jk123bc

Maisha ya ndoa ni safari ndefu.Wengi waliomo ndani ya ndoa wanakiri kwamba ni safari ndefu,ngumu inayohitaji uvumilivu na umakini wa hali ya juu lakini pia yaweza kuwa safari yenye kila aina ya raha na mafanikio.

Ndio maana unapotimiza mwaka au miaka fulani katika ndoa,ni jambo la kheri na linalostahili kusheherekewa.Hivyo ndivyo ilivyokuwa hapo jana wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Salma waliposheherekea miaka 20 ya ndoa yao.

Sherehe hiyo fupi ilifanyikia Ikulu jijini Dar-es-salaam na kuhudhuriwa na ndugu,jamaa na marafiki wa karibu wa “First Family” ya Tanzania.Pichani ni Rais Kikwete akimlisha keki mkewe Salma kusheherekea kumbukumbu hiyo.BC inaungana na wote wanaowatakia kheri kuwapongeza na kuwatakia kila la kheri katika maisha yao.

jjb

Naitwa…

jjb2c

Photo/Kennedytz

kilangobc

Hivi karibuni,Marekani,kupitia ubalozi wake nchini Tanzania,ulimtunukia Mheshimiwa Anne Kilango,tuzo ya Mwanamke Jasiri kwa mwaka wa 2009.Tuzo hiyo ambayo hutolewa kwa wanawake ambao wameonyesha ujasiri na uimara katika uongozi,imemwangukia Mheshimiwa Anne Kilango kutokana na juhudi zake za kupinga ufisadi na kukabiliana nao bila uoga.

Mheshimiwa Kilango ambaye ni mke wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania,Mheshimiwa John Samwel Malecela, ni Mbunge wa Same Mashariki mkoani Kilimanjaro kupitia chama tawala cha CCM.

Pichani ni Mheshimiwa Anne Kilango akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania,Larry Andre. Pembeni ya Anne Kilango ni mumewe,Ex-PM,John Malecela.

Tunampongeza Mheshimiwa Anne Kilango.Hongera,unastahili.

sadc

Viongozi wa nchi za SADC wanakutana huko katika jumba la kifalme la Lozitha huko nchini Swaziland,kusini mwa bara la Afrika.Rais wetu,Jakaya Mrisho Kikwete(kama anavyoonekana pichani) ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria.

Mojawapo ya mambo muhimu yaliyopo juu kabisa kwenye ajenda ni suala la kujaribu kuisaidia Zimbabwe ambayo uchumi wake umeyumba kupita kiasi na pia kuzungumzia hatua za kuichukulia nchi ya Madagascar ambayo hivi karibuni imepitia “mapinduzi”.

Pamoja na hayo,mijadala kadhaa imezuka mtandaoni kuhusiana na “fashion statement’ ya Mfalme wa Swaziland.Wengine wanasema alistahili kuvaa suti kama wenzake ili aonekane kuwa “serious” na mambo kama hayo.Wewe unasemaje?Ni kweli kwamba kuvaa suti ndio kunafanya mtu aonekane “serious”?

Na je hivi ukitokea mwaliko unaoamuru kwamba kila kiongozi avae vazi lake la Taifa(vazi la Mfalme Mswati ni la kitaifa kwa Mfalme) wa kwetu atavaa nini au ungemshauri avae nini?

handsomebc

Bila shaka umezoea zaidi kusikia mashindano ya urembo/uzuri yakiwalenga zaidi kina dada au kina mama.Hilo lisikudanganye kwamba mashindano ya kina kaka au kina baba hayapo nchini Tanzania.Yapo.

