huskiesbc

Yapo mambo mengi hapa duniani ambayo hatuwezi kuwa na uhakika nayo.Lakini yapo machache ambayo tunaweza kuwa na uhakika nayo.Mojawapo ni kwamba kijana Hasheem Thabeet anafanya vizuri katika mpira wa kikapu vyuoni nchini Marekani.Anaendelea kuwa “balozi” mzuri wa Tanzania kupitia michezo.

Majuzi nilipata nafasi ya kuongea naye machache. La msingi nililotaka kujua ni mipango yake kuhusu kujiunga na ligi ya NBA hapo mwakani. Hasheem anasema ni mapema bado kuliongelea swala hilo kwani hivi sasa anajaribu kuelekeza nguvu na akili yake katika michezo ya vyuo inayoendelea huku timu yake,maarufu kama The Huskies (kama wanavyoonekana pichani) wanaendelea kufanya vizuri.Hivi sasa wanatajwa kuwa miongoni mwa timu bora kabisa za mpira wa kikapu za vyuoni nchini Marekani.

Kesho(Jumamosi) saa nane mchana kwa saa za mashariki (2:00pm Eastern Time),The Huskies wanapambana na vijana wa Notre Dame katika mchezo wa marudiano.Katika mchezo wa kwanza The Huskies walishinda kwa vikapu 69-61. Mchezo wa kesho utaonyeshwa katika vituo vya CBS na vingine vingi vya michezo.Kila la kheri.

Update: Mchezo umekwisha na The Huskies wameshinda 72-65. Good job Hasheem na wenzako.

ddcNi ijumaa tena.Mwezi wa pili ndio tunaupa kisogo taratibu.Kwa maneno mengine,mwaka 2009 ndio umeshaanza kuyoyoma tayari kabisa kuukaribisha 2010 mwaka ambao kile kipute cha Kombe la Soka La Dunia kitapigiwa nchini Afrika Kusini au “Bondeni” kama baadhi ya watu wanavyopenda kupaita. Kama una mpango wa kushuka “Bondeni” hapo mwakani,kumbuka tu kwamba tiketi zimeshaanza kuuzwa. Tembelea tovuti ya FIFA ili kujua taratibu zaidi.

Kama kawaida Ijumaa ni siku yetu.Ni siku ya Zilipendwa.Leo tunao DDC Mlimani Park ambao hivi karibuni wataanza kujulikana kwa jina la Mlimani Park bila maneno DDC pale mwanzoni.Sababu?Kama ulipitwa unaweza kusoma hapa ili twende pamoja.

Wimbo unaitwa Hiba. Ni lalamiko la penzi.Nini husababisha mke au hata mume kubadilika? Ni nani wa kulaumiwa?Pata burudani.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

uyowa2bc

Irene Uwoya

wemabc

Wema Sepetu

Kwa muda sasa jamaa wa Global Publishers,kupitia gazeti lao la Ijumaa,wamekuwa wakiendesha shindano lililojulikana kama Ijumaa Sexiest Girl.Kilichokuwa kinafanyika ni kwamba kila wiki mrembo mmoja alikuwa anatolewa baada ya kupata kura za chini kushinda wengine.Wapiga kura walikuwa ni wananchi,wasomaji wa gazeti la Ijumaa.Kulikuwa na namba ya simu +255 784 275 714 ambapo wananchi walikuwa wanatuma ujumbe mfupi wa maneno(SMS) wakimpendekeza msichana ambaye kwa mujibu wao anastahili kushinda.Jumla ya warembo 12 walishirikishwa katika shindano hili.Unaweza kusoma zaidi kuhusu shindano hilo kwa kutembelea tovuti ya Global Publishers na kisha katika Search andika Ijumaa Sexiest Girl.

Sasa baada ya mchakamchaka mzima,warembo wawili, Irene Uwoya na Wema Sepetu(pichani) ndio wamebakia na mshindi anatarajiwa kutangazwa Ijumaa ijayo. Inawezekana hukupata nafasi ya kupiga kura wakati shindano lilipokuwa linaendelea.Pamoja na hayo,hapa una nafasi ya kutoa maoni yako.Nani unadhani ataibuka mshindi?Kwanini?

ay-bc

Msanii AY ametoa wimbo mpya ambao tayari umeshaingia kwenye vituo mbalimbali vya radio na mtandaoni kama hapa BC.Wimbo unaitwa Leo na umetengenezwa katika studio za Hermy B. Video ya wimbo huu inatarajiwa kuanza kutengenezwa wikiendi hii chini ya kampuni kutoka nchi jirani ya Kenya inayojulikana kama Ogopa Video. Usikilize wimbo huo kwa kubonyeza player hapo chini.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

inafrikaband

Bila shaka unawatambua wana Inafrika Band.Hivi sasa bendi hiyo machachari wapo katika ziara ndefu ya nchi za Ulaya.Wakiwa huko huko ziarani,Inafrika wamekamilisha albamu yao ya pili ambayo imekuwa mastered nchini Ujerumani. Wanatarajia kuitoa rasmi watakaporejea nchini Tanzania mwezi Aprili.Albamu itakwenda kwa jina Mbeleko.

