MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

nurubc1Anaitwa Nuru Magram.Makazi yake ni ndani ya jiji la Stockholm nchini Sweden. Bila shaka unamkumbuka kwa vibao vyake kama vile Walimwengu na Msela ambavyo ndivyo vilimtoa katika ulimwengu wa muziki.

Hivi karibuni amekuwa studio akikamilisha project yake mpya ya muziki ambayo itakamilika hivi karibuni.Lakini kuonyesha jinsi ambavyo bado hajajiweka kando na mambo ya muziki, hivi karibuni mnamo tarehe 22 Novemba anatarajiwa kufungua show ya mwanamuziki mwingine wa Bongo Flava, Ali Kiba.Show hiyo itafanyikia jijini Stockholm.

Ali Kiba inasemekana ameweka rekodi ya kuwa mwanamuziki wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kufanya tour ndefu kushinda zote zilizowahi kufanywa na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya.Nuru ameahidi kufanya vitu visivyo vya kawaida hiyo tarehe 22 Novemba.Kazi kwenu wakazi wa Sweden na nchi zilizo jirani.Unaweza kumcheki Nuru hapo chini katika wimbo wake Walimwengu.Ni zouk iliyokuwa imetulia na yenye ujumbe mzuri.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • E-mail this story to a friend!
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

63 Responses to “NURU KUFUNGUA SHOW YA ALI KIBA NCHINI SWEDEN”

  1. Comment by binti-mzuri on November 16th, 2008 9:21 pm

    huyu ali kiba kweli kavunja rekodi! afu pia umesahau kuongezea .. zaidi ya kufanya tour zuri,amedeliver na pia kapendwa kuliko wote. aliku analikwa mpaka majumbani mwa watu lunch and dinner. mtoto anajituma.. wajameni bongo artists,igeni mfano wa mwenzenu.nyie mnakuja,mnalewa tu kabla ya show,mnaimba nyimbo mbili mnazima..huyu kaka kafanya kazi kama vile kina jay-z .. anatoa burudani kwanza,mengine baadaye.big up ali kiba! jamani interview sooon!!tunataka tumsome!but dont overwork yourself ali kiba,be care!

  2. Comment by BLACKMANNEN on November 16th, 2008 11:19 pm

    Ndugu zanguni nyote wana BC, leo ni siku ya kumwaga misifa hapa, maana “NURU” ni mwanangu, mtoto wa dadaangu. Hata kama atakuwa wewe hakufurahishi wewe, lakini mwaga misifa. Nadhani tumeelewana eeee ndugu zanguni. Binti-Mzuri, Matty, Majita, Nalitolela, Mama wa Kichagga, mpo? Msiniangushe.

    Bond=James Bond……..NO, I mean, Black=Blackmannen

  3. Comment by muniii on November 17th, 2008 5:06 am

    Jamani ali kiba si mchezo, yani hapa uholanzi anatesa sana kwenye redio za kidutch, i am so proud of him maana nimeisikia cinderella inatamba kinoma hewani. Well done kijana ali kiba unanifurahisha sana kwani naona sound tu ya nyimbo inawapendeza sana watu hadi wanairusha tu, hongera hongera hongera. Nuru ni mrembo ila simfahamu lakini kila la heri nae

  4. Comment by Majita on November 17th, 2008 6:27 am

    aah mimi hapo sisemi mengi.Mimi tu-meno twake tuuu.Jamani mwee???umetuchunguza vizuri na jinsi anavyojua kutuchezesha mdomoni??halafu tweupeeee,kama tumezidi hivi,kama katuchonga vile,kama…ssshiiiiii mamaaa nasreem asinisikie na kuniacha kabla ya “ndowa”

  5. Comment by mary on November 17th, 2008 7:35 am

    i love her……..big up nuru na ongeza bidii

  6. Comment by nchekube on November 17th, 2008 7:40 am

    ujumbe murua, ni kweli ukiwa na mali kila mtu atakujua,zikiisha mwe!

  7. Comment by Matty on November 17th, 2008 8:09 am

    Mtoto halafu mzuri kama Binti-mzuri jamani kina kaka semeni hapo je?huyu sasa mtoto awe wa Gervas hahahahaha Blackmannen umepata mkwe maana kaka zangu naona kila mmoja anajipatia kimwana hapa hapa mimi nafurahi kupata wifi Mrembo!
    Blackmannen hongera kwa kuwa na mwana mrembo kama huyu na anaimba vizuri nimependa wimbo wake ila nasikia ni half cast au??
    Binti-mzuri huyu kijana anajituma sana me too mtu mzima namzimia kijana anajituma ile mbaya!hana utani na kazi yake ana wimbo mpya mtamu huo!

