uislamu = ugaidi. And that is what opposers of Obama try to play with
Wewe Blackmannen Kichwa chako kinahitaji kuchunguzwa na Daktari wa Ubongo ‘Psychiatrist’ and Um prepared to pay for the treatment!No favours.Wewe ni mgonjwa wa akili.Unajua akili ina afya yake.Ukiona ina ‘underperform’ ujue kuna tatizo! Ugonjwa siyo Malaria tu pekeyake. Obama siyo Mwislamu pure and simple! Yeye kasema hivyo na Mama yake Mzazi anatambua hivyo.Kwanini ulazimishe?Alilelewa na single parent,katunzwa na wajomba zake na kasomeshwa na mama yake akisaidiwa na kaka zake! Tatizo liko wapi? Asipokuwa Muislamu kuna tatizo gani? Eti anajipendekeza kwa Wamarekani Weupe na kuwadharau au kuwapuuza Wamarekani Weusi ili apate kura za Weupe, Kauli hii ni ya Kijinga kabisa kutolewa na mtu anaye jiita Mwana wa Afrika! Uafrika wako uko wapi? Kichwani, Tumboni au Matakoni? Nimeshindwa kabisa kuvumilia ujinga huu. Kama huwezi kujieleza bora ukae kimya.Lakini siyo kujifanya unajua sana na una akili sana kumbe zumbukuku mzungu wa reli.Usitutie aibu katika Jumuiya ya Kimataifa.Hata katika Bara la Afrika wapo Waafrika wenye akili sana na busara nyingi sana pengine kuliko hata hao weupe unaowapapatikia! Better Shut Up!
Mbarak Mwaruka Mwinshehe FOREVER! Hatutakusahau Mbaraka kwa Tungo zako nzuri za kuliwaza na zilizo kwenda shule. In your times you had been immensely an illustrious inspirational role model, extra ordinary musician of outstanding ability, mpiga solo mashuhuri, mtunzi na mwanamuziki mahiri! Ulitupa burudani tosha ambayo hadi sasa hapajatokeza mwenye kipaji cha kulingana na chako akatufanya tusahau yaliyopita! Uliipandisha chati Morogoro ya Waluguru! Will alwayz be remembered by all your fans and patrons worldwide! Kama alivyotuusia yeye mwenyewe kwamba ‘HAKUNA DAWA YA MAPENZI, hiyo uitafutayo ni ya kumuua mpenzi wako’. Akisha kuwa zezeta umepata faida gani? Na pengine hata kifo kumfika.Je!
Hey matapishi touch arogant hizo mhh tutafika!
RIP MY MOM……..
NAKUMBUKA KABLA YA KIFO CHAKO, KILA JUMAPILI UNASIKILIZA NYIMBO ZA ZILIPENDWA, NA KIPENZI CHAKO KIKUBWA ALIKUWA MBARAK MWINSHEHE, MWENYEZI MUNGU AWAONGEZEE NEEMA NA UPENDO. MISS U ALL
1.DAWA YA MAPENZI
2.MAPENZI YANITESA
Matapishi!
Kabla ya yote, nakutakia utapishi mwema, maana uliyonitapikia hapa si haba ndugu yangu. Mimi kwa vile sipendi kujibishana na watu aina yako, nakuomba usome comment namba 14 ya “Willo”, majibu ya maswali yako na matatizo yako rohoni utayapata hapo.
Baraka Obama ni msaliti wa asili yake na rangi yake, japo kalelewa katika malezi ya watu weupe. Kwa mantiki hii, ndiyo maana anaukana ukweli huo.
This Is Black=Blackmannen
matapishi kweli katapika… debate without matusi basi,kila mtu na opinion zake
ni vip wabongooo! wenzangu!
jamani dawa za mapenzi zipo lakini watu zinakuwa mara nyingi sio za kudumu zina mwisho na mapenzi ya kweli hayana mwisho mwisho wake ni kifo kti ya mmoja au mwingine atakae tangulia.
acheni jamani mapenzi hayana kitu cha kufanana nisha mapenzi ni kitu kingine kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
daaaaaaaa hio kibao cha mmbaraka ni kizuri sana
dawa ya mapenzi ni kumwelewa mwenzako na kusaidiana kwa hali na hamali.bali si kwa watuba mbao au kwa yeyote yule.