Miongoni mwa sauti za wanamuziki/waimbaji nchini Tanzania ambazo huwa hazihitaji kutumia msuli sana kuzitambua ni ile ya Muumini Mwinjuma. Na kwa wale mnaozikumbuka enzi za nyimbo kama “Tunda” mtaelewa zaidi ninaongelea nini.
Burudani yetu ya leo inatoka kwake huyo huyo Muumin Mwinjuma. Wimbo unaitwa Kilio Cha Yatima.Ni utunzi wake Muumin na umeimbwa enzi akiwa na kundi zima la Double M Sound maarufu kama Wana Mshikemshike.
Wimbo huu ulikuwa ni kati ya nyimbo za Muumini za mwanzoni kabisa baada ya kujitoa kwenye bendi ya Tamtam.Wimbo huu aliuimba maalum baada ya kugombana na mwajiri wake wa kwanza pale Muumini alipokwenda kumuuguza na hatimaye msiba wa baba yake mzazi Mzee Muumin Mbughuza (RIP).
Kwa sasa Muumini ameunda kundi lake jipya linalojulikana kama Bwagamoyo Sound na kwa sasa wako kambini wakijiandaa na uzinduzi wa kundi lao ambalo anasema litakuwa moto wa kuotea mbali.Pata Burudani na Ramadhani njema.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Habari na burudani ya leo imeletwa kwenu na Pius Mikongoti anayeblog kupitia Spoti na Starehe.Bonyeza hapa umtembelee.
**Shukrani kwenu wote mlionitumia salamu za pole na kunitakia afya njema.Nipo fiti sasa.Zawadi yenu hii hapa.Wimbo unaitwa Kuteleza sio Kuanguka kutoka kwake Lady Issa.Unamkumbuka?
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Page 1 of 3 | Next page