kawawa3

Hivi majuzi,Mzee wetu, Rashid Mfaume Kawawa, alizindua kitabu kinachoelezea maisha yake.Kitabu hicho ambacho kimeandikwa chini ya usimamizi wa Mkuu wa Chuo Cha Mwalimu Nyerere Cha Kivukoni,Prof.John Magoti,kimepewa jina la Kawawa.Uzinduzi huo ulifanyikia Ikulu jijini Dar-es-salaam.

Ingawa tunaweza kusema imemchukua muda mrefu sana Mzee Kawawa kuandika kitabu chake,ni lazima tumpongeze sana kwa uamuzi wake huo ambao sio tu wa busara bali pia ni mfano wa kuigwa.

Tulipofanya mahojiano na Mheshimiwa Zitto Kabwe mwaka juzi,tuliliongelea suala la kuandika vitabu na kujisomea.Mh.Kabwe alionekana kukerwa na tabia ya viongozi wetu(na hata sisi wananchi wa kawaida) kutopenda kusoma achilia mbali kuandika! Ni utamaduni ambao tupende tusipende hatuna budi kuiga.

Uandishi ukisindikizwa na usomaji ni msingi mzuri wa maendeleo.Wenzetu katika nchi zilizoendelea ni mabingwa wa kujisomea.Miji ya wenzetu imezungukwa na maktaba. Ukiingia kwenye ndege,treni au basi sio ajabu kukuta watu kadhaa wakijisomea vitabu,magazeti nk.Kwanini wanapenda kusoma?Jibu ni rahisi;wanapenda kuongeza ujuzi,kujielimisha na hivyo kuendelea kuwa mbele katika suala zima la maendeleo.

Miongoni mwa watu mashuhuri waliohudhuria uzinduzi wa kitabu cha Kawawa ni pamoja na maraisi wastaafu Ally Hassan Mwinyi na Benjamin William Mkapa. Swali ambalo lilibakia kichwani kwangu ni kwamba viko wapi vitabu vyao? Ni lini tutasoma kitabu cha Mwinyi,Mkapa,Warioba au hata Edward Lowassa na wengineo?

Ni matumaini yetu kwamba Kawawa amefungua tu njia na kwamba wengine watafuata.Hongera sana Mzee Kawawa.

Pichani ni Mzee Kawawa na Rais Kikwete wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.Kwa nyuma unaweza kumuona Rais Mstaafu B.W.Mkapa.Picha kwa hisani ya Ikulu.

Feedback / Comments

13 Responses to “HONGERA “SIMBA WA VITA””

  1. Comment by Emily on March 1st, 2009 11:25 am

    This is good news… very important for our leaders to do this. Hapa tunaweza kuelimisha vijana, at the same time kuwaambia umuhimu wa kujisomea. Huu ni mfano wa kuigwa kwa wakubwa na wadogo.

  2. Comment by mtanzania on March 1st, 2009 11:48 am

    Viongozi wa zamani kama mzee kawawa walikuwa ni waadilifu ndio maana hanajitoa kuandika hishoria za maisha yao. Lakini hao viongozi wengi wa sasa watakