fabc1

Hakuna ubishi kwamba kijana Hamis Mwinjuma au maarufu kama MwanaFalsafa(MwanaFA) ni miongoni mwa wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao wamefanikiwa.MwanaFA amefanikiwa sio tu kufikisha ujumbe alioukusudia kwa jamii bali pia kuwa na uwezo wa kuendesha maisha yake kupitia muziki.Miziki yake imekuwa ikiimbwa na watu wa rika mbalimbali.Hayo nayo ni mafanikio.

Pamoja na mafanikio ya kimuziki au kisanii aliyonayo MwanaFA,anabakia kuwa mfano wa kuigwa linapokuja suala zima la elimu,muziki na maisha.Hivi karibuni alithibitisha hilo pale alipoamua kurejea tena shule.Safari hii ameelekea nchini Uingereza.

Nini kinamsukuma kijana huyu katika nyanja ya elimu? Na je hivi karibuni alipoachia wimbo unaokwenda kwa jina “Msiache Kuongea” alikuwa anamjibu Inspekta Haruni?Anazungumziaje maisha ya nchini Uingereza?Fuatana nasi katika mahojiano haya mafupi na MwanaFA

BC: Pamoja na mafanikio mazuri katika muziki kule Bongo bado umeamua kurudi tena shule.Nini kinakusukuma?Hapo UK umeenda kusomea nini na katika chuo gani?

FA: Kuna mengi yanafanya nifanye nnachofanya.Lakini kubwa na la msingi zaidi ni kuwa na nguzo nyingine kwa ajili ya maisha ninayoishi(Plan B).Kama unavyojua muziki pamoja na kuwa unakwenda vizuri lakini hautabiriki sana.Ni ngumu kujihakikishia nafasi ya moja kwa moja kwa angalau miaka 10 ijayo.

Na zaidi ni kuwa naona kama kuna muda mwingi kama msanii wa kibongo nakuwa naupoteza kwa kutofanya chochote baada ya kurekodi(ambayo sio kila siku),kufanya shows(mara nyingi huwa weekends),matangazo(mara chache kama una bahati) na interviews ambazo nazo sio kila siku.Kwa hiyo kwenye wiki kunakuwa na muda mwingi unaenda bure ambao nimeona ni vyema nikautumia kufanya kitu kitakachozalisha.
Hapa UK nasoma Msc Finance na nipo Coventry University.

BC: Una mpango gani na muziki kwa hivi sasa?Kama utaendeleza muziki na shule vilevile,lini labda wapenzi watarajie albamu yako mpya?

FA: Nimeacha album ikiwa tayari,inaitwa ‘mabibi na mabwana’ na naomba maswali kuhusu hiyo ayajibu Hermy B,ndio ipo mikononi mwake..sijapumzika kabisa muziki,ila nimepunguza kiwango ninachoufanya kwa sababu ya umbali.Ngoma zitaendelea kushuka kama kawa..patience kidogo inahitajika nitulize haya ya kwa Bi Eliza kwanza.

BC: Katika wimbo ulioutoa hivi karibuni kabla hujaondoka Bongo(ukishirikiana na Lady Jay Dee),inaelekea kwa namna fulani umemjibu Inspekta Haruni na wengineo wengi.Kwanini umefanya hivyo ikizingatiwa kwamba ulishasema siku za nyuma kwamba hutomjibu?

FA: Kama utakuwa umeniskiza vizuri sikumjibu..nilisema ‘…nisemeni hadharani hata bila hoja kama Inspekta’,nikimaanisha natoa ruhusa kwa kila mtu kunisema hata kama hana sababu za msingi za kufanya hivyo kama alivyofanya jamaa.Na,aina ya mziki tunayoifanya hairuhusu kabisa unyonge,ilikuwa haki yangu ya kimsingi.Watu wengi wanaongea vitu vingi vibaya siku hizi,hivyo inabidi niwaambie najisikiaje wakifanya hivyo.

Ukweli ni kuwa hawaingii kwenye lines zangu za maisha na wananipa nguvu na hasira za kufanya vyema zaidi.Na sio kwangu mwenyewe,kila mtu ana matatizo yanayofanana na yangu kwa namna moja ama nyingine kwa hiyo anaweza kuitumia kimpango wake.

BC: Umekuwa ukiingia na kutoka nchini Uingereza mara kadhaa.Ni mambo gani ambayo unadhani unayafurahia hapo UK na ambayo labda nchini kwetu tungeyaiga yangesaidia katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo?

FA: Uingereza kama nchi imejipanga.Ni dunia ya kwanza.Kuna mengi tunaweza jifunza,siwezi hata kuorodhesha.Lakini napenda namna wanavyoheshimu utawala na nguvu za sheria.Natamani kwetu kungekuwa hivi kwa kuanzia.

BC: Una mpango wowote wa kushirikiana kimuziki na wasanii wa hapo UK?Ni kina nani ambao unawazimia?

FA: Muziki wa UK hauendani sana na wa kwetu.Wana muziki tofauti na sisi.Pamoja na umbali wa kimaendeleo waliotuacha nao sijui hata wanamuziki 10 wa hapa.Hata rap/hiphop ya hapa siamini kama inapendwa mahala pengine popote zaidi ya UK.Haina mafanikio makubwa nje ya hapa.

Hata hivyo napenda mziki wa Lemar na Jay Sean na natamani nifanye nao kitu kama ninavyotamani kuifanya hii shughuli na 2face.

Nimekutana na Amit(Mentor) ambaye apparently ndio amemtoa Jay Sean(japo sasa Jay amepata record deal Cash Money),na tunajaribu kuona nawezaje kufanya mawili matatu toka nyumba yake ya muziki.Huwezi jua..nasubiri nione kitakachotokea!


Feedback / Comments

84 Responses to “SALAMU ZA FA KUTOKA COVENTRY”

  1. Comment by Sophie on February 16th, 2009 5:43 pm

    Safi sana FA…naona umeamua sasa kweli music na shule…vipi sasa ndoa lini na yule demu wako wa SInza……mshikaji ulifanya certificate how come sasa unafanya masters??

  2. Comment by any on February 16th, 2009 6:52 pm

    Sophie, thats too personal. leave him alone, wee kwani una mangapi zaidi ya hayo yake hiyo siri yako, na kwa vile wewe sio celebrity, ndio maana hatuyasikii, otherwise, this guy is just like any other human being, same needs, like shelter, food, mavazi and of course SEX!

  3. Comment by bantu on February 16th, 2009 8:01 pm

    Mh,we sophie.Si alifanya advance diploma ya insurance ifm?

