
Ninapoona picha za viongozi waliokuwa wanaheshimika na pengine hata kupewa sifa za “uadilifu uliotukuka” wakiwa kizimbani kujibu shutuma za kujifanyia mambo wanavyotaka kwa manufaa ya matumbo yao na yale ya ndugu,jamaa na marafiki zao,huwa siishi kujiuliza swali lililo kwenye kichwa cha habari hapo juu;Mwalimu Nyerere angekuwa hai angesema nini kuhusu watu kama hao?Wakithibitishwa kuwa na hatia,angeshauri wapewe adhabu gani?
Feedback / Comments
57 Responses to “ANGELIKUWA HAI ANGESEMAJE?”
Leave a Reply


sending...
Angekuwa hai angesema dah “Sijui kwanini sikumtabiri kijana kama JK kuwa raisi toka akiwa kwenye late 20′s”
Atakumbukwa milele, Mzee asie jilimbikia mali, Mzee wa shoka, asingelituletea mambo ya mahaka ya kadhi upuuzi mtupu, you will be missed forever!!!!!!!!!
Matty,
Hebu bana sauti na uigilize sauti ya Nyerere na uanze kusema maneno yafuatayo:-
“Yaani hata wewe Basil? eeh!! ni upumbafu upumbafu tu mnataka kulisha wenzenu majani kumbe ninyi mnakula kuku kwa mirija.This is ridiculous….Nilishasema kiongozi mzuri ni yule anayehakikisha wananchi wake wana vision ya kujinga’ua kutoka katika lindi kubwa la umasikini.Ninyi mnakalia kuwa na slogans za ajabu ajabu kana kwamba mliumbwa na shetani. (badili sauti) ooh ndege ya uchumi inapaa,mara Ooh tutaleta mvua ya kutengeneza, (rudia sauti yake) this is amazing kuona mtu anaeitwa mheshimiwa anakuwa na akili za konokono”
(geuka kidogo) ooh shhhhhh basi bana mtoto wa masaki yupo asije kuanza kutukana hapa si unajua akawii kusema Nyerere alikuwa anaomba chumvi kwao??hahahahaha
Kwanza kabisa hiyo picha hapo juu ina majibu tosha ya jinsi Nyerere alivyokuwa mtu wa kawaida sana asiyekuwa na makuu, licha ya kuheshimika na kutambulika duniani kote!
Hebu ndugu zangu jiulizeni leo hii ni viongozi wangapi wa humuhumu Tanzania achilia mbali Afrika wanaoishi maisha ya kufuru yaani utajiri unaonuka(Filth Wealth)? Hizo pesa wamezitoa wapi na kwa njia zipi huku wakiwaacha Watanzania walio wengi wanataabika?
Mwalimu alishasema mengi sana katika hotuba zake kuhusiana na rushwa, ufisadi, kuupuza katiba na mengine mengi, labda angekuwa hai wasingeyafanya wanayoyafanya ama asingesita kuwakemea!
Sasa basi nakumbuka katika hotuba yake ya tarehe 14 Machi,1995 pale zamani Kilimanjaro Ballroom sasa hivi Kempinski alisema hivi kuhusu rushwa:
“Msidhani katika awamu ya kwanza hapakuwa na rushwa, rushwa ilikuwepo, lakini tulikuwa wakali!! Tulitaka viongozi wetu watambue hilo, hatukufanya mchezo na rushwa hata kidogo! Na kiongozi akishathibitika amepokea rushwa, kazi hatukumuachia hakimu peke yake, Ehe viongozi wetu mnakula rushwa? (kicheko)! Akishathibitika amekula rushwa, alihukumiwa kifungo kisichopungua miaka miwili jela, viboko ishirini na vinne, kumi na viwili siku anaingia na kumi na viwili siku anatoka akamuoneshe mkewe vizuri!(kicheko)!
Wote wawili tuliwapa msukosuko, aliyetoa na aliyepokea, kwa hiyo hatukuwa na mzaha na rushwa hata kidogo”!
Alishasema ikulu ni mahali patakatifu, kuwa rais kwenye viinchi masikini kama Tanzania ni mzigo mkubwa matatizo matupu! Unatembea barabarani unawaona akina mama wanauza vitumbua, watoto hawana viatu ule ni mzigo wako rais! Wengine wanamatumaini ya kula, wengine hawana, tofauti ya matumbo hiyo peke yake inatosha kuvuruga umoja kama huu tulionao Tanzania. Huyo ndio kiongozi pekee aliyekuwa na uchungu wa dhati na Tanzania. Hatusemi hakuwa na makosa yeye ni binadamu ana mapungufu yake.
Lakini nasema hivi Nyerere atakumbukwa daima anayebisha na aseme! Aluta Continua!!!
Pumzika kwa amani babu mpenzi jamani!
Wewe ulikuwa na uchungu na nchi yake kabisa sio hawa kina Rostam Aziz,Lowassa,BWM,karamagi,yona,mramba na wengine ambao wanajijua!
Nadhani ungekuwepo hawa mafisadi ungeamuru wahame nchi au la sivyo wachomwe moto tu!
