
Wimbo uliomtoa ulikuwa ni ule uliokuwa ukiinadi rangi ya blue.Pengine ndicho chanzo cha yeye baadaye kuja kujulikana kama Mr.Blue.Pamoja na hayo wimbo wake ulioitwa “Mapozi” ndio ulikuja kutamba kwa staili ya aina yake.Baada ya hapo ikawa ni mapozi nawe,mapozi nawe.Lakini kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya anabakia kuwa Mr.Blue.Hivi karibuni alikuwa katika ziara ya muziki nchini Uingereza.Ni miongoni mwa vijana walioko katika fani ya burudani kupitia muziki nchini Tanzania ambao wanaweza kusema “wanafanya vizuri” katika wanachokifanya.
Mcheki hapa chini katika wimbo wenye ahadi nzito nzito za kurejea kulifuata penzi.
Photo courtesy of Abdallah Mrisho
Feedback / Comments
101 Responses to “WANAMUITA MR.BLUE”
Leave a Reply


sending...
Jamani kajamaa kametulia alafu kana kipaji somehow…hivi BC nilickia ati aliacha shule kwa ajili ya umaarufu…je hebu niambie amerudi school?kama bado namuomba amuige mwana fa plz…vinginevyo mimi namkubali na haswa kwa ule wimbo wake wa MAPOZI NAWE WE NA MAPOZI NAWEEEEE….
selebrity wa leo bahati mbaya ni mgeni kwangu.SIMFAHAMU mchango wake katika game.Ila inaonekana anakuja vema vema.
Achilia mbali picha aliyopiga imejitahidi kunipa picha…yupo katika kundi la ‘umri’ gani na hata mtazamo wake kimaisha unaweza kuwa katika ‘umri’ gani.
Kwa wadau wengine wote wa tz..poleni sana kwa sisi tusikuwa na umeme.Najua sehemu kubwa ya nchi ipo kwenye giza tororo sijui na bongo wameingia kwenye kipindi cha ‘otumu’.
Najua kuna wadau wengine maoni yao tutayakosa kwa muda huu wa mgao ..ila Inshaalaah Mungu atasaidia umeme utarejea karibuni.MAISHA BORA NDIYO HAYO.
Tupige kazi kwa bidii,wa kusoma wakamue kwa bidii..ipo siku nawaambia ..TUTAFIKA TU kwenye ile nchi yetu ya ahadi..ila sio kupitia hawa wanasiasa.
Siku njema
Ndugu yangu hiiyo ni tatoo au umechora na peni msuli huna basi kichekesho mtindo mmoja
kipaji unacho …but, u need to go back to school kijana!!
Bado safari ni ndefu…..na sijui kama tutafika. Labda wasanii/producers wajaribu kumix beats na style za mziki wa kiasilia na huu wa kizazi kipya. Lakini miziki hii tuliyonayo inakuwa na market ndani ya nchi tu and not beyond that. Wasouth Afrika ndiko walikoibukia. Mfano Saida karoli alianza na idea hiyo, sijui kaishia wapi. Wasanii wetu wanakalia tu kulundika albam, mwingine kwa miezi mitano anakuambia ana albam tano na kulalamika kuwa watanzania hawanunui kazi zao….. tujiulize miziki yenyewe inauzika?
Thanks God ubalozi wa Marekani unakatalia visa hawa watu. Hebu imagine hawa watoto wangekuwa wana hang kwenye suits za ATL au Htown?
Hizi Hardcore tattoo kama mwizi… For god sake what is wrong with youngstars in Tanzania?
When i see that i feel like throw up…..
hivi huyu bwana mdogo shule ndio basi tena ama vipi,maana sijawahi kusikia swala la kujihusisha na elimu
Thanks BC u made my day,nampenda sana huyu kijana,go blue
Waswahili wanasema ” Ujana ni nyonjwa, kila mtu huonja…” Huyu naye (Mr Blue) anauonja ujana kwa “style” yake! Maana wengine husema ujana ni nusu ya uchizi.. huyu naona ni robo tatu (3/4)ya uchizi! Ndio ujana ni maji ya moto ukiyachezea yatakuchoma, huyu mwenztu hayako mbali kumchoma, kama hayaja mchoma…! Ameacha shule kwa ajili ya kubana puwa (kuimba), mziki wenyewe wa bongo una ng’ara msimu mmoja msimu ujao uko nje ya game, ukishindwa kujipanga vizuri ndo ntolee tena..!
Huyu anahitaji mshauri kabla mambo hayajazidi kumharibikia…!
BC chonde chonde.
nakuomba unisaidie au mtu yoyote anipatie wasifu wa huyo dogo.
naona wadau wameanza ooh..kaacha skuli kafuata umaarufu..SIAMINI KAMA KWELI KIJANA KAMA HUYO ANAVYOONEKANA NA UPEO MKUBWA aamue kuacha shule kwenda kubongoka flava.
kama kweli dogo rudi shule..plz BC NAOMBA MAHOJIANO ya MR BLUU kama yupo tayari kutoa ushirikiano.
kila la kheri mr bluu
kijana aende gym atengeneze mwili asiwe kama dem, miili hutengenezwa haiji yenyewe.
Enzi zetu miaka ya 70s kwenda shule au kusoma ikuwa ni wajibu (labda kwa vile Elimu ilikuwa bure) tofauti na siku hizi.
nilisikia wazazi wa Kibongo wakilaumiwa kuwa wanawalazimisha watoto wao kusoma au somea masomo fulani hata kama watoto hao hawapendi shule.
Ikadaiwa kuwa “wazungu” (kitu ambacho sio kweli)huwaachia watoto wao wachague wanataka kufanya nini kwenye maisha yao hali inayowafanya watoto hao kuwa na maendeleo (inategemea anafanya sanaa gani) sasa basi huenda wazazi wa huyu kijana wamejaribu kuwa “wazungu”.
Nakubaliana na wote wanaoshauri dogo arudi shule, lakini napenda kusema kuwa anajitahidi sana kwenye sanaa anayoifanya.
Eid njema….
Dogo babu namkubali ….mbona mzuka..hana magumashi wala nn!!!!makamuzi yake n mwendo wa kujimwaga tu.
kip it Blue…
Bwa’ mdogo anaimba vizuri, anachoniboa tu ni kwamba hataki shule. Nenda shule mdogo wangu utrakapo zeheka hakuna atakaye nunua mziki wako, utabaki umechoka kama shaban dede.