  4. Comment by Gwantwa on February 16th, 2009 8:12 pm

    kanajibu vizuri maswali.kana akili akili kumbe

  5. Comment by Mkali kwanza on February 16th, 2009 9:37 pm

    Si hatuachi kuongea FA, Vipi hapo kwenye CERTIFICATE hadi MASTERS how come.

    tunataka kujua kama inawezekana tutamrusha Mr blue toka fom 2 hadi 6 na yeye asome.

  6. Comment by mjanja on February 16th, 2009 10:18 pm

    hongera sana man inapendeza shule ni jambo la msingi sana keep it up

  7. Comment by Foster on February 16th, 2009 11:24 pm

    In the UK, but in some universities and colleges, you may register for a masters level and opt for an early exit whilst having to follow from a certificate, diploma and finally to a master degree. So, is no wonder that this fellow-MwanaFA has opted to follow such a route, and that means if you ask him what level he is aiming to achieve, yes, he will definitely say a masters level. It does sound POA yeah?

    Is it right to say so? On the one hand, it is right to say so if he is really determined to achieve the finals but, on the other hand, he may be deceiting if he will not be able to finish to masters level. Many people who enroll in this kind of program have tended to opt to leave their course at a diploma level. They say “Too many years and too much work to do buddy” Sort your self up.

    By the way I saw this guy in one of the place where I usually visit on Friday midnights for disco. He was with another feller and got into this music hall quietly but later I noted repeatedly some guys mentioning of Tanzania for many times and it shove me to have a look to see who these guys are on the stage. You know what they were throwing their trucks like no one else in the hall and every TZmania in the house/ hall was already crazy. I too was, but already had 6000 mls of alcohol intake, which made a complete night for me. Not bad for once a month!, it is permitted. This was London, E13. Club Afrique on the 30th,January 2009.

    KEEP IT UP FA

  8. Comment by nice2 on February 17th, 2009 12:18 am

    Sophie… hiyo certificate unayoongelea ni kama miaka mitano iliyopita, inaelekea uko nyuma ya wakati sana, tembelea japo website yake for more info. Na zaidi, kama vile una wivu na huyo demu wa sinza hivi ( ni mtazamo tu)
    Keep it real B, you’re the DON you know……

  9. Comment by jaysan on February 17th, 2009 1:21 am

    Kwa taarifa tu FA alifanya Advance Diploma pale THE IFM. Hivyo ni sahihi kufanya masters provided advanced diploma ya IFM ni equivalent kabisa na degree.actually sasa hivi inaitwa degree.haa haa habari ndo iyo.

  10. Comment by asa on February 17th, 2009 1:41 am

    we sophie nae kujifanya unamjua sana mwana fa kumbe hamna kitu sasa mwana f.a kwataarifa yako kasoma certificate na advance diploma pale i.f.m incase udidnt know

  11. Comment by kaka mkubwa on February 17th, 2009 2:33 am

    nana kakwambia alifanya certficate wewee? ndiyo ninyi mnaoongea hovyo. Mbona mm nilikuwa naye darasani sasa wewe hizo habari za cert. umezitoa wapi? huo ndiyo udaku bora uende kule kwenu utamu ikifufuka

  12. Comment by mr degree on February 17th, 2009 4:16 am

    Mh! mbona coventry hakuna MSc finance? au ndo changa la macho? manake huyo jamaa ni Mr misifa jamani. nakumbuka alipofanikiwa kupata admission ya kusoma certificate pale IFM akaanza kujiita majina kibao ya kujifagilia. mara ‘college boy’ mara ‘the don’ na kila kitu anapenda kujipa sifa sana huyo.sasa anatuambia anasoma Msc finance isije ikawa ndo yaleyale yo solo thang!

  13. Comment by Kafura on February 17th, 2009 5:25 am

    Issue ni kutoka ATECH 1 kwenda MSc FINANCE. hapo ndo hujatueleza huo ujanja.

  14. Comment by PUZZO Frm Dodom University on February 17th, 2009 6:12 am

    sophie una uhakika na unachokisema? Ingawa mi sio msemaji mkuu wk…Bt Am talkin as his biggest fun!!!!Jamaa alipiga Advance Diploma pale IFM….Big up Bro FA Unajua unachofanya!!

  15. Comment by till on February 17th, 2009 7:58 am

    let him leave his life jamani kuwa msanii cio kwamba hawezi fanya mambo personal evryone gotta live thr life big up FA mi nakufil vibaya mno i wish u ol the best.

  16. Comment by Riziki on February 17th, 2009 8:22 am

    we sophie unajifanya unamjua binamu kumbe la u r just those haters..amesoma certificate then advance diploma pale IFM na above all amepata work experience NBC ndo maana yuko zake masters…stop hating alikupiga kibuti nn maana unaulizia anaoa lini? big up binamu ni jambo la muhimu uliloamua they say education is the best succeful key in life…tuko pamoja tunakutakia kila la kheri..God Bless uuuuu!!!

  17. Comment by mr degree on February 17th, 2009 10:22 am

    jaysan unamaanisha nini unaposema advance diploma ya IFM ni equivalent kabisa na degree? unaijua degree wewe? na unajua tofauti ya institute na university? au hujui maana ya IFM? hata kama sasa wanatoa degree lakini yeye hana degree. na hiyo Certificate yake na advance diploma yake ya kudesa sio sawa na degree. kwa kuwa waingereza wapo kibiashara inawezekana wakampa admission ili mradi alipe tuition fee tu.any way hiyo sio ishu, swali langu ni kwamba hicho chuo hakina MSc finance anayodai anasoma. niambieni anasoma chuo gani hasa maana nyinyi mmezoea kudanganywa na kushangilia tu!

  18. Comment by Jazzy on February 17th, 2009 11:58 am

    Haya mi simo…

  19. Comment by Mwanamke wa shoka (UK) on February 17th, 2009 12:35 pm

    teh teh teh…inachekesha…..
    take it easy pals….lol

    …HE knows what he’s doing….

  20. Comment by Kweliman on February 17th, 2009 12:44 pm

    mwana fa hongera sana kwa kazi nzuri za sanaa(urban music) nimefurahia sana kazi zako.

  21. Comment by mjanja on February 17th, 2009 4:35 pm

    hongera maneno ya wanafki tu hayo! ndo maana kwenye t-shirt yake kaandika hi haterz u see me? acheni wivu hata kama anadanganya mnaona nyamazeni maana atakuwa anajidanganya mwenyewe pia

  22. Comment by doli on February 17th, 2009 4:58 pm

    we mr. degree.
    haya link hii hapa…toka kwenye website ya coventry university…inaonyesha hiyo msc finance…
    http://wwwm.coventry.ac.uk/postgrad/postgraduate/pages/pgft.aspx?itemID=56..
    go ahead playhating and he’s doing it..kweli hamuachi kuongea!