I think hizi habari za kurudi back na kusema what will mwalim said kama angekuwa hai ni off line. Tanzania people doesn’t diserv kinachofanywa na viongozi wao, it doesn’t matter Mwalim angekuwepo au asingekuwepo.
Hawa Mafia wangefanya what they believe is okay kwao. I think mfumo mzima upo corrupted, i think watanzania we’re insane. I can prove that we’re insane, sababu tunafanya same thing over and over na kuexpect different results.
Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu mwadilifu na mcha Mungu. Alifanya kazi yake kwa maadili ya imani za kumcha Mwenyezi Mungu. Kama angekuwepo hapa leo akashuhudia maovu yanayofanywa na viongozi wachache wa serikali, wenye maadili mabaya. Nyerere angeutumia uwezo wake aliopewa na Katiba Ya Jamhuri Ya Mwungano Wa Tanzania kwa kuwaweka kizuizini “Watuhumiwa” wote, wakati harakati za vyombo vya sheria vikijipanga kuwashughulikia ipasavyo.
Enzi za Nyerere, “Watuhumiwa” hawa, mbali ya kusota (lupango) kizuizini, kwa kipindi kirefu wangefirisiwa mali zote, ambazo zingeshukiwa kuwa, wamezipata kwa njia isiyo halali. Mwalimu Nyerere alikuwa akilinganisha kipato (mshahara) cha mtuhumiwa na mali aliyokuwa nayo, kabla na baada ya kupata kazi serikalini, kama zinakubaliana.
Enzi za Nyerere, “Watuhumiwa” walifilisiwa mali, tangu watoto hadi ndugu zao. Kila mtu alichunguzwa na kuangaliwa uwezo wake wa kuipata mali waliokutwa nayo na muda waliopata.
Kama Nyerere angekuwapo na kweli akashuhudia viongozi wa chama chake wakifanya maovu kama haya mbele ya umma wa Kitanzania, angekivunja (kama alivyoyavunja Mashirika ya Umma, yaliyokuwa mzigo kwa Watanzania) na kuanzisha chama kipya chenye mwelekeo na maadili mema. Mwalimu Nyerere, angechagua viongozi wapya waaminifu wenye kuilinda Katiba Ya Chama na Katiba Ya Tanzania. Angechagua viongozi wenye uwezo, ambao wangewatumikia Watanzania kwa imani na upendo, badala ya kutumikia matumbo yao na ya ndugu zao.
Mwalimu Nyerere alipofariki, Watanzania wengi tulimlilia kwa uchungu wa kuondokewa na kiongozi wetu mwadilifu. Kumbe wenzetu wengine walikuwa wakilizwa na furaha za kuondoka kwa mtu (Nyerere) aliyekuwa kikwazo kikubwa chao katika kujinufaisha katika mambo yao. Kumbe usemi usemao kuwa, “Kwenye Safari Za Mamba, Kenge Pia Huwemo” ni kweli kabisa.
It’s Great To Be Black=Blackmannen
Haya anzeni kama kawaida yenu!!!!! nawasubiri!!!! wadau!!!!!
kabla ya yote si kwamba angesemaje kama wangepatikana na hatia bali wanahatia tayari,na mwalilmu kwa kuwa alikuwa jasiri angesema hivi
1. `kabla hawajaingizwa kizimbani wachapwe viboko nusu ya umri wao kila mmoja halafu wakandamizwe vingine nusu ya umri wao siku ya kupelekwa mahakamani ili wasiwe na uwezo wa kukalia viti visivyokuwa na dhambi kama zao[viti vya mahakama]
2.asubiliwe fisadi mwenzao mwenye kihelehele cha kuwatolea dhamana ya mabilioni ya hela hizo aulizwe kazitoa wapi kisha afilisiwe na afungwe maisha yake yote.
3.wafilisiwe mali zao zote,wafungwe kifungo ambacho ni cha kipekee[typical] ili kutoa fundisho kwa mafisadi wengine wasiojiheshimu-walitumikie taifa kwa kufanya kazi za shulubu ili kuliingizia taifa pato ambalo ni sawa na wizi walioufanya.
4.kwa kuwa wana genes za ufisadi basi na watoto wao pia wachunguzwe ili wasipewe madaraka yoyote kwani na wao ni wahujumu tu-mtoto wa nyoka ni nyoka.
”nakuja na mada nyingine sasa………………………111111Nawaomba waandishi wa habari wamuulize huyo fisadi alimaanisha nini alipokuwa akisema nihalali watanzania kula majani ila ndege ya raisi inunuliowe,je familia yake inaujua utamu wa majani? kauli na kiburi na jeuri kama hiyo alipewa nani mpaka kuwatukana waungwana na wazalendo ambao kodi na jasho lao ndilo lililokuwa likimvimbisha tumbo-kumbe mafisadi kauli zao ni za kejeli,jeuri mauzi na upuuzi mtupu.
Wafanyabiashara tunaomba mtuletee bunduki za kichina kwa maana tunaona watu wanataka kutuletea zengwe mbele ya maslahi ya nchi-mtu anapelekwa kizimbani anatabasamu wakati kaiba,huu utani sasa!!!!! halafu polisi nae anamchekea eeeeeeeeeehee!!!!!! hivi watanzania tuna uchungu maisha/jasho letu kweli.