    Edwin Ndaki uko wapi siku hizi??

  8. Comment by Adam Tensta on November 17th, 2008 8:42 am

    Ali kiba ni noma mwanangu wakati wako huu,ila angalia sana usifanye show mpaka watu wakuchoke,jipange na fanya show za maana,sio mpaka ktk birthday wéwe unafanya show tu,jaribu kuwa international,dont go only for money,jaribu kuangalia utamaintain vp ur status na usichuje,just to remind u walipita wengi before you na jiulize wako wapi now?.ila kwa kweli mwnangu uko JUU SANA.HUYO NURU JAMANI MBONA MNAMJUA UKO BONGO TU SISI UKU HATUMJUHI KAMA NI MUIMBAJI,NA WAPI ANAKOFANYA SHOW ZAKE?,HUWA TUNAKUTANA NAE CLUBS NA KTK PARTY TU,NA SIJUHI KAMA HUWA ANAFANYA SHOW UKU MAANA SISI WATU WA VIWANJA TUNGEMUONA TU JAPO MARA 1,KAMA NI KWELI ARTIST ASEME HUWA ANAFANYA SHOW WAPI,SIO KUWAONGOPEA WABONGO TU KTK WEB…WEWE NURU HIZO SHOW UKU UNAFANYA WAPI NA ULISHAWAHI KUFANYA LINI?

  9. Comment by Frank on November 17th, 2008 9:40 am

    Wakilisha dada, fanya mambo

  10. Comment by halima on November 17th, 2008 9:55 am

    Jicho hilo mwanawane mmmmhh

  11. Comment by fadede on November 17th, 2008 10:18 am

    ebwana bab kubwa kila la kheri nawatakia kazi njema

  12. Comment by Lalola on November 17th, 2008 11:27 am

    Jamani I’m new. Manake huwa nasoma hizi comments za aina mbalimbali tangu siku nyingi halafu naishia kuumia mbavu zangu tu. Kwa kweli inafurahisha sana. Ila leo uzalendo umenishinda, inabidi niwasabahi wadau. Jamani kina binti mzuri, halima, matty na wengineo mmepata shosti mpya na kwa mamen mmepata dada mpya. Tehe tehe tehe!!!!

    Lol!!!!

  13. Comment by bidada on November 17th, 2008 1:54 pm

    i like ALikiba he real perfoms well ,i tried to watch one
    of his shows in Wichita was very nice.
    keep it up we admire u

  14. Comment by kweliman on November 17th, 2008 1:58 pm

    nimeangalia hiyo video yes! kwa maoni yangu dada sura ni nzuri kwa kifupi ni mrembo hongera sana na uendelee kujitunza vyema
    Ile artistic apeal yako/stage apeal , wow ! you can’t be greater ,you’ve got it all mama, kwa kweli una potential siyo siri

    Video-video yako kwa maoni yangu nimeona ina kiwango cha chini japo si kama zingine mbaya kweli kweli nilizowahi kuziona za bongo flava hapa nazungumzia ubora wa picha yaani cinematic quality.sijui wameshoot ni camera ya kiwango gani lakini jinsi inavyoonyesha i wouldn’t be surprised kama ni hizi camera za kushoot ubatizo na mambo ya nyumbani yaani domestic au labda inaweza kuwa prosumer fulani hivi

    energy- actually sijaona ukionyesha the right energy inayoendana na pace ya mziki na substance unayoimba ktk huo wimbo yaani sijaona uwiano kwa maoni yangu iko flat

    shots- combination au flow ya shots siyo mbaya ni nzuri tuu haina shida labda nyongeza yangu kwa maoni wangu ktk shots ni hili
    kwa kuzingatia pace na substance of the song au theme ingependeza zaidi kukata between location story scene (MOT) na lip sync performance

    Angles/ type of shots - sijaona anything dynamic.mfano vitu kama slomo( hasa ukizingatia pace ya mziki wenyewe)
    sijaona aina zingine za shots kama tracking tilts na dolly
    lakaini hii si hoja kubwa labda director wako wa video ana mtazamo tofauti kutokana na mazingira yake ya kiusanii
    lakini kwa maoni yangu ingekuwa bora zaidi ya hapo kama angeongeza dynamic shots