  23. Comment by mkaku on February 17th, 2009 5:26 pm

    Mseme msiseme kama ni kwenda shule kaenda, na nyie mnaojidai kuwa mnataka kujua sana anasoma chuo gani mtamsaidia kulipa? Si ajabu mmepiga boksi miaka zaidi ya kumi na shule hamjamaliza. Fuateni ya kwenu na mmalize ya kwenu, alisha sema yeye bado yupo yupo sofia unataka nini? Watanzania ndio maana hatuendelei kazi kutafuta udaku mdogo mdogo kuwarudisha nyuma wenzenu. Mkiona mtu amelosti ndio furaha yenu acheni hizo. Na wanaokuja ulaya kusoma msiwaingize mkenge na wao wasimalize shule kama nyie. Tuwe na malengo ya kuendelezana

  24. Comment by shababi on February 17th, 2009 7:05 pm

    asenti doli.hiyo ya link itasaidia sana,nilikuwa nashindwa kuchangia nikawa nafuatilia tu.kuna mijitu haina information kazi yao chuki tu.unatamani uichome sindano za sumu.nilikuwa ifm wakati jamaa anafanya advance diploma yake maskini na mpaka alipomaliza na akaanza kazi nbc,ana juhudi sana.aliweza kubalance vyote na vikaenda sawa,mziki na shule.badala ya kuwapa moyo hawa wasanii wasanii wetu wasome ndio mnafanya juhudi wajiskie vibaya na kuwakatisha tamaa…sijui mnatakaje,wakisoma balaa wasiposoma balaa.wabongo wajinga sana!mnafanya na hapa panakuwa kama kwenye utamu kule mlivyojaa ulimbukeni na kupenda kukashifu badala ya kuunga mkono maendeleo.
    FA usikate tamaa mwanangu,piga shule.hii mijinga itakuwa inatamani ingekuwa wewe.iache iongee we get your masters degree homie na iendelee kubishana.

  25. Comment by doli on February 17th, 2009 7:20 pm

    mr degree,msc finance ipo coventry university,link hii hapa..

    http://wwwm.coventry.ac.uk/postgrad/postgraduate/pages/pgft.aspx?itemID=56

    kingine???

  26. Comment by Sophie on February 17th, 2009 7:50 pm

    mmechonga sana kuhusu mimi..sina kinyongo wala wivu na FA..tatizo langu ni kwamba why come utoke certificate mpaka MSc…jamani angalieni sana..Masters si mchezo..thanks mdau juu kwa kusema yale yale kama ya Solo thang….msikubali kudanganywa tu kama watoto..I know FA..mzee wa misifa sana…sasa ona kadanganya vibaya kumbe cho hakina hiyo program….may god…….

  27. Comment by mimi on February 17th, 2009 9:31 pm

    Acheni ufala na mabishano yasiyowasidia chochote,haya asome asisome nyie kinawahusu nini?iwepo isiwepo nyie mwataka nin haswaa?Mbona mko washakunaku sana lakini? hamna la kufanya kazi umbea tu.Chuo hamkijui,elimu hamna mmekalia kubishabisha tu.Ashasema yuko coventry university then mnauliza chuo gani kama si ufala ninini?nendeni google mkakitafute hiko chuo na mtaiona hiyo course,kama haipo pia sio kazi yenu kufwatilia kwani hamumchangii ada.

  28. Comment by nice2 on February 18th, 2009 1:51 am

    Wewe unaejiita “Mr Degree”, usione wivu kuona mwenzio kapiga hatua na sasa anasoma masters, whether you like it or not, HABARI NDIO HIYO. Unasoma coventry uni hakuna Msc finance wakati hata mtu asiye na info zozote kuhusiana na hicho chuo akitembelea website yao tu akatafuta hiyo course anaikuta, au mwenzetu unaongelea chuo gani!
    One thing guys we should accept maendeleo ya wenzetu na kuacha chuki binafsi, kama FA is proud of what he’s doing whats wrong with that sasa? hata hiyo “certificate” unasema alipopata alikua anajidai, wasanii wangapi wamejaribu na wakashindwa, then kwanini asijidai yeye kamaliza na akasoma Adv Dip and now masters?????
    Big up mwana FA, you’re the real DON…..

  29. Comment by Mkwe on February 18th, 2009 2:12 am

    We mr.Degree una uhakika kuwa Coventry hakuna Msc Finance? Kwa taarifa yako ipo. Unabisha!tutakuchapa vibao. We utakuwa na wivu tu. Na mtu mwenye advanced diploma anastahili kabisa kusoma masters degree provided that ana upper second pass au first class. Kwanza masomo ya advanced diploma hayana tofauti na ya bachelors degree isipokuwa ni tofauti ya majina tu, umeelewa sasa! Big up Binamu, waache hatters waongee.

  30. Comment by sabrina on February 18th, 2009 3:26 am

    huyu aliyekasirika kabisa tunadanganywa na tunachekelea tu utasema kuna kitu anaweza fanya kuzuia jamaa asisome.tehtehteh,ovyo

  31. Comment by angela on February 18th, 2009 3:15 am

    hahahahaaaa kaaazi kwelikweli.
    mi naona tatizo hapa ni la kisaikolojia.hasa kwa mr degree(sijui ni ya nini) na wenzake,kuwa hawako tayari kuwa na rapper wa bongo fleva mwenye masters,tena ya finance.FULL STOP!
    kwa kiwango chetu cha elimu lazima tukubali masters ni over average,sio kiwango wengi tutabahatika kufika.mr degree inaelekea ndoto yako ni degree na bado hujaipata(lete vyeti tuone,hahahah)
    a fellow is doing it jamani.msc finance..
    stop hating,compliment.

  32. Comment by asa on February 18th, 2009 5:29 am

    WE MR DEGREE YAKUDESA ME NIMESOMA ADV DIPLOMA I.F.M NA SASAHIVI NNA MASTERS FALA WE WHY NOT MWANA F.A? WE BAKI NA DEGREE YAKO HUNA HATA LOLOTE WENZIO TUNAPAA TU HALOOOO

  33. Comment by clarasita on February 18th, 2009 6:19 am

    fa i just wish you luck in every ting u do.. do ur thing. no one has to decide for you.. sawa.. i hate idea crashers.. why do people have to discourage you… SUCESS. you have my love clarah

  34. Comment by carin on February 18th, 2009 10:16 am

    Ni kweli wabongo wanashangaza kwa kufananisha Advanced diploma na Degree! kama ingekuwa sawa si ingeitwa degree nayo hiyo advanced diploma!? Ebo? danganyaneni huko huko! Hizo daraja za elimu zina uzito wake jamani oho!
    Kwani mnaongoza pia kwa kupeana vyeti ovyo ovyo! aangalie mwana FA UK mjini jamani asijeliwa vipesa vyake vya mziki bila kupewa Masters! haya!
    Mimi sio hater wala nini Mwana FA namkubali lakini sikubali elimu kubakwa!