Nilikalilishwa tangu msingi kuimba……………….mapinduzi nitakulinda mpaka kufa……….nijipe matumaini eti mimi ni kiongozi wa kesho,ipo siku mafisadi watakiona cha moto,dhambi na udhalimu wao ufika mwisho na tutawahukumu sisi wenyewe-muumba awape uhai ili tuje tuwafundishe kazi kwani tz inaamka!!!!!!!!!!!!!
” im proud of being a peaceful tanzanian”
hayaaaaaa..mdau nazama ndani ya dimbwi hili la maoni,naandika kama vile sioni,ebana angekuwepoingekua mambo laiiiiiiiiniiii kama unanawa,laiiiiniiii kama unanawa tena maji ya sabuni.ebana angeagiza jeshi liwashike alafu wapigwe vidole hao.
Angesema ROSTAM AZIZ anyongwe mpk afe.
Yona na mramba wafanyie mchezo wa KIARABU gerezani keko.
Lowassa atobolewe Masikio.
Chenge atupwe Baharini aliwe na papa.
Kikwete akacheze mdundiko kwa Bagamoyo.
Megji atembezwe uchi Manzese.
Karamagi aambukizwe Ukimwi kwa lazima.
Jeetu patel azikwe akiwa hai.
Na mimi niwe waziri mkuu wa Wadanganyika.
mimi nafikiri hawa wanastahili adhabu ya kunyongwa hawa ndo wanaotufanya tukimbie nchi yetu kuwa watumwa ktk nchi za watu huu ukimbizi wa uchumi utaisha lini kwetu wenyewe na familia zao wanakula kwa upole tu watuona sie wajingaaa mhh haya bana kula kwa zamu
Majita kakangu na wadau wengine,
naomba msishtuke na hili jina pia (Mattylda) maana jina la Matty Original pia linasarandiwa na huyo matty mpya,anyway mimi ndo matty wa zamani, but now nimeamua kuliacha hilo jina baada ya kuona linasarandiwa na mtu mwingine!
Anyway kubana sauti ya nyerere sitaweza ila wewe Majita nakuaminia kwa kumuigiza hahahahahaha au mpaka utoke kuoga kule mtoni???
Eve wat do u mean?
Kwanza naomba nitumie mistari miwili kuwajulia hali wenzangu.
Gervas,Majita ,Matty kwa niaba ya wengine wote NIMEREJEA kuendelea na safari yutu..TUTAFIKA TU.
Naona mambo mengi yamenipita mara TOP aka TID mara Ndege kachomoka Tunduni wakati anakula bata dar mpaka Arusha wanadai anatuhumiwa “kula chakula ambacho hajaiva” yaani kadokoa..kama ni kweli siyo fresh..ila kama saundi..basi pole kwake..
Kwa kifupi nimerejea na thipidi ile ile..
Majita nimejityuni nikaimba kasauti ka mwalimu kweli “WAHESHIMIWA WATUHUMIWA” wamechemsha..tuacha mahakama ifanye kazi yake..
Ila kubwa naomba kuuliza..maana naona MATTY ORIGINO…ina maana ndiye yule Matty wetu kajitoa EATV na sasa ni Matty origino?
Matty naomba ufafanuzi au kwa yoyote mwenye jibu iwe Chris,mama wa kichanga,kekuu ,Any etc
Tupo pamoja..Tutafika hata kama tumechoka
sasa nimerejea
Unayejiita maty Orijinal,
unatakiwa uumize kichwa kwa kufikiri kabla ya kutenda sio kufanya tu kama mtoto wa nasary school!
Mtu mstarabu hakai akaiga kama ulivyofanya wewe matty mpya, haitoshi unaonesha ni jinsi gani ulivyo mvivu wa kufikiri utaishia kuiga hata visivyoigika!hata kama na wewe una jina kama langu u better change kidogo kwani hata ungejiita matty 2,matty wa tabora,mbeya,uk et.c kuna mtu angekuuliza?mtu mzima ovyo!
Wadau jamani hebu nisaidieni huyu mrembo matty mpya naona ananitafuta ajue undani wangu!
Kama mwalim Nyerere angekuwa hai angewapa onyo hawa wahalifu halafu angewabadili sehemu zao za kazi ili kulinda heshima zao.
hamna lolote chochote hapa katika komenti zote nilizozisoma. This same man who brought socialism, ujamaa wa ajabu ndio unaleta iflation tanzania inayo kwa sasa. najua nyerere wewe ni mtu muungwana na tunakusifu kwa yale uliyoyafanya japo yeyote angeweza kuyafanya ila ulipata mwanya huo,ila kusema mambo kama ‘mcha Mungu’ nyinyi mnajuaje.
NYie watu kweli mna chekesha, eti Nyerere alikua simple na hiyo picha inaoneysha, hivi mnaakili kweli nyie’?
Nyerere hakuwa simple, alikua ana kila kitu anachotaka na alihakikisha ana pension nzuri ya kumuwezesha kuishi kama mfalme miaka yote ya maisha yake, watoto walisoma CUba na Urusi, wewe mtoto wa mkulima wa kawaida uliweza kuishi hivyo?
