Mwaka 2008 upo mbioni kuelekea ukingoni mwake.Zimebaki wiki kadhaa tu kabla hatujaona zile fataki hewani na kusikia ving’ora vikitusindikiza kuumalizia mwaka.Kwa vyovyote vile mwaka 2008 utaenda na historia kadhaa zenyewe kuvutia kwa wengine na kutia simanzi kwa wengine.Ndio maisha.Ni mwaka ambao hakuna atakayeweza kamwe kusahau kwamba mtu mweusi wa kwanza amechaguliwa kuliongoza taifa kubwa la Marekani.
Lakini nchini kwetu pia ni mwaka ambao tunaweza kusema tumeshuhudia mengi ambayo siku za nyuma yalionekana kuwa hayawezekani.Tumeona viongozi kadhaa wakijiuzulu nyadhifa zao.Tumeshuhudia wengine wakipandishwa kwenye karandiga.Tumeona wazee wengine wakipandwa na pressure kwa sababu wanajua walishaharibu na hawana uhakika na kesho.Nadhani tunakubaliana kabisa kwamba miaka kadhaa ya nyuma,ilikuwa ni kama ndoto kusikia kiongozi akitangaza kujiuzulu.Mifano ya waliowahi kujiuzulu ilikuwa ni michache sana.
Najua kuna ambao mnasema yote hii ni “changa la macho” na kwamba kinachofanyika ni mchezo wa aina yake wenye wingu zito la kisiasa.Inawezekana kabisa(hakuna lisilowezekana katika dunia hii).Lakini pamoja na yote hayo,tofauti na siku za nyuma,hata kile kitendo tu cha kuwaona waheshimiwa wakitokwa na jasho kwa sababu hawamo ndani ya yale “mashangingi” yao na badala yake wamekalia yale yale mabenchi ambayo hawakuwahi kuona umuhimu wa kuyakarabati kwa sababu “hayakuwahusu” na huku wakiwa wameegemea zile kuta ambazo hela yake ya rangi waliipeleka kusipotakiwa,ni vitu ambavyo vinaufanya mwaka 2008 uwe na lake katika historia.Bado tunasubiri kuona jinsi “changa la macho” litakavyopelekwa.Tupo na tunatizama kwa makini.Anayedhani tumelala anajidanganya.
Ni wikiendi tena.Ni wakati wa kujikumbusha zile tulizowahi kuzipenda kama ilivyo jadi yetu hapa BC.Kwa sababu wiki hii tumeshuhudia kiasi kuhusu niliyoyaongelea hapo juu,basi sio vibaya kama tukiwakumbuka Nguza Viking na mwanae Papii Kocha ambao wapo gerezani ambako ndiko tunapotarajia “waheshimiwa” watakuwa wamehifadhiwa.Wimbo unaitwa Seya.Pata burudani,wikiendi njema.
Feedback / Comments
43 Responses to “SEYA-NGUZA VIKING”
Leave a Reply


sending...
Nawatakia siku njema..
Mapumziko mazuri ya mwisho wa juma.
Kubwa ya yote na ungana na wazalendo wezangu wooote kuwaombea Mwenyezi Mungu awafariji na kuwatia moyo ndugu jamaa na marafiki waliopoteza maisha yao kwenye ajali iliyotokea Singida.
May God rest thier soul in peace.AMINA
Wananchi wengi mara nyingi wamekuwa hawana imani na Mahakimu wetu, kutokana na vitendo vya rushwa vinavyofanyika kila kukicha, hasa katika Mahakama zetu za chini. Lakini sio kila Hakimu anapokea rushwa, wapo pia waadilifu.
Mahakimu wetu wa Mahakama za chini, nionavyo mimi ni kwamba, mbali ya kuweka “mshiko” mbele pia, hawana ELIMU ya kutosha katika kusimamia na kutoa haki kisheria.
Sheria za KUUA na KUBAKA, ni sheria kali sana na adhabu zake ni kali. Lakini kunautofauti mkubwa wa adhabu zitolewazo na Mahakama za chini, na zile Mahakama za juu. Mahakama za chini hazina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji, na badala yake, kesi hupelekwa Mahakama za juu.
Adhabu zitolewazo na Mahakama za juu, mara nyingi zimewaridhisha wananchi, kwani wahalifu hufungwa katika kiwango tofauti kutokana na hali halisi ya tukio lilivyokuwa. Wahalifu hufungwa maisha na wachache hupata adhabu ya kunyongwa.
Kesi za kubaka husikilizwa na Mahakama za chini, na kama ambavyo tumeshuhudia, adhabu yake mara zote tunaona wahalifu wanafungwa kifungo cha miaka 30 au kufungwa maisha. Je, kwani katika kesi za kubaka hazina utofauti wa kimazingira zinavyotokea, kiasi cha kumfanya mhalifu akaonekana kwamba hakudhamiria kufanya kosa hilo? Je, adhabu yake ni hizo mbili tu?
Kutokana na hali za namna hiyo, watu wanakuwa hawana imani na mahakama za chini, maana adhabu ya kuua na ya kubaka, adhabu zake zinatofautiana sana. Pia ukiongezea kuwa kesi za kubaka huendeshwa huku milango imefungwa, watu sio rahisi kuzichambua , ni nani anakuwa haki, na nani kaonewa.
Watu wengi wanajiuliza, ni kweli Nguza Viking na wanaye, walitendewa haki kufungwa maisha? Katika hali kama nilivyosema hapo juu, hatuna hakika kama ni kweli walitenda kosa 100%, iliyobaki ni kumwachia Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye aliyekuwa na haki kati ya “Washitaki na Washitakiwa”. Mimi namwachia “Mkuu Majita” atusaidie kutuchambulia zaidi kisheria katika hili.