Sisi hapa BC hatuna la zaidi bali kuwatakia Inafrika Band ziara njema. Endeleeni kutuwakilisha huko.Ni matumaini yetu kwamba mtatutumia japo single moja kutoka ndani ya Mbeleko ili nasi tuiweke hapa ili wapenzi wa muziki wapate nafasi ya kusikia vionjo vilivyomo.

mama-maria

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Maria Nyerere ambaye hapo jana alimtembelea pale Ikulu jijini Dar-es-salaam. Ni muhimu kuwatembelea “wana” na hususani wale ambao kipenzi mumewe,Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwaacha wakiwa na dhamana ya kuliongoza taifa.

shivjibc

Ni wazi kwamba tukiuliza swali kwamba kwanini Tanzania bado ni nchi ambayo,pamoja na rasilimali zote ilizonazo,bado haijaweza kupata maendeleo ya kiuchumi inayostahili,majibu yatakuwa ni mengi na pengine yanayotofautiana sana.Pamoja na tofauti ambazo zinaweza kujitokeza tunapojadiliana, mijadala ya namna hiyo ni muhimu kufanyika kwani inatupa mwanga wa nini pengine kifanyike ili tusije warithisha wanetu nchi ambayo hata wakitaka kuiuza,wasipate mnunuzi.

Miongoni mwa watu ambao wanatarajiwa kuchochea mijadala kama hiyo ni pamoja na wasomi mbalimbali tulionao.Haishangazi basi kusikia kwamba leo Prof.Issa Shivji(pichani) anatarajiwa kuzindua kitabu kinachoainisha mambo mbalimbali yanayosababisha nchi yetu kutopata maendeleo makubwa ya kiuchumi tangu tupate uhuru miaka arobaini na ushee iliyopita.Kwa habari zaidi bonyeza hapa.

jdbanana

Wiki iliyopita,katika viwanja vya Leaders Club kulianzishwa Shirikisho la Wasanii wa Muziki Wa Kizazi kipya. Shirikisho hilo limepewa jina la Tanzania Flavour Unity.

Kuanzishwa kwa shirikisho hilo kulikwenda sambamba na zoezi la kuchagua viongozi wake ambapo Lady Jay Dee alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Banana Zorro akichaguliwa kuwa Katibu wa umoja huo. TID alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.

Mojawapo ya malengo makubwa ni pamoja na kujiweka sawa kupokea msaada mkubwa wa Mastering Studio  ambao Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliwaahidi wasanii wakati alipozungumza wakati wa sherehe za kutimiza miaka miwili ya kituo cha kulea vipaji cha Tanzania, THT(Tanzania House of Talent).

ally-and-farha

Pichani ni wabunifu wa mitindo ya mavazi Farha(kushoto) na Ally Rehmttulah(kulia).Picha hii ilipigwa na Mpoki Bukuku wakati wabunifu hao walipokuwa wanahudhuria onyesho la mavazi lililoitwa Lady in Red hivi karibuni jijini Dar-es-salaam.Ukitaka kupata vitu zaidi kuhusu kazi za Ally Rehmttulah unaweza kuitembelea tovuti yake kwa kubonyeza hapa.

maina

Mwisho wa wiki umewadia.Ni muda wa kupumzisha tena akili ingawa kimsingi sio kupumzika haswa bali ni kubadili muelekeo wa majukumu.Badala ya kuniga tai na kuelekea “mjini” kazini au kutafuta kazi,huu unakuwa ni muda mzuri wa vikao mbalimbali kama vile vya kifamilia,harusi ya rafiki,ubatizo,ubarikio nk.

Imekuwa wiki ngumu kiasi.Hapa BC tumekuwa “bize” kidogo tukijaribu kufanya mabadiliko kidogo kwenye mtandao.Bado tupo matengenezoni.Tunatumaini kwamba tutakapofikia tamati ya matengenezo basi tutakuwa na kitu bora zaidi na ambapo tutakuwa na uhuru zaidi.Tunashukuru kwa uvumilivu wako msomaji.

Kama ambavyo mmeshasikia,wiki hii fani ya muziki nchini Tanzania ilipata pigo la kuondokewa na mwimbaji mahiri wa Msondo,Joseph Maina(pichani). Maina alifikwa na mauti ndani ya daladala akiwa njiani kuelekea studio kufanya kile alichokuwa akikipenda maishani mwake(kuimba).

Kifo cha Maina ni pigo sio tu kwa wana Msondo Ngoma bali wapenzi wote wa muziki nchini Tanzania,ndugu,jamaa na marafiki.Tunatoa pole za dhati kwa wahusika wote.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Katika kumkumbuka Joseph Maina,bonyeza hapa umtizame Joseph Maina anavyolalamika katika wimbo Kalunde.Pumzika salama Maina.

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page