  35. Comment by EDO on February 18th, 2009 10:53 am

    mwana FA WE CONCETRATE NA SHULE YAKO ,HAPA COVENTRY KUNA WABONGO WENGI WANA WIVU WAMEMBEA NA MAJORITY KISOMO ZIRO,USIJIIUMIZE NAO WEWE KAMA NI BOX BEBA ,ISHI VIZURI UPASI SHULE YAKO BASI ACHANA NA WAJINGA.

  36. Comment by babie on February 18th, 2009 1:56 pm

    hivi mr degree ule mwaka mwanafa alipoanza kusoma ifm we ndio ulidisco pale ama ilikuwa mwaka kabla ya huo?heheheeeee..

  37. Comment by anita on February 18th, 2009 4:04 pm

    jamani fa sa kwanini uliniacha karibu unaondoka jamani c ungenivumilia kidogo at least ningekuwa na chat na wewe ona sasa cingii hata kwenye net, now a dayz….
    n wayz mafanikio mema wangu….

  38. Comment by msongo on February 18th, 2009 5:45 pm

    mr degree anasema ukweli hakuna hiyo programme hapa conventry university and oh yeah adv.diploma IS NOT EQUAL TO a degree infact ni kichekesho eti mtu kafanya Adv.Diploma in Insurance aruke to Masters in Finance very doggy :-)

  39. Comment by watu bwana on February 18th, 2009 7:36 pm

    siri ya mtungi aijuaye ngata.hongera mtanzania mwenzangu kwa kujituma,kama kweli umekuja kusoma soma kaka.watu hawajui muziki ni bahati,akili kichwani.chochote ukikipata kutokana na muziki,kiinvest. sababu muziki hautabiriki,na hauna future kwa bongo.usipo fanya cha maana mapema,utakuja ishia nilikuwa,nilikuwa,nilikuwa,kipindi hicho huna hata dala mfukoni.

  40. Comment by nod vizzo on February 20th, 2009 1:33 am

    Ebana kwanza kabisa napenda kutoa saluti zote kwa mwanajeshi Fa kwan mchiz yuko juu sana kutizama life la bongo.wadau wa bc bnawaomba sana muelewe elimu ni sawala la muhimu katika maisha ya mwanadamu hivyo mtu mzima kujikataa zake kiwanja kusaka maelimu ni swala la msingi sana.big up mwana fa

  41. Comment by kelvino_ on February 20th, 2009 1:52 am

    nakupa hongera mwana fa we piga shule, kwa kawaida wabongo hawaachi kuongea,mambo mengine hayana msingi kabisa hasa we soph hizo isssue ni zake binafsi sasa wewe zinakuhusu nini,au ndo ulitaka akuchukuwe wewe?

  42. Comment by mr degree on February 20th, 2009 3:05 am

    kwa credible university yoyote kama unataka kusoma mastes lazima ukutane na ktu hiki. “Applicants should hold a good honours degree in a relevant academic discipline”.sasa wewe na kidploma chako cha kuunga unga endelea kufananisha na degree tu.na kila nikiperuzi kwenye sifa za kusoma hiyo kozi anayodai kuisoma, nakutana na kitu hiki,You should have a degree with at least lower second class honours in accounting and finance, or a related subject, with sufficient background of accounting and finance.napata tabu kuelewa kama hiyo insurance yake inampa sifa ya hiyo kozi anayodai kuisoma. nyie wapumbavu msome tuu kwa wizi lakini degree ni degree na vyuo vyenye hadhi vinaitambua kama entry qualification kwa masters!mnaijua MSc nyinyi? tuulizenu wenye nazo! hatukurupuki tunafahamu tatizo lenu hamtaki kufahamishwa si mshazoea kufanywa wajinga!

  43. Comment by sanaa on February 20th, 2009 7:05 am

    msongo na sofia,hamjui kusoma?link si hiyo hapo inaonyesha coventry university wana msc finance?kadanganya nini?sofia umehama kutoka madai ya kuwa ana certificate sasa upo kwenye hakuna hiyo course.we msongo nae unasoma coventry ya wapi isiyo na msc finance?…HATERS!
    mr degree,any credible university yenye sheria hizo inaweka pia equivalent qualifications ya hizo ambazo najua ndio zilizomuingiza fa hapo,besides ametoka institute of FINANCE management.umenotice anything hapo?do your homework.nilichogundua ni kuwa wewe ni muongo na mkurupukaji,sasa unasema nini?hakuna hiyo course ama hana qualifications?kuna aliyechangia ulidisco ifm,kuna ukweli wowote hapo?sio tumjadili fa peke yake tu,tuelezee na yako tafadhali.

  44. Comment by bamdogo on February 20th, 2009 7:10 am

    kwani ina maana hiki kitu anachofanya fa ni kikubwa kiasi hicho mpaka watu msiamini anaweza kukifanya au nini?sielewi mimi

  45. Comment by sabah on February 20th, 2009 7:28 am

    ama kweli msiache kuongea..hebu mzee wa bc muweke mr blue tusikie maoni yatakuwaje

  46. Comment by Mzozo on February 20th, 2009 7:28 am

    [Intro: 50 Cent - singing]
    Many men, wish death upon me
    Blood in my eye dawg and I can’t see
    I’m trying to be what I’m destined to be
    And niggaz trying to take my life away
    I put a hole in nigga for fucking with me
    My back on the wall, now you gon’ see
    Better watch how you talk, when you talk about me
    Cause I’ll come and take your life away

    Many men, many, many, many, many men
    Wish death ‘pon me
    Lord I don’t cry no more
    Don’t look to the sky no more
    Have mercy on me

    [Verse One]
    Now these pussy niggaz putting money on my head
    Go on and get your refund motherfucker, I ain’t dead
    I’m the diamond in the dirt, that ain’t been found
    I’m the underground king and I ain’t been crowned
    When I rhyme, something special happen every time
    I’m the greatest, something like Ali in his prime
    I walk the block with the bundles
    I’ve been knocked on the humble
    Swing the ox when I rumble
    Show your ass what my gun do
    Got a temper nigga, go’head, lose your head
    Turn your back on me, get clapped and lose your legs
    I walk around gun on waist, chip on my shoulder
    Till I bust a clip in your face, pussy, this beef ain’t over

  47. Comment by Mzozo on February 20th, 2009 7:53 am

    Hii ni kwa all yo haterz out there…sijui Mr Degree,sijui Anita, Sabrina, Jil na the whole lot of hatterz out there…what does it take to appreciate on a brother’s success…what wil it cost you ro morally support a brother…

    Mnakuwa na wivu wa ki#$&ge sana usawa huu eti ooh hasomi ama andanganya na blah blah nyengine nyingi… One thing you should know ni kwamba Hamis didn’t bullshit his way to where he is right now…he is self made and he is living the dreams of all yo MOFOs who keep on hating!!!…he made it from scratch…the fruits of his success are his own Blood, Sweat and Tears…

    Yupo chuo, anafanya masters,he should be proud….and its okay for him to brag about it…he made a name for himself and he is making music that you listen to…he is a huslter pia…he should brag as well… he got it all…got what it takes to be him and even if you hating you can never be him so go on hating…one thing for sure you can never be him…

    hakuwa na Godfather to guarantee his success…you see him rolling foes you hattin…?Keep on Hating He is Living His Life!