Binti-Mzuri umeadimika, Mattylda jina zuri kuliko la zamani, Gervas kacharuka kwa maoni siku mbili hizi, Pearl, halima, Chapombe, Tommy, any, Edwin Ndaki, mpoooo????????
It’s Great To Be Black…………..Blackmannen
Ohhh jamani i wish hawa watu wangepewa hata msamaha wa rais mweee the way nawa admire ni siri yangu!
Nakumbuka kibao cha seya wanipalllll seya seyaaaa, vaa vizuri mpenzi wangu upendezeeee, vaa vizuri mpenzi tutoke leo, uwiiiiiiiiiii jamani Binti mzuri uwapi shosti na halima tupokezane hilo song mhhhh, watu na talent zao, anyway sina la kuongeza!
Ni kweli kama BC ulivyosema huu mwaka una mengi sana kwetu Tz, lililonipa moyo ni la hao wahesh.kupanda karandinga maana washazoea viyoyozi so kule ni mwendo wa kujisaidia kwenye debe, kuna mtu alisema waheshimiwa eti wanaspecial care kule sasa sijui ni kweli au laa!!!!!maana daaa natamani kama wangewekwa kunako mbu wengi na maji kibao na ule uchafu mzito kwa pamoja ili waonje joto la jiwe hata kama watatoka BUT, wawe na special memory!
wknd njema wote jamani pamoja na wewe matty mpya, ingia kwa step anga zaku sawa???
thanks Blackmannen, thats ma real name!
thanks Blackmannen, thats ma full name!
Tanzania ni nchi ya kuonea wanyonge kama akina babu Seya na watoto wake. Mimi naamini kwamba hawakustahili hukumu waliyopewa. Sababu inayonifanya niseme hivyo ni kwamba hata kama ni kweli walifanya vitendo hivyo vya uhalifu wangeadhibiwa tofauti, huyo mtoto wa miaka kumi na saba hakustahili kufungwa kifungo cha maisha.
Viongozi wanaoiangaminza nchi kwa kujinenepesha na pesa za wananchi bado wanatembea huru na wanaendelea kushikilia madaraka. Habari niliyoisoma sasa hivi kwa Mjengwa ni kwamba Yona na Mramba wameachiwa huru! Je kweli kuna matumaini ya nchi yetu kuwa na maendeleo?
Hata mimi nakiri Mattylda jina lako limekuwa zuri kuliko zamani. Kumbe ndo maana huwa unaongea pointi!!!
Mimi mpaka sasa siamini kama baba na watoto wanaweza kuwa wote wabakaji. Mahakama naona ilichunguze hili suala kindani zaidi
masikini babu seya jamani inatia uchungu ili tuzidi kuwaombea kwa mungu..nikweli kabisa mahakama ichunguze maana duh!
KWAKO NDG BLACKMANNEN # 2 hapo juu.
Kwanza kabisa napenda kukiri mbele ya wana BC kuwa mimi ni mpenzi SANA wa miziki ya Nguza na Papii Kocha.Pili ndg yangu Blackmannen nikushukuru kunilenga kujibu hoja zako hizo hapo juu japo SIJUI sheria sambamba na wadau wengine hapa uwanjani na naamini wapo wanaozijua zaidi yangu sheria hizi nao watakuja kutoa maoni yao na TUTAYACHAMBUA kama kawa..
Kesi ya Nguza kwa mtazamo wangu haina shida hata kidogo hadi tuhoji kama ni kweli walistahili kushinda au kushindwa. Shida ipo hapo kwenye je,walistahili adhabu kubwa kiasi hicho????Labda nikumbushe kuwa kesi hiyo mashahidi wengi walikuwa watoto chini ya miaka 10.NAPATA SHIDA KUAMINI KUWA ETI WAKILI WA NGUZA ALISHINDWA KUWAKAMATISHA WATOTO HAO (wasiojua kitu) na kujua ukweli kama kweli walifundishwa kusema uongo (kama ilivyokuja kusikika mitaani eti watoto walikochiwa kusema hivyo).Kama kuna wakili alishindwa hata reveal ukweli toka kwa mtoto wa miaka 7 au 8 au 10 basi napendekeza TUMNYANG’ANYE hicho kibali cha uwakili na arudi shule.Naamini hata ROSS akipewa kumhoji mtoto wa miaka 10 aliyefundishwa kusema uongo atamkamatisha na mtoto huyo itafikia pahali ataongea ukweli waziwazi,ijekuwa wakili??tena mahakamani?????
Hapana hilo tuliache.Wakati huo pia fikiria angekuwa mtoto wako au mdogo wako wa umri huo ukisikia amebakwa na MAJITA utamfanya nini majita wa watu.Afadhali ubake mtoto wangu wa miaka 16 lakini wa miaka 7 walah nakukata makende yako.
Mkuu Blackmannen,
Kesi ya KUBAKA na MAUAJI ni tofauti sana japo adhabu zake kidooogo zinafanana.
