
Bila ubishi Inspekta Haruni ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Flava ambao wanastahili na wana haki kabisa ya kujiweka katika lile kundi la “wakongwe katika fani”.Pia Inspekta anadumu katika lile kundi la “wataalamu wa vina(mashairi) na tunzi ambazo baada ya kutoka hewani hugeuka zikawa misemo ya mitaani.
Kama hukubaliani name,basi jaribu kuusikiliza kwanza wimbo mpya kutoka kwa Inspekta unaokwenda kwa jina la Haina Ngwasu kwa kubonyeza player hapo chini.
Na kama jadi mpya ya wasanii wa bongo flava mashairi ya wimbo huu yanaelekea kuwa “ujumbe” kwenda kwa mtu fulani au watu fulani?Mawazo yangu.Sikiliza na wewe utuambie.Pata burudani.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Photo/Ahmad Michuzi
Feedback / Comments
16 Responses to “HAINA NGWASU-INSPEKTA HARUNI”
Leave a Reply


sending...
Hongera zenu wana”Ngwasuma”, mimi nawakubali. Kila sehemu mnapofanya vitu vyenu, huwa ni vya uhakika, kila mtu huridhika navyo. Wanenguwaji wenu ni moto wa kuotea mbali……!!!!!! Kazi ndiyo hiyo dada zanguni, tupo pamoja nanyi.
Ahsante Jeff kwa kutuwekea bonge la burudani la wikiendi
This Is Black=Blackmannen
Sorry “Inspekta Haruni”, nilikufananisha na “AKUDO – Wanangwasuma”. Lakini baada ya kukusikiliza nikagundua kuwa jina la wimbo “Haina Ngwasu”. Mtu unatakiwa kusikiliza kwanza kabla ya kutoa maoni. I’m sorry!!!!
This Is Black=Blackmannen
Blackmanen kaka angu vp umesoma vizuri hapo mbona kama ume chemsha maelezo na picha ni tofauti
kweli babu nabii hakubaliki kwao kwa ngwasuma umerudisha heshima.
Haina Ngwasu hiyo babu Inspector kabisa wasikutie doa.Katika wasanii wa bongo wanao imba mashairi yakaeleweka babu uko juu sana na nina kufagiliaaaaaaaa sana kila kibao unatoa kina eleweka.Asante kwa burudani murua bila ngwasu aawwww!!!!
Yaani hapo juu vp mbona mnamix mambo?
dude hili c mchezo Babu umewaonyesha kwamba wewe ni nani..kip it up bro..TMK 4life
Ni kweli dada “halima”, nimechemsha kinoma, maana hata hao wanangwasuma ni FM-Academia na wala sio Akudo. Ulevi wangu wa wanenguaji wa Akudo ndiyo unaonisumbua. Msema kweli Mpenzi wa Mungu!!! Wanenguaji wa Akudo ni moto wa kuotea mbali.
It’s Great To Be Black=Blackmannen
Babu karudi nami inabidi nirudi, Nabii kweli hakubaliki kwao babu umesema. Nashangaa yaani hata ukitoa maujumbe ya nguvu watu bado tu hawakubali, hivi mnataka babu afanyeje ili mumkubali? Mtoto wa geti kali, Asali wa moyo nanyingine kibao kawasifia, na kuwakuza sana kinadada, Bado upoupo kawatetea wanawake na akina dada, lakini watu wakaponda, sasa mkongwe anaongea kwa sauti ya busara, bado hamkubali….Haiwezekani mkawa hamjalewa, binti mzuri upo?
Its a good piece of work….Hongera Babu!
you know what i love this song..unachezeka kweli!hmm.. new billicanas inabidi twende jamani! sijui kama una madongo au lah,i was all about the ‘eeeh, haina ngwasu bado natesa(sijui ndo alivosema!?)’
mtu umenichekesha..i feel you! babu kama alipindika mara akaenda taarab mara akarudi,we cant deny the fact that the guy has had his mchango to bongofleva wether in a minor or major way..ndio maana babu..mmh
nime kuku bali mzee wa katuni yani nyimbo imekwenda vidato vyote. monti kalloss umenipata ipe viwango. gwantu hapa
haroun na marko chali,kitu imetulia.mi namzimika mchizi huyu kitambo,nilimwona stejini miaka ya nyuma kidogo,sasa naweza ku-imagine yukoje.ningekuwa promoter ningesham-beep tayari,sema mi napendanga kusikiliza tu.kazi kwenu hatters
sana tu inspector kweli we mbaya nimekukubali man si mchezo tmkeeii uko juu kama kenya vile oraaa umeona mbereee? au unamberaaa! unasogoaaaa!
hey haroun ur song kweli imetulia yaani inahit ile mbaya naamini kweli ur realy babu kip it up mkubwa.
HAHAHAHA NAAMKA ASUBUHI NINA BABALAZI NASTUA KWA….. NAPIGA SIMU KWA MIKE PIMA TUNAENDA KWA MZOLI MAMBO YA MILLERS NA NYAMA ZA KUCHOMA MPAKA UNGAZIANGALIA HAHAHAHA FAGILIA BABU WE STILL WATING 2 COME BACK AGAIN IN DA CAPE TOWN . HII HAINA NGWASU KALI KALI KWELI KWELI KITU KIMESIMAMA FAGILIA BABAKE
hilo zigo limesimama 2 sana mwanangu.madude yako yote huwa huchemshi.nakupa saluti.