Anajitahidi sn, ila rudi shule coz ni muhimu u still young bwa mdogo.
kaka Ed na MAtty,
Mimi nashukuru kwa comment zenu. Unajua mimi nacheka sana nikirudi home na nikiona vijana wanavyojaribu kuiga MAblack Americans; mimi naishi Europe ila naenda sana USA na najua matatizo ya Black Americans moja wapo hawaendi shule na pia ni masikini WA KUTUPWA JAPO sio wote but the majority..
sasa vijana wetu wakiweke Tatoo ndio wanajiona ma nigger sana it makes me so sick…
kaka yangu na mimi pia nashukuru kwamba US embassy haiwapi visa maana hata kama wanascholarship wakifika USA wataingia mtaani na kuwa majambazi na kuuliwa na polisi kama manigger wanavyokufa..
Kuhusu huyu mwimbaji;
mdogo wangu nenda shule, take an example ya waimbaji wenye degree zao wale wa jirani hapo Kenya..kumbuka muziki wa Bongo haulipi kabisa…pole kwa comment yangu ya wazi..
Mimi nimechoka kuona vijana ambao shule hawataki ndio wanaingia kwenye fani ya muziki kwa mtindo huo ndugu zangu muziki wa bongo hauwezi kuendelea kabisa..
hao mapromota wenyewe ndio matapeli kabisa.. sijui kama tutafika. Namkumbuka sana dada Saida Karori jamani huyu dada anakipaji lakini sijui ilikuwa walimtapeli mpaka sasa hatujui yupo wapi…
hivi jamani jina lake halisi ni nani !
Shule muhimu..but u r gud!
Wabilah Toufiq! barakatu la idd all of you guys! am taking this opportunity to wish you all the very best in all your endeavours,though BC umetunyima kibao cha idd.members pls receive greetings from me!
Any,
Amina,
Kekuu,
Mama wa Kichagga,
Pearl,
Olive,
Halima,
Binti-Mzuri,
Ramla,
Queen,
Pendo,
Kahindi,
E.Ndaki,
Chris,
Nalitolela ps.
Black manenn,
Mzanzibar 100%,
Gervas,
Hombiz,
mtajiju,
Majita kidogo nikusahau hahahahahaha najua ungedai salamu za Idd tu
BC WENYEWE PIA
Jamani niliowasahau so sorry nina haraka sana!
May Allah Subhanahu bless you all with joy, health, peace, prosperity and the warmth & love of all dear ones always.
Wana BC wooooooooooote nawatakia idd njema, mshereheke kwa kiasi, lile jungu lililovunjwa lijengwe upya, hahahahaaaaa bc umetusahau na sie ungetuwekea japo kaswida tuselebuke na idd!!!!!!!!!!!!
WIMBO NI MBOVU, KWANZA HAENDI NA BITS NA KISWAHILI KIBOVU, HILO NI TATIZO LA KUTAKA KUMALIZA KUYATAMKA MANENO YOTE KATIKA WIMBO KITU AMBACHO WABONGO WENGI WANAKOSEA SI LAZIMA UTAMKA NENO LOTE KATIKA MUSIC, MUSIC NI SANAA, AND ENTERTAINMENT, LAKINI HAPO AMEIMBA VIBAYA SANA NI MBOVU SIJAPATA ONA
tattoo ya korosho hiyo..kwi kwi kwi!
he needs to go back to school! He better waste no time neither!
Matty kidooogo nibomoe hii screen kwa kichwa coz kusahaurika tena ingekuwa noma.Nilikodoa “mimajicho” roho ikawa inapwita ninajisemaea rohoni “nimesahaurika” hahahaha
Haya wewe dogo watu wote tunasema S H U L E.
Oya Mbona wote mmechangia ande shule! Me naenda Tofauti kidogo…Me Namwambia Ajitahidi kufikiri baada ya miaka kumi atakuwa vipi? Akipata Jibu Ndo Alifanyie Kazi..Unaweza Ukaenda Shule Ukawa na maisha ya kawaida..Mr.Blue Yupo Darasa La Saba Lakini Ananipita Hata Mimi kwa hela wakati me nina Degree! Mbona Prof.Jay hana Degree,Lady Jay-Dee Mbona Form 1V Lakini Ana Hela Zaidi Ya MILLION 500Tsh,Ambazo Nynyi Wabeba Box Hamtozipata Mpaka Mnakufa na Midegree Yenu Hiyo,cha msingi tumshauli kwamba achukulie mziki kazi ili aje kufanikiwa..Duniani Kote wenye hela ni watu wa mabizness na co wenye elimu 2 kazi kusubiria mshaara,mshaara wenyeye Gros 900,wakikata kodi na nsss unabaki na laki7,hiyo laki7 unaweza kupush vogue?
Acheni ushamba nyie…Aende Shule akajiendeleza na co kama aciposoma ndo hatafeli maisha..Mbona anamaisha mazuri 2,,Ana gari 2,ana nyumba yake fresh..
Habari ndio hiyo Haters
E bwana cha msingi mtu uwe na hela.Mbona Maprofessor Wengi Wapo Na hawana hela wanayo hela ya kula tu?
Hivi Unaweza Kumlinganisha Professor Luanga na Lady JD kwa Hela?
Bob Sambeke kweli wewe ni kichwa cha panzi! Hivi bado tu haujafahamu kuwa “mali bila daftari huisha bila habari!”. Elimu ni hazina ya aina yake. Elimu unaweza kuifafanua kwa kauli nyingi zenye kuleta maana. Kwa mfano:
1. Elimu ni ufunguo wa maisha
2. Elimu ni ujuzi unaomuwezesha binaadamu kuyakabili na kuyabadili mazingira yaliyomzunguka ili yaweze kuwa bora zaidi
3. Elimu ni kitegauchumi
4. Elimu ni siraha ya kupambana na njaa, ujinga, na maradhi.
Hizo ni baadhi tu ya definition za haraka haraka juu ya elimu.