Kesi ya kubaka imejikita sana kwenye Maadili wakati ya Mauaji imejikita kwenye uharifu.Hizi kesi kimsingi ni ngumu na zinahitaji utulivu sana.Lakini makosa yote hayo kubaka na mauaji ili yawe makosa lazima kuna ELEMENTS zake zinazo verify makosa hayo.Lakini kubwa zaidi ni kuwa ili kosa ma kuua liwe kosa na mtuhumiwa hatiwe hatiani LAZIMA TUANGALIE INTENTION YA MTUHUMIWA wakati wa kutenda kosa hilo la kuua.Yaani je,huyo mtuhumiwa ali-intend kuua wakati wa tukio hilo????hapo ndo tutapata jibu la ndio au hapana vinginevyo tutaita KUUA BILA KUKUSUDIA (manslaughter) ambapo mtu atafungwa si zaidi ya miaka 3 au mtuhumiwa tutamwachia huru.
kuna kesi 2 nilizisoma wakati nahudhulia masomo yangu ya MEMKWA hapa kijijini kwangu Majita nitazitoa hapa ili ujue namaanisha nini juu ya kuangalia INTENTION ya mtuhumiwa.
1:
Kuna dreva wa daladala (hiace) alikuwa naendesha gari lake kila siku huku likiwa halina breki.Kutokana na uzoefu wake alikuwa anatumia gia kubwa ama mbinu zingine kusimamisha gari.Na alifanya hivyo kila siku zaidi ya miezi kadhaa.Siku moja bila kutarajia wakati anataka kusimama gari halikusimama na akasababisha vifo vya abiria wote.Kama kawaida akashitakiwa kwa kosa la mauaji na baada ya uchunguzi wa polisi ikaonekana zaidi kuwa gari lake hilo halikuwa na breki siku nyingi tu kitu kilichosabababisha ajali hiyo na mauaji.LAKINI BAADA YA UTETEZI JAJI ALIMWACHIA MTUHUMIWA HUYO na badala yake akashitakiwa kwa traffic case ambapo alilipa faini ya sh.elfu 25.
Nadhani nimeeleweka.Hapa nina maana kuwa dreva intention yake ilikuwa kufanya biashara na si kuua.Isitoshe amekuwa akiendesha bila breki kwa siku nyingi tu.Kwa nini hakuua jana yake?Utaona kuwa hapo kosa ni dreva kuendesha gari lisilokuwa na breki ambalo ni kosa la makosa ya usalama barabarani.
2:
kuna mkulima mmoja (siyo majita lakini) alikuwa ameivisha karanga zake huko shambani kwake.Lakini kuna wanyama walikuwa wanamsumbua sana kwa kuzila na kuziharibu kabla hazijakomaa huko shambani kwake,hivyo akaamua kuwa anazilinda kama ilivyokuwa kawaida hapo kijijini.Basi akiwa lindoni kwake huko shambani usiku tena kukiwa na mbalamwezi,aliona kama kuna kitu shambani kwake,akapiga kelele weweee wewewee lakini hicho kitu kikawa kinainuka na kupotea basi huyo mkulima akajua ni mnyama mwaribifu hivyo akatupa mkuki.Ile kutupa mkuki akasikia kelele “mamaaa nakufa” kumbe ilikuwa ni jamaa mmoja alikuwa anafanya mapenzi na dada mmoja hivi.so huyo mkulima akawa ameua huyo jamaa kwa ule mkuki na akawa ameshitakiwa kwa mauaji lakini baada ya utetezi huyo mkulima aliachiwa huru na jaji kwani hakuwa na kosa katika grounds kuwa INTETION yake haikuwa kuua.so nahisi umeelewa.
Nilikirudi upande wa Intention kwenye kubaka “kamwe bila ku-intend kubaka huwezi kubaka”Kwa sisi wanaume bila Intention ya kufanya mapenzi huyo jamaa hawezi ku-erect kwa hiyo tunaamini kuwa kila anaebaka huwa ana maanisha kubaka ILA PIA HUWA TUNAZINGATIA ELEMENTS ZA KUBAKA kama nilivyoelezea kule kwenye thread ya Juma Nature.
Ni kweli kuwa mahakama za mwanzo mara nyingi HAKI na taratibu za kimahakama huwa zinakosewa,lakini mahakama kuanzia ya Wilaya ni tofauti sana.Hapo taratibu na HAKI huwa zinaangaliwa SANA achilia mbali makosa madogo ya kibinadamu as rushwa na mambo mengine.
Si kweli kuwa kesi za kubaka kuwa wanafunga milango bali huwa inatokea wakati wa Cross Examination na wakati ambapo mahakama itaona kuwa kuna haja ya kuficha mambo fulani fulani hasa ukizingatia maadili ya kitanzania.Utajisikiaje hata kama wewe ni mshitakiwa na sasa mlalamikaji anataka kuelezea uume wako as kuthibitisha kama ulimbaka???hope hapo lazima tutafunga milango..
Zaidi nakaribisha majadiliano na niko tayari kuandika zaidi,nawahi kuchunga ng’ombe zangu ila siendi kulinda shamba langu japo linaliwa na wanyama najua nitamkuta ROSS anafanya vitu vyake na Mdegedege.hahahahahah
Ndaki eeeh!!
Siku zingine ukienda ka likizo kadogo uwe unaaga.
Ona sasa umechelewa hapa kijijini kwetu hadi matty kaamua kubadilisha jina na kuwa mattlda.Pole Matty wetu.Anyway tutafika tuu hata kama Majita nayo itachukuliwa na mwingine.Mimi wakichukua majita najiita majita wa Bush najua hapo hakuna mtoto wa kishua aka masaki atakae lipenda jina hilo.
Hivi unamjua ROSS wewe??? Shauri yako.hahahahaha.Aidha wadau wenzangu nawatakia weekend njema.Blackmannen kama sijakujibu swali lako hapo juu mkuu unaweza kuuliza tena.Ila nimependa ulivyouliza swali kwa hoja kali kali.Bravo kaka
asante kamanzi wknd njema!
jamani mimi huwa siamini kama baba/wana wote kwa pamoja walibaka mhhh kiini macho.