    B… Always be You!

  48. Comment by Mzozo on February 20th, 2009 7:56 am

    T.I.
    No Matter What lyrics
    l
    Yeah, I say still i stand
    Ay, shawty here i am
    hey

    (Verse 1)
    Never have you seen in ya lifetime
    A more divine southern rapper with a swag like mine
    Facin all kinda time but smile like I’m fine
    Brag with such passion and shine without tryin
    Believe me, pains a small thing to a giant
    I was born without a dime
    Out the gutter I climbed
    spoke my mind and didn’t stutter one time
    Ali said “even the greatest gotta suffer sometimes”
    So I huff and puff rhymes
    Lyrics so sick wit it
    Set the standard in Atlanta how to get get get it
    So you up and coming rappers wanna diss, just kill it
    I’m officially the realest…point, blank, period
    Whether I still live in the hood or just visit
    Whatever you can do in the hood I done did it
    That’s why the dope boys and the misfits feel it
    This still his city long as TIP living, listen

    (Hook)
    I ain’t dead (nah) I ain’t done(nah)
    I ain’t scared(of what?), I ain’t run(from Who?)
    But still I stand (yeah)
    No matter what pimpin here I am(Yeah)
    No matter What

    Remember I ain’t break(never), I ain’t fold(never)
    They hate me more(so?)
    Yeah I know(Ha, Ha)
    Here I go(Yeah)
    No matter what shawty, here I go
    No matter what shawty

    (Verse 2)
    Let the blog sites and the magazines tell it
    I’m sure to be in jail till 2027
    Rather see me in the cell then
    Instead of this new McLaren
    God will take you through hell, just to get you to heaven
    So even tho it’s heavy, the load I will carry
    Grin and still bear it, win and still share it
    Apologies to the fans, I hope you can understand it
    Life can change ya direction, even when you ain’t planned it
    All you can do it handle it, worst thing you can do is panic
    Use it to your advantage, avoid insanity manage
    To conquer, every obstacle, make impossible possible
    Even when winning illogical, losing still far from optional
    And, Yea they wanna see you shot up in the hospital
    But, when life throw punches, block and counter like a boxer do
    Been locked inside mi casa too long, I did a song
    To make it known that the king lives on pimpin

    (Hook)
    I ain’t dead (nah) I ain’t done(nah)
    I ain’t scared(of what?), I ain’t run(from Who?)
    But still I stand (yeah)
    No matter what pimpin here I am(Yeah)
    No matter What

    Remember I ain’t break(never), I ain’t fold(never)
    They hate me more(so?)
    Yeah I know(Ha, Ha)
    Here I go(Yeah)
    No matter what shawty, here I go
    No matter what shawty

    (Verse 3)
    Even in solitude, there’s still no hotter dude
    I show you how to do, what you do, you ain’t gotta clue
    All you do is follow dudes
    Sound like a lotta dudes
    I’ll weather whatever storm
    Make it out without a bruise
    I understand why, ya’ll when my hands tied
    They take shots, cause if I’m out there it’s a landslide
    But revenge is best served as a cold dish
    And suckas will get served nigga no shit
    Guess it was understood, for me it was over with
    But I don’t quit, if you ain’t noticed yet
    They couldn’t wait to say goodnight shawty
    So they can try to rhyme, act and look like shwaty
    Go get a beat from Toomp, and make a hook like shawty
    Before ya know it I’m back what it look like shawty
    I lost my partner and my daughter in the same year
    Somehow I rise above my problems and remain here
    Yeah, and I hope the picture painted clear
    If your heart filled with faith then you can’t fear
    Wonder how I face years and I’m still chillin
    Easy, let go and let GOD deal with it (Ay!!)

    (Hook)
    I ain’t dead (nah) I ain’t done(nah)
    I ain’t scared(of what?), I ain’t run(from Who?)
    But still I stand (yeah)
    No matter what pimpin here I am(Yeah)
    No matter What

    Remember I ain’t break(never), I ain’t fold(never)
    They hate me more(so?)
    Yeah I know(Ha, Ha)
    Here I go(Yeah)
    No matter what shawty, here I go
    No matter what shawty

  49. Comment by EVE on February 20th, 2009 8:07 am

    Hahaaaaaaaaaa msinichekeshe nimewasikiliza mpaka mie mwenyewe nimesoma hicho chuo na sasa nakandamiza PHD kwa kweli msipende kuongea vitu msivyovijua hiyo course ipo kwani tatizo ni course au ni yeye kwenda kusoma? maana nimejaribu kucalculate multiplier hapa naona jibu ni wivu tu na chuki binafsi huo ndo ukweli hakuna habari za kuendelea kubishana si ndivyo wadau au nimekosea?

  50. Comment by watubwana on February 20th, 2009 7:21 pm

    kwikwikwikwikwi….
    hehehehehehehe…..
    hahahahahahaha…..
    mbavu zangu jamani uwiiii……..
    kaka nenda kasome si tuache tubshane hapa.
    hongera BC kwa kutupma akili,wivu,chuki watanzania wenzako.
    umegundua kitu ee??hatupendi mwenzetu akiwa anaendelea,badala ya kupeana moyo,tunakatishan tamaa.
    kaka wala huku usimuogope mtu,ubraza meni weka pembeni,usiogope mtu atakucheka ukibeba box,kuchambisha vzee,kufagia, we waache waseme wanavyotaka,ilimradi utimize malengo yako na mkono uende kinywani,kwani ukirud bongo utaenda kufagi,kuchambisha vizee ama kubeba box?ishi upendavyo na si wapendavyo.kanyaga twende.thanx

  51. Comment by watubwana on February 20th, 2009 7:29 pm

    na hili box mnalo penda sana kutusakama nalo watu tulioko majuu,ndilo linatulisha wengine,tunasaidia wazazi wetu nyumbani,na ada tunawasaidia wazazi wetu kulipa.na shule tunamaliza,kwa wale wote wanaopenda sana kuwasema wabeba mabox mtu ukiwa huku na malengo yako na ukijitambua kuwa wewe ni nani na umekuja huku kufanya nini?shule utasoma,kazi utafanya na kila kitu kitakiwa shwari.go FA