Msitudanganye hapa, kwanza mwenzako alikwu anapanda Cidiz kwenda kazini, akisafiri ni first class, kwanini asingepanda Econnomy kama Lipumba livyotaka kutudanganya eti akiwa raisi atajaribu ku save kwa kusafiri kule Econnomy class.
Nyerere kafia LOndon, kwanini asinge fia Ocean Road kama Watanzania wengine ?, kwani aliondoka TZ akiwa na akili sio mahututi ,kwanini kama angekua simple asinge goma na seme atibiwe hapa hapa Bongo kama Mtanzania mwingine sababu yeye ni simple. hivi mna ijua St THomas Hospital nyiie? acheni kutudanganya hapa.
Angejilaumu kumpigia debe Mkapa a.k.a. Mr clean(kiranja wa mafisadi), mpaka akawa Rais!
Ed….I real dont get your point here, ndo maana BC amesema angekuwepo angesemaje its just an imagination, kwani nani hajui watanzania wanachukia ufisadi? …Majita kweli umempatia mwalimu!!!
Nyerere pia kuna watu wake alikuwa na udhaifu nao kwa sababu azijuazo mwenyewe lakini!
Angekuwepo nyerere hawa viongozi mafisadi wange firisiwa mali zote nashangaa watu wame kwiba pesa wanapewa dhamana tena dhamana ni mabilioni wanaonesha ni jinsi gani walivyo na pesa kila day na mkumbuka baba wa taifa mungu mlaze mahara pema peponi Amina, tanzania bila ufisadi ina weza kusonga mbele
Mi nafkiri angekua hai hakuna hata mtu ambae angethubutu kuiba hata elfu hamsini,Kwa sababu enzi zile ukienda kinyume na matakwa yake ujue utapigwa chini.na ndio maana watanzania hawawezagi kuongea wako kimya tu walikua wanamwachia mwalimu tu aongee maana walidhani anajua kila kitu.Siku hizi ndio watu wameanza kuongea na kujua kuiba.
Pole Matty walimwengu hao…mada ya leo,laiti kama
basi angecheka sanaaaaaa kusikia walioiba wanaruhusiwa kuludisha na sio wezi tena wala joto la Segelea halitawagusa hiyo kali sana…Wengine waliokuwa rumande wanaruhusiwa kupewa dhamana nusu ya wizi walioiba watakuwa njeeuku kesi yao ikiendelea ili nusu ilibakia wagawane na waganga pamoja na naniii?MATTY GERVAS NA BINT MZURI NATUMAINI MTAMALIZIA
hombiz
Hapo umenifurahisha sana yani nilikua na maana hiyo niliposema “Angekuwa hai angesema dah “Sijui kwanini sikumtabiri kijana kama JK kuwa raisi toka akiwa kwenye late 20’s””
Kweli kabisa alitudanganya kua eti kuna Mtu safi kabisa yuko na kufaa kua Raisi na ndio akaonekana Mkama alikuw ana nYumba Dar na NYumba Mtwara na Ki gari cha Mercedz Benz kimoja,.
Nadhani JK akijitahidi na kuwa mkali na kutuonyesha yeyte ana weza kwenda keko na uhakika in ten years time, watanzania culture ya rushwa na kitu kidogo na kuonakama ukiw ana cheo nchi ni yako itabadilika kabisa na kuwa watu tunauchukai ufisadi.
Bado kazi kubwa hao kina Mramba na wengine ni sehemu ndogo tuu, sehemu kubwa iko kwenye huduma za jamii na rushwa za kila siku mitaani huku hilo ndio tatizo kubwa ,ila na amini kazi ndio imeanza, next waanziwe ha wa marketing manegers wanao taka rushwa nao wadhibitiwe wanatukwamisha kazi nyingi.
MWALIMU NI MTU WA SHERIA ANGEWAFUNGULIA MAKARATASI YA SHERIA NA VIFUNGU VYAKE,KILA FISADI ANGEJIJU
watu wasioelewa kazi alizozifanya (Nyerinyeri) Nyerere sirahisi kuwaelewesha wakaelewa maana pengine hawakuwatayari wameshazaliwa, huwezi kumlinganisha mtu kama huyu na mafisadi kama hao hapo juu, hakuwahi kujilimbikizia mali hata kidigo,watoto wake wameishi maisha ya kawaida sana na shule hapo hapo Bongo si hawa ambao wanasomesha watoto yao nje kwa jasho la wanainchi, hivyo mwacheni Muzee apumzike kwa amani habari ndo hiyo, asiependa naajinyonge.
Nadhani kiboko yao alikuwa ni Moringe Sokoine. Yeye aliwaita kiwaziwazi wahujumu uchumi na enzi zake watu walitupa hela na mali walizoiba mtoni. Nyerere yeye alikuwa soft kidogo chukulia watu kama akina Kighoma Malima, Diria walicheza tiktaka mbele yake. Mrema pia angeweza kuwa supastaa lakini walimdhiti mapema.
Asante DUNDA GALDEN, najua ni utoto tu akikua ataacha!