Mungu awalinde huko jail!
Pamoja na matokeo yanayozidi kujitokeza kuelekea mwisho wa mwaka huu kama vile Amerika kuwa na rais wa kwanza mwenye asili ya kiafrika, waliokuwa “Nusu Miungu” (Mawaziri)wa BONGO kufikishwa mahakamani na hata kulazwa keko,, sasa tufanyeni kampeni ya nguvu kwenye vyombo vya habari na hata barabarani ikibidi ili rais JK awaachie huru NGUZA NA WANAE ambao wamefungwa maisha kwa kosa ambalo naamini asilimia 90 (90%) ya Wabongo hatulielewi kiufasaha.
Jamani tusongeni mbele na tuzidi kuamuka, hawa wanaotuhumiwa kuhujumu uchumi wa BONGO 99% walikuwa ni vijana watendaji watiifu wa MWALIMU wakati huo, Je mnafikiri wamekuwa wakiyafanya haya leo tu au hata wakati ule ambapo mlikuwa hamuwezi kumzungumzia muungu mtu?
Wake up it was happening then but you were not allowed to say anything or if you did, you could have been kept somewhere for a keep. Wabongo hamsomi na mkisoma hamuelewa je bado mnasoma kupass mitihani?
i’ve ALWAYS said in this blog kwamba as much as i like the song seya, i still think he should perish under the sun. I know kuna mada zingi zimeibuka over years,some saying kamuibia fisadi mkewe,mara kasetiwa na serikali n blah blah blah. wat i dont understand is, why would 10-12 parents allow their children who are all under 10,to endure such torture if this whole thing is a setup. I DO NOT BELIEVE, hata kama mzazi ana njaa gani,kuamua kumdhalilisha mtoto kwa kiasi hicho.. watu wengi hawakubalianagi na mimi..but mi naona kwakweli seya alibaka. na kama majita alivosema, mtoto aliekochiwa,lazima tu ukweli ungemtoka at some point. njia ya mwongo fupi. mkubwa mwenyewe ukimpiga gia mbili tatu,its very easy kumkamata. na kama majita alivosema, advocate mwenye vishahada,kweli utashindwa kuobtain the truth. my belief is,this man bakad the children..kama ilikua ridhaa yake, kama masharti ya mganga, whatever the case..NIGA ROT IN JAIL. You people love the songs,and miss seeing him performin sijui mango garden,sijui diamond jubilee..fair enough..but what you guys fail to see.. IS THE TRAUMA THAT THOSE CHILDREN HAVE TO LIVE WITH FOR THE REST OF THEIR LIFE. the fact that their virginities were robbed, their security, their clean ness, their trust.. i hope serikali iliwalipia watoto kuona psychologist,because i have a cousin sister who got raped..and everytime i look at her life,i wanna cry..SHES NEVER BEEN THE SAME PERSON. nguza viking i hate u so much ryt now!.. ukitoka jela,ntakuchoma moto mimi na tairi langu mwenyewe mbakaji mkubwa we! LOH.. sura mbayaa
sasa mnaosema kasetiwa,how do u explain those children missing kwenye vipindi kadha wa kadha wakiwa pale shule ya msingi mapambano. ujue msidhani kesi hii imekwenda tu nyap nyap… kulikua na ushahidi wa kutosha. ushahidi umeanzia kwa mwalimu aliewekwa ndani aliekua anawatoa watoto.even tho huyo mwalimu katolewa coz ilikuja thibitika ‘eti’ alikua hajui watoto wanafanyiwa mchezo mbaya. babu seya ivi kweli ulishindwa hata kwenda pale kwa macheni jamani,kujizolea zobazoba mmalizane mpaka uwachukue watoto wa wenzio!au ulikua unatafuta vi-virgins!?mchawi nini wewe? zaa vitoto vingine,tutume makomando yoso wakubakie na wewe ndo uone utamu wa mboga.. u sick peadophile!i hate u so much ryt now!..nasikia katoto kamoja kalisema ‘ babu seya alikua anasema tulambe pipi,afu pipi itatoka uji’!… MZAZI KAMKOACH MTOTO ASEME IVO? people wake up and hear the song here..dance to the rhythym!.. NGUZA VIKING YOU SHALL PERISH! naskia ushakonda huko jela,na bado!..debe utanyea sana tu..wapambe msisahau kumpelekea machungwa na mananasi kidogo.
i was here!
‘sasa tufanyeni kampeni ya nguvu kwenye vyombo vya habari na hata barabarani ikibidi ili rais JK awaachie huru NGUZA NA WANAE ambao wamefungwa maisha kwa kosa ambalo naamini asilimia 90 (90%) ya Wabongo hatulielewi kiufasaha.’
kalikanje are u kiddin me? yani we baada ya kuandamana mafisadi yafungwe, au bajeti ziwe za msingi..unataka kumuandamania nguza,afu u stil have guts to say ‘ Wabongo hamsomi na mkisoma hamuelewa je bado mnasoma kupass mitihani?’ we kalikanje rafiki angu,apo umejipiga dongo mwenyewe.. ujue kusoma na kupata degree doesnt guarantee you kwamba you have a broad mind.. ushauri wa bure,kaa chini na kufikiri before you come out with ur facts, hayo maandamano utaenda we peke ako..wenzio wapo wanatafuta solutions za uchumi,sio kuwapigia debe wabakaji watolewe.. while ur at it,unaweza mtumia protein drinks aboost health yake. na hiyo asilimia 90% ya watanzania ambao hawaelewi kosa lake, HAMUELEWI KOSA LA MBAKAJI.. aisee mi sometimes mpaka nafikiria bora nifie kwa wazungu! hii nchi bwana.. tutafika tu lakini.. mwaka 2035. ask urselves, why mada ya nguza was never raised as an issue,kwenye vyombo vya habari,au well-known talk shows like hamza kassongo and jenerali ulimwengu… watu wa mtaani na wa kwenye blog ndio wanayayapa about these issues..because we fully dont do our homeworks.