  52. Comment by Boaz on February 21st, 2009 3:23 am

    Big up keep it up

  53. Comment by Boaz on February 21st, 2009 3:27 am

    Umeonyesha njia wasanii wengine waige watafika mbali

  54. Comment by mama Liv on February 21st, 2009 4:46 am

    Watubwana, EVE (hongera dada kwa PHD maana PHD kwa bongo ni chache sana), MZOZO nawapa respect yangu. Mimi nashukuru EVE kwa kusema kwamba hiyo degree ipo huku Coventry jamani wabongo wivu utawamaliza…na kama mdau alivyosema hapo juu ukiwa ulaya bwana ni kujitambua na kupiga shule na kubeba mabox kama kawa…after all nyie HATERS ndio wale ambao shule hamjaenda na mnawaonea wivu wezenu waliokuwa majuu na kupiga shule na nyumbani kwao wanasaidia wadogo zao kama kawa (kwa kazi hizo hizo za kubeba mabox na huku ulaya ni cleaning jobs). Kaka FA achana na haters wewe piga shule yako na usiogope kubeba mabox just do it and save your money kwa ajili ya familia yako…na let me give you a good advice huko uliko achana na wabongo ambao ni ma HATERS. Maana mimi nipo Europe kuna wabongo kibao ambao ni ma HATERS hawajitambui wanachofanya hapa (kazi kunywa pombe ect) nina wakwepa kabisa bec they turned to be haters wakiona wewe unapiga shule yako na kubeba mabox ili uwasupport wadogo zako huko Bongo..so sio kila Mbongo ni ku associate nae, wewe jichanganye na makabila mengine at times they are better to associate with kuliko mahaters wa kibongo…nyie wote wenye negative comments ni ma haters tu na hamtaendelea n´gooooooooo sh..i zenu nendeni shule na kama shule haipandi basi ndivyo acheni walioenda shule wajenga taifa

  55. Comment by Chiku on February 21st, 2009 4:50 am

    ACHENI WIVU NYIE MA HATERS LOHHHHHHHHH maana hapa wengine wana hasira wao visa walinyimwa pale ubalozi wa UK sasa wanamuonea wivu huyo FA yeye alipata visa ki ulaini…ndio hivyo nyie haters kila mtu na bahati yake mungu ndio anatoa. Subirini bahati zenu eboooooo.

  56. Comment by Lie on February 21st, 2009 5:07 am

    Mdau WATUBWANA my respect kwa your comment ni wivu tu unawasumbua Wabongo wengi (sio wote of course)humu ndani. Mimi si nipo hapa Bongo naelewa sana situation ya watu wengi, mishahara yao ni midogo kiasi kwamba wengi wao humu ndani hata kuwasaidia wadogo zao ni issue sasa wakiona nyie mpo huko majuu na mnapiga kazi(ambazo sio professional jobs ila zinalipa kupita wao hapa bongo basi ni shida tupu) wanaona wivu kwamba wao wapo ma ofisini na kimshahara kidogo na akitoka kazini akadandie dala dala (maana sio kila mtu ana gari) duhhh na haya majasho ya bongo basi si unajua tena mdau wivu lazima uwepo. Mimi nina dada yangu kaolewa huko majuu we misaada kwa sana, sisi wote wadogo zake tumesoma CBE,IFM kwa msadaa wake (na sasa tumemaliza wote tunamshukuru kweli kweli, sasa kama dada yangu huko ulaya anabeba mabox au anafanya cleaning jobs..who cares ili mradi anafanya kazi ambayo it is legal na sio vinginevyo..NYIE MA HATERS ACHENI NDUGU ZETU WABEBE MABOX ILI WATUSAIDIE..pum&vu zenu acheni wivu..jamani wote mlikuwa majuu jamani msisahau wadogo zenu hapa Bongo hao Ma HATERS ni wakupita tu na mawivu yao.. kaka FA angalia mbele tu na piga shule yako.HATERS WAPO NA WATAKUWEPO KILA SIKU CHA MSINGI IGNORE THEM fanya kama hawapo vile sawa?

  57. Comment by Ross on February 21st, 2009 9:11 am

    Mimi Mbaka nione cheti, huyu Bishoo aisje tudanganya hapa!

  58. Comment by watubwana on February 21st, 2009 10:14 am

    asanteni sana ndugu zangu,tunashukuru kwa kutupa moyo wenzenu.tunawaomba muwasisitize WATANZANIA wenzenu walioko huku majuu wasome na wakumbuke walikotoka.wengine huku hawana mbele hawana nyuma,shule wengine wameacha,hawasomi,viza zao zimeisha kurudi hawataki wanajuwa wenyewe wanavyoishi,na wengine kila mwaka wanarudia tu
    kile kile sababu hawako serious na masomo.kazi kusemana semana ovyo tu,UMBEA na KUCHUKULIANA wanaume na wanawake.kujifanya kwenda na wakati kuparty kwa sana na kujisahau kitu gani kilichowaleta,ukiwatizama walikotokea anajua MUNGU,na wengine kujifanya kwao mambo safi sanaaaa,ACHENI hizo,kama wazazi wako wanapesa ni zakwao SOMA UTAFUTE ZAKO.wengine kupenda miteremko tu nakupenda kuhudumuwa na kuishia kufanya umalaya,kuptiwa na kila kabila duniani,kazi hawataki kufanya,mnaona ufaharii kufanya umalaya??SIO MNAKUA MIILI TU KUWENI NA AKILI pia.
    FA KAKA waepuke sana WATANZANIA WENZAKO WASIO NA MWELEKEO,WATAKUPOTEZA HUKU.ni mtazamo tu KAKA

  59. Comment by EDDY on February 21st, 2009 10:07 pm

    Inawezekana kufanya MSc moja kwa moja, lakini ni mara chache sana kwa watanzania kufanya Masters moja kwa moja hata wenye degree za mlimani wengi wakija huku Ulaya au America wanashariwa kufanya Postgraduate Diploma then Masters, kuhusu Advanced Diploma kuwa equivalent na degree hilo halina ubishi ni kweli kabisa, ukienda USA au Canada, hata hapa UK ziko body zinachambua elimu za nje na Advanced diploma inawekwa katika group ya first degree. Mimi nilisoma IFM AVANCED DIPLOMA IN BANKING sasa hivi nina Masters in Business Administration toka University of Salford Manchester, my wife as well ana two masters za UK university na alisoma IFM pia. kuna walimu kibao hapo IFM walisoma hapo advanced diploma na sasa ni maprofesa na PhD holders walikuja huku kwenye vyuo vya UK, pia nimeona watu wengi tu wenye degree za mlimani wakianza na postgraduate diploma then masters, NI VITU VINAWEZEKANA TU. HAPAUK PI UPO UWEZEKANO WA KUFANYA MASTERS HATA BILA DEGREE YOYOTE.

