
Pichani ni Jenerali Ulimwengu.Huyu ni miongoni mwa waandishi wa habari nchini Tanzania walio na uwezo wa aina yake katika kujenga na kubomoa hoja iwe ni katika maandishi au maongezi.Makala zake siku hizi zinapatikana katika gazeti la Raia Mwema.
Photo/Bob Sankofa
Feedback / Comments
49 Responses to “JENERALI ULIMWENGU”
Leave a Reply


sending...
nafungua computer naona sura ya mtu ambae kwenye maisha yangu ana mchango mkubwa sana.
Nilimfahamu huyu baba miaka mingiu iliyopita.Nilipenda sana kazi zake.Nilizidi kuvutiwa zaidi alipokuwa anaandika ‘RAI YA JENERALI’ kwenye gazeti la ‘Rai’ lilipokuwa ‘hai’
Katika umri mdogo nilijikuta nanunua gazeti la rai badala ya kununua magazeti “pendwa”(udaku).
Ulimwengu alinivutia nikajikuta naipenda fani ya habari pamoja na bwana mmoja kutoka uganda ambaye kwa sasa kajikita USA..Shaka Sali(sina uhakika na jina kama nimeliandika vema)anayeendesha kipindi cha straight talk africa.
Ulimwengu ni mwanahabari mzuri sana.Nakimis sana kipindi chake cha jenerali on maonday chanel ten.
Mola akupe afya njema ..wewe ni really BONGO CELEBRITY.
Kama usemavyo BC. Huyu jamaa ni zaidi ya Talk Show hosts wengi tuwaonao. Ana upeo wa ajabu na anatambua, kuchambua na kuchanganua mengi saana awapo kwenye kipindi (na hata katika makala zake).
Naheshimu saana kazi zake na naamini kwa wenye upeo mwema wanaweza kulitambua hili na wale wasiopenda ukweli na uchambuzi makini wataendeleza jungus zilizomfanya aambiwe si raia.
Blessings Jenerali
Edwin Ndaki & Mzee wa Changamoto, nakubaliana na nyinyi kabisa. Jenerali Ulimwengu, hiki ni kichwa!. Nimesoma makala zake nyingi sana ktk Gazeti la Raia mwema na kumkubali sana huyu mtaalamu. Anapembua mambo kiyakinifu na ananyumbulika kulingana na mazingira. Nafagilia sana wasifu wake wa nje!. Endeleza lieneke kaka, una haiba tosha kabisa ya kuwa muandishi wa habari..
Be easy bro!
Sawa kabisa.Huyu bwana ni nguli wa habari na mimi nilikuwa mmoja wa wapenzi wa gazeti la RAI kabla halijabadilisha sura yake ya cover hapo miaka ya 2007.Ila swali langu na hofu yangu ni kuwa:-
Hili gazeti wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (aliyepatikana Kikwete) lilikuwa linaandika habari nyingi sana za ku-critisize serikali na kuanika uliokuwa unajulikana kama “uozo” wa serikali,sasa je hatuoni kuwa hizi zilikuwa ni chuki binafsi kwa mh.Mkapa vs ulimwengu pia walilitumia kama kampeini ya kumuuza kikwete jambo walilofanikiwa na sasa tunaonja joto ya jiwe ya wanahabari hawa?????
Kama hii wasiwasi yangu ni ya kweli bwn Ulimwengu ulisaidia kumuweka kikwete hapo alipo na ahadi zake za ari,nguvu na kasi mpya baaasi “Maisha bora kwako utayaona uko siku za usoni pako.”
huyu jamaa unapozungumzia uandishi wa habari basi yeye anastahili sifa zote,nakumbuka katika makala zake za miaka ya nyuma alipokua akikosoa ama ukuwafumbua watz juu ya mabaya yafanywayo naviongozi wetu wa serikali kuu basi akasingiziwa kesi ya kuwa si raia wanchi ili afukuzwe, sasa sijui iliishaje maana niliondoka lakini namuona yupo anaendeleza libeneke la uandishi, mungu amzidishie
nakubaliana na wadau waliotangulia, Jenerali is a class apart katika suala la uandishi wa kalamu na pia mahojiano ya televisheni. Kila ninapokuwa Tanzania najitahidi sana niangalie Jenerali on Monday. Navutiwa na Bwana Ulimwengu alivyo mpembuzi mzuri wa mambo mbalimbali ikiwamo siasa, uchumi, mahusiano ya jamii, n.k. Ni mcheshi na mchangamfu na ana ufahamu na uelewa wa mambo mbalimbali. Kabla hajaja katika ulimwengu wa luninga tulikuwa tunapata makala yake ya kila wiki ya “Rai ya Jenerali Ulimwengu”katika gazeti la Rai, ambapo sasa makala hiyo imehamia gazeti ya Raia Mwema na inaitwa “Rai ya Jenerali”.