Kumbuka wachumi walisema “life is full of uncertainty. You never know what will happen to you”. Even if you have billions of money in the Bank, you still need some type of security (education) in case anything happens to your finance. Mfano mzuri ni hii hali ya kuharibika kwa uchumi wa marekani hivi sasa. Watu wengi waliokuwa matajiri wamepoteza pesa zao, nyumba zao na sasa ni malofa wa kutupa. Sasa wale walio na elimu zao kichwani, zitawasaidia kuanza tena kupambana na maisha from the scratch kwa kutafuta kazi na wakizipata kuzifanya kiufasaha. Lakini kwa yule aliyekuwa na pesa nyingi bila elimu, huyo itakuwa vigumu sana kuyaanza maisha from the bottom all the way up. Vile vile kumbuka, vipaji vya sanaa (muda mwingi) havidumu milele. Wasanii huvuma sana na baada ya muda Fulani huchuja na kupolomoka. Ni wachache sana wanaovuma for the life time. Therefore, education is important. Tazama Mr 2. Alivuma na mwisho akachuja na sasa yuko marekani anaitafuta elimu ambayo hakuwanayo hapo awali. Sasa heri yake yeye aliyeweza kupata nafasi hiyo ya kusoma hivi sasa. Na pia at least alikuwa na pa kuanzia kwani tayari alikuwa na elimu kidogo. Sasa anngekuwa hana kabisa, sijui ingekuwaje.
Come on Bob Sambeke! Be realistic about these things dude!
Kwako BOB SAMBEKE,
baada ya kusoma bandiko lako hapo juu,nimegundua kuwa ama hujui maana ya Elimu au maana ya tajiri au kuwa na hela.
Mifano yako unayotoa ya profesa sijui nini mwenye hela ni mfu.
Tunapokuwa tunasema mtu fulani ana hela nyingi maana yake ni kuwa kuna uwiano wa hela yake na mahitaji yake.Hakuna kiwango chochote duniani ambacho kimewekwa ili mtu akikifikisha basi na yeye anajulikana kama tajiri.
Bob Sambeke,nakupa mfano:- Nilipokuwa mdogo kule kijijini kwetu Majita kulikuwa na tajiri SANA.Alikuwa anamiliki vitu vingi hadi akawa amenunua baiskeli yake ya Phoenix mpya na watoto wake wote walikuwa na baiskeli za swala.Tulimuona tajiri sana na duka lake pale kijijini.SIFA zikamulewesha,akaenda Musoma mjini.Guess what??nafikiri unajua jibu.Yaani baada ya kufika Musoma mjini yeye na baiskeli zake alikuwa kati ya watu masikini.Hapo Musoma akatokea tajiri mwingine tena.Yeye alikuwa na gari zake.Nae akaondoka akaenda Dar,ile kufika tu Dar wala hakuhesabiwa kati ya Matajiri.Sasa endeleza huo mlolongo hadi ulipo na ulinganishe na tajiri wako.
Tunapozungumzia ELIMU kwa huyu bwn mdogo ni ili tumsaidie awe na upeo wa kuelewa mambo.Bob Sambeke una-sound kama uko nje ya nchi.Hebu nambie mwanamuziki wa kimarekani ambae ana Elimu kama ya huyu bwn blue.Kwa bandiko lako hili naku dadicate mwimbo wa “GRADUATION” wa Kanye West.
Pia sikuachi hivi hivi,nakupa kazi ya ziada ya kutafuta maana ya neno Elimu na Tajiri.
Wasalaaamu.
Majita
Hombiz, Umenena!!! Nashukuru kwa kuandika ujumbe huo. Vijana wengi sana bongo wamebaki kujifananisha na black americans na kujipa false hopes in the amount of money they have in the bank.
Yardsticks wanazotumia kwa kujipima maendeleo nazo ni hoi vilevile.
Bob Sambeke usimdanganye mtoto wa watu. Uwezo wake ni mdogo sana kuhimili mabadiliko ya uchumi na maisha kwa ujumla. The poor boy has a backbone which can only last him 5 more years if he is lucky. What next?? the boy ain’t 25 years old even !! Do you think those 2 used vehicles and a house will secure his future? The future of his family? Think again.
Lady JD and mr Blue are in two different leagues. JD has corporate support and power, Mr Blue has none of that. Let him go back to school and polish the minute knowledge he has.
Mina El Faidhina Ustaadhi Matty. Na kwa wote mliobaki… Eid pilau kwangu bwana (kama unakujua na unaweza kufika)…. vinginevyo mkono wa Eid nitawapa tukikutana hahaha.
Edo naona uliondoka kitambo na bado hujarejea ku nyumba. Dogo huyu bwana ni bwana mdogo sana, kiumri na kifani.. si wa zamani. Alianza kuwika kipindi sipo Bongo.. nikaenda likizo 2004 nikakuta yupo juu na kibao BLUE BLUE. Niliikubali kazi si kitoto mzee. Mara akaja na mapozi, then Nipo, n.k.
Kwa ushauri.. uwe unafuatilia youtube track mpya na pia waulize ndugu jamaa na marafiki popote walipo Tz.
By the way waungwana… nimekumbuka kipindi cha KLABU RAHA LEO… SHOOOWWWWWWWWW!!!!!!!!!! hahaha.. old skool eh?
BOB SAMBEKE INAONEKANA NA WEWE HAUJASOMA
COZ HAUWEZI KUTETEA UJINGA KAMWE HUWEZI
MLINGANISHA MTU MWENYE ELIMU TENA PROFFESOR
NA LADY JD PESA SI KILA KITU KATIKA MAISHA
UKIWALINGANISHA WATU WAWILI KAMA HAWA
NI KAMA UNAKUWA UPOTEVU WA NIDHAMU
PROFFESOR NI PROFFESOR
HUYO LADYJD NA PESA ZAKE KUNA MAMBO MENGI
YUPO NYUMA KIMAISHA PESA CANT BUY YOU THE WORLD!
MTAKE RADHI PROFESSOR LUANGA
Kumbukeni UFUNGUO una FUNGA na KUFUNGUA,Huu usemi wa kusema elimu ni ufunguo wa maisha !!!!
wengi wemefungiwa na fungo Elimu,kwahiyo ni kijana kujipanga tu,ukiwa na hela unaajiri wasomi waprogram maisha yako!!!!
wabeba box wako wengi na degree zao,Pata hela,tangaza ajira uone,watakavyomimina mibarua,wote wamechoka na kazi za box
matty shosti asante kwa salaam za idd
Oh God help these people from Ignorance. Humu wamo wasiojua wanachokisema na wengine wanosema mambo coz ndivyo yasemwavyo na wengine.
Guys you need to understand what you are looking for in life kabla ya yote. Kama unataka kuwa daktari lazima uende darasani mana udaktari si kipaji ni shulee, vivyohivyo kama wataka kuwa na fani nyingine. But it does not mean lazima kila mtu awe na degree duniani!!! Huo ni ulimbukeni na ushamba wa mambo. Waloenda shule wakapata fursa ya kusoma falsafa watakuwa wanajua kuwa Aristotle alishasema kila mwanadamu anatafuta furaha. Happiness ndio ultimate goal ya kila mtu. So ni njia gani utaipata ni kupitia mambo mengi lakini dunia imeamini usipokuwa na pesa huwezi kuipata. So money is just a means to achieving happiness. Sio shule sio kuishi ulaya.
