OBAMA UBARIKIWE-SAMBA MAPANGALA & ORCHESTRA VIRUNGA

Zikiwa zimebakia siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa Rais wa Marekani kwa mwaka 2008,wanamuziki wengi wamezidi kujitokeza na kuwaunga mkono wagombea wawapendao kwa kutumia sanaa ya muziki.Hili sio huko nchini Marekani tu bali pia barani Afrika.Miongoni mwa wanamuziki hao ni Samba Mapangala,mwanamuziki mwenye asili ya Democratic Republic of Congo(zamani Zaire) na mwenye makazi ya kudumu nchini Kenya.Huyu huwa anatamba na kundi lake maarufu la Orchestra Virunga.

Kama ambavyo unaweza kuhisi,Samba anamuunga mkono na kumtakia kila la kheri Mgombea kupitia Chama Cha Democrat,Seneta kutoka jimbo la Illinois,kipenzi cha wengi,Barack Hussein Obama.Wimbo unaitwa Obama Ubarikiwe.Usikilize hapo chini.Shurkani Subi kwa wimbo huu.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

 1. Dunda Galden, 09 October, 2008

  Ubarikiwe Obama lakini kazi bado ndefu
  chafosa

 2. Frateline, 09 October, 2008

  Hi Guys kutoka Helsinki-Finland

  Kwa kweli ninampongeza huyo mwanamuziki kwa kumpa support mpiganaji Baraka Obama, Mimi ninafurahi sana kama ambavyo nimewahi sema hapa BC kuwa nikiona mtu mwenye asili ya Africa anafanya vizuri kwenye ngazi za juu kabisa za Uongozi wa Dunia kwa kweli ninapata faraja sana maana wazungu walikuwa wanataka kutufanya kama second class global citizens, (mfano Dr. Migiro nilifurahi sana) na ndiyo maana baadhi ya wazungu wale wabaguzi bado wanatoa kauli za ajabu na baadhi yao ni wanasayansi kama watson wanaamini uwezo wa mtu mweusi ni mdogo kulinganisha na mzungu, lakini sasa dunia inaanza kubadilika taratibu, tumuombee sana huyu jamaa awe Rais ili tuweze kupata pia First lady mweusi ktk Taifa kubwa duniani, mungu mubariki Obama , mungu mubariki-michelle-Obama na Mungu wabariki WaAfrica wote popote pale walipo duniani.

  Frateline

 3. EDWIN NDAKI, 09 October, 2008

  Hakika namshukuru Mungu kuona BC mmerejea kwa kasi ya ajabu.

  Ila kubwa ya yote kuna kitu ambacho wadau wa hapa BC watakubaliana nami.Bc tangu ijumaa iliyopita walikuwa mitini.

  Itapendeza kabla ya kuendeleza libeneke “MTUPATIE FIDI BAKI” nini kilichowasibu.Maana kuendeleza libeneke bila kuambia nini kilitokea haijakaa sawa.

  Najua Matty,Gervas,mama wa kichaga,majita,chris,ney,Any,mswahilina,binti mzuri,kekuu na na wadau wote ambao sijawapata mlishuhudia jinsi BC walivyopotea.

  Kwa leo ni hayo..ijumaa njema..wimbo mzuri nami pia kila la kheri kwa Obama.

  TUTAFIKA TU

 4. Hombiz, 09 October, 2008

  In 1963, Dr Martin Luther King once said
  “I have a dream that my four little children will one day live in a nation where they will not be judged by the colour of their skin but by the content of their character”. Now the time has come.
  Kwakweli seneta B. S. Obama amefanya kazi kubwa sana kufikia hapo alipofikia. This is unbeliavible! Mimi sina shaka kuwa seneta Obama atakuwa ni mmarekani mweusi wa kwanza kuwa Rais wa Marekani. Mpaka sasa anafanya vizuri ktk kampeni zake ukilinganisha na mpinzani wake seneta McCain. Namuombea heri na fanaka ili atimize ndoto za hayati Martin Luther King.
  Kila la kheri seneta Obama
  MOLA amrehemu, ampumzishe kwa amani Dr. King. AMEN

 5. Amy, 10 October, 2008

  it’d be nice to have a bit of an eye candy 🙂 he is young, gorgous and carismatic…ooh … he is African too…well African American…good luck Obama.

 6. binti-mzuri, 10 October, 2008

  keshatungiwa wimbo…sasa abarikiwe kwa lipi hasa,au the fact of being black and running for presidency

 7. Gervas, 11 October, 2008

  Tuimbeni tu Obama ubarikiwe..lakini nahisi kuna uwezekano mkubwa kabisa ushindi wa Obama ukazua sura mpya kabisa ya ubaguzi na revenji kati ya blacks na whites marekani ndani na nje. what do you do when haters hate you because of your skin colour?

 8. Mswahilina, 11 October, 2008

  Nasikia Samba Mapangala amesilimu ili “apate vimwana”.

  Wimbo mzuri,

  BC. Kazi nzuri.

 9. eva moses, 11 October, 2008

  Asante sans Samba. ‘Yes we can and yes we will. No way no how no McCain’. I like the song. I am heading to canvass tomorrow in Virginia – we’ll make this state blue!