KAMA WAMESINGINGIZIWA/SETIWA, POLE SAAAAAAAAAAANA, VINGINEVYO, NIKUVUNA ULICHOPANDA! SIHURUMII WABAKAJI, I GOT KIDS MEN, CANT IMAGINE MWANANGU AKITENDWA NITAKUWA NA HURUMA NA MTUHUMIWA!
WEWE HAKIMU MAJITA PAMOJA NA HOJA ZAKO PENGINE KUWA SAHIHI, LAKINI HUJUWI MAZINGARA YA KESI YA AKINA BABU SEYA WAO HAWAKUKAMATWA READY HANDED WAKIBAKA KESI ILIKUJA BAADA YA MIEZI MINGI KUPITA, NI HIVYO MMOJA WA WATOTO ALIKUTWA NA BABA YAKE AKIWA NAPESA KAMA SIKOSEI NI SHS 100. ALIPOULIZWA AMEIPATA WAPI AKASEMA AMEPEWA NA BABU SEYA, NDIPO BABA ALIPOCHACHAMA NA KUANZA KUMPIGA MTOTO NA KUMUULIZA ALIKUWA WEWE KAMA NANI KWAKI NDO AKASEMA ANAMBAKAGA, NA MMOJA WA WALIMU WAO NDIYE ANAMFANYIA CONNECTION BABU SEYA YA WATOTO WA KUBAKA. CHA AJABU MWALIMU ALIACHIWA HURU NA HAWA KUFUNGWA MILELE, WALA HAKUKUWA NA USHAHIDI WA KUBAKA KWA VILE KAMA NI KITENDO CHA KWELI KILIPITA MIEZI KADHAA ALIYOPITA. NA CHA AJABU WEEK HIYO HIYO BWANA MMOJA HUKO MBEZI BEACH ALIMBAKA MTOTO NA YULE BINTI ALIRUDI NYUMBANI HUKU AKITEMBEA KWA KUTANUA MIGUGU KWA MAUMIVU MAMA YAKE ALIPOMUULIZA ALISEMA AMEBAKWA NA JAMAA FULANI SAA HIZO HIZO, KILICHOTAKIWA HAPO NI KUMPELEKA HOSPITALI KUMPIMA KUPATA UCHAFU MBEGU ZA KIUUME ZILIZOINGIZWA NA JAMAA NA KUPATA DNA ZA KULINGANISHA NA ZA YULE JAMAA NA KUWA USHAHIDI NA KUMPATIA ADHABU YAKE LAKINI HILO HALIKUFANYIKA NA WALA KESI HAIKUFIKA POPOTE NA ALIACHIWA HURU, SASA IWEJE SEYA AFUNGWE MILELE KWA KITU KILICHOPITA MIEZI KADHAA KAMA NI KWELI KILITOKEA NA HAKUKUWA NA USHAHIDI WA MOJA KWA MOJA. KUNA HABARI BABU SEYA ALIKUWA ANAGOMBEA MWANAMKE NA KIGOGO WA SERIKALI MKUBWA NDIYE ALIYE-MFIX, TUOMBE KIKWETE AWASAMEHEE TU KIFUPI WAMEONEWA TU HILO HALINA UBISHI
Mkuu Majita,
Haki ya Mungu umenikosha kwa kila kitu. Ufafanuzi wako wa kesi umeniweka katika hali ya uelevu wa hali ya juu. Nashukuru sana kuwa na mtu kama wewe hapa BC. Maana, mimi itanipa hamu ya kuingia hapa kuchangia mambo mengi, ya maana na utani. Mimi mwenyewe napenda sana utani, lakini, tunapokuja katika swala muhimu, sina utani na hasa katika siasa za kuitetea nchi yangu Tanzania au Afrika, na viongozi wake, sina utani na mtu kwa hilo.
Ross ni “she-Male” wetu, analo, kwa kwa hali zote. Sasa tumezua joka letu lingine, la kufugwa “Mr Madegedege”. Iko kazi. Lakini tutafika tu, maana kipenzi chetu Mattylda sasa ana jina tamuuuuuuu!!!! Jina lake la kike, linalotutamanisha sisi ma-men, sio jina, kama nchi ninayokaa mimi, madume pia yanaitwa “Matty”. Duh!!! hata kama ulikuwa na hamu, basi hamu yote inakutoka, maana mimi sio wa vile. Mimi ni wa “Moja kwa Moja”. I mean “Straight”. Mattylda, tunakupenda, tena sasa tunakupenda zaidi ya zamani. Waambie pia Binti-Mzuri, Pearl, halima, any na wengine.