In other words i support what this young guy did as long as yuko fucused. Kuna wajinga wengi tu wanasoma coz baba ana ada ya kumlipia lakini hana dira, na at the end of the day maisha ni misery kwake tu. But wapo wengi wamefanikiwa bila kwenda vidato viiingi maadamu wamepata universal primary education ya kuwaongoza maishani.
Kuna mwehu mmoja hapo juu anasifu marekani kuwanyima visa na anashoboka na mitaa ya US as if kwao..sasa mtu kama huyo atamshari vipi Blue kusoma wakati kama yeye amesoma ndo akili yake imeishia hapo??? Jacko Wacko alianza music at 13 years sijui kama alikuwa ashagraduate by then na sijui kama graduates wa kibongo kuna anayemzidi hata housegirl wake kipato.
Acheni ufinyu wa mawazo tuliosoma its for us and our children, waliojaliwa vipaji they have equal chances to win better life. Huyo anayejidai kasoma na yuko US kubeba box na kuosha vyombo hotelini hawajui akina Lil Wyne na Cash money nzima, 50cent, wote waliokimbia shule but wanaishi kama wafalme???
Blue you keep yo head up …you have a bright future son.
Bob Sambeke ungekuwa jirani ningekupa lager mbili! kila mtu kakomalia shule shule, si kila aendae shule ana mafanikio, wapo walioenda shule na wanasaga lami mtindo mmoja, kutwa kucha wamebeba tumifuko twa karatasi tuna CV ndani, kama yeye kachagua mziko ni his option! matty uko wapi na personal decision ya mr blue. haaaaaaaaaaaaa. weekend njema.
kijana anajitahidi lakini kitu muhimu ni kumix ngoma za kinyumbani na za kisasa na pia kuacha kujiweka kimarekani maana wamerekani hawatanunua nyimbo zako lakini sisi wa nyumbani tutanunua. Kama shida yetu ni kusikiliza wasanii wanaofanana na wamarekani basi hatuna haja kusikiliza wenzetu bali wao wenyewe.
Matty asante kwa salam za idd, nashukuru nimekuwa wa kwanza kutajwa kwenye list, thanks mami
mdogo wangu umependeza sana .but do me a favour….. go back to school get your GED……..We love you hommie dont think we hates you…. No matter what go west or south.. Diploma fir…………..st……….., No body going to ask you about
tatoo,the gona asking you where the white paper not tatoo.
where are you now, wake up hoooommmmiiiiieeeee
Much love hommie
Shule inabaki kuwa ni jambo muhimu hapa!. Nyie wote mnaopinga swala hilo vigezo mnavyovitumia, haviingii akilini kwangu hata kidogo. Kama nilivyotanabaisha hapo awali, elimu ni jambo muhimu sana ktk maisha ya mwanadamu. Mchangiaji # 30(mimi),hapa kinachoongelewa ni umuhimu wa shule kwa hawa vijana wadogo waliojikita kwenye fani ya bongo flavar bila kuipa elimu kipaumbele. Swala la furaha hiyo ni topic pekee inayojitegemea kabisa. Unaweza kuwa apechi alolo na bado ukawa na furaha. Kwa mfano, kuna documentary niliangalia kwenye TV ambayo ilionyesha maisha ya bush man ambao hawajasoma kabisa lakini wanafuraha na maisha yao ile mbaya huko polini. Ila wangekuwa wamesoma, pamoja na furaha yao, elimu ingewasaidia kuyakabili na kuyabadili mazingira yao na kuwa bora zaidi kulingana na wakati. Pia kwa taarifa yako Michael Jackson yuko kwenye matatizo makubwa sana ya kifedha kutokana na matumizi mabovu ambayo bila shaka yanachangiwa na ufinyu wa elimu yake. He has a billionaire’s spending habit, but a millionaire’s budget. Michael is” a “spendaholic” who racked up $35 million in annual bills while earning just $12 million a year. Sasa angekuwa na elimu nzuri kweli angefanya ujinga huu wa mali bila daftari?.
Kwa mdau aliyezungumzia visa ya marekani, huyo sijui ana maana gani. Nnavyofahamu mimi ni kwamba ubalozi wa marekani haumnyimi mtu viza kwa ajili ya kuwa msanii wa bongo flavar na sababu nyingine zisizoleta maana. Sababu pekee wanayompa mtu visa ni kutimiza matakwa yao. Kama hutimizi matakwa yao, basi hawampi muombaji viza. Huo sio ukweli hata kidogo.
Wakati huo huo mchangiaji namba 30, sio kuwa kila mtanzania aliyesoma anayeishi marekani, anaosha vyombo hotelini kwa wazungu na kubeba box. Kuna watanzania wengi wasomi wako Marekani Kaskazini ambao wamesoma vizuri na wana kazi nzuri sana zinazowalipa vema kabisa.
Swala la kina Lil Wayne na wasanii wengine wengi ni kweli ma-milionea. Lakini kwakuwa shule haipo kichwani, basi na matendo yao yanalingana na uwezo wao waufahamu. Ndio maana wengi huishia kwenda jela kwa uhalifu wa kijinga na wengine hufilisika kama Mc Hammer.
Ngoja niishie hapa kwani siwezi kumaliza hii topic nnayopenda kuitetea kwa nguvu zote.
mhh hii kali!
Any nipo mamangu wewe tena lazima uwe wakwanza kwenye salamu zangu aisee, ila hz personal decision za MR.BLUE NI BALAAA!!ngoja kwanza na mimi nimtapikie bob sambeke!
anyway BOB SAMBEKE umeraruaraua hasira zako lakini mshamba ni wewe unayeropoka tu sijaona point hapo, hv ingekuwa ni mwanao huyo ungemshauri afocus mbele ipi??without education?au kwa kuwa ni mwana wa mwenzio??