  60. Comment by Nice2 on February 22nd, 2009 6:28 am

    Ha ha ha haaa,tangu tumembaini Mr. Degree kwamba alifeli IFM naona automatically amekua disqualified kujadili maswala ya elimu. Pole sana, mtandao ni mpana, you can run but you can not hide…..

  61. Comment by sisterTZ on February 22nd, 2009 9:06 am

    Please shake off the haters haraka sana…na tuwazomee hiyo mi HATERS hioooooooooooooooooooooo

  62. Comment by sisterTZ on February 22nd, 2009 9:16 am

    WEWE unayejiita umenichekesha sana..eti wengine wanajifanya eti mambo yao safi huku Bongo..wengi ni waongo..na mbaya zaidi wengi wao wazazi wanaitaji msaada wao na wao wapo ulaya wanafanya ujinga (na umalaya) na hata senti tano hawawaletei family zao…kuna kijana mmoja eti alikuwa anamuomba mama yake amtumie pesa kutoka DAR kwenda UK yaani alichekesha jamii huyo…KWA TAARIFA TU NYIE MLIOKUWA ULAYA, kumbukeni wazazi wenu huku bongo maaana wengine wamechoka sana jamani mpaka wanatia huruma. Mimi na wajua watu kadhaa ambao watoto wao, wapo majuu wazazi wao wameshaacha hata kuwazungumzia bec hawasadie hata chembe…tunajua maisha ya Ulaya ni mgumu lakini ndio hivyo bwana sisi ni wabongo lazima usaidie kwenu KUMBUKENI MLIKOTOKA…na nyie msiowasadia ndgu zenu wazazi wenu wanachekwa huku bongo…

  63. Comment by sisterTZ2 on February 22nd, 2009 9:26 am

    MIMI kazi yangu inanilazimu kusafiri mara kwa mara kwenda USA na Europe (yaani i had the feeling waTZ wengi walioko Ulaya at least wanasoma na kujielewa wanachofanya)…Ila nilievyoenda for 3 months US niliwashangaa wabongo na wakenya pia wanavyoishi jamani, wengine wanaume eti wanasuka nywele na kuwa na tabia za (wenyewe wanase ki nigga)na kuvaa suruali chini ya matako, kunywa pombe na madawa ya kulevya. Na shule ndio kabisa hawaendi na visa zao zimeisha. Basi wakati wa kuondoka zangu kurudi DAR nikawaambia sasa mna mzigo gani wa kupeleka TZ (hapo i meant kama wanavijisenti kidogo kwa ajili ya wazazi wao)…majibu niliopata ni kasheshe tupu wengi walidai eti pesa walishatuma kwa westen Union hmmmmmmmmm???…nilivyofika DAR wazazi wao wakaniuliza vipi vijana wetu uliwaona??..nikajibu ndio, ila wameniambia wametuma mizigo yenu kwa westen union na posta..hao wazazi husika wakaa kimya na mimi jibu nikapata..si mnajua tena utu uzima. Nyie mlikuwa nchi za watu jaribuni kutafuta maisha na sio kucopy tabia za watu esp tabia mbaya..kama kucopy tabia tucopy vitu vizuri ktk nchi nyingine na sio mabaya… duh naona jina SisterTZ linamtu so mimi ni SisterTZ2

  64. Comment by simple on February 22nd, 2009 7:09 pm

    @ sisterTZ2
    1.MIMI kazi yangu inanilazimu kusafiri mara kwa mara kwenda USA na Europe (yaani i had the feeling waTZ wengi walioko Ulaya at least wanasoma na kujielewa wanachofanya) – SIFA ZA KIJINGA kucross continents siyo issue siku hizi
    2.Basi wakati wa kuondoka zangu kurudi DAR nikawaambia sasa mna mzigo gani wa kupeleka TZ (hapo i meant kama wanavijisenti kidogo kwa ajili ya wazazi wao)…majibu niliopata ni kasheshe tupu wengi walidai eti pesa walishatuma kwa westen Union hmmmmmmmmm??? – UNAFIKI
    3.nilivyofika DAR wazazi wao wakaniuliza vipi vijana wetu uliwaona??..nikajibu ndio, ila wameniambia wametuma mizigo yenu kwa westen union na posta..hao wazazi husika wakaa kimya na mimi jibu nikapata..si mnajua tena utu uzima – UMBEA HUO WEWE UMEULIZWA MLIONANA HAWAKUULIZA WAMEKUPA CHOCHOTE AMA?
    4.Nyie mlikuwa nchi za watu jaribuni kutafuta maisha na sio kucopy tabia za watu esp tabia mbaya..kama kucopy tabia tucopy vitu vizuri ktk nchi nyingine na sio mabaya – UMEONGEA POINT YA MAANA
    inaelekea wewe mwenyewe ni hater wa kichinichini maneno yako yanakusuta dada wa kitanzania namba mbili

  65. Comment by KAKA MKUBWA on February 23rd, 2009 12:22 am

    MSIACHE KUONGEA

  66. Comment by Bingo on February 23rd, 2009 1:14 am

    Dogo hongera sana. inaonekana una kipaji, kukamua shule mamuziki si issue ndogo. inabidi wakina dudubaya, mr nice nice na wengine wajifunze kwako.

  67. Comment by Azeez on February 23rd, 2009 1:32 am

    Hey guys mambo vipi?
    i was following hii discussion yenu hapa and then i came to find out that you are no good but good hypoctrites.
    Ni lini wabongo tutajifunza not to comment kama hatujui?most of the guys do not know the system of education ya Tanzania na England and then wana comment ili waonekane wanajua kuongea.

    Back to the story, FA yuko eligible kupursue masters abroad for two crucial reasons.
    First if you have Advanced Diploma hiyo ni equivalent to Bachelor and u can enroll into masters kama umeperform vizuri. Na ikiwa hukufanya vizuri then utaanza na PGD(post graduate diploma before you are enrolled.

    second reason ni kwamba ingawa tuna system inayoshahibiana na UK it doesnt mean we are the same,wenzetu wanaruhusu pia mtu kuenroll for collage/uni after graduating secondary school, again this depend on your performance..
    SASA ni akina ambao kwa umbavu wao wa kutopenda SHULE wanacomment kuhusu enrolment ya mwanaFA?
    Ifike pahali wanaopenda shule wapewe support, wasanii wenu wasipokwenda shule mnawaponda wakiamua kwenda bado mnachonga,sasa sijui mnataka nini?