Hivi majuzi pale New Africa Hotel jijini Dar-es-salaam,palifanyika shindano la kumsaka The Most Handsome Man in Tanzania au ukipenda Mr.Bongo kwa mwaka 2009. Jumla ya vijana 11 walifikia fainali hizo ambapo mshindi aliibuka kuwa Khalid Mohamed(pichani).Mshindi huyo ambaye bila shaka ndio ashaanza kuingia katika lile kundi la “umaarufu”,alijipatia zawadi ya US $ 1000 na shopping ya uhakika katika maduka ya Zizzou Fashion.

handbc

Majaji wa shindano hilo walikuwa Steven Kanumba, Christina Isabbela na Richard ambaye alikuwa mshindi wa Big Brother 2007.

Picha zote kwa hisani kubwa ya John Bukuku

dokiiNatumai hujamsahau. Jina lake halisi ni Ummy Wenceslaus.Kwa mashabiki wa sanaa ya uigizaji ukimtaja kwa jina la Dokii watakuelewa kirahisi zaidi. Enzi za kikundi cha uigizaji cha Mambo Hayo, Dokii alijizolea umaarufu kwa jinsi alivyoweza kuigiza katika lafudhi ya kiswahili cha nchi jirani ya Kenya.Ilifikia mahali wengine wakaamini kabisa kwamba Dokii ni Mkenya!

Baada ya hapo,kimya kilitanda.Dokii akabadili uelekeo wa maisha baada ya “kujisalimisha kwa Bwana”.Akahamia kwenye muziki wa injili ambapo hakuna uhakika sana kuhusiana na kutamba au kutokutamba kwake.

Sasa Dokii ameamua kurejea tena kwenye uigizaji na filamu.Anakuja na filamu itakayokwenda kwa jina “Bad Friend”.Anasema katika filamu hiyo,lafudhi si ya kikenya tena bali safari hii ni kijaluo.

Yote hayo na mengine tele hususani suala zima la kuokoka na kuigiza amemueleza Eugenia Kimolo wa Tanzania Daima.Bonyeza hapa usome zaidi.

Photo/Darhotwire.

bushokebc

Jina la Bushoke ni jina linalotambulika kirahisi miongoni mwa wapenda muziki katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki na hata mbali zaidi ya hapo.Baba alikuwa muimbaji maarufu akijizolea umaarufu katika uimbaji na utunzi wa nyimbo zenye ujumbe maridhawa.Aliitwa Max Bushoke. Wapenzi wa Mlimani Park wanamkumbuka vizuri sana.Unaweza kumsikiliza baba mtu katika wimbo Ndoa ya Lazima kwa kubonyeza hapa.

Alipoamua kustaafu muziki na kuelekea nchini Afrika Kusini kwa kazi ya utangazaji,bila shaka Max alimuambia mwanawe,Rutta Maximillan Bushoke (pichani) kwamba ‘mwanangu kazi kwako’.Mtoto naye hakumuangusha.Hivi leo ni miongoni mwa vijana wanaofanya vizuri katika medani ya muziki wa kizazi kipya.

Hivi karibuni aliachia albamu ambayo inakwenda kwa jina la “Dunia Njia”.Albamu hiyo sio tu imezidi kuthibitisha kipaji alichonacho Bushoke bali pia ni miongoni mwa albamu zinazofanya vizuri zaidi sokoni. Usambazaji wa albamu hii unasimamiwa na kampuni ya Zizzou Entertainment.Mojawapo ya nyimbo zilizomo katika albamu hiyo ni ule uliotolewa hivi karibuni uitwao Inawachoma.Usikilize wimbo huo hapa chini.Wimbo uko katika yale mahadhi ya zouk fulani hivi ambayo ukiniuliza mimi nitakwamba ni “signature” nzuri ya Bushoke.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Wakati wa sikukuu ya Pasaka,Bushoke atakuwa mkoani Kagera wilayani Bukoba kwa show kabambe.Show ya kwanza inatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Linas Club na show ya pili itakuwa katika uwanja wa Kaitaba.Kazi kwenu wakazi wa Bukoba,wilaya na mikoa ya jirani.