Tunachosema umri mdogo anatakiwa arudi shule, mambo mengine baadae KAMA kitabu kikidunda poa tu atasaka life kwa kubana pua, suala ni kuwa AMEACHA SHULE SABABU YA KUFLOOOOOOOOOOOOOOO (MZIKI)
HOMBIZ umemaliza KAKA! Bob Sambeke get a life!
watu wanavyo jifanya kuijua US hatari,utadhani walizaliwa huko.mr blue we kamua,kama muziki unauwezo wa kukupa hela za kujenga/kununua nyumba,mlo wa kila siku,kuwa na kagari kamoja ka kuzungukia hapa na pale,kwa kifupi maisha mazuri,we endelea,kama show 1 inauwezo wa kupata mfano Million 4 poa sana, mtu unafanya kazi mshahara kwa mwezi laki 2,hiyo M 4 itafika lini si miaka?
unaweza pia kusoma ukiwa home na siku ya paper unaenda kufanya au hadi uvyae uniform ndo wajue unasoma?watu wote tuna tafuta pesa,cha muhimu uweze kusoma+kuandika+kuelewa.kama muda huu ndo channel za pesa zipo wima sasa plzzz bora utafute kwanza, elimu haina mwisho kama unania ya kusoma utasoma tuu hata gumbaro. pesa tafuta ukiwa kijana,uzee kupumzika.
huyu bwana mdogo kwa nini katika kila picha anayopiga ni lazima abetue midomo…mara ajing’ate, mara arambe ulimi, mara sijui afanye nini…..mimi sijui kwanini labda waungwana mnielimishe kwamba ameshauriwa afanye hivyo kwani ndio anapendeza au vipi……
CHUKUA HII
1.Habari Zenu Wabeba Box,Hombiz,Majita,sexycecy,bimkubwa,matty na wengine wanaonidiss me kwenye comments na kumdiss
blue kwa uamuzi wake
2.Big Up Mh Lukamba,Mimi na Any kwa kuwa na mtazamo mkubwa wa maisha wa kuangalia pande zote za shilingi na co ao
wenye mitazomo ya mwaka 47.
3.Nyie watu kumbukeni Elimu ni pana sana na co mnavyofikiria.Kuna 4mal and in4mal education nadhani mlitambue hili
wazeya.inawezekana kabisa mr blue asiwe na 4mal education hiyo mnayong’ang’ania ya kukariri madesa but akawa best kwenye
in4mal education ambayo inamuwezesha kukabiliana na mazingira halisi kumbuka hata charles Darwin alisema kwamba “It is not
the strongest of the species that survives, nor the most intelligent, but the one most responsive to change” kama wewe unafikiri
kwamba ukisoma ndo maisha utayaweza kweli wewe utakuwa una upungufu wa kufikiri kichwani(UKUKI) hata mari andrreti
anakwambia “If things seem under control, you’re just not going fast enough.”,Life its all about challenge and how you overcome
those challenge me nampa 10 na co 5 mr blue…Keep it on ..hustler
4.Na wewew hombiz unaongea pumba tu..Ushawahi kumuona m2 anapush vogue kwa kutegemea mshahara wa kila mwezi,acha
ujinga wa mawazo Kila m2 atafanikiwa endapo atakuwa serious kwa ki2 ambacho anachokifanya,big up mimi kwa kuwaeleza kuwa
kuna specialization co kila m2 awe na degree ona 50 cent ajaenda shule lakini he the richest rapper ever na anabuni miradi
mbalimbali sasa anatumia nini kubuni hiyo miradi wakati shule ana? you get my point
HABARI NDIO HIYO
matty al faidhina best duuh umeona wadau walivo na hasira? frank ndugu yangu hizo ndo poz za wanamuziki wetu wa bongo flavour, wangekuwa na uwezo wangeng’ata hata masikio.
Bomb Sambeke!
Relax ma dear unakuja kiswahili swahili sana mbona???
Hakuna nini wala nini dogo arejee shule thats all!hakuna changamoto yoyote ile ya kufikirisha bila kuwa na elimu hasa kwa dogo kama huyu BLUE, labda kama tunasadikika na never hawezi kujifananisha na hao kina 50 cents kimafanikio.
Bob Sambeke! Tatizo lako ni: “hujui kwamba hujui”. Ingekuwa afadhali kidooogo kama ungekuwa, “unajua kwamba hujui!” Na ni jambo baya saana kumpigia mbuzi gitaaa!. Kwani akitikisa mkia wewe utafikili anafurahia milindimo ya gitaa lako kumbe mbuzi yule anafurahia utamu wa majani.
Education is the vision for one’s eyes to see the world:
Education encompasses teaching and learning specific skills, and also something less tangible but more profound: the imparting of knowledge, positive judgment and well-developed wisdom. Education has as one of its fundamental aspects the imparting of culture from generation to generation . Education means ‘to draw out’, facilitating realisation of self-potential and latent talents of an individual. It is an application of pedagogy, a body of theoretical and applied research relating to teaching and learning and draws on many disciplines such as psychology, philosophy, computer science, linguistics, neuroscience, sociology and anthropology. Nashukuru wadau mnaothamini elimu kwa kujaribu kumshauri huyu bwana mdogo. Shukrani zangu ktk hoja hii ziende kwa wachangiaji wafuatao:
Matty, Usinijue, Mzangibari 100%, Edwin, Ndaki, Dinah, tongenyama, kekeu, Winnie G (ingawa sikubaliani na wewe “Winnie G” ktk swala la kuwanyima viza za U.S.A. vijana wa Tz), Sister TZ, Olive, sexycecy, na neema. Kwa wengine waliotoa hoja za kupinga swala la elimu, nasema “shame on them!”. Natarajia mtalitazama swala hili upya na kuepusha kutokea kwa disfunctional families ktk maisha yenu!
Always,
SHULE KWA KWENDA MBELE, HAKUNA KUKIMBIA UMANDE!
Tatizo nyie wa2 wa madesa mnakasumba nisome nipate kazi niwe na maisha mazuri lkn ukimaliza unasaga lami we mpaka sole zinaisha,mvua na jua lako,kila siku upo barabarani na mifuko ya kaki..Na ukija kupata kazi ,kazi yenyewe gros 200-900usd.Then kwa mshaara huo unaweza ukatoka na maisha haya.kwahyo utaona wa2 wengi wakiajiriwa wanatafuta dili za umo ofcn kwao ili waweze kuinua kipato,ndo wanaanza kuibia mashirika na makampuni mengine.
Kwa wa2 kama ao elimu inawasaidiaje,we utaibaje kwenye kampuni au shirika unalofanya kazi we auni ndo mwanzo wa kulifirisi shirika?
