huskiesbc

Yapo mambo mengi hapa duniani ambayo hatuwezi kuwa na uhakika nayo.Lakini yapo machache ambayo tunaweza kuwa na uhakika nayo.Mojawapo ni kwamba kijana Hasheem Thabeet anafanya vizuri katika mpira wa kikapu vyuoni nchini Marekani.Anaendelea kuwa “balozi” mzuri wa Tanzania kupitia michezo.

Majuzi nilipata nafasi ya kuongea naye machache. La msingi nililotaka kujua ni mipango yake kuhusu kujiunga na ligi ya NBA hapo mwakani. Hasheem anasema ni mapema bado kuliongelea swala hilo kwani hivi sasa anajaribu kuelekeza nguvu na akili yake katika michezo ya vyuo inayoendelea huku timu yake,maarufu kama The Huskies (kama wanavyoonekana pichani) wanaendelea kufanya vizuri.Hivi sasa wanatajwa kuwa miongoni mwa timu bora kabisa za mpira wa kikapu za vyuoni nchini Marekani.

Kesho(Jumamosi) saa nane mchana kwa saa za mashariki (2:00pm Eastern Time),The Huskies wanapambana na vijana wa Notre Dame katika mchezo wa marudiano.Katika mchezo wa kwanza The Huskies walishinda kwa vikapu 69-61. Mchezo wa kesho utaonyeshwa katika vituo vya CBS na vingine vingi vya michezo.Kila la kheri.

Update: Mchezo umekwisha na The Huskies wameshinda 72-65. Good job Hasheem na wenzako.

Feedback / Comments

19 Responses to “HASHEEM AND THE HUSKIES!”

  1. Comment by Mubelwa T Bandio on February 27th, 2009 7:19 pm

    Well! Kwa kila anayefuatilia michezo hii anajua uwezo wa Hasheem. Anafanya vema sana na hili si la kupinga. Ukiingia kwenye upigaji kura wa wachezaji wanaofanya vema utamuona. Na hata katika kuonesha michezo hiyo, huwa wanamuongelea na kumuonesha sana. Alikuwa na tatizo ama mapungufu ya kutoutumia urefu wake kwenye offensive rebounds lakini sasa anaelekea kunakotakiwa. Kama alivyosema, japo anafanya vema saana akiwa na The Huskies ambao ni timu namba moja katika nranking za vyuo, bado anahitaji mambo machache kabla hajatinga NBA kwa kishindo. Si unakumbuka ulivyokuwa m’babe ukiwa la saba halafu ukiingia form one unaonekana goloko?
    Keep it up H. T

  2. Comment by mr degree on February 28th, 2009 1:41 am

    ameanza kulikana jina la HASHIMU THABITI,mwisho ataukana na u tanzania huyo bishoo!

  3. Comment by Dinah on February 28th, 2009 5:59 am

    Nenda kijana wangu nendaaa!
    Mr degree hajalikana jina lake bali wanamuita na kuliandika linavyotakiwa (vinginevyo wangemuita “Hashaimu”) Mf ni Karim(Kareem)…Salim (Saleem)…Said(Sayeed)…Juma(Jumaa),Hassani(Hassan), Yusufu(Yusuph),Haruna(Haroon) n.k

    4 once watanzania jivunieni vijana wenu wanapofanya vizuri nchi za watu…..wakivuruda kelele, wakifanya vema fujo na name calling mnataka nini sasa?

    Kuweni wazalendo….Angalia Uingereza wanavyojivunia watu wao wanaowawakilisha US na ni kanchi kalikoendelea kuliko sisi TZ.

    Ni ushauri…..msinitoe macho!

  4. Comment by Ole Sendeti on February 28th, 2009 6:22 am

    Annony 1:41 am, acha kashfa hilo jina amepewa huko America wana tendency ya ku-americanize names to b readable properly with english alphabets!

  5. Comment by Mgugule on February 28th, 2009 7:09 am

    Mhuuu kuna kitu hapo Mr,Degree ana sababu zake binasi huyo. TAHADHALI asije Akajikana Jinsia yake hapochacha patakuwa patamu.

  6. Comment by sisterTZ on February 28th, 2009 7:36 am

    Wewe Mr. Degree vipi wewe??..hata kama Hashimu kwa sasa inaitwa ´Hasheem´ why not?? (nothing wrong with that kwa mtazamo wangu) mbona huko Hollyhood ma Star wanabadilisha majina for the sake of kutafuta pesa?? Acha wivu wewe…vile vile acha m-TZ mwenzetu apate pesa ya maana na sio kubeba mabox ebooo

  7. Comment by SISI on February 28th, 2009 7:39 am

    Mdogo wetu HASHEEM hongera sana bwana soma zako hiyo College na pia cheza zako kikapu kama kawa,that is the way to go bwana

