Huyu ndiye mbunge mpya wa jimbo la Tarime.Huyu ndiye aliyekitoa kamasi chama tawala cha CCM katika uchaguzi wa hivi karibuni kutafuta mrithi wa Marehemu Chacha Wangwe.Anaingia bungeni akikabiliwa na kibarua kizito cha kuziba pengo lililoachwa na Wangwe.

Pichani ndipo alipokuwa akila kiapo bungeni Dodoma hapo juzi.Anaitwa Mwera Charles Nyanguru. Je na yeye atakuwa na cheche alizokuwa nazo Marehemu Wangwe?Tusubiri kuona na kusikia.

Picha kwa hisani ya ofisi ya Waziri Mkuu

Feedback / Comments

12 Responses to “MBUNGE MPYA WA TARIME ALA KIAPO!”

  1. Comment by Bongo pix on October 30th, 2008 8:43 am

    KARIBU NDANI YA JUMBA.

  2. Comment by halima on October 30th, 2008 10:01 am

    Haya baba mikoba ya chacha wangwe ndio hiyo unakabidhiwa sasa ukiwachanganya tu wale wana tarime ahhh mbona utawakoma hawaoni hasara kukuchinjia baharini

  3. Comment by binti-mzuri on October 30th, 2008 10:21 am

    Mwenyezi Mungu amlinde katika kazi yake!Ameeen

  4. Comment by Simon Kitururu on October 30th, 2008 10:47 am

    Kila la kheri!Usijisahau tu!

  5. Comment by Edwin Ndaki on October 30th, 2008 11:24 am

    Namkumbuka marehemu Wangwe wakati wa uhai wake alikuwa wakipelekeshana sana mh Spika.

    Siku moja kwenye kikao cha bunge aliambiwa aombe radhi kwa kauli yake ya kusema serikali inaua wananchi Tarime.

    Mh Wangwe alipoona maji yamefika shingoni hakukubali kujisalimisha aliona bora afe na tai shingoni kama wakina Mkwawa jibu alilompa Spika alisema.

    “mh Spika nimefuta kauli ILA MESSAGE DELIVERY!” …

    Hakika Ras Wangwe ambaye alikuja nyoa rasta zake baadaye alijitahidi sana kuwakilisha sauti za mamia ya wananchi wake waliokuwa wananyanyaswa na kuporwa haki zao kwenye Mgodi wa North Mara unaomilikiwa na East African Mines.

    RIP Wangwe..Mwera usije jisahau alafu utegemee 2010 ukawaulize Tarime hivi kweli mlisema mnavaa viatu saidi ngapi?

    Kumbuka visima vya kale havifukiwi mjomba…

    Ndimi kwangu pakavu nakusalimu salaaam Mwera

    Tutafika tu

  6. Comment by majita on October 30th, 2008 2:01 pm

    tata amang’ana ghao mura.Nina wasiwasi hapo alikuwa anakandamiza kikurya kwa kwenda mbele.Karibu sana mjengoni

  7. Comment by hombiz on October 30th, 2008 5:33 pm

    eeeh Mheshimiwa Mwera Charles Nyanguru.
    Tafadhali katuwakilishe vema huko bungeni sisi wananchi wako. Usicheke kabisa na mafisadi na vibaraka wao! Kafanya kazi bila woga wala kuchoka.
    Nasubili kuona cheche zako mheshimiwa
    Nami nasema kama Edwin Ndaki….Kumbuka visima vya kale havifukiwi mjomba…
    Stay Blessed.
    Peace out!

  8. Comment by mdau on October 30th, 2008 5:37 pm

    tunataka changamoto Bungeni,siyo khrrrrrrrrrrrrrro,khrrrrrrrrrrrro.Nafikiri wadau mmenipata.

  9. Comment by Matty on October 31st, 2008 5:36 am

    Mura heheeheheheh mtani wangu huyo i love u hahahaha ila sasa pls usituangushe wanainchi wako, fuata nyayo za Chacha wangwe.
    Kila la heri bro!

  10. Comment by kahindi on November 1st, 2008 1:32 am

    -hope hutakuwa mmojawapo wa wale walalavi ndani ya mjengo….kila la kheri….

  11. Comment by Gervas on November 1st, 2008 1:51 pm

    Tunasubiri tu hiyo CCM itengane maanake tayari mtungi ni wamoto saizi. ANC wameshaonyesha njia. Hapo ndo tutapata at least Upinzani wa maana Tanzaia…maana watakuwa wanasemana wao kwa wao, maanake njia za wizi wanazijua ati wenyewe. Kwa sasa bado wanaogopana sababu wameshindiliwa wote ndani ya mtungi mmoja ambao tayari umeshapigwa mtikisiko na nyufa zimeshaonekana. RIP baba wa Taifa!!

  12. Comment by hombiz on November 4th, 2008 11:40 am

    is gonna get there Gervas! Watch!.

Leave a Reply