Edwin Ndaki, karibu sana usishangae shangae sana, mimi ndo yule Matty wa enzi zile, sasa kuna matty mwingine katokea so na mimi nikaona ni bora nijing’oe EATV kama ze comedy na kuwa Matty Original basi hiyo haitoshi mrembo matty mpya akadai bado yeye ndo matty original eti nimemuibia jina lake,nikaona safi basi mimi nitatambulika kama Mattylda sasa nataka nione kama atanifata tena!
Ross naona unataka kuchafua hali ya hewa hapa, unauhakika na unayoyasema??au unataka kuusemea moyo wa Mwalimu Nyerere??
Asante DUNDA GALDEN, TUKO PAMOJA!
naomba Nianze kwa kusema zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM nanyi naomba mjibu zidumu milele!…….watanzania bwana sijui tumelogwa au vipi! wanamsifia mtu ambaye ameiletea ummaskini wa kutupwa nchi hii kwa ujamaa usiowezekana. wanamsifia mtu ambaye amebadilisha historia ya nchi hii na kusomeka kuwa inaanzia mwaka 1960 pale yeye alipochukua nchi na kuzika historia ya waasisi wote wa kudai uhuru kama mzee dossi, Rupia,Tambaza,sykes n.k! tuseme ukweli kuna mtu anajua undani wa roles za wazee hawa katika kudai uhuru?hamuwezi kujua kwa kuwa nyerere alifuta na kuandika upya historia ya Tanzania inayomtaja yeye tu na kwa kweli amefanikiwa ndo maana tunamuita baba mpaka leo! nyerere ndie aliyemmuweka mlea mafisadi mkapa na sasa tunalia je tumesahau haya?! kweli alikuwa na hotuba zinazovutia na zinazochekesha lakini kiutendaji mzee huyu alika hovyo na ni bora tukamkumbuka kwa mabaya yake pia kama mwandishi maarufu wa jarida la wallstreet journal la marekani alivyowashauri watanzania wakati wa msiba wa nyerere!
Hi guys kutoka Helsinki
Kwa kweli Mwalimu angekuwepo hangesikitika sana kwa sababu kijana wake Beni mkapa richa ya kuwa alifundishwa na Mwalimu Pugu, halafu akawa mwandishi wa Raisi Nyerere na baadaye akawa waziri , Nyerere alimwamini sana mkapa lakini Ukweli wa mambo baada ya kifo cha Nyerere mkapa ameonyesha makucha yake na umbo halisi- Kwanza mkapa ni bepari, mbinafsi na mbabe na pia alifanya biashara akiwa Ikulu, ndiyo maana mawaziri wake akina mramba na Yona walifanya wizi, Mramba alinunua ndege feki kwa pesa nyingi 40 billion, na tunakumbuka jeshi la polisi wakati wa mkapa lilivyokuwa mstari wa mbele kufanya dhuruma kama vile Zombe na kashifa nyingi za mahita na mkapa alikuwa anawalinda, hivyo kwa ujumla Mkapa hakuna hata chembe moja aliyojifunza au kuiga kutoka kwa nyerere, LAKINI RAIS WETU WA SASA JK ; YAANI KIKWETE ANA MAMBO MENGI ANONYESHA KWA WAZI KABISA YANAFANANA YA NYERERE; KWA KWELI KIKWETE NI KIJANA WA NYERERE; MIFANO NI MINGI, NITATAJA MICHACHE
1. JK ametoa adabu kwa jeshi la polisi na Zombe ni mfano-sheria ni msumeno
2. Jk kamtosa Lowasa
3.JK kamtosa Mramba na Yona
4. JK kaongeza uhuru wa vyombo vya habari alimtembelea Saidi Kubenea
5. Jk anasikiliza watanzania
Sasa Ben mkapa sijui kama atanusurika maana serikali yake ambayo iliwekwa na Nyerere ilituuza na kufanya kila aina ya ufisadi
hongera sana Kikwete historia itakukumbuka,
Aruta kontinua
Frateline
1. Angelikua hai Kikwete asingekuwa Raisi, maana kila kiendeleacho sasa hivi source imeanzia kwa Mkapa na Kikwete yumo kwenye huo mkumbo!
2. Baada ya KIkwete kuwa Raisi, kwa maana kama angeshindwa kushawishi asiwe Raisi, naamini… kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu, angejitoa CCM na kuunda chama kingine, pale tu ambapo angesema wafilisiwe na kupelekwa mahakamani nako kama kungeshindikana.
3. Tanzania tunahitaji mtu kama Sokoine lkn atakaekuwa na uzalendo lkn na mtizamo wa ulimwengu wa sasa.
“Simon Katururu”, # 21 kama ni wewe, katika BLOG yako, mimi nakushukuru kutuwekea mziki wa “Kingwendu – Demu Mapepe”, kwa ajili ya kutuburudisha wikiendi. Tack så mycket, hej då!!!!