Mr.Blue Komaa na gemu,kwani kusoma mpaka uvae uni4m na utangaze kwenye magazeti unasoma kuna open school kibao
kwahyo we komaa…Dogo unatisha full respect unawapiga bao wa2 kibao wakiwemo wabeba box ndo wanaokudiss sana kama ukichunguza…Inakuwaje we una nyumba wakati wao wanalala chumba kimoja wa2 10..Halafu wanatuma maemail hooo nina maisha mazuri sana huku kiwanja,kumbe hamna ki2 chochote! Kila m2 ana nafasi ya kuwin no matter umesoma au ujasoma?
Y’ all heard ..Matty na wenzako
cn u email me on arianeu94@hotmail.com
plz!!!!!!!!!!
Wewe unaejiita bob Sambeka huo ushauri naona kama unawafaa ukoo wenu wote ni vizuri kama utawashauri kizazi chako chote kisiende shule ili baadae waje kuwa kama 50 cent. HABARI NDIO HII
Matty…..aksante kwa salaamu za eid
hhaha kazi kweli kweli!
Matty huenda alishajipima akaona akienda school atazungusha, so akajiwahi sekta ingine! unless kama alifaulu kabisa kuendelea akagoma,. mi simjui background yake, so i cant say much!
Dogo, Elimu ni muhimu, pesa utazipata, zitakwisha lakini ukiwa na elimu ni hadhina kubwa. Popote utapokelewa lakini ukiwa ignorant nani atakuchukua?
du ishakua soooo
Hicho kitoto kimeanza kuota ndevu.tumekilea naona sasa kimeanza na kutunisha misuli.Ila big up dogo.kusoma nini.dodo ame identify mziki kama proffessional na anakipaji.mwacheni aendelee.graduate analipwa shilingi 300,000 take home ktk nchi ya Tanzania.wakati dogo akifanya tamasha moja basi ana uhakika wa zaidi ya 500,000.na halipi kodi.acheni usenge.tatizo mmzoea kwamba kila mtu atatoka na shule.
Bob Sambeke!
hahahahahhahahahaa hujui kama hujui tu na utabaki kutojua tu!Hombiz chukua big 5 umemaliza!
Utaweza iba vipi bila ujanja kichwani hata mafisadi wa EPA, RICHMONDULI pia wamesoma.
Acha zako wewe bob sambeke dogo arejee skonga tu!
nditu kiswahili sanifu…hazina na si hadhina,upoooo?
kula 10 mtu wangu halima kweli huo ushauri unafaa kizazi chake chote, naona ameshaanza kwake siunaona hata mawazo yake ni ya mtu ambaye hajaenda shule come again bob sambeka usijeukampeleka shule hata mjukuu wako wote watakuwa nyamihela utakula kiulaini, huku ukiendelea kuota huku unakimbia halafu baadaye utaona maisha yanaendaje.
wewe kuku wa kienyeji acha kutoa maneno machafu kwenye hii blog kumbuka humu kunawatu wenye akili timamu, so jaribu kuwa muungwana sio unatukana watu hapa. Nani umemuona ameshikishwa ukuta hapa? jaribu kuwa mstaarabu
Mr blue umekosea mahesabu ungeenda shule halafu mziki, unafata muziki upo tu, ungepiga tu mziki na watu wangeukubali,lakini shule ina inapendeza kusoma ukiwa na umri mdogo yaani bila majukumu, wewe unawaza shule tu, sio kama ukiwa na mke au watoto ambaoo nao wanamatatizo yao, shule haiyendi vizuri.ushauri wa bure ufanyie kazi.
siri ya mtungi aijuaye ngata,blue kaka rudi shule,muziki kwa TANZANIA ni bado sana,JAPO UMEKUA KIDOGO SANA
si wakuutegemea.NI WA UMAARUFU TU,UKIJIANGALIA MFUKONI HUNA KITU.INABIDI UTUMIE AKILI SANA ILI UWEZE KUISHI NA SI MUZIKI PEKE YAKE.usanii bila shule haufiki popote ndugu yangu.mimi baba yangu nae alikua msanii kama wewe,ila ALIENDA SHULE, alisoma enzizileee,NA ALIKUA MMILIKI WA BENDI KUBWA TU TANZANIA KAMA UNAIJUA SAFARI TRIPERS ILA WENGI WANAJUA ILE BENDI NIYA ……….,YULE ALIKUWA MWIMBAJI TU,ILA MMILIKI NI BABA YANGU,BABA YANGU NDIE ALIEMFUNDISHA MUZIKI YEYE…..KUPIGA GITAA,KINANDAA,NGOMA,KUIMBA NA NK.
…..ALIKUA AMEAJIRIWA NA BABA YANGU.BABA YANGU ALIPEWA NA BABU YANGU MTAJI WA KUANZISHA BENDI.WALINUNUA KILA KITU KINACHOHUSIANA NA BENDI YA MUZIKI,AMBAVYO VITU VYOTE HIVYO VIPO NYUMBANI KWETU…… HADI LEO HII.HAJAUZA HATA KITU KIMOJA.BENDI ILIPOKUFA,ALIPOANZA KUUMWA,HAKUWEZA KUENDELEA NA MUZIKI.KISOMO NDICHO KILICHOKUA KINAMSAIDIA.KIPINDI HICHO ALIKUA NAKAZI YAKE NZURI TU.HADI ALIPOZIDI KUUMWANA KUACHA KAZI.
WANAMUZIKI WENGI WA TANZANIA HAWAPENDI KUWAPA UMAARUFU WALE WALIOWAFUNDISHA MUZIKI.MARA NYINGI WANAMUZIKI WAKIHOJIWA WANASEMA OHHH MI NILIANZA KUPIGA GITAA,KINANDA TOKA NIKO MDOGOOO.NI UONGO WA HALI YA JUUU.HATA MUNGU HAPENDI.KUWENI NA UPENDO KWA WENGINE.HAKINA MAREFU YASIYO NA NCHA
Aiseee!!!!!! mbona baba yangu zimekuwa nyingi hapo duh sielewi wajameni mada imetoka out imekuja baba yangu insha mhh na hiyo methali hapo mwisho mhhh iko sawa kweli?
mchangiaji “watubwana”. Umetoa comment nzuri sana!. Natumaini itasaidia kuleta mabadiliko chanya kwa wasanii wengi wa muziki wa bongo flavor!
nashukuru sana hombiz kwa kunielewa,asante sana.
