ddcNi ijumaa tena.Mwezi wa pili ndio tunaupa kisogo taratibu.Kwa maneno mengine,mwaka 2009 ndio umeshaanza kuyoyoma tayari kabisa kuukaribisha 2010 mwaka ambao kile kipute cha Kombe la Soka La Dunia kitapigiwa nchini Afrika Kusini au “Bondeni” kama baadhi ya watu wanavyopenda kupaita. Kama una mpango wa kushuka “Bondeni” hapo mwakani,kumbuka tu kwamba tiketi zimeshaanza kuuzwa. Tembelea tovuti ya FIFA ili kujua taratibu zaidi.

Kama kawaida Ijumaa ni siku yetu.Ni siku ya Zilipendwa.Leo tunao DDC Mlimani Park ambao hivi karibuni wataanza kujulikana kwa jina la Mlimani Park bila maneno DDC pale mwanzoni.Sababu?Kama ulipitwa unaweza kusoma hapa ili twende pamoja.

Wimbo unaitwa Hiba. Ni lalamiko la penzi.Nini husababisha mke au hata mume kubadilika? Ni nani wa kulaumiwa?Pata burudani.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Feedback / Comments

One Response to “HIBA-DDC MLIMANI PARK”

  1. Comment by BLACKMANNEN on March 6th, 2009 3:38 am

    Wazee kama hawa DDC Mlimani Park, tukiwaacha na ZERO – Maoni, ni noma sana. Kwa sababu wimbo “Hiba” umetulia, na una maneno mengi yaliyoimbwa katika wimbo huo, yanatuhusu sana sisi wote, wanaume na wanawake katika mahusiano yetu kimapenzi.

    Mimi leo nitaongelea kidogo upande wetu sisi wanaume wa Kitanzania na pengine Afrika.

    Wanaume wengi wa Kitanzania, hawana mazoea ya kuwaita wake zao “MPENZI” kama wimbo wa Hiba, unavyoimbwa.

    Mara nyingi mwanaume humwita mwanamke “mpenzi”, yule mwanamke ambaye ndiyo kwanza wameanza mahusiano. Lakini baada ya mahusiano yao kudumu kwa muda mrefu na pengine kuoana. Neno “MPENZI” hubadilika, na jina la “WEWE” huchukua nafasi yake.

    Mwanaume anaona shida kumwita mke wake “Mpenzi”, na kwa baadhi waliojaliwa kupata watoto, badala yake, hutumia majina ya watoto wao k.m. Mama Wema au Mama Kanu n.k, lakini wasiobahatika kuwa na watoto jina lao linabaki kuwa “Wewe”, basi. Ingawaje basi mtu umwite basi mkeo kwa jina lake, badala ya kumwita “wewe”.

    Baadhi ya wanaume wa Kitanzania, hawaombi radhi kwa wake zao wanapokuwa wamewakwaza kwa hili ama lile, kama wimbo wa “Hiba”, unavyoimbwa. Badala yake wanauchuna na kuonyesha uso wa ukali ili kuzima soo, asiulizwe kosa alilolifanya.

    Mwanamke anapouchuna, na anapotaka na yeye kuitumia silaha yake kali, aliyojaaliwa na Mwenyezi Mungu, kwa kulala na “KUFULI”.

    Mwanaume hugeuka mbogo, na humgeuzia mkewe kibao kwa mateke na magumi, na mwisho wa yote, unakuwa ni ugomvi mkubwa wa kuita wasuluhishi kutoka nje. Mtu anaumizwa viungo vyake na mtu mwingine kwa kitu chake mwenyewe, alichopewa na Mwenyezi Mungu.

    Katika nyimbo nyingi za zamani kama huu wa “Hiba”, kuna mambo mengi sana ya kujifunza, na ni vizuri sana tunapowekewa nyimbo hizo hapa BC, ni vizuri kuzisikiliza na kuzitafakali kwa undani.

    Mafunzo ya nyimbo hizi yatatusaidia kuwafunza watoto wetu ambao, hatuna nafasi ya kuwasimulia mambo mengi yahusuyo tamaduni zetu. Watoto wanakuwa na maadili yasiyofaa na bila ya kuwa mwelekeo mzuri wa kimawazo na maendeleo. Wanaishia kubwia unga.

    Pia, sisi wanaume, huu wakati wa utandawazi ni wakati muafaka wa kubadilika kimawazo na kuachana na tamaduni zisizofaa. kama vile kwa kuwadharau wanawake.

    Mwanaume eti, hujiona kadhalilishwa na kutukannwa matusi ya nguoni, anapolinganishwa matendo yake kuwa kama “Mwanamke”. Je, wanaume wenzangu, mtu kuwa mwanamke ni vibaya? Au ni tusi? Mwanamke sio binadamu kama alivyo mwanaume? Naomba majibu yenu….!!!

    It’s Great To Be Black=Blackmannen

Leave a Reply