Black=Blackmannen
huyu mzee nyerere alitumia muda wake mwingi kuangalia ni jinsi gani angeweza kuheshimika na dunia na si kuboresha maisha ya watanzania. akaweka kambi ya wapigania uhuru wa afrika kusini tanzania na haohao wa afrika kusini wanaua ndugu zetu kila siku. akatumia nguvu na fedha nyingi kwa vita vya kagera kisa alitaka swaiba wake obote awe rais wa uganda.ikumbukwe idi amini hakuichokoza tanzania ila nyerere alimchokoza idi amini kwa kuwa alitaka obote ndo atawale uganda na sio idi amini na hapo ndo mgogoro wao ulipoanza ( hapa wenye akili tu ndo watanielewa) vita hivi vimeigharimu sana nchi yetu na ndo chanzo cha umasikini wetu. nyerere huyuhuyu alipigania ukombozi wa zimbabwe angola na msumbiji na kupeleka askari wetu huko badala ya kujenga uchumi wetu mchanga askari wengi walikufa leo hii anaitwa mchamungu ama kweli watu ni wavivu wa kufikiri! nyerere alipenda watanzania wawe masikini na ndo maana mwinyi alipojaribu kututoa ukungu kwa kutuletea television na magari nerere alimtukana kama mtoto wake tena mbele ya hadhara! leo anaitwa mchamungu huyu? ikumbukwe hata katika kipindi chake watu waliichezea nchi hii na hakuwafanya kitu ila wale waliohatarisha nafasi yake tu kama kambona na profesa babu,kassim hanga n.k ndo aliwashukia lakini ikumbukwe pia kina msuya walijenga kwao Mwanga kwa fedha zetu wakati alipokuwa waziri wa fedha na waziri mkuu.huyu hakuguswa na mchamungu nyerere pia yupo aliyekuwa gavana wa benki kuu muhindi amir jamal. huyu alikuwa swaiba sana wa nyerere amefariki lakini familia yake ipo canada na wanaishi maisha ya kifahari. hapa unaweza kugundua kitu kuwa hata nyerere alikua na uswahiba na mafisadi kwa hiyo hata angekuwepo angewachamba wale anaowachukia tuu. kuna kimtu hapo juu kinasema eti alikuwa mwadilifu na mchamungu! msiseme tuu eti kisa watu wanasema au kwa kuwa imeandikwa hivyo. have a time to think!
ENZI ZA MWALIMUUUU…..
Angesema…….
UPUZI MTUPU!!!!
Mtanzania,
tmajaliwa@yahoo.com
Ha-haaaa, jina la Matty limeingiliwa kirusi…..Mattylda, inabidi uli-scan. Edwin..karibu na upunguze kupiga Arua!!. Mr.degree, Ross na Simon Kitururu……Mkumbuke kuwa Nyerere alikuwa ni binadamu, na km binadamu hawezi kuwa 100% safi mapungufu lazima yawepo. Sasa ubora wa mtu huwa unapimwa kwenye mizani ya mazuri na mabaya, na hamna atakeyebisha kuwa scale ya mazuri ya Mwalimu iko juu kuliko mapungufu aliyokuwa nayo labda awe chizi. Alikuwa na nafasi ya kujilimbikizia mali lakini hakujilimbikizia mali.
Tukivokuwa High school tulishawahi kumtembelea mwalimu Butiama mwaka 1997 (tulikuwa pia na Edwin Ndaki)na tulienda naye shambani kwake kuvuna viazi na mihogo ya kula wanafunzi tukajaza lorry. kwa kifupi alikuwa na Gari tatu tu kwake, Nissan patrol alilopewa zawadi na ccm baada ya kung’atuka, isuzu canter ndogo ya kubebea mazao shambani na ki-landrover chake cha enzi zile za uhuru ambako huendea shambani kila jioni. Hapo hapo tukamkuta mwanae Makongoro na Rose wamechafuka kweli wametoka kulisha kuku wanaowafuga. Ilikuwa vigumu kuamini maana hawa walitakiw wawe wanakula “bata” somewhere. Naona vitoto vinavopiga kelele hapa…(ROss & Mr. Degree) they dont know shit…yawezekana vilikuwa nursary sikuli enzi hizo….lakini ni haki yenu kuosha vinywa.
Mr Degree
Nakuelewa sana una chosema, .Watanzania wengi walikua brain washed na kudhani Nyerere alikwua kama Mungu, mbaka kuna watu walisema wanataka atajwe kama Mtakatifu.
Nyerere alikua mlinzi wa ma terrorists (wapigania uhuru) kuanzia huko kusini mwa Africa na walio pigania kurudishwa kwa Obote,Iddi Amin alichokozwa na ye alijilinda na ndio Vita ya kagera, ila tulidanganya kuwa Nduli ndio alituvamia.
Nyerere alijilinda na kuhakikisha ana tutisha wa Tz kiasi tusiweze kufikiri na kutaka kujua haki, na ndio mana alihakikisha kiswahili kinatumika ilitusijue nini kinaendelea nje ya TZ, tusijue uhuru una maana gani.
Hotuba zake sioni cha maana alicho sema zaidi ya kutisha watu kwa misimamo yake yeye aliyo kua anaamini ili kujilinda, alizungumzia sana kuhusu kuweka watu ndani , ili watz wengi watishike, na hakuwa simple kama watu wanavyodhani.