  8. Comment by Edo on February 28th, 2009 8:10 am

    hongera mtanzania mwenzetu,sasa wewe hapo juu alikuambua amelikana hilo jina acheni kuchafuliana,

  9. Comment by kamau on February 28th, 2009 9:16 am

    Kila la kheri Hasheem Thabeet,nadhani ilibidi wabadili jina lake linavyoandikwa ili waweze kulitamka barabara. Mfano wangeandika Hashimu lingetamkwa hashaimu na thabiti lingetamkwa thabait kiasi kwamba lisingeleta maana,kwa hiyo mdau acha tu liandikwe hasheem thabeet na wala c ubishoo kama ulivyosema

  10. Comment by Mzee wa ££££ za kutosha on February 28th, 2009 7:54 pm

    hahahaha longo longo kibao, kwani sikila m2 na maisha yake jamani, kijana anatupeperushia flag letu wandugu.
    Kalagha bao.

  11. Comment by mr degree on March 1st, 2009 1:33 am

    wewe unayesema wamarekani wana tendency ya ku-americanize names to b readable properly with english alphabets unasemaje kuhusu DIKEMBE MUTOMBO? mbona hawakosei kulitamka jina hilo na mkongo huyo hajaondoa hata herufi moja kwenye jina lake la asili? hamuelewi kama jina ni identity? nyinyi endeleeni kujivunia lakini sisi wenye kawaida ya kuhoji tushagundua tatizo hapo! hata ukimsikiliza vizuri inteviwes zake utagundua kitu hicho! anaji-americanize mpaka anaboa!

  12. Comment by PJ on March 1st, 2009 5:21 am

    Hasheem kaka hongera sana..songa mbele tatufa pesa yako ya nguvu bwana..

  13. Comment by JoJo on March 1st, 2009 10:33 am

    Jina,jina ninii?
    Madaktari na mawakili mnawachagua kwa majina au ujuzi na uzoefu?
    Isitoshe majina yetu mengi si ya kiafrika au kikabila asilia?
    Mungu ndiye anagawa vipaji,na kila mtu ana chake.
    Acheni unafiki,muda mnapoteza wakwenu wenyewe
    mwenzenu anfurahia ndoto yake awe Hasheem au Hashimu yote sawa.
    Taifa halitasonga mbele kwa kujadili majina ya watu!
    Uchumi na afya zenu unaendaje miaka ishirini
    ijayo wanenu WATASOMA wapi?

  14. Comment by babuu on March 1st, 2009 12:15 pm

    huyu mr degree sjui ana matatizo gani?ye lazima aponde tu,mjinga sana..sina hakika ye anafanya shughuli gani hapa!bwana BC,hebu mtafute nae uweke mahojiano yake hapa tuone kama anastahili kujadiliwa hata kwa sentensi 1..sababu ya kueleweka umepewa..hasheem ni hashim tu kutegemea na matamshi ya lugha husika..jamaa kakwambia hapo lingeandikwa hashim wangetamka hashaim,now sema dikembe wangekoseaje?wangetamkaje?hawakuwa na shida ya kuliandika vingine sababu walikuwa wanaweza kulitamka.hata kareem abduljabar ni karimu ufahamu!acha kuwa HATER,mbwa wee..

  15. Comment by babuu on March 1st, 2009 12:21 pm

    bingwa la haters mr degree(ya kuhate nadhani) unakera sasa,huvumiliki..naona huwezi kubali wenzako waking’aa,unatia kinyaa kwa wivu wako wa kike huo..eti hata ukisikiliza interview zake utagundua,amesema nini cha kuuponda utanzania na kuutukuza umarekani kwani?acha upumbavu,muunge mkono..besides huna cha kufanya kumzuia wewe.

  16. Comment by Mattylda on March 2nd, 2009 1:00 am

    yaiiiii wivu kidonda ukishiriki utakonda litakaye mchoma kwakweli ajipange upya next time!!!!!!!!!!!!!!!!
    back to topic Hasheem wewe mrefu jamani kuliko wote hapo pichani safi sana dogo kamua!!!!!!!!!!!

  17. Comment by jakize on March 2nd, 2009 1:35 am

    Safi Hasheem inavutia sana!,Watu kama akina mr degree lazima wawepo ili watu wafanikiwe zaidi

  18. Comment by kasava on March 3rd, 2009 12:18 pm

    tunamtaka wema alivyopelekwa segerea na ualibifu wa mali

  19. Comment by PJ on March 3rd, 2009 4:45 pm

    Jakize na babuu mnajua watu kama MR DEGREE mie ndio nawapenda sana bec due to their being haters ndio wana ni drive nijitaidi kupata maendeleo zaidi (they are just driving me to do better no to do my best ability) ndio maana achana nae kabisa. Hasheeem mdogo wetu watu kama MR DEGREE wanakuonea wivu so work harder to prove them wrong.

Leave a Reply