This Is Him……… I Mean, Black=Blackmannen
eti huyo mattlyda sijui matty comment 12, haamini kama mtu na watoto wake wanaweza kubaka? jee ukiambiwa kuna watanzania wanachuna ngozi wenzao na wengine wanaua albino wachanga utaamini? ndo shida ya watanzania vya kuamini hawaamini na visivyotakiwa kuaminiwa wao ndo wanaamini.hovyo kabisa !!
thanx Majita duu umefafanua vya kutosha,kumbe kichwa kimetulia hivyo,safi sana! Blackmannen mhh haya bwana yote heri! Wee Mr.degree huelewi nini sasa??pamoja na Majita kutufafanulia vyote hivyo bado tu??yes 4 ma opinion am not the first to say those words and still i cant blv this,issue ya kupikwa kama haikupikwa let them enjoy the jail!
It is true BC Staff. A lot of GREAT things happened universal wise this year. Kuanzia kwa President-elect Obama kuweza kupasua mawimbi na kuwa the 1st African-American being elected President of U.S.A. Pia on the presidential level, rais wa Pakistan Musharav kujiuzuru na pia Rais wa Afrika kusini Thabo Mbeki, kujiuzulu pia. Hii ni demokrasia ya kweli ulimwenguni.
Kwa upande wa Tanzania, mimi ninafurahi kuona Demokrasia inakuwa (japo taratibu) ktk nguzo tatu za utawala: Serikali, Mahakama na Bunge.
Kwanza, inapendeza kuona wabunge mashujaa, wameweza kuwa na sauti bungeni na kufichua uozo mwingi unaofanywa na MAFISADI madarakani. Mfano wa wabunge mashujaa ni, Mh. Zitto Kabwe, Mh. H. Mwakyembe, Mh. Dr. W. Slaa, Mh. A. Kilango. Just to mention the few. Nawapongeza sana wabunge mashujaa. Mnafanya kazi yenu kama inavyotakiwa. Zama za-ama kusinzia bungeni ua kuwa “YES SIR!”, zimepitwa na wakati.
-Pili, inapendeza kuona walau,Serikali (weather under pressure or not) ikijaribu kuitikia wito wa wananchi kuchunguza na kuwafikisha MAFISADI mahakamani ambao siku zote nia yao ni kujineemesha kwa kuihujumu nchi yetu changa, bila kujali maslahi ya taifa.
Natumaini mahakama itawatia hatiani MAFISADI wote na hatimaye kuwahukumu kwa kuwapa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia mbaya ya kufisadi taifa-“leo au kesho”. Kwa wale wanaodhani hili ni “changa la macho!”- tusubili tuone! Hata hivyo-days are numbered!
NB: Kuhusu Babu Seya, msimamo wangu mimi uko palepale. Kama kweli alifanya makosa aliyotuhumiwa nayo, basi adhabu hiyo ni sahihi kwake. Ila kama aliuziwa kesi(kesi ya kubambikiziwa) basi aliyemtendea hivyo ametenda ukatili mkubwa na awe tayari kujitetea mbale ya MWENYEZI MUNGU siku ya hukumu iwapo hatatubu hivi sasa.
Ndg LASWAI # 18,
Nashukuru kwa hoja zako.Ila napenda kukuakikishia kuwa MIMI SIYO HAKIMU na wala sijawahi kusomea uhakimu. Nitafurahi zaidi ukini-address kama mkulima-mvuvi wa samaki.Mimi ni mTZ mpenda haki na nafuatilia sana masuala kama hayo ili kujifunza haki za jamaa zangu waTZ.
Nashukuru umeliona hilo la mimi kutokujua mazingira ya kesi ya Babu Seya et al,ila nakuhakikishia namaamini naweza kuwa najua undani wa kesi ya Babu seya et al kuliko unavyoweza kuhisi.Haikuhitaji kujua sheria kujua ukweli wa tukio lile bali mtu yeyote mtanzania aliweza kujua kwa kina kilichofanyika kwani lililipotiwa SANA.LA MSINGI NI KUTOFAUTISHA STORY ZA KIJIWENI NA UKWELI HALISI WA TUKIO HILO.
Ndg Laswai,
Kesi ya kina Babu Seya haikuhitaji ushahidi wa ready handed kutokana na mazingira ya kesi ile.Zingatia kuwa matukio yale ya kuwabaka watoto wale hayakutokea siku Babu seya et al walipokamatwa.Ni vitendo walivyokuwa wanawafanyia watoto wale siku za nyuma,tena kwa siri kubwa na tahadhali ya hali ya juu.Pia zingatia kuwa victims wa kesi ile wengi ni watoto tena wadogo wa miaka chini ya 10 na kimsingi sheria,maadili na taratibU zoooote za kimahakama zinawalinda watoto wa umri huo kwa misingi kuwa watoto wale HAWAJUI WALITENDALO.
Sheria zipo kuwalinda na kuwatetea wanyonge na watoto ni ZAIDI ya wanyonge hao.
Kumbuka pia kuwa kesi ya kubaka/kudharirisha kama ile haiishii tu kupata ushahidi wa shahawa kwenye uke wa watoto wale,wala kupima DNA,wala kuwakuta na michubuko au kuchaniwa nguo zao.Kumbuka pia kuwa kuna watoto walitoa ushahidi kuwa walikuwa wanamnyonya babu Seya uume wake hadi anapizi.Sasa kama walikuwa wanamnyonya wewe bwana Laswai ukienda kumpima huyo mtoto shahawa ukeni kwake UTAZIKUTA??????????? Je ukipima michubuko ukeni kwao utaikuta??????Jamani tuwe makini kidogo.
Sina uhakika na kesi ya huyo unaemuelezea wa Mbezi kuwa alibakwa na kama unavyosema kuwa ilikuwa hearsay mimi kamwe siwezi kuongelea kitu cha kusikia tu.Zingatia pia kuwa hearsay siyo ushahidi mbele ya mahakama,so mimi hilo siliongelei.
