Hivi karibuni tulipotambulisha single mpya ya AY inayokwenda kwa jina Freeze, palitokea mabishano makali sana kuhusiana na kama ni kweli AY ni established artist ambaye ana mpaka ofisi yake inayohusiana na suala zima la burudani na muziki. Umuhimu wa elimu ya darasani (formal education) pia ulizua gumzo.Nadhani wote tunakubaliana kwamba elimu siku zote ni suala muhimu na lisilofaa kubezwa hata kidogo.Kama mtu ana nafasi na uwezo kusoma tunamshauri afanye hivyo!
Lakini pia kulikuwepo na maelezo tofauti tofauti kuhusiana na kuwepo au kutokuwepo kwa ofisi ya AY na sehemu ilipo.BC iliamua kuwatuma baadhi ya wanachama wakereketwa ili kujaribu kupata undani kidogo wa suala hili.Tuliamua kufanya hivi ili kuwapatieni ukweli baada ya kuona kuna maelezo mengi yanayopingana au kupishana.
Ukweli ni kwamba AY anamiliki kampuni inayokwenda kwa jina la Unity Entertainment Company Limited.Ipo Mikocheni kwa Nyerere,Rose Garden Road pale Jued Business Centre Wing B 2nd Floor. Kampuni hiyo inajishughulisha na Event Coordination and Organizing(kuandaa na kuratibu matukio) na pia ni Events Booking Agency.BC pia ilifanikiwa kupata picha kadhaa za ofisi hiyo kama unavyoziona hapo chini.
BC inapenda kumpongeza AY kwa ujasiriamali na umakini huu katika masuala ya muziki na burudani.Ni matumaini yetu kwamba wengine nao watafuata nyayo za AY.

Unity Ent.

Unity Tanzania
Page 1 of 3 | Next page