Photo/Global Publisherz

 

chengebc1Mbunge wa Bariadi Mashariki,Andrew Chenge “Mzee wa Vijisenti” yupo matatani…tena.Safari hii ni kwa kupata ajali ya barabarani(kugonga) na kusababisha vifo vya watu wawili ambao walikuwa ndani ya usafiri maarufu kama “Bajaji”.Waliofariki inasemekana ni wanawake wawili ambao ndio walikuwa abiria katika Bajaj hiyo.Dereva wa Bajaj hajulikani alipo.

Tukio hilo limetokea alfajiri ya leo katika maeneo ya Oysterbay(karibu na nyumbani kwake).Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar-es-salaam, Afande Kova, Chenge alikuwa akiendesha gari aina ya Pick Up-Hilux yenye namba ya usajili T512 ACE.Bajaj iliyohusika kwenye ajali ina namba za usajili T736 AXE na imeorodheshwa kama mali ya Zuwena Feith Nassoro wa SLP 2595 Dar-es-salaam.

Baada ya tukio hilo,Mheshimiwa Chenge alijisalimisha katika kituo cha Polisi Oysterbay na anaendelea kuisaidia polisi.Habari hii bado inaendelea…

tancut

Leo naomba nikiri jambo moja.Kila ifikapo Ijumaa mimi hupatwa na msisimko wa aina yake.Kwangu mimi Ijumaa ni ishara kwamba bado ningali hai na ndio naelekea kuimaliza wiki kwa maana ya mwanzo wa wikiendi.Huwa najitahidi kuitumia Ijumaa kama mwanzo mpya.Pia hupenda kuitumia Ijumaa kama mwanzo wa kutafakari yaliyojiri katika wiki nzima,kusamehe walionikosea,kuomba msamaha kwa niliowakosea,kuhakiki malengo ya mwezi/mwaka nk.Unaweza pia kuitumia Ijumaa kwa staili hiyo au ukipenda jumamosi au hata Jumapili kwa maana hiyo.

Naomba pia leo nikujulie hali.Mambo yanakwendaje?Najua hali ya uchumi bado ni tata,hauko peke yako bali tupo wengi.Cha msingi ni kwamba usikate tamaa.Endelea kupigana,endelea kuwa askari mahiri mwenye kila nia na sababu ya kushinda.Hakuna siri zaidi ya hiyo.

Leo tunao Tancut Almasi Orchestra.Wimbo unaitwa Samahani ya Uongo. Imeshawahi kukutokea mtu akakupa samahani ya uongo?Pata Burudani.Furahia wikiendi yako.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Picha kwa hisani ya Issa Michuzi.

malecela

Kama unafuatilia habari na matukio ya kisiasa nchini Tanzania,bila shaka utakuwa umegundua jambo moja;siku hizi wanasiasa wetu wanapenda sana kujongea kwenye vyombo vya habari kujielezea,kujikosha,kukanusha habari au tuhuma na pia kujaribu kuweka mambo sawa.Hapo zamani kidogo mambo hayakuwa hivi.Enzi hizo mwananchi alionekana mjinga,mbumbumbu na asiyepaswa sana kujua mambo ya serikali,uwajibikaji wake kwa wananchi na jinsi inavyoendesha mambo yake kwa ujumla.Serikali ilikuwa “sirikali”.Ni wazi,kwa maana hiyo,mambo yanabadilika.Yaliyokuwa magumu kuyajua kama vile sayansi za kurusha roketi,siku hizi yamekuwa marahisi kama vile hesabu za shule ya chekechea kwa mwanafunzi wa Mlimani!Ni mwendo wa kutajana na kunyosheana vidole.Nina uhakika mwananchi atakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuchagua ifikapo mwakani,mwaka wa uchaguzi.

Katika mlolongo huo huo wa viongozi kuweka bayana mambo kadha wa kadha,jana ilikuwa zamu ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania,Mheshimiwa John Samweli Malecela kueleza ya kwake.Amesema nini?Bonyeza hapa usome mwenyewe.

Picha/Mroki Mroki

Read the Next Page →

↑ Go Back to Top of Page