Kuna habari kuwa Babu Seya alikuwa anagombania mwanamke na kigogo hiyo tena kwangu ni hearsay.Siwezi kuiongelea.Hata hivyo hakuna logic Babu seya agombanie MWANAMKE halafu kesi ya msingi ni kubaka vitoto.Yaani havihusiani kabisa.Ugomvi wa MWANAMKE vs KESI YA KUBAKA VITOTO!!!!????mmmmmh.Ingeweza ku-make sense kama ungesema Babu Seya alikuwa anagombania hivyo vitoto na huyo Kigogo ndo maana akashitakiwa kuvibakavitoto hivyo au kama kesi ingekuwa kubaka huyo mwanamke waliyekuwa wanagomnania.That could ve been something else.
Aidha nikutakie uchambuzi mwema.
Laswai ndugu yangu, hapo ni kwamba tuombe kikwete amrudishe huyo mbakaji wa mbezi ili kesi yake ifufuliwe upya na yeye afungwe,siyo tuwaombee wabakaji wengine watolewe just because mbakaji mwengine hakufungwa. hayo ni mawazo finyu sana. halafu kwa taarifa yako fupi tu,sio kwamba nguza kabaka mtoto mmoja tu,na sio mara moja tu.. kila mtoto alikua na kesi yake…alikua na shtaka zaidi ya moja..upo hapo?hala!.Yani mauaji mangapi yametokea,ila wauaji hawajapatikana..sasa wauaji wengine waliopatikana waachiliwe,just because wengine wameua ila hawakuchukuliwa sheria .. wanchekesha mie.lol
lol yani we blackmannen kakangu,umemgeuka miriam odemba kwa kibuti,now matty? na ndoa si ulishatangaza?kazi kweli kweli hapa BC.lol
majita ,
You made my day haaaaaa
mnyama anainama na kuinuka haaaaaaa! Sio siri huo ulikuwa mtihani kwake na fundisho la mwizi siku zake 40!
Haaaaaaaaaaaaaa
huyu mattyda mara nyingi nimekua nikimwona kama chizi flan
hivi……
ukweli wa ya nguza na familia yake
kwanza nashukuru BC kutuwezesha kuichangia kwa mara nyingine hii topic.
nakiri kwamoba napata vitu vipya saana, swali nnalojiuliza niaje hao watoto waliokua wanabakwa na babu seya wasababishe familia nzima iingie jela???
yani hata kama ni kweli au uongo kuwa walibaka bado kuna
hisia za KISASI hapo au mnaonaje wenzangu….?
IT CANT B…
majita sasa sikubali mi nataka nikuone uso kwa uso,hebu nielekeze huko kijijini kwenu nije. Kaka uko fit kwenye kutathmini mambo!!!! au ndo nikija ntakukuta uko mtoni unaoga na Ross mtoto wa kishua, hehehehehehe!!!
halafu jamani haya mambo ya ubakaji acheni tu!!!!! mie sisemi mengi ila yaliyowakuta wanaelewa uchungu uliopo moyoni. Binti mzuri mi naelewa hizo feelings ulizonazo towards hawa wabakaji.
mattylda usiwe na hofu na wabakaji wa majina ya watu,blackmannen nimekupata vilivyo mkuu.
Halafu we E.Ndaki ulitoroka bila kuaga halafu umerudi hata kunipeperushia salaam hakuna!!!!!???? haya welcome back,sijui ushapewa nyepesinyepesi za hapa BC wakati haupo!!!! ila kwa kifupi hapa kuna watu wanaitwa mr……, sorry edwin ntakumalizia story baadae ngoja nimeitwa na majita anataka niende mtoni kumletea maji kwasababu hayo majina huwa yanampa hali kama ya kutapika na blackmannen huwa hayo majina yanamjazia inzi,nakuja sasa hivi.
Maoni ya ya Binti-mzuri… kweli una elimu na mtandao wa maisha unao… mungu akulinde daima… kumi ka wewe kwenye blog basi tutaendelea. fan wako DK
Naona habari zinachanganyika hapa, someni!!! Huko Siera Leon wana usemi at a being a fool at 40 is a fool for ever. Ni zaidi ya miaka 40 toka Bongo iwe huru na hali inabadilika kidogo kidogo saana leo. Langu ni kwamba mafisadi walikuwepo toka zamani ila kulikuwa hakuna wa kuwaonyesha kidole na hawakuwa wanazikana na hivyo kufichana get the point.. swala la EPA kwa mfano limeibuliwa na “Patel” ambaye alitiwa ndani na wachezaji wa timu hiyo ya mafisadi, je uliisoma hiyo toka mahakamani?
Pili swala la Nguza ni story ndefu ambayo hata wadadisi wengi tumeshindwa kupata lolote kiufasaha imepinda sana hiyo habari na kwa nini haijulikani.
JK hatayaweza hayo labda akaimalizie kazi yake uhamishoni kwani hawezi kuwageuka waliompigia debe na kumuweka hapo na usiseme ati ni wananchi hapana ila wananchi tuliidhinisha kuwekwa kwake.
JK awe na moyo wa LIWALO NALIWE na awaondoe wote waliokuwemo ulingoni toka awamu zote zilizopita.
Pearl,
Maisha ya huku kijijini utayaweza kweli ndg yangu??
Ni juzi tu nimetoka kununua mashuka mengine Mapya manake nimesugua machacha aka masagama (unayajua hayo??) lakini naona bado yananitoka tuuu na mashuka nachana kila kukicha.