blue nenda shule,kinacho hitajika katika maisha ni DESTINATION yaani kule unakoelekea,FUTURE na si sasa,sasa hivi utakua maarufu na kupata pesa,je unainvest sehemu?zitaweza kukusaidia hapo baadae?elimu ndio ufunguo wako,nenda shule.nakumbuka kuna wimbo kabisa uliimbwa unaitwa ROZA NENDA SHULE,kama unasikilizaga zilipendwa.
lil wayne yupo university of houston longtime since when he was promoted CEO of his label CASH MONEY so man dont just run ur mouth…u got do lil research b4 u drop some lines dont mislead peeps
one love, watubwana!
stay up, always
kuna watu wanatoa hot point mpaka basi yaani,na sababu hii inawafanya wajenge uadui na wenye point pumba. but worry not,keep it up! blue just go back to school,hao wanaosema usiende shule ukichunguza sana wana biashara za ajabuajabu tu hawana future direction. siku zote mtu aliyekwenda shule anakupa shauri mzuri. Hao wanaosema eti kuna watu wamesoma na wanasaga lami hawana target ya maisha na wanaagalia kitu kimoja, i mean hawana alternatives to their future. Sasa we mtu labda kasomea science,may b ana ndoto ya kua engineer akashindwa(fail) mitihani,sasa kama huna alternatives to your future lazma utasaga lami na kusema elimu haina mpango. Kumbe wewe ndio huna mpango. Mtu unaweza kuamua hata kwenda ualimu,japo haulipi ila unaweza ukawa na tution inakuingizia kipato,sio muuza vocha anaewaza utajiri. La unaweza kuamua kujiunga na upolice kutokana na level yako ya elimu,japo pesa ndogo ila mwisho wa mwezi unaingiza,kusoma sio lazma upate mamilioni acheni mawazo ya kitoto. Kwa sababu polisi huwezi kumfananisha na muuza mitumba anaefukuzwa na mgambo kila siku.Zipo mbinu nyingi za kufanya kufight life hata kama umefanya vibaya shuleni ila ukikata tamaa lazma usage lami uje sema elimu haina mpango.Watu wengi wenye mafanikio sio kwamba walipata a kwenye vyeti vyao.Huwezi ukaishi kwa kutegemea entertainment wakati kuna competition ya ajabu inayokuja nyuma yako,wanamziki kila siku tunawasikia wanajiita maandagraundi, Sikia kitu chochote ambacho ni participated by society kinakua competitive,na lazma uwe competent.Ndio mana msanii leo kavumaaaa,kesho kaingia mitini maana hawezi huo ushindani.Akina mr nice walikua na pesa sana tu,mbona alifilisika,low knowledge.Ukiwa na elimu bwana hata kama hauna pesa ur still the best!Nchi yetu bado inaendelea msije kujifananisha na nchi za wenzetu walioendelea ambako hata mtu ukiwa huna kazi basi utaclaim benefit unaishi kwa kulipiwa nyumba na kupewa pesa ya chakula. Wasanii wa bongo wanatakiwa waishi kama wako kwenye developing country na sio developed ones,mkifanya hivyo lazma mtapoteza.Mambo ya kufananisha tz na america mnakosea sana jama,hivi america wametuacha nyuma mile ngapi?tchao
i up grade u hilly.thanx 4 the comment.
du!imeshakuwa topic
BLUU USIWASIKILIZE WAJINGA WOTE WANAOKUSILIBA UNAJUA NA UNAWEZA ENDELEA HIVYO HIVYO MAISHA KOKOTE SIO UKISOMA NDIO UTAWINI MTU UKISHAJUA KUTAFUTA ELA TU KUSOMA INAKUWA MTIHANI AU HAWAJUI TAKE CARE HAPPY VALENTINE MAN………………………………….LILFUE
MR BLUU UNAJUANUSIWASIKILIZE WAJINGA WANAOCHONGA OHH SHULE HATA MZIKI SHULE HAWAJUI NINI?
mwanangu nakufagilia sana.
kwa mtaji huu wa kupeana ushauri usio na kichwa wala miguu,MUZIKI NAO NI ELIMU EE???nyie ndio walewale.BLUE kaka unapta tu hapo,baadae u wl need 2 stand 4 ur slf no 1 wl b there 4 u that time,hao wanaokushauri elimu is nothing,wanakupotosha,rudi shule,tafuta anything usome,hata kozi yoyote rahisi soma na muziki wako fanya ila usiitupe ELIMU.Ikitakusaidia siku moja,na si muziki wa TNZANIA,WEWE bado ni kijana mdogo na unanafasi ya kubadilika na kukubalika katika jamii.plz nenda shule.mcheki FA anaaltenatives nyingi za maisha,si msifii bt ndio ukweli,muziki ukiwa ovyo bado anaelimu yake na hatolala njaa.na ataheshimika vilevile.anaweza fanya kazi na kukaa popote pale cz of education.ni hayo tu kaka
ur gud bayser,i really apreciate what u do in musics, but to be fare go back to skull mto be in safe side musics is there any time,whereever ur will get more as ur hav skul in ur mind.stay blessed i do support tanzanian musics, i do support you
Upo juu mwanangu wa ukweeeeeli unatisha mbaya…ila kama hutojali 2tafutane nikupe ma idea yatakayokufanya uzidi kuwa juu na juu ndani ya miaka mita2…..mfadfadia@yahoo.com/0653011313
napenda sana music yako
Kijana ulipo c kitu unachokifanya ndicho muhimu,kaza buti na kile unachokipenda, maneno maneno kawida yao.
MZEE BLUE KWANI UMEWASAHAU WABONGO KWA KUWAKATISHA WATU TAMAA? HASA WAKIGUNDUA KUNA MAFANIKIO ? IMEKULA KWAO HAO WENYE NTANDIO WA UBONGO, JIFUNZENI KUWATIA MOYO WENGINE WENYE MAFANIKIO ILI WAENDELEE KUSONGA MBELE KWANI SAFARI NI NDEFU YA MAISHA HAIJALISHI NI KTK NYAKATI GANI ! OK ! G9T
BIG UPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPPP!