Ndaki amemtaja mtu mmoja wa maana sana pia. Shaka Sali. Star TV walikuwa wanarusha kipindi chake toka VoA
hiki ndo kichwa aisee nampenda sana huyu baba walai!
Safi sana! Hiki ni kichwa haswaa! Fani iko ktk damu. Hakulazimishwa kuwa mwana habari. Endeleza libeneke!
Nakupa heshima zote maana huna na huandiki majungu!
Nadhani huyu anaweza kuitwa mwandishi-nguli mwandamizi, gwiji wa uchambuzi, mtaalamu aliyebobea, mwenye upeo wa juu katika habari Tanzania. Huandika na kusema anachokiamini kwa nadharia yakinifu. Tunahitaji vijana watakaoweza kuendeleza libeneke kama yeye.
ubarikiwe Jenerali, kalamu yako idumu milele
Briliant man, ana upeo mzuri sana!
pia ni handsome, is he single? was just wondering.
Jenerali Ulimwengu ni kati ya waandishi wachache ambao bara la Afrika linatakiwa kujivunia.Ni watu wachache wanaweza kuwa na kipaji kama cha Jenerali.Mimi namfananisha na Charlie Rose wa PBS hapa USA.
Ni kati ya watu walio objective na kazi zao! Hajavamia fani ya uandishi! Ulimwengu ni zaidi ya muandishi! Ni mwanataaluma alietukuka katika uandishi na uchambuzi wa mambo mbalimbali.
Si mtu wa kukurupuka! Makala zake zimeenda “shule” haswa. He’s so inspirational kwa kweli!
Hi Guys kutoka Helsinki-Finland
Kwa kweli hata mimi ninamkubali Bwana ulimwengu, nimekuwa nafuatilia sana Siasa za Marekani tokea march, 2008 mwaka huu, nimependa sana waandishi wa habari wa Marekani kama Chris Methew, Davi Gregory, Rachel, Todd Chuck na wengine wengi ambao wanajulikana kama News analysts na wengine wako NBC political news analysts, kwa kweli hawa watu wanaonyesha uwezo wa kupambanua hoja mbali hasa hasa kuhusu kampeni za marekani, sasa kwa upande wa bongo ni waandishi wachache wenye uwezo kama ulimwengu, maana fani ya uandishi wa habari nchini bongo bado imevamiwa na waandishi wanaojulikana kama Kanyanga ambao wengi ni waandishi wa habari wasio na sifa wala Elimu ya uandishi wa habari. Lakini tatizo jingine bongo wamiliki wa vyombo vya habari ni wanyonyaji wanapenda kulipa pesa kidogo na kuajili watu watakao kubali mishahara ya kinyonyaji, ndiyo maana mtu kama ulimwengu amejiajili, mwenyewe
hongera ulimwengu
stay blessed
frateline
Any, naona umekuja na nguvu mpya ngoja asikie mkewe hahahahahahahahaha mimi namuona kazeeka lakini!
jenerali ulimwengu na wenzake na gazeti lao la Rai. ya dhamani zile ndiyo walionifanya nianze kupenda kusoma habari za uchunguzi, na mpaka leo sijaacha.
jenerali unastahili hongera kwa makala zako nzuri na zenye kujenga na ambazo huwasaidia watawala kuangalia mienendo yao. hongera mzee jenerali.
Mzee jenerali elewa kwamba umma wa watanzania unakupenda na umekuwa mmoja kati ya watetezi wakubwa katika jamii hii.
Mimi nakuomba urudishe ujasiri wako wa zamani.jenerali wa sasa nikama umebadilika kidogo na unaonesha kuwa muoga,generali wa sasa hivi,hajakemea richmond wala Eppa? na unaongea kwa mafumbo sana.
