MASHAKA ANA KWA ANA NA AFANDE KOVA

Kama wewe ni msomaji mzuri wa BC,bila shaka jina John Mashaka halijakutoka kichwani.Tulipofanya naye mahojiano mwezi April mwaka huu,mahojiano yale yaliingia kwenye lile kundi la mahojiano ambayo yalizusha mjadala mikali zaidi na hivyo kupata maoni tofauti tofauti chungu mbovu.Wengi walimuunga mkono.Wengi walimpinga na kumkatisha tamaa kwa kila namna walivyoweza.Wengine walibaki katikati wakisubiri afanye kitu ili wajue jinsi ya kumuunga mkono au vinginevyo.Kama hukupata bahati au nafasi ya kuyasoma mahojiano yetu na John Mashaka,unaweza kufanya hivyo kwa kubonyeza hapa.

Kwa bahati nzuri au mbaya,yaelekea John ni mtu anayejua anapotaka kufika,anachojaribu kukifanya na haelekei kuyumba katika nia yake.

Hivi majuzi,John Mashaka(yupo Bongo hivi sasa) aliandaa kongamano lililoitwa Tuwajali Wenzetu.Kongamano hilo lilifanyikia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar-es-salaam.Je kongamano hilo lilihusu nini?Mashaka aliongea nini?Ni yepi yalijiri katika tamasha hilo?Kupata undani wa kongamano hilo na picha kadhaa mtembelee Ahmad Michuzi JR kwa kubonyeza hapa. Habari njema ni kwamba,kama inavyoonekana pichani,Kamanda wa Polisi wa Dar-es-salaam,Afande Suleiman Kova amekubali kuunga mkono jitihada za John Mashaka.

Page 1 of 3 | Next page