    Acting - acting yako haijaniridhisha inaonekana ni STAGED
    this is atleast true to nobody else but me
    hasa pale nilipojaribu kuingalia hiyo video bila audio it was so obvious, to me

    Audio- ni nzuri .japaokuwa sijaona anything dramatic au exceptional naona ni sawa tu na bongo flava zingine yaani sounds so CHEESY, CANED NA CHEAP.sijaona kama umeimba bongo flava nimesikiliza mziki wako una sound zouk kabisa wala siyo bongo flava kama vile ulivyoelezewa kwenye habari hapao juu jamani mimi sifahamu hasa bongo flava ni nini lakini ktk mziki wako nilichosokiliza ni zouk was great though

    vocal performance -uimbaji wako ni mzuri na una potential ya kuwa great.maoni yangu chukua vocal lessons utagundua siri ya kuimba am sure huko sweden vocal coaches wapo wengi ,hii itakusaidia kuachana na mambo ya kupanda na kushuka kweli dada yangu hujachelewa ukichukua vocal lessons in six months utaona wewe mwenyewe jinsi utungaji wako na uimbaji wako utavyochukua another level

    Mwisho naomba uelewe kwamba you got my recognition.
    you’re one heckuva dropdead gorgeous ,redhot and most of all you ‘ve got a talent with great potential,period!
    goodluck

    Kweli man

  15. Comment by Gervas on November 17th, 2008 2:26 pm

    Matty dah, umenipendelea kweli..sijui nisemeje tu….Blackmannen, mambo?…shikamoo!! Umesema tumwage sifa….Aisee!! kwa kweli kako nechuro, namimi pia ni Half -cast wa Kidengereko na mmatumbi. Ila kama unavojua Matty mi mlevi wa Ulanzi si kataniacha mwanawane?

  16. Comment by DUNDA GALDEN on November 17th, 2008 3:59 pm

    Kweli jamaa kala miguu ya kuku safi sana ndio kujitangaza
    ukipata nafasi itumie ipasavyo
    Zaidi ongera sana kwa jitihada zako.je na uku Australia mwisho wa dunia lini nasi tujirambeeee?pia mbona hamjaandika Uko Sweden atakuwepo ukumbi gani

  17. Comment by francis on November 17th, 2008 4:59 pm

    huyu dada anajituma sana yani i hope naye atafika level hiyo ya alikiba inshallah………..nuru ni mzuri na anzidi nayeye kurepresent bendera ya hom tanzania……kila la kheri mwanangu fanya mambo na mjita alikiba big up bro

  18. Comment by Nalitolela, P. S. on November 17th, 2008 6:08 pm

    Nilikuwa sijamsikia before kusema kweli. Nimepanda kazi yake; she’s talented… and pretty too!

  19. Comment by any on November 17th, 2008 9:33 pm

    NYIE WAKAKA APO JUU MTAKULA KUONA MWAKA HUU! haaaaaaa,. MENTAL MAP!ukute apo munamu “undress” mtu kwenye screen. lol

  20. Comment by BLACKMANNEN on November 17th, 2008 10:56 pm

    Matty, Gervas, Majita na wengine wote, nashukuru sana kwa kuitikia ombi langu kwenu la kumpa misifa mwanangu “Nuru”.

    Nuru ni Mtanzania pure. Rangi aliyonayo ni ya Baba yake, ambaye ni Mzanzibar. Nuru, ni msichana aliyelelewa katika malezi yenye maadili, kwa hiyo jinsi mnavyomwona kwenye video na ukikutana naye yuko hivyo. Yeye siku zote yuko “Natural”, hata katika mazungumzo yake.

    Nuru anaheshima, kwa wakubwa na wadogo, hajivunii usanii wake. “Kweliman”, ahsante sana kwa ushauri wako mzuri ambao nina hakika Nuru ataufanyia kazi. Endeleeni kumpa ushauri.