Nilionana na Ross akanipa namba ya simu mimi nikaandika tu mkononi na kijiti hadi nilipofika nyumbani nikapata pen na karatasi nikaiandika.Unacheza nini.Ila huku bwana mtu hasikwambie.Maisha swaaafi kabisa.Mafuta yangu Rays na Mamiz na Mwalimu ninayo na yananukia kinoma.Kandambili zangu nimezichukua jana kwa fundi kwani zilikuwa zimeachia na kazishona imara kabisa,zilikuwa zimeachia yale mashikio yake.Utanikuta niko bomba kabisa.Je bado unataka tu kuja huku kijijini kwetu Lulu jamani??Haya,nitakupa ramani.Utafika tu na karibu sana kijijini kwetu.
Nitaku-hook up na ROSS na utapata wenyeji kibao na kukuonyesha sehemu ya kuogea wanawake huko mtoni.Sisi tunaoga juu nyie mtaoga chini.
He he he he heeeee Binti-Mzuri, naona umecharuka na hao wabakaji. Huna mswalie Mtume na hilo!
Binti-Mzuri, mimi na Miriam mambo yanaenda vizuri wala sijampiga kibuti. Miriam sasa anajitahidi kula msosi wa nguvu ili again kidogo ka-mwili ili aweze kuhimili rigwaride la “Dume” mwenye misuli isiyo ya kawaida “BLACK”.
Binti-Mzuri, Mattylda ni dada yangu, ninampenda kama dada yangu, na si vinginevyo. Jina lake jipya ni zuri kuliko lile la zamani. Jina jipya la Mattylda ni feminini zaidi.
This Is Black=Blackmannen
# 27 mattyda mpya,ur confusing even name????(if the name is urs wld u confuse the spelling??)
u must stop ur bad habit upon touch arrogant to me , infact u do know me, i don’t feel u!u better refrain from those verbal!
being calm and steady temperament is very important leave me alone mshamba wewe!
Pearl, sina shaka na huyu limbukeni anayenifata fata kama kakosa cha kufanya!
Majita,
Mie ntakuja tu majita,please give the address.
watu mnaosema kabaka ushahidi mnao au ule mliousikia kutoka kwenye media jamaa kafanyiwa kitu mbaya sio lazima huwe profesa kujua hilo
hao mawaziri kulala rumande (kwenye viyoyozo n.k.) naona ni kama ni changa la macho tuu….tena nimesoma kule BC kuwa wameshatoka kwa mdhamana…(majumba yao yenye zaidi ya bilions zilizohitajika kama mdhamana….)
wezi wa epa naona bado wanadunda kama vile ni mashujaa…so what?…Why this kidding business??….Tunaelewa uchaguzi upo karibu na ni muhimu kuwahamasisha wapiga kurA KWA KUWASWEKA LUPANGO HAO VIBOSILE ili wapiga kura waone shughuli inafanyika……
nipo nasubiria hatima ya yote haya….
huku kunaganda lol
Mattylda original #27
Naomba unisamehe kwa maneno machafu niliyokuambia, infact i regret that. u do not confuse me…am confusing my self.
pls lets b friends okay….
BC,HUNITENDEA HAKI,MAONI YANGU DHIDI YA MATTY MWIZI WA JINA LANGU UNAYAMINYA,MUACHE ASOME PLS!!
Wewe matty mpya #37 na 27 hapo juu am not a fool kama wewe unayekalia kunifatafata mimi,yatakushinda!
Jeff pls naomba usifumbie macho hili suala blog ni yako inatakiwa tuiboreshe na sio kuivuruga,ngoja nione kama na hii utaibania!
“Mattylda”, mbona hivyo???? Mara uombe samahani kwa mwizi wako mara utake urafiki, sasa sisi, tukuelewe vipi????
Black=Blackmannen
Blackmannen,
naomba nikufafanulie kwa kina uelewe, matty no. 27 na 37 hapo juu sio mimi, bali ni yule matty mpya(mwizi) anajifanya yeye ndo mimi kwa kuniiga jina kila kona, nishamuuliza tatizo lake nini mpaka ananifatilia kiasi hicho sipati jibu!
Inshorti mimi sio mtoto kama yeye, mtu mzima na akili zake hawezi kuwa stupid kiasi hicho!
Matty mpya,
This is last,ukinifata tena nipo tayari kukuachia hili jina pia unaona nafaidi kitu gani????ushamba tu umekujaa, mtu mzima ovyo!!
Sitojibishana na wewe kwa lolote utakaloandika hapa iwe kujikomba kwangu au kugeuza maneno, i can’t argue with u fool!
Kaka Jeff pls usiminye hii!
serkali corrupt inaendesha mambo yake kwa mabavu ikiwa ni pamoja na washindani wa walioko madarakani. hivi uliona watu kesi ya kushindania demu ikageuzwa kuwa ya unajisi wa watotot. hivi kweli ni kwa nini yule yuko huru hadi leo ingawa alisemakana kushiriki katika kuwapeleka wale watoto kwa vikingi na wanawe. mla rushwa na mtoa rushwa wote ni wahalifu kwa hiyo uegemevu(biasiness of the case in question creates another of ambiguity even among the juristic lawyers.
kama Mumgu yupo basi mkono wa waliotenda haya utaumbuliwa kwa ukoma wa kutisha.
ninaomba sana mzee nguza atoke hicho kitendo awezi kutenda baba na watoto kuweni na moyo wa uluma jamani miaka yote aliyokajera jamani ujafa ujaumbika reomimi kisho yule
0712233044 .