mchizi nampa big up kwani yuko juu
u r my favourite male artist in Tanzania. big up sn
Some guys really turn me upside down, hivi wat’s big deal between Music(Talent)and a formal (class) education? One needs to get a school background purposely to surface his/her slim chances towards proper stuffs management in which case i wish to catigorize them into two broad aspects; TIME and MOVEMENTS(tolerance,charity,respect,job searching, and even the talent itself, etc)where then, having good encompassement of the above two recipes attracts stable financial position all the way out….!!! Never the less, Ikiwa hauna elimu kama hiyo tunayomshauri Rapa Kabayser kuwa nayo bali una kipaji cha kufanya music au kitu chochote kile ambacho matokeo yake sio tu ku-make excess money na kuishi platnum life style isipokua ni pamoja na kuwaajiri hao waliosoma (The Graduates) kukutengenezea misingi bora ya kufuata katika maisha yako yote ili kamwe usiporomoke basi unaweza ukajiuliza yanini kurudi darasani wakati you almost have everything in place.Kama 50 Cent ameweza kutumia zaidi ya 40% ya mapato yake kuajiri watu na systems mbalimbali for self security atashindwa vipi Mr Blue a.k.a Byser na hawa wote hawana elimu? Sipaswi kuilinganisha America na Bongo but talent does not see whether you from Asia,America or Africa, in the poor country like Tanzania thus why you now can see and feel the taste of African stars Akon and Drogba (Just to mention some) hitting the history of America and Europe all over. The same can be done by a so called Dogo, Tanzanian musician Mr.BLUE without admiring standard of education to propel him away to the World of Wonders and even go across the streets of New York,Califonia,Los Angels etc, and enjoy the rest part of his life time there.
******************************************
Kwa upande mwingine najaribu kulinganisha mada hii na swala lililozungumzwa na kiongozi mmoja wa maswala ya sanaa ya Tanzania pale Leaders Club kwenye Tamasha fulani la wasanii wa muziki wa tamaduni za Africa (Tanzania), alimponda Mr.Blue kwa kuonesha kutofurahishwa na tungo zake zinazoelezea mapenzi kwa kina ilihali yeye bado ni mtoto mdogo,hajui mapenzi,anawezaje kutunga na kuimba vitu vikubwa hivyo. Mzee, hiyo ndiyo Talent, maana yake ni kuweza kufanya kitu ambacho mwingine hawezi sasa unashangaa nini hapooooooooooooooooooooo? Lakini pia unapaswa kukukumbuka kwamba kuimba wimbo sio kutunga wimbo, wapo wanaoimba bila kutunga,wanaotunga bila kuimba na pia wapo wanaoweza kufanya vyote mfano wake MR.BLUE a.k.a Byser a.k.a Lil Sama a.k.a Platnum rapa a.k.a Babylon a.k.a Bishoo…… Am out.
unataka kupigana na nanio maana ulivyouma hayo meno kaka,hiyo tatuu umechora na peniiiiiiiii?
KWA KWELI DOGO UMEWAKOROGA WOTE.
Bayser babu,unaona vipi ukijiingiza ktk swala zima la kucheza movie?
Kama wasanii wa mbele(nje) yeah!Are da one inspired us,pliz!put diz on practice cuz we mkali na unaweza babu!
blu ur the eva best!! ur my favourite tz muscian!! U ROCK!!
kip t up
whats up
Asalaam!
Nimefurahia pande zote mbili zinazotoa comment juu ya Mr Bluu..music au shule.mimi niko upande zaidi wa music.
mimi naona hapa shule anayohitaji mr bluu..ni ya kuendeleza muziki wake tu na kuwa na utawala bora.haitaji shule tunayoifikiria wengi wetu hapa.japo nchi yetu haijaendelea kama zingine hiyo aijalishi.pesa anayotengeneza ni nyingi alafu ni dogo..music utahitajika sikuzote za maisha na ni umaarufu zaidi ya hata kuwa daktari.nikiwa DAKTARI NTAKULA RUSHWA NITOKE.mwanamziki hela yake ni halali alafu nyingi.so hiyo pesa yake aliyonayo amnunue mdau mwenye shule ya mziki na utawala bora. kazi iendeleee akimwibia amfukuze kazi, atafute mwingine.hata yeye mr bluu sio mjinga akiibiwa atajua..ndooo maana bado dogo na akili yake iko juu kajenga nyumba na ana magari so Mr Bluu.bigup.somea kupiga tarumbeta na kinanda kwa ajili ya mziki wa badaye tukizeeka tusikilize..tusiboreke.
hey,hey ppl
mr.blue is taken by me so stay as far as you can from him mr.blue + arbay forever tume pendana mpako mwisho…. he is my everything
ahhh i freak’n love you bby
keep rockin…
mpenzi wangu mr.blue
we ni nowmaaa,untachabo baysa,yang babilon, smart guy, u rock tz, we ni mareee
tsup ma people!!!1
dah mshikaji(Blue)anatisha mbaya yani me nampa 100% kama kwenye hii ngoma mpya ya Jay Dee ametisha mbaya.
KIP IT UP BRO….!!!!
Elimu ni chekeche inayochekecha na kutenganisha kinachofaa na kisichofaa;inabainisha lipi jema na lipi baya.Elimu inamuongoza mtu kufanya linaiofaa na kuacha lisilofaa.Kwa kusema hivyo namaanisha kuwa ELIMU NA MAADILI YA JAMII HAVITENGANI.Daima wote wasio na elimu(chekeche) wanaiga au kufanya mambo yasiyokubalika na jamii,mfano wanaume kusuka,kuvaa hereni,kuweka nywèle dawa na upumbavu mwingine usiokubalika kijamii.
Kwa ufafanuzi huo juu,si Mr.Blue peke yake aende shule;na wasnii wengine kama HEMEDI,BANANA na wengine wanaofanya mambo ya kike na wote wanaofanya mambo yasiyofaa,hata wasio wasanii(hata sisi tunaochangia mad hii katika blogu hii)
Kwa hiyo;uwe una uwezo,uwe kapuku au uwe na hali yoyote kiuchumi,kama somo la maadili linakushinda kulitekeleza kuna mambo matatu;
(1)Huna elimu.
(2)Una elimu ila haikusadii(mzembe).
(3)Una elimu angamivu-elimu inayoangamiza kama siyo kubomoa.
Yapo mengi ya kusema kama siyo kuandika,kwa sasa acha niishi hapa.
E bana uko juu m2 mzma,Ila unajua nn blu…Go back skonga yan ila mpngo mzma unafnika kichiz Dogo!
kabayser nnakuubali sn jembe langu,ujue nn swagger zako ni noumeeeeeeeeeeeeer.pamoja sn mzazi
bob sambeke…
kati ya wajinga wote waliopo duniani wewe unaongoza
mi naomba usiige utamaduni wawenzio usipo jichora huonekani huonekani kwan hereni zanini kaka
Namiss Mr. BLUE!Bado yuatamba ama ndo vipi?Namtakia kila la kheri hayo mapozi jo!Nammiss tu xana!!!!