    It’s Great To Be Black=Blackmannen

  21. Comment by binti-mzuri on November 18th, 2008 12:25 am

    hee blackmannen kumbe huyu mtoto wa ki half casti mwanao.. mbona mzuri hivii.. hongera!! nilikua simjui,ila now nimemjua!safi sana

    kweli man umeniacha hoi.. me no comment,ngoja nisikilizie

    matty comment yako nimechekaa HAHHAHHAHAH lol kazi ipo kimwana, we unawachagulia wenzio sio,mbona we hujishushi hapo kwa mtoto ali kiba au unamuogopa cinderella jamani!?

    he jamani kweli bc raha, lalola shosti karibu,tunazidi kuongezeka kwenye chama! hapa utamkuta huyo bibie matty, halima, pearl, mama wa kichagga,kahindi,star,sisTZ,solange,michelle,maureen,debra,trii, kekuu mmh yani ni wengi balaaa .. kwa tani yako.

  22. Comment by Matty on November 18th, 2008 3:02 am

    Welcome LALOLA feel at home, BUT take care ukiboa humu watu tunasawazisha, anyway nisikutishe, inshorti tupo mashosti wa kumwaga kama unavyotusoma na kina kaka tunao shosti si kidogo pia!halafu shosti wewe unanidhamu sana humu sio kina Ross hata hodi hawapigi kazi kuingilia watu maungoni hahahahahahaha Ross kashaingia mitini now days!
    Kweliman, mimi sio mtaalamu wa muziki lakini mbona kawimbo kametulia tuuuuu??/mambo ya angels,vocal,audio tena hapo???
    Gervas kakangu nimeona nikuwahie mrembo maana Majita hakawiagi kubadilisha mawazo!!anyway wifi mrembo tutamfundisha taratibu kunywa ulanzi tena basi itapendeza kama atajifunza kunywea kwenye mbeta hahahahahah!

  23. Comment by halima on November 18th, 2008 5:49 am

    Latoya ahhh jokes lalola karibu ma sister kwenye ukumbi wa BC hapa kuna raha mfano hakuna yaani utafikiri tunaishi nyumba moja na Obama.

    Gervas changamkia toto hilo kaka angu mbona hivo unaanza kutoa visingizio tena? au tumrushie mpira mzee mzima Hombiz hahahahhhh

  24. Comment by Matty on November 18th, 2008 9:32 am

    Binti-mzuri, si unajua tena lazima kakazangu niwaangalizie vifaa murua hahahahaha wifi mie nae gubu lol!eti nawachagulia wakuletewa simtaki lol!

  25. Comment by hombiz on November 18th, 2008 2:21 pm

    Not bad. However, hard work is highly recommended!

  26. Comment by BLACKMANNEN on November 18th, 2008 6:57 pm

    Dada “Lalola”,

    Karibu sana, karibu mpaka ndani dada yetu, jisikie uko “HOME”. Binti-Mzuri na Matty, mtandikieni mkeka mgeni (Lalola) akae!!!! Majita atakuwa kaenda kuoga mtoni, atarudi baada ya muda si mrefu. Gervas yeye bado anaangalia video ya “Nuru”.

    The Man Of Actions……Black=Blackmannen

  27. Comment by wa watu on November 18th, 2008 7:37 pm

    Mpaka tumuone huyu Nuru live, maana bwana vyombo vya studio hatujui uwezo wake, ila kama anaimba hivi hivi hata live basi hongera sana mw’ana w’ane!!!!!!!!

  28. Comment by raphael on November 18th, 2008 11:01 pm

    Haya wakubwa naona kweli mmeamua na BC mimi na mbavu zangu tuu, nicheke hadi basi hahahahahah

  29. Comment by Gervas on November 19th, 2008 4:06 am

    Halima …wala usijali naamini sana Matty hawezi fanya makosa maana ukichaguliwa mchumba na wadada heshimu, kwa taarifa tayari amesha propose harusi itakapofanyikia…ufukweni Zanzibar na kasema huo ulevi wangu ndo unamfanya azimike na mimi, maana kwa kunywa pombe bei rahisi inaonekana ni jinsi gani ninaiishi Economics sio kuisomea tu…subiri kadi tu, nitahakikisha kuwa wana BC wote watakuwepo

  30. Comment by Lalola on November 19th, 2008 6:52 am

    Tehe tehe!!! Nasukulu i mean NASHUKURU kwa kukaribishwa. Jamani Binti-Mzuri na Matty mmeambiwa mnitandikie mkeka na Blackmannen. Uwiii mbavu zangu jamani. Mweeee!!!!

  31. Comment by Pearl on November 19th, 2008 8:46 am

    Lalola shosti tunakukaribisha sana.

    Blackmannen nina swali la kizushi, kuna siku nilimsikia Nuru mwanao anahojiwa Star tv kuhusu wimbo wake mmoja ila nimesahau unaitwaje, akasema wimbo huo ni kweli yalikuwa yamemtokea kuwa huyo ambaye angekuwa awe mkwe wenu alimpiga kibuti vibaya after staying for long in the relationship. Vipi ni kweli!!!??? kwasababu niliposikiliza hiyo interview nilimuhurumia sana Nuru. She is so cute.

  32. Comment by Matty on November 19th, 2008 9:52 am

    hahahahah Gervas na wewe nae usijali kwa hilo tuuu tena nakuandalieni beach party la nguvu na lazima mtoto anyenyuliwe upenuni mwa bahari huku Pearl akichukua shooting kamera! that would be ya karne aluuuuuuuuu unikute msimamizi Matty hahahahaha habari ndo hiyo, wifimrembo lazima ajidai!

  33. Comment by mtu on November 19th, 2008 10:29 am

    Tathmini aliyoitoa muheshimiwa Kwelimannen, imeenda shule bahati nzuri hata mimi nilikuwa na mtazamo huohuo, lakini uwezo wa uchambuzi bro, hapo juu amefunga kazi. Kwa tathmini hiyo inanifanya niseme kuwa bibi mrembo Nuru, tafuta fani nyingine. Ulimbwende ungekufaa lakini nadhani umri umekupiga chenga, lakini mamtoni huko mambo ni mengi ya kufanya. tafuta tu

  34. Comment by mtu on November 19th, 2008 11:16 am

    Naomba nami nichangie kidogo japo nilikuwa kimya kidogo, siunajua nilikuwa semester ya kushehekea ushindi wa Obama mitaa ya kisumu hukoo ndanindani kabisa, huko ni kamongo mtindo mmoja.
    Wanamusician wetu, wanajitahidi sana kutuburudisha, viwango vyao vimepanda sana ukilinganisha na miaka hiyo. Tatizo la wanamusician wetu ni kwamba wamejizatiti zaidi kwenye playbacks, wanapo kwenda ulaya anakwenda mwanamuziki mmoja tu, kitu ambacho wazungu hawapendi kabisa matokeo yake basi, Hao tunao waita mastar wetu huishia kutumbuiza jamii ya watanzania waishio ughabuni tu tena kwenye viholi vya mashule vichochoroni. Lakini vyombo vyetu vya habari vinaandika mfanoonyesho lilikuwa funika bovu, wakati silolote si chochote. Mi nadhani hatua za lady JD, Banana kuanzisha bendi na kufanya live perfomances ni lakupongezwa. Hata hapo watakapo perform Nuru na Alikiba ni shuleni, hakuna media iliyotangaza kuhusu onyesho hilo zaidi ya mablog ya kibongo, na sms za wabongokwa wabongo. na ndo hivyo ilivyokuwa huko unyamwezini. Safari ni ndefu na bado hatujafika.

  35. Comment by MKULU on November 19th, 2008 11:59 am

    Blackmannen hii sio blog ya kuwafagilia ndugu zako wewe na wala kuwatafutia wachumba

  36. Comment by Hombiz on November 19th, 2008 1:11 pm

    Halima mimi nikirushiwa mpira, nadhani unaweza kuwa mwingi na kutoka nje……..teh-teh-teh! Lakini enzi zangu, ilikuwa balaa! Nilikuwa nafunga penati kwa kichwa..kwi..kwi..kwii!…Majita pasha viungo. Dakika za majeruhi hazijafika bado. Muda unao kaka!

  37. Comment by juma on November 19th, 2008 8:05 pm

    WAtu ambao ni haters watakuwa na kubakia kuhate kila siku nani kasema alikiba na nuru wanaperform shuleni jamani…kwanini watu wanapenda kudanganya kwanza ilikuwa alikiba haji sasa mnatafuta sababu nyengine kama hutaki kuja kuona show baki nyumbani n watch tv….mtu ummecomment safari ni ndefu we akilini mwako unafikiri jay z anaimba na band o a dj na bado nyinyi o wewe unalipa 500 kwenda kumuona..mtanzania mwenzako 200 tu unalalamika lord jesus…safari hatutofika as long as we have haters n not supporters,,,,

  38. Comment by BLACKMANNEN on November 19th, 2008 10:40 pm

    Ndugu zanguni nyote WanaBC!!!