Nilizisoma kwa makini barua zako za wazi kwa rais mpya katika gazeti lako la zamani.kwa jinsi ulivyokuwa unaandika ilionesha kwamba ulikuwa na imani kubwa sana na serikari iliyoingia madarakani na ukadhani mzigo umetua na wakati wa kupumzika hata uandishi sote tuliamini hivyo.
baada ya kuona mambo yanaenda tofauti na ulivyotarajia umerudi tena lakini safari hii unaonekana muonga. yawezekana ni mtazamo wangu tu.
katika yote tunakuunga mkono na gazeti la Raia mwema ndilo gazeti letu makini
kila laheri mzee jeneral.
Nimeanza kumsoma Jenerali miaka ipatayo kumi sasa. Sasa hivi nikizikosa makala zake huwa sipati amani. Najisikia kuumwa.
Naomba Bongo Celebrity mtupatie mahojiano ya watu kama hawa. Nadhani kuna mengi sisi vijana wa leo twaweza kujifunza kwao. Vichwa kama Padri Priva Karugendo, akina Ryoba ni muhimu vikatafutwa viseme na kizazi cha leo.
Hekima na busara zako ndizo zinazo weza kuliongezea ili taifa letu wale wanao elewewa nini maana ya kile unachikiandika,moja kati ya Nakala zako zinafundisha nusu ya kizazi kipya manufaaa makubwa ya leo na kesho
Frateline, nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa kuhusu waandishi wa TZ. Lakini pamoja na baadhi yao kuvamia fani na wengine kuwa kanyaga twende, still wapo waandishi wa kweli na wasiopenda kuyumbishwa kama bwana Generali Ulimwengu.
Kuna jambo jingine kubwa ambalo mwenyekiti Maggid Mjengwa wa http://mjengwa.blogspot.com/ aliwahi kuliongelea kwenye makala zake. Jambo hili linahusu selikali kuwabania waandishi ktk swala zima la kuwapatia ruzuku. Alitoa mfano kwa kusema, utakuta muandishi wa habari anaambatana na mkuu wa Wilaya ktk msafara wake wa (ziara)kwenda kuhutubia sehemu fulani. Ktk msafara huo, muandishi anamtegemea mkuu wa Wilaya ndiye amlipie nauli ya kwenda na kuludi. Sasa unategemea muandishi huyo atakuwa huru kuandika vibaya kuhusu mkuu wa wilaya iwapo atafanya vibaya ktk ziara yake? Pengine anaogopa kuwa akiandika vibaya, mkuu wa wilaya anaweza kumwambia kuwa sikulipii nauli ya kurudi, na mambo kama hayo. Huu ni mfano mmoja tu, lakini ipo mingi kwakweli. Inaniuma sana ninapoona waandhishi wa kweli wanateseka na kufanya kazi ktk mazingira magumu kama haya. Wengine hufikia hatua ya kuhatarisha maisha yao kv kumwagiwa tindikali ama kuuwawa kabisa mithili ya Stan Katabalo aliyekuwa mwandishi wa kipelelezi, aliyefuchua kashfa ya roliondo iliyowahusu vigogo wa juu serikalini. MOLA amrehemu Katabalo. S. Inapendeza sana unapoona kuwa waandishi wa kweli wanaweza kujikwamua kutoka ktk ukilitimba wa kuendeshwa na waajili wao na badala yake kuweza kujiajili na kufanya kazi zao binafsi (za kiandishi) kwa uhuru wa kutosha.
Hi guys kutoka helsinki
Bwana Hombiz kwa kweli nikupata hoja zako za msingi kabisa, ndiyo maana kwenye comment yangu nimewalaumu wamiliki, waandishi wa kweli wapo ndiyo ila mazingira ya kazi bongo ni mabovu sana,je tutafika?
Frateline
Unapozungumzia waandishi wa habari,basi mzee jenerali ulimwengu,si mwandishi bali ni nguli wa waandishi wa habari ambaye anaijua taaluma hiyo vilivyo na kuheshimu miiko ya uandishi,acha waandishi wengine ,ambao wananunulika kama dagaa sokoni,ukitaka kujua kichwa cha huyu mzee ulimwengu ni hazina ya nchi,basi soma makala zake kwenye gazeti la raia mwema ndiyo utamjua huyu jamaa ni nani ktk uaindishi,mzee ulimwengu MUNGU akupe afya njema na akubariki ktk shunghuli zako
asante baba
Wee Matty, temea chini kabisa, kazeeka wapi! mi namwona bado kabisa.
we Matty.hata kama kazeeka.lakini kumbuka kuwa ujuzi hauzeeki,alafu kuzeeka kwake we kunakuhusu nini?
mi namkubali kwa pamba zake…
kwani ni lazima useme umetoka finland?makubwa…….namimi hi guys im fom kijtonyama dar hahhahhahhha
mmmmh! Frateline, sijuwi kama kweli tutafika kwa mwendo huu ndugu yangu! Kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa ki-imla hivi sasa, sipati matumaini sana!