Sokoine alijaribu, ila naye asitudanganye Mtoto wake alikwua Nje ya Nchi masomoni siku ana fariki , kwanini asome nje wakati yeye ni simple ana suruali mbili na Safari boot moja, sababu ya kubana matumizi?
blackmannen # 34 umeshusha ki-swedish nini.. umenikumbusha ze comedy mpoki alivosema huu mziki mnene ni wa kiswideni.. haha
kweli nimeamini bongo tunaoshwa vinywa.. we ross nani kasema watu walitaka nyerere awe mtakatifu jamani! mbona nimecheka..LOL..i appreciate the guy’s hardwork big time..ila mambo mengine ni kuvuka mpaka. NYERERE R.I.P, we still wish you were around to guide these young guys in the game,maana ni vijizi ajabu.. havimuogopi hata Mungu.
matty = mattylda? jamanii na mimi itabidi nitafute ‘a.k.a’
@Blackmannen #34: Ni mimi. Kumbe we Mswidi?
Ross na Mr.degree,
Ni vigumu kuwabishia mnavyoamini kwa sababu hiyo ni imani yenu.Mimi mtu akishaanza na kuamini huwa namwacha aendelee na imani yake.Leo hii ukimwambia mtu aliyesoma marekani atamke herufi “Z” atasema “Zii” wakati aliyesomea Tanzania atatamka “Zedi” na kila mmoja anaamini yuko sahihi kuliko mwenzake.
So imani yenu na mtazamo wenu kwa Nyerere naomba niuache ili muendelee nao,
Ila kabla sijawaacha naomba mfahamu kuwa nchi zote duniai huwa zinaongozwa kutokana na mabadiliko ya kisiasa ama matakwa ya kisiasa duniani.Mtu serious huwezi kutoa mfano wa TV katika issue ya kuliendesha Taifa.Dunia inakua na inaendelea,ila ni lini tuta-copy hiyo situation ya maendeleo ndo suala la kujadili.Naamini leo mtu kama marehem sokoine afufuke akute Internet anaweza kusema sasa dunia watu wameamua kuwa wachawi,lakini je Taifa kama taifa linajiandaa vipi na maendeleo kama hayo???
Wakati Tanganyika inapata uhuru ilikuwa ni ama uchaguwe kuwa Mjamaa au mbepari japo kuna wengine kama Zambia waliamua kuwa ma-Humanism.Hivyo basi watu makini tulikuwa tunampima rais Makini kwa kuchagua kati ya hayo mawili na jinsi anavyojisimamia kutetea uamuzi wake.Nyerere aliweza kusimamia na kutetea uamuzi wake.Sitaki kuelezea habari za vita baridi kwani inafahamika SANA.
Vita ya Tanzania na Uganda naomba jaribuni kupitia foreign Policy yetu inasemaje na tujaribu kuwa critical kidogo kuliko kuishia na story za kwenye vijiwe vya kahawa.Nafikiri kuna hatari tunajadili mambo ambayo yako beyond our knowledge.
Ross,naona unajaribu ama unamuona Sokoine alikuwa Bora kuliko Nyerere.Ni sawa ni mtazamo wako.Wakati huo huo unaliona suala la yeye kumsomesha mtoto wake huko nje ya nchi kama moja ya failures zake.Ni sawa ni mtazamo wako,lakini wakati huo huo unasahau kuwa hata mimi MAJITA mtoto wangu anasoma nje ya nchi japo mimi ni mvuvi hapa kijijini kwangu.Sasa hapo nashindwa kupata pointi yako ni ipi hasa.
Sokoine alikufa zamani saaana.Lakini hadi hivi ninavyoandika mtoto wake yuko Marekani na anafanya vizuri katika mambo yake,(samahani bwn Sokoine kukuandika hapa) sasa sioni kama ni kosa kwa sokoine kukaa hapa marekani na kufanya kazi kisa anaitwa Sokine.Je ni watanzania wangapi wako nje ya nchi na baba zao siyo Marais ama mawaziri???Mbona Hashimu Mcheza kikapu anasoma MAREKANI????Mbona huyu Nanii siuji nani yuko Marekani na Urusi kwa ufadhiri wa Serikali.
Swali Je,ni mtoto yupi wa Nyerere anaekaa Marekani ama Urusi ama huko unakopaita wewe nje ya Nchi???Kwani alishindwa nini.Mnaambiwa walikuwa wanalisha kuku huko butiama.Mbona mtoto wa Kikwete sijui Ridhiwani leo tuu kesha kuwa jina kuuuuubwa huko CCM.Acheni masikhara bwana.
mimi nakuhakikishia mimi ni mvuvi na mtoto wangu kamwe hatosoma Tanzania.Nina sababu.Lakini siyo Rais wala ukoo wangu wote hakuna hata Katibu tarafa.Mimi nafukuzana na kina ROSS tu mitoni wakati wa kuoga.
ananishangaza sana huyo gervas hapo juu anayedai kufahamu mali za mwalimu nyerere,msome vizuri Ross hapo juu comment 38 wewe ni mmoja ya walio wengi waliokuwa brain washed,hata kama unatuzid umri bt kwa mtazamo wako tunakuzid uwezo wa kufikiri.we endelea kuamini tu kuwa mwalimu alikua masikini na watoto wake ni masikini.