    Maswali yote yamhusuyo “Nuru”, ni vizuri ayajibu Nuru mwenyewe. Ili kufanikisha hilo, nawashauri watu wote wenye maswali kuhusu NURU, wayaandike maswali yao hapa, na mimi nitaongea na Nuru aje hapa BC, kuwajibu maswali yenu wote.

    My Name Is Black=Blackmannen

  39. Comment by Majita on November 20th, 2008 12:17 am

    Hombizi umeniua.uwiiii mbavu zangu.
    Hiyo penati uliyokuwa unafunga kwa kichwa sipati picha pua kama ilisalimika.Inabidi tukuchunguze makovu ya pua.Dua!!
    Lakini mkuu Hombizi mimi ngoja nipige jalamba

  40. Comment by Matty on November 20th, 2008 3:21 am

    MKULU unasond kivingine ohhhh nisije nikaomba BC atupe RAHA P na kibao chake haya hayakuhusu…………………………we are here to relax and have fun! try to differentiate jokes and veracity!

  41. Comment by amee on November 20th, 2008 6:56 am

    samahani kuleta topic hii, kuna website moja chafu sana na inampakazia vibaya sana nuru, roho inaniuma kupita kiasi, lakini we acha tu

  42. Comment by Matty on November 20th, 2008 8:12 am

    amee, wapi hapo nikaoshe kinywa??? wanamharibia wifi yangu mtarajiwa ohh jamani hebu weka wazi wapi hapo kabla Gervas hajabadilisha mawazo, asije akaghaiiri bure!

  43. Comment by kweliman on November 20th, 2008 11:32 am

    curious, mimi niko concern kwamba hatuzungumzii kabisa juu ya video au kazi ya kisanii ya dada nuru .naomba tungeli-stick kwenye more constructive (negative an positive ) comments juu ya kazi ya nuru kwa maoni yangu nafikiri tutakuwa tumemsaidia sana huyu dada ktk kuboresha kipaji chake
    samahani hasa kwa wale woote hapo juu amabao inaonekana kuwa ni watu manaojuana sana kwa karibu labda a don mean to inturrupt issue zenu
    kweliman

  44. Comment by rosa on November 20th, 2008 1:35 pm

    I am just not feeling her…… SORRY

  45. Comment by Hombiz on November 20th, 2008 1:41 pm

    Lalola, karibu sana kwenye wanja la BC although you are “old to the new”!

  46. Comment by papuu on November 20th, 2008 3:43 pm

    nuru mwimbo huu hauna maudhui. ‘wanadamu ni wazuri ni wana mali. mali ikiisha huwaoni’ unahitaji msaada wa kuandika nyimbo nimeelewa point yako ila mistari iko hafifu sasa ni wazuri ni wana mali haijaendana hapo. video yako umeiweka kujionyesha urembo wako badala ya kuweka kuendana na mwimbo wako ungeonyesha hao wenye mali mpaka wakapuputika wakakosa marafika na kadhalika sasa wewe umeweka fashion show. kama nilivyomshauri AY una mwendo mrefu sana dada AY karibu anafikia chalinze we ndio kwanza safari hujaanza all the best. nadhani mwana falusafa aliwahi sema sio lazima wote tuimbe

  47. Comment by chichi on November 20th, 2008 8:25 pm

    kama mtu hana chakusema bali anpenda tu kuongea aonekane mjuaji its betta to just shut the fuck up,,,binadamu wote tuna rite ya kuwa na opinion but jielimishe kwanza kabla hujafungua mdomo wabongo mnapenda sana kuongea n iv noticed hapa mnaccoment vitu vengine hamna mtu aliyouliza..the issue was nuru anamfungulia alikiba show meaning ye ni opening act na mmewekewa video kuona kazi yake…ndio nuru ni mzuri hatukatai lakini swali halikuwa kama ye ni mrembo that is what ppl r seing kwamba nuru is a beautiful girl…hata we ukae uongee mavi nuru ni mzuri but is that the issue here,,,???
    wimbo either u like it o not bass imetosha sio sijui kamera ya ubatizo angle blablabla kwani we director fanya yako uweke nasisi tucomment….
    hee huyu nuru kafanya show wapi eeee nani kaongelea kuhusu nuru kufanya show… yet again issue ni nov 22 nuru is going to be the opening act ya alikiba simple as that

  48. Comment by kelly on November 21st, 2008 7:58 am

    you Chichi u better watch ur mouth na ujue unajbu ni nini,sio kujibu watu as if ww ni Nuru,majibu yako yanaweza kusababisha hata Nuru akazomewa siku ya show,just be calm wacha hawa watu watoe comments zao wakichoka watakaa kimya,Nuru ataprove that day how good she is,unapoanza kulumbana na watu utafanya Nuru asiwe na confidance siku ya show kama atakuwa anasoma hizi comments…au hukujua kuwa kuwekwa kwa video ya Nuru kutakuwa na comments positive and negative?…BE CALM CHICHI…I HOPE NURU WILL PROVE HOW GOOD SHE IS TMRW.