Let`s keep our heads up and see what happens!
lakini kweli Any si ndo kama ule mpasho wa shosti wetu Malkia wa mipasho aluuuuuuuuuuu eti ng’ombe hazeeki Maini….walai yule mama kiboko hahahahaha!
majita acha uzushi
Matty mi nampenda bwana, ivi si mnatoka nae kijiji jirani niunganishie basi.
Hivi wadau mnajua kwamba kitaaluma JENERALI ULIMWENGU SIYO MWANDISHI WA HABARI?
HUYU BWANA KITAALUMA NI MWANASHERIA. ALISOMEA PALE UD. ILA UANDISHI NADHANI NI KIPAJI CHA DAMU. HONESTLY, MIMI SIKU NILIPOGUNDUA KWAMBA ULIMWENGU HAKUSOMEA UANDISHI DARASANI SIKUAMINI.
ANYHOW HE KNOWS WHAT HE DOES. MUNGU AMZIDISHIE BARAKA TELE.
Any, kwa hilo tu usijali nitaunganisha shosti!
Kahindi bibie nipishe nipite ujumbe wangu unakuhusu nini?? ulijuaje kama si……………………..
BC unabana sana mwanangu sikuhz!
WE MATTY UMEANZA KUSHUSHUANA LINI,WE SI ULIKUA UNAJIFANYA MTU MWEMA
HAYA MATTY…PITA BIBIEEEEEEEEEEEEEEE…ILA MI NAMUONA HAJAZEEKA.
BINTI MZURI…HABARI ZA SIKU SHOSTI?
Binti Mzuri Mimi ni mwema siku zote ulikuwa hujui??? jibu la swali lako kuwa nimeanza lini kushushuana ni hili (kushushuana nimeanza tangu nipo nasery school!!!!!!)
Kahindi Bibie asante kwa kunipa njia!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
heko Jenerali Ulimwengu, as your names appear – wewe ni General wa Ulimwengu wa Habari, kama kweli mwana wa mkulima anasema ukweli kuwa haujagusa hata darasa la habari, sasa sijui ungetia mguu ingekuwaje….ila sometimes ukae na hawa “Auxiliary mgombo” wa habari waache kunuka rushwa za kupamba watu, akipewa 500 anakuandika vzr, ukimnyima 100 ya nauli anakundika vibaya
JENERALI ULIMWENGU gwiji la habari,mwanasheria,mwanafalsafa,mzalendo wa kiafrika,mjamaa,kamaradi,mfuasi na mtoto wa MWL JK,amewahi kua katibu mkuu wa vijana afrika,mkuu wa wilaya na mbunge.ameshiriki vita kumtoa mkoloni msumbiji,anaijua vizuri afrika anayoipenda mno.lkn pia anaijua dunia,ni mtu wa msimamo usioyumba ktk mambo ya msingi anayoyaamini,yeye ni daraja la watukufu wachache nchi hii imewahi kupata km vile dk salim a.salim,warioba,issa shivji,othman haroub na wengineo.kama kuna dhambi kubwa nchi hii imepata kufanya ni kuwabagua wa tz hawa wazalendo salim na ulimwengu na dhambi hii imeanza kututafuna na km hatutatubia na kubadilika itatuangamiza kabisa km taifa,jamani ulimwengu ni tembo na mimi kipofu nimeeleza sehemu nilizopapasa nawaachia wenye macho na walio karibu nae (niko kijijini msalala-geita)watuelezee zaidi,kwa mwenye kuhitaji makala zake za nyuma kipo kitabu cha makala zake kinaitwa RAI YA JENERALI ULIMWENGU.namwombea MUNGU ampe maisha marefu na yenye baraka.
Kitu pekee kinachokuja bila juhudi ni Umri. kinachokuja kwa haraka ni Makosa, na kinachokuja mwisho ni Majuto. Wao hawatambui ni kipi cha kwanza na kipi cha mwisho. Lakini kipindi cha ukombozi wa kweli kupitia vijana wazalendo wa nchi hii wakiongozwa na maazo ya wazalendo wasiotiliwa shaka wa nchi hii kama Ndugu JENERALI ULIMWENGU, ni katika kipindi hiki watakapo tambua maana ya msemo huu. Mapinduzi Daima.