  Obama/Biden ’08

 10. sisterTZ, 11 October, 2008

  Jamani waafrika hivi mnadhani kwamba Barack Obama ataleta maendeleo Africa au? Sasa ngojeni apata huo urais muone..kaeni chini na kufanya kazi ili kuleta maendeleo Afrika tusisubiri misaada kutoka nje kwa sababu misaada kutoka nje kamwe haiwezi kutuletea maendeleo…tujue hilo

 11. eva moses, 11 October, 2008

  yes we can.

 12. mwandiga, 11 October, 2008

  Jamani kuna kitu hawa wenzetu wa kongo wanatuzidi kimuziki.
  Sikiliza mziki huu na ujumbe wake.Hauna maneno mengi kama riwaya lakini yale machache yanamaana sana. Nimtumia simple laptop na headphone,lakini nimeweza kusikiliza kila chombo.Solo inasikika,rythym gitaa linasikika,bass,percusion,saxaphone,trumpet na kila kimoja kwa wakati wake.Muziki unachezeka.
  Hivi hawa wakwetu hawawezi kuangalia mambo haya,maana ukisikiliza mwijuma,choki n.k utasikia hadithi tuu halafu vyombo vyote vinapigwa kwa wakati mmoja.
  Mimi nadhani watu wasikiliz akina afro70 ,balisidya,jamhuri jazi,akina simba wa nyika,less wanyika,ahmed kipande,salimu abdalla,akina fadhili william,halafu wajilinganishe na utumbo wanaouweka siku hizi.
  Watu awajui kuwa muziki unauzika wenyewe kwa mpangilio.
  Angalia prof Jay na JD wao wanaweza kukaa hata mwaka laikni wakiibuka wanatoka kikamilifu.
  Tena niwakumbushe tu kuwa watu kama njenje muziki waliopiga 10 years nbado unatamanika yaani ‘unforgettable’. Sasa siku hizi mtu anaingia studi na kutoka na vibao13 sijui amevifanyia tahmini lini.
  Tukabali kutokubaliana wakongo wapo makini na kazi yao.

 13. Matty, 13 October, 2008

  hahahahaha Mwandiga umerudi???tutafika!

 14. pyupyupyu, 13 October, 2008

  mswahilina ameslimu,au usawa mgumu? huyu jamaa amekosa mradi for sam taim now

 15. mwandiga, 13 October, 2008

  Matty nipo tu,sijatoweka BC ni kwangu enzi na enzi.mzuka unapanda wakiboa. salama lakini

 16. any, 16 October, 2008

  Haa, Weusi wa Kimarekani wanachukia waafrica kuliko wazungu wanavotuchukia. habari ndio iyo! ila yeye sio afro american ni mluya

 17. Matty, 16 October, 2008

  peace to you Mwandiga sijakusikia kipindi though aminia!

 18. binti-mzuri, 17 October, 2008

  jamani eh,huyu baba is originally half kenyan but he isnt a kenyan citizen .. tusipotee hapo.

 19. kahindi, 22 October, 2008

  dunia tunapita ee.hakuna kitu kitabakia,itabaki milele eee ni milima,warogaroga watu baba,waumiza waafrika wenzio,madaraka wapigania kampuni sio yako………ni ya muzungu……wape haki zaooooooooooooooo…..nampeenda sana samba mapangala jamani.

 20. Basi, 25 October, 2008

  ANY waambie hao kwamba Black Americans wanachukia waafrika sana kupita wazungu wanavyotuchukia..

  unajua watu wengi huko nyumbani wanadhani BLACK American ndio role model wao maana wengi si hawajawahi kwenda USA ila wangekaa US then ndio wangewajua vizuri mno hao ma BLACK na kamwe wasinge jifanya wao eti Black americans..maana mimi nakaa area ya wazungu and kamwe siwezi eti kwenda kupanga maeno ya hao ma BLACK subutu si watakuuwam maana wanaumasikini kibao..

  unajua ma Black wengi hapa US ni wachovu ila watu huko Bongo hawajui tu….

 21. halima, 28 October, 2008

  kwa hiyo ma white man ndio matajiri wa ulaya? na wewe unaejiita BASI acha kukandia wenzio inamaana wewe ni tajiri au ndio nyinyi mliosahau mlipotoka hamjui mnapokwenda?

 22. BasiNImaskiniFikra, 02 November, 2008

  I don’t wish to defend the blacks , lakini Basi hapo umekosa. Hufai kumchukia mtu kwa kuwa ni maskini. Hawo unawowaita MaBlacki ndio walikupigania miaka ya Hamsini na 60’s otherwise fursa ya kuishi kando ya hao wazungu unaopenda sana HAUNGEPATA. LABDA WEWE MMOJA WA WALE WANAOKWENDA NG’AMBO , baada ya kupata vijisenti kadhaa hutaki kurudi Africa kwa kuogopa kuombwa.
  Haibu

 23. godfrey Adolph, 06 November, 2008

  O-Origin
  B_Born
  A_In Africa
  M_Managing
  A_America
  Hiki ndio kirefu cha OBAMA Na Tafsiri ya Martin Rutta!
  YES WE CAN! WHY NOT AFRICAN?NOW THEY KNOW
  YES WE CAN!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Copyright © Bongo Celebrity