  49. Comment by Frank on November 21st, 2008 11:12 am

    Papii hujaskiliza wimbo vizuri umerukia ku comment. Uli mstarti unasema ‘binadamu ni wazuri UKIWA na mali, mali ikiisha watu wote huwaoni’. Sasa hapo kigumu nini kuelewa?? Cha!

    Nuru sio mwanamuziki full time, anafanya kama hobbie, sio kwamba ye anategemea kuishi kwa mziki. Hivo hawezi invest millions kwenye cutting edge video wakati sio source yake kuu ya income.

    Nuru keep it up.

  50. Comment by Gervas on November 21st, 2008 11:51 am

    MMmh..leo BC umeniamlia kweli, comment zangu mbili zote umeminya!!!! aiiseeee…tutafika tu lakini, zilikuwa za Dada Matty. naona na hii ataibinya tu..ngoja tuone

  51. Comment by kweliman on November 21st, 2008 1:41 pm

    kwako wewe unyejiita chichi.ujumbe wako mimi binafsi nimeuelewa nimefurahi kwamba umetumia haki yako kama vile ilivyo yangu kuexpress maoni kuhusu dada Nuru na kazi yake .
    kitu kimoja ningependa kutofautina na wewe ni kwamba hapa mimi binafsi siongei kujifanya mjuaji ” betta” bali ninaongea kwa sababu AM CONFIDENT NA NINAJUA . and if thIS FACT BOTHERS YOU.HEY ,CAN’T HELP IT, SUCK IT LIKE A REAL WOMAN OR REAL MEN!
    Kuhusu hiki ulichosema ” wimbo either u like it o not bass imetosha sio sijui kamera ya ubatizo angle blablabla kwani we director fanya yako uweke nasisi ”
    Jibu langu ni kwamba YES! MIMI NI DIRECTOR na pia najifunza kuwa producer lakini mimi sina kipaji kama cha Nuru yaani mziki .No. Na siwezi fanya video yangu ya muziki mimi sio mwanamziki bali i got a fairly good knowledge and skills bout
    music video and film making.am not here to BRAG MY SELF OR DEMOSTRATE MY SKILLS AM HERE TO EXERCISE MY RIGHT TO SHARE MY OPINION SPONTENEOSLY IN THE BEST POSSIBLE WAY THAT DOES NOT OFFEND OTHER MEMBERS.
    THIS IS A PUBLIC DOMAIN anybody is welcomed!

    “wote tuna rite ya kuwa na opinion but jielimishe kwanza kabla hujafungua mdomo wabongo mnapenda sana kuongea n iv noticed ”

    I recognised here that wewe una “RITE” ya kuwa na opinion . Chichi, that’s Good for you! You can have your RITE AS MUCH AS IT PLEASES YOU .That said ,i would rather have the RIGHT ya kuwa na opinion and that,s what exactly am practicing now! fyi!

    Speaking of Kufunga mdomo-Chichi, i don mean to offend you but you you better recognise that words like MUM and SHUT UP are not part of my vocabulary and personality.
    i can speak bout anything ,wherever and whenever it pleases me and as much as possible provided its consisitent with the existing acceptable social norms
    i am not intimidated or dictated to by any individual Chichi,especially if that indv ni MSOMI na MWELEVU wa hAli ya juu kama WEWE.Chichi ,forgive me if i offended you WITH THIS!
    Nimetoa maoni yangu kamA vile wewe ulivyotoa yako ni si kwa sababu ya kukuplease wewe chichi
    Nuru is a young and upcomimg artist , i recognised that she’s got great potential ofcourse after watching the video repeatedly.Sponteneosly i decided to comment with good intentions at heart,honesty and in my own perspective .why? a don have to explain this .to you cause to me you are nothing but just another member troubled and choked with my personal opinion over Nuru’s video.Chichi from your comments ,it so obvious to me . You got a problem with my comments. Reason?.Not the tiniest clue,and a don really care