    FA,u dont have to listen to these morons, they pretend to know things they dont know. i usually stay away from discussion of this type, but this one forced me to say something because ignorants are likely to take the lead..and as a part of educated community i would let them destroy NO the effort of those who want to join in this BIG IN THE WORLD BUT SMALL COMMUNITY IN TANZANIA.(Community ya waliosoma)

    Wise Say:”THE MORE YOU KNOW THE MORE YOU KNOW THAT YOU DONT KNOW”

  68. Comment by Bwax Bwizo(B Bwax) on February 23rd, 2009 4:07 am

    Hey
    B
    Whatz up! plz take out all Haters and do what u think can make ur future to Better.
    coz no 1 can pay any thing from there in case of support! so keep it Real Niger
    its me ur homie
    B 4 real,as usual

  69. Comment by mr degree on February 23rd, 2009 5:34 am

    ……..Comments zangu zote hazijaeleweka sababu nchi ya Tanzania imejaa wajinga wasiojua ku reason. any way, Time will tell then, tutajua kama certificate na advance diploma ya insurance ni njia ya kumpa mtu Msc!

  70. Comment by jaki on February 23rd, 2009 6:16 am

    we mr degree s***w urself! i dont know why is it so hard for u to understand a very simply thing that every1 else has been saying over and over to u! A.Diploma is equivalent(notice the word equivalent) to a degree! if u posses first class, upper second class u are eligible for admission!and by the way im shocked at ur inability to noticed something very obvious, IFM is an institution of FINANCE, and ur talking about FA doing Insurance?! get ur facts together and do ur homework..dont just make judgements inappropriate!

  71. Comment by Riziki on February 23rd, 2009 8:12 am

    mmh mr degree stop hating na tunasikitika kutuita watanzania wenzako wajinga but hapana anayeonekana mjinga ni wewe usiejua mambo tupo in real world mi nimesoma IFM na sasa nachukua MSc in finance hapa UK sasa kama wewe umesoma hiyo MSc kwanini unajiita mr degree instead of mr MSc? stop hating… binamu keep up ni jambo la kawaida sana katika dunia yetu hii ya leo watu kutopenda maendeleo ya wenzao kama mr digrriii,sophie uliempa kibuti na msongo…. wivu tu hawana lolote!!!! all the best binamu tuko pamoja and above all God is on top of u there is nothing those haters can do!!!!

  72. Comment by Mattylda on February 24th, 2009 1:50 am

    Humu kuna mambo jamani lol!!!!!
    Mwenzenu sijapita hapa siku nyingi naona mandhari imechange ohhh jamani atleast lakini flavour haijawa nzuri kama ya kale sorry BC ni macho yangu!

    Pole sana Sister Tz kwa kuibiwa jina lol!i don want to remember those days jina la matty lilivyotokea kupendwa hahahahahaha nicheke mie!

    Binti-mzuri upo?Any je?Halima??missing u guys.

    Back to topic Mwana Fa KAMUA BABA KWA RAHA ZAKO KULA BUKU acha waseme mchana usiku watalala haijalishi elimu elimu tu iwe ya kuunga unga au iwe mnyoosho mradi kufika,ALL THE BEST!

  73. Comment by WA WOTE on February 24th, 2009 5:17 pm

    TUFUNGE MJADALA FA PIGA SHULE KAMUA RUDI BONGO DAKA KAZI YA MAANA TESA….ACHANANA HAO WAZUSHI WA UK..kwanza wamekudhulumu hela yako ya SHOW..hawana dili hao…hivi usaanza kitabu kukamuaaaaa…

  74. Comment by KABEYA on February 25th, 2009 7:22 am

    FA, Big up,Keep it up.Ni kawaida watu kuchonga.Yesu aliponya viziwi,vipofu na hata kufufua wafu lakini walimkill.Ziba masikio soma

  75. Comment by Annie on February 26th, 2009 7:09 am

    Big up, FA. Kwanza nakupongeza kwa kufika apo ulipo na kwa kusoma pia. Kitu kimoja nachotaka kukwambia ni kwamba usisikile maneno ya watu… watz tunapenda kuongea sana na mtu akisonga mbele lazima tu kitaongelewa kitu. cha msingi wewe ni fanya mambo yako na umshumkuru Mungu alipokufikisha apo ulipo thats all. “Dont listen outside”

  76. Comment by kelvino_ on February 26th, 2009 9:42 am

    BIG UP FA,wameongea mengi juu yako lakini wabongo wenzangu ni kwamba inawezekana FA ndo atakuwa miongoni mwa wanamziki wa Bongofreva ambaye amepiga shule akimaliza masomo yake,coz wapo wachache ambao wana degree e.g simple x

  77. Comment by Sting on March 27th, 2009 6:10 am

    Watz up bongo ppl wat’u @!
    Big up 2 Binamu 4 wht u decided to do broda!
    Bongo ppl let our fellah FA do wht he gat 2 do n lets pray 4 hs success instead of dissin hm! We gat 2 shoot fe**k ni**”@z like so called MR DEGREE! Snitch n**”@Z lik u deserve to die!
    Lets cheers 4 our BONGO Celebrity n not diss em like tht! big up once again FA.
    We been 2gether out thr @ IFM i was pursuing ADIT. Now am workin thn after i will tak ma masters in Business Adm with IT. Simply coz i got an UPPER SECOND CLASS!
    Fu@***%k HATERZ.

  78. Comment by Ben on April 28th, 2009 7:27 am

    Big up Fa vijana tupo nyuma umefanya yanayowezekana kwa wanaioweza ila kwa wasioweza yatabaki majungu na fitina.Coventry si mchzo wachache wanaofika na watakaofika

  79. Comment by mima on April 24th, 2010 8:44 am

    FA uko juu kaka,cha ajabu nini kufanya masters?kama inakuuma andamana,acheni majungu kutaka kumchokoa mtu mpaka kwenye viatu haihuuuuuuuu!

  80. Comment by Jane Honosily on June 30th, 2010 5:48 am

    Big up FA!!!!KEEP ON ROCKIN MAN!!!!

  81. Comment by George on August 23rd, 2010 7:18 am

    THATS SO GREAT FETTY, YOU DOING SO FLEVE!!!!!

  82. Comment by freddy on April 18th, 2011 8:48 am

    drop dem down B.I.N.A.M.U

  83. Comment by stanslaus on November 20th, 2011 11:09 am

    na kukubali huigi mambo ya njee upo poa kaka
    ila oa kwanza

  84. Comment by orlando on December 24th, 2011 3:38 pm

    MwanaFA nakumbuka enzi za Mabinti Damu damu… me myself nakukubali!

    keep it up Bro!

Leave a Reply