Gervas hahahahaha nitaliscan lisi4jiwe tena lol! binti-mzuri, sijajipa a.k.a,by the way kuna mrembo matty mpya kaingia hapa so nikaamua kujitofautisha nae haitoshi kanifata tena so nimeamua kutumia ma full name kama vp aje na hapa pia,anyway ukitaka na ww kubadili jina ni uamuzi wako bibie! Gervas ni kweli kabisa ulichosema,me too niliona madaraka anahojiwa na station moja ya tv ktk kumbukumbu ya mwalimu last yr jamani anasema dingi alikuwa soo hata kwenda nje ya nchi aliwanyima wanae so madaraka went out by panya road mkatae mkubali kiongozi gani wa sasa atafanya hivyo?the reason hapa ni kuwa Nyerere alitaka watoto wake wawe katika the same class na watoto wa wakulima,kwa mfano tu kama hao watoto wake wangekuwa wamepatiwa maisha ya kifisadi leo hii si wangekuwa mafisadi tu!ROSS MTOTO WA MASAKI UPO??
mattylda hapa kuna uvamizi shosti,yaani wamevamia na kukuchukulia jina lako!!!!!!????? pole dada,usijali mimi nakutambua.
mr. degree…unaniambia nimwelewe ROss kwani yeye ni nani? Hizi story mnazozishusha hapa mnazipata kutoka source gani? vijiweni? au magazeti ya udaku?….. mimi nimeongelea personal experience yangu ya maisha ya Nyerere. naona napoteza muda wangu tu apa !! Majita, Mattylda… waacheni vijana waoshe vinywa.
Mie nasali kuwa hii shughuli aliyoianzisha JK kweli iwe shughuli kwelikweli…isiishie kuwa changa la mcho…..ngoma ya kitoto…((labda kamchezo ka kutafutia KURA kwenye uchaguzi ujao….)) kweli watu wawajibishwe na sheria ichukue MKONDO WAKE……hivi tutawaeleza nini kizazi kijacho kama mambo ni holelea kiasi hiki…?????
Inauma saana.
Nikiona picha ya MWALIMU huwa natokwa na machozi mno. Huenda Mwalimu anageuka huko aliko pindi huu UCHAFU unavyoendelea kufanyika….na kufanywa na watu ambao wakati akiwa hai aliwaona kuwa ni watu wa kufaa……pesa za nchi kuchukuliwa na watu wasio na huruma kwa WATANZANIA wasio na hata senti za kununulia a single pain killer tablet…..
Unajiuliza hivi pesa zote hizo wanafanyia nini??….hata kama wakizikwa nazo hukoo kaburini…zitawasemesha ama ni aje….
People should start THINKING BIG……acheni upumbafu…….ACHENI WIZI…..tunawapa KURA ILI mtusaidie kuongoza nchi…..sio KUIBA…..
MUNGU IBARIKI TANZANIA
ok pearl tuko pamoja shost!
Bwana Kitururu, comment # 41, mimi sio Mswidi, ila nakifahamu Kiswidi na nilisoma Profile yako uliyokuwa umeiandika kwa lugha ya Kiswedish, nilikudhani wewe ndiye Mswidi.
Binti-Mzuri, comment # 39. Mimi naongea lugha zaidi ya 5, Kiswedish kikiwa moja ya lugha hizo. Mimi ni msafiri sana katika dunia yetu hii, usishangae siku moja, nikija kukugongea mlangoni kwako huko uliko.
Mtu yeyote, anayeniletea unyambilisi, kumweka mikononi mwangu sio kazi kubwa. Binti-Mzuri na Simon Kitururu, na wengine, hamjanikwaza, nitafurahi kuonana nanyi wote.
This Is Black=Blackmannen
Hv Pearl ile email yako mbona inabounce??nitumie ipi kukupata?
misifa mingine bwana sasa tafikiria umeulizwa unaongea lugha ngapi hapo utakuta lugha yako yenyewe ya kitanzania inakupiga chenga unakazania lugha za wenyewe
mattylda shosti tumia email hii pearl.sam40@yahoo.com
thanks Pearl, noted!
“Pearl”, mambo yanaenda vipi na ndugu yangu “Majita?”. Au sasa wewe ni tayari wewe ni shemeji yangu? Au Mkuu Majita, bado anaendelea na shemeji “Nasreem?
OOOho, This Is Him, I know, I mean, Black=Blackmannen
Nyerere was a nice guy but wasnt perfect. Nikikumbuka yanga na sabuni ya unga na colgate na imperial leather ilikuwa inauzwa kimachale, haipatikani, yaani hivo havikuwa necessities, nachoka sana. RIP baba, isingewezekana uweze vyote.
kama baba wa taifa angekuwepo nadhani hawa viongozi haramu katika nchi yetu wangenyongwa tu bila shaka?pumbuzika kwa amani baba wa taifa you will be missed.
nyie wote mmelala hakuna rais au kiongozi sio mwizi hata nchi tajiri duniani viongozi wao wamejilimbizia mimali toka kwa wanyonge kwani mapadri hawadhini? haya tuzowee tu ni pote ulimwenguni