    Nuru dada, check this out, please don get too personal with my comment,i work in the film and video industry.i got the skills and knowledge .ofcourse it may not be like spielberg or spike lee but to me and especially to me it’s worth my life and my career.
    i gave my opinion based on what i know and on what i saw it may not sound so damn pleasing as you would probably wish. i got one opinion 4u .Take any criticism of your work as an opportunity to motivate u and 4u to grow in your music career .The way to stardom is so rigid and rough and always stormed with tonnes of disappointments,discouragement and all sorts of nasty shockers .
    God gave you great looks,talent and the will use them ,stay focused and some day you gonna get there.
    If u ever get showered with false praises ,don pay attention to them .Always look out 4 criticism and learn from them bout your work.
    Nuru samahani dada yangu kama nitakuwa nimekutibua kwa sababu ya maoni yangu na pia samahani kwa member wengine woote kwa kuwaboa na maoni yangu na jibu langu kwa Chichi
    Kweliman

  52. Comment by Matty on November 22nd, 2008 2:00 am

    Gervas ulisema nini kwani???hahahaaaaaaa unaweza kuwa ulisahau kuapply tasfida ndo maana!

  53. Comment by amee on November 22nd, 2008 4:40 am

    Nimekupata kweliman, chichi alikosea sana, ni lazima kila mtu awe na opinion yake in life,kama yeye alikuwa positive but in the other hand you didnt see that way then you have every right to bring what you thought was right on your opinion. Basi maneno yaisha and i hope we both understand both of you, chichi was a little defensive over someone she loves so does anyone, kwahiyo watu wasimuelewe vibaya, kila mtu hufanya hivyo sometimes so, her bad and hope we both understand that. Weekend njema

  54. Comment by kakam on November 23rd, 2008 1:58 am

    jamani i went to see the show nuru nuru na nasema tena nuru ont give up we demu ni nomaaaaaaaa..yaani umefunika jana mwanangu mie sema ukweli nilijua studio tu hiyo nikaja mwanangu umenifunga mdomo n ahsante sana kwa kutokugive up tunahitaji talent kama wewe bc tuwekee picha ya show….na cinderella man nae alijitahidi

  55. Comment by BLACKMANNEN on November 23rd, 2008 5:52 pm

    Dah!!!!! Dada Matty….”tasfida”…..kiswahili kikali hicho, mie sijaona ndani!!!

    Black=Blackmannen

  56. Comment by Matty on November 24th, 2008 2:21 am

    Blackmannen si unajua tena mimi mwalimu wa kiswahili so tasfida muhimu jamani ili kupunguza ukali wa maneno!

    Jamani blue monday ina mwonekano gani wadau?

  57. Comment by Moi on November 24th, 2008 4:45 pm

    SO THIS IS NURU NICE
    SHE CUTE
    VERY CUTE :)

  58. Comment by hombiz on November 24th, 2008 5:56 pm

    Matty Mimi naona swali la Blue Monday tumuulize “Mr. Blue, au!?

  59. Comment by Matty on November 25th, 2008 2:17 am

    Haya kaka Hombiz MR.BLUE njoo ujibu swali langu!

  60. Comment by chapombe on November 26th, 2008 7:28 am

    we bwana kule juu namba 8,unayekwenda kwa jina la Adam Tensta,mimi nakushauri huko sweden ulikokuwa,ujitahidi kubeba maboksi,ili ukirudi kijijini kwenu uwe na pesa kidogo ya kununilia jembe la kuazia kilimo cha kufa na kupona,kuliko kuwawekea ntima nyongo wabongo wenzio pasipo sababu.embu soma vizuri hiyo habari jamani,umeambiwa anatarajiwa kufungua show ya mwanamuziki mwingine Ali Kiba.sasa wewe umekurupuka,utafikiri umevuta bhangi mbichi,ooh,aseme show afanyaga wapi,sisi huku sweden tunamwonaga kwenye pati tu,sijui anadanga wabongo.kwani nani kwambia anatudanganya?

  61. Comment by chapombe on November 26th, 2008 7:32 am

    lalola,swali,je umeolewa?

  62. Comment by cityboy on December 2nd, 2008 2:18 am

    Jamani tutakufa wote, watabaki vichaa tu, wa muhimbili, hahahaa!!!

  63. Comment by shueb on March 15th, 2009 1:24 pm

    una salamiya

Leave a Reply