ndanda-kosovoZimebakia siku chache tu tuumalize mwaka 2008.Weekend inapojongea namna hii ni kuashiria kwamba ni wakati wa kuburudika,kupumzisha akili,kutembeleana,kuhudhuria vikao vya harusi,mwali kutolewa ndani,vikao vya familia,kiti kirefu(cha kaunta),nyama choma nk.

Kwa wengine huu ndio wakati wa maandalizi ya krismas.Ni wakati wa kuwaza na kuwazua kuhusu zawadi za x-mas.Ni wakati wa kupamba miti ya x-mas.Wakati wa kuweka pamba kwenye miti eti kuashiria barafu!Ama kweli wenzetu wanatupata.Hapo sijajiuliza kuhusu mambo ya Santa Claus na jinsi ambavyo wabongo tunamshobokea bila hata kujua au kudadisi chanzo na mwisho wake.Ajabu tukiambiwa kwamba tuna kautumwa ka akili tunakuja juu ile mbaya!Hivi ni lazima kila siku tuige kila kitu wanachofanya “wa magharibi”?Wao wanaiga nini kutoka kwetu?

Anyway,ngoja niyaache hayo kwa sababu kadri ninavyozidi kujiuliza ndivyo ninavyoshindwa kujizuia kumkumbuka rafiki yangu Ampeninimungu aliyewahi kunionya kuhusu madhara ujinga.Leo ni Ijumaa,ni siku ya kuburudika.Ndio jadi yetu hapa BC.

Wiki hii Rais ametangaza msamaha kwa wafungwa 4,306.Miongoni mwao ni mwanamuziki TID.Msamaha huo ndio ulionifanya nikumbuke wimbo kutoka kwa FM Academia(Wajela jela Gwa) au The Dream Team.Enzi zilee za kina Ndanda Kosovo(pichani).Wimbo ni Jela.Wasikilize hapo chini.Wanasema jela…jela…jela ni mbaya.Wikiendi njema.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Burudani ya leo imewezeshwa na DJ Dennis ambaye huwa kila jumamosi anavurumisha midundo pale Bongo Radio

Feedback / Comments

9 Responses to “JELA-FM ACADEMIA ORIGINAL”

  1. Comment by Rebbygod on December 14th, 2008 12:53 am

    Duh!!!!!!!!!
    Yani umenikumbusha mbali Jeff……………….
    Nilikua namzimikia huyu jamaa na nyimbo zake,
    Anyway I miss my home, I miss Tanzania……..

    Rebbygod

  2. Comment by Bob Sankofa (a.k.a Babukadja) on December 14th, 2008 1:33 am

    Nimependa sana hilo dongo la Santa Claus, kuna Krismasi ya mwaka fulani nilipata kumshuhudia muigizaji mkongwe wa hapa nyumbani, Mzee Small, akiwa amevaa yale manguo mazito ya Santa huku akigawia watoto peremende pale mnara wa askari, mchana wa jua kali eti. Nikajiuliza, “Hawa jamaa waliomvalisha huyu mzee wa watu haya manguo na joto lote hili wanamtakia heri kweli?”

    Sasa leo ndio nimegundua kuwa kuiga kubaya. mtu unaweza ukafa hivihivi.

    Tusherehekee sikukuu ya Noeli, lakini kwa namna yetu sisi.

  3. Comment by Frateline on December 14th, 2008 1:19 pm

    Hi guys

    Nimekumbuka wakati wa uzinduzi wa hiyo album yao ya wimbo wao huo, nilikuwepo pale pool side ya zamani kilimanjaro hotel kwa sasa hakuna tena hiyo pool side wala kilimanjaro , najua kwa sasa kuna Kempisk-Kilimanjaro Hotel- Wimbo wao ulikuwa ume tulia sana,

    Hongera sana BC yakale ni mazuri kukumbushana

    Frateline

  4. Comment by hombiz on December 14th, 2008 1:25 pm

    Chozi la munyonge malipo kwa mungu babaaaaa!
    Acha waseme sisi ni kazi babaaaa!
    Jela…jela ni mbaya
    jela…jela ni shida
    Jela…jela mateso
    Week end yangu imekamilika.
    Kazi muzuri kabisa FM-A!
    Thankz BC

  5. Comment by Mattylda on December 15th, 2008 5:18 am

    Thanx BC leo umenikumbusha mbali sana, huyu ndanda Kosovo namkumbuka mwaka 2001nilimuona live jamani mkaka aliwekaga brichi kichwani ya msalaba lol!,aluuuuuuu(Uko wapi Hilarya Ng’oma???unamkumbuka Ndanda Kosovo????) naizimia hii nyimbo ya JELA NI MBAYA!!sijui yuko wapi jamani huyu mtu!

  6. Comment by Lalola on December 15th, 2008 8:43 am

    Mhhh, jamani BC mnenikumbusha mbali kweli mwanawane!

  7. Comment by yaya alfani on December 17th, 2008 8:57 pm

    mwanzo ni mugumu

  8. Comment by Toto tundu on December 23rd, 2008 7:29 pm

    Hivi bongo imekuwa Zaire?. Kwanini miziki inapigwa kama ya Zaire?. Heri miziki ya Kingwendu.

  9. Comment by binti-mzuri on December 23rd, 2008 11:15 pm

    ivi hawa si ndio waliimba ule mwimbo wa kidedea..kichezaji shoo chao kilikua kinakatika..

Leave a Reply