MZEE JENERALI, ukweli ni kwamba umekuwa kinara wa kutoa misimamo katika masuala mbalimbali yahusuyo Taifa na hasa unapobaini kuwa mambo yanaelekea pabaya. ushauri wangu kwako ni kwamba kwa kuangalia Taifa hili tuna FURSA kuu tatu ambazo aidha hazitumiki au zinatumika visivyo nazo ni NGUVU KAZI na RASLIMALI ZILIZOPO VS UOGOZI (VIONGOZI) tulionao katika ngazi mbalimbali. fursa hizo zimekuwa hazina ushirikiano na hii ndicho chanzo cha kukumbatia umasikini tulionao na kinachopelekea vijana wetu wengi kushinda vijiweni kwa kudai eti wanajitafutia maisha kwa kuendesha piki piki na baiskeli na kupelekea kuuwa vifua na kusababisha ajali zinazosababisha baadhi yao na abiria wao kubaki na vilema vya maisha huku kila kukicha tunalalamikia kushuka kwa uchumi wetu, je hao viongozi wetu tuliowaweka madarakani kwa ushindi wa kishindo wamefanya nini kwa kishindo au ndio wanasubiri 2010 tena watupatie MISEMO YA DAGANYA TOTO? HONGER SANA KWA UADILIFU WAKO KIUANDISHI KAZA BUTI 2010 UNA KAZI YA ZIADA UMEONA ULICHOKIFANYA 2005 KIMETOA MAUA TU BADO TUNASUBIRI MATUNDA.
Big up mzee JENERALI ULIMWENGU,MUNGU AKUPE AFYA NA MAISHA MAREFU DUNIANI. ILA NAPENDA KUJUA JE UNASHIGHULIKA NA HABARI ZA KISIASA TU AU HATA KIJAMII KAMA UNYANYASWAJI WA WANAWAKE, NA WATOTO KUNYIMWA HIKI ZAO ZA MSINGI?.
Ulimwengu si kitu kingine chochote bali zawadi kwetu watanzania ambayo bahati mbaya sana ni wachache ambao wameiona nakuitumia.Ni mwanahabari na mwanafalsafa wa wakati wake. Labda niazime kidogo maneno ya kiingereza kusema hivi: Go and taste him,he excudes insight,wisdom and intelligence.
One of a kind! To me widely read. Ninachompendea zaidi hana tabia ya kujipendekeza. Kwake spade ni spade not a big spoon, sio mlamba viatu, ndo mana nimemgoogle to find what he is made of apart from early graduate of UDSM nadhani kawagroomed na long experience, reading widely na kuwa mahali anapopapenda, hobby.
I admire this man greatly.jenerali ulimwengu …from an early age i have had the privilege of reading his works, the first being his compiled essays ‘rai ya jenerali’ and then later his articles in the old raI newspaper amd watched many of his talk shows on channelten every monday.He inspired in me a deep patriotism,a love for journalism and a liberal mind better than anythng i could have hoped for in this current Tanzania, were politics is all a facade a race to the honeypot,a constant string of lies and unfulfilled promises.I consider myself lucky to be exposed to his ideas before i, like many youths my age had fallen pray to the monster of political indifference which is almost inevitable in this enviroment, were politics and patriotism are one and the same,represented by unproductive leaders who talk endlessly about plans to develop and improve this and that but in the end do nothing .I am lucky because i have been exposed to a great example of what true patriotism,politics,intellectualism,and freedom fighting is all about,Jenerali Ulimwengu.Through his journalism he has without doubt fought for the Tanzania TANU promised, for the Tanzania CCM is still trying to promise this society..a Tanzania mwalimu Nyerere had in mind.Had i not been exposed to our hero i would have needless to say been among the millions of youths today who do not care about any sort of politics let alone understand the meaning of patriotism or even why be patriotic to such a nation as this?.it is only when you understand the dream and vision of Tanzania that mwalimu had in mind that u will understand the necessity of bringing immediate change to this country and the true meaning of a patriot.note that Powerful and corrupt politicians have tried to destroy what jenerali has worked hard to achieve.but like a true freedom fighter he did not compromise his principles and ideas in the face of adversary and his contribution to this countrys politics still burns stronger than ever.The truth shall always prevail and so we pray that free media prevail too.long live jenerali..u give us a glimpse of what true politics and a honest tanzania is all about…be blessed.
Jenerali, toka nikiwa shule nakusoma, sasa naanza kuelekea uzeeni nakusoma, hujaacha, huachi wala huelekei kuacha kazi na wajibu wako wa kihistoria.
Umekuuza na kutukuza kiwango cha uandishi hasa wa habari Tanzania na ungali mfano wa kuigwa na kufuata, Afrika Mashariki, ukisimama dede enzi zileee na hizi. Watu kama wewe ni kioo furaha ya jamii yetu.
Ninachopenda kuliko vyote (ukiacha maudhui yako) ni ustadi wako wa kilugha. Ni kati ya Watanzania wachache wanaoandika Kiswahili na Kiingereza fasaha, bila kuchamba chamba na kuparaganya ganya kama wehu.
Mfano wa kuigwa na kila mtu.
To those who cannot read Swahili, please learn the language from guys like Brother Ulimwengu. But I have this to say about Jenerali. I was reading him while still at school, and we are talking early 1970′s, I am still reading him. The man is a moving vehicle with an engine that does not stop running; oil no oil, water or no water. Consistent.
Iam personally, proud to be a writer because of guys like you, brother. Keep it up.
Jenerali nakupenda sana kwa makala zako za aina yake zenye wingi wa misamiati na nahau nyingi zenye kila aina ya bashasha unapozisoma.
Junaweza kusema mambo mengi sna mazuri juu ya Jenerali Ulimwengu hata kuwaudhi wakubwa kwa kuwa wengi wao hawependi kuona walio chini yao wakisifiwa kuliko wao; lakini ukweli unabaiki kuwa Jenerali Ulimwengu ni mmoja wa watu wachache waliosalia nchini wanaoweza kuusema ukweli bila kujali nini kitakuwa gharama ya ukweli walio usema. Tanzania ya leo viongozi wetu hawapendi kuambiwa ukweli hasa kama ukweli huo unagusa mabaya yao!
I like the person alothugh i have never seen him phyisically,kama mwana habar, J Ulimwengu ananipa matumaini ya mbele sana hasa katika kufanya self emloyment. Kwa mfano hoja za juzi katika mdahalo wa katib ni moja kati ya shule kubwa san kwangu.I have a suggestion kwamba UDASA kile kipindi wafanyie bacu up nakuweka katika CD then wapeleka katika local meadi za wilaya zilizopo miona au mikoani kwa sababu ain ile ya mdahalo sidhani kama itafanana na midahalo mingie kwa hizo local media zitaweza kurusha kwa muda fulan ili kutoa awarenes kama ilivyosemwa katika wat forwad with new constitution.Nipo Njombe kuna radio,Makete Irnga,Songea,nk Nafuhi sana kupata nafa hii kazi yako sio bure itazaa matunda
Jenerali is unique Journalst.I agree with others
MI NI MTU FULANI TU AMBAE KTK MTAZAMO SIPASWI HATA KUJIITA KIPOFU MAANA WAPO VIPOFU WALIPOFUKA KUTOKA KTK HALI YA KUONA. ILA NATAKA KUSEMA HIVI: Adamu na hawa walipotenda dhambi ilituelemeaLIMWENGU NI DARALI ANAYENADI MATATIZO YA WATANZANIA KWA SERIKALI YA JK; HAJITAMBUI KI UTU, BORA ATANGULIE KWA BWANA ILI WATAKAOBAKI WAFAIDI MALIPO YA SERIKALI ZIJAZO KWA WATANZANIA BAADA YA JENERALI KUPATA WATEJA(SI JK NA JAZZ BAND YAKE)
MI NI MTU FULANI TU AMBAE KTK MTAZAMO SIPASWI HATA KUJIITA KIPOFU MAANA WAPO VIPOFU WALIPOFUKA KUTOKA KTK HALI YA KUONA. ILA NATAKA KUSEMA HIVI: Adamu na hawa walipotenda dhambi ilituelemea sisi uzao wao kwa hiyo mtu yeyote anaepinga ukweli kwamba Jenerali Ulimwengu ni Mtanzania anaenadi matatizo ya watanzania serikalini bora atangulie kwa bwana ili uzao wake ubakie kubeba mzigo huo kipindi watanzania watakapolipwa mauzo ya matatizo yao kupitia kwa Jenerali Ulimwengu (si kwa ‘eti Dr JK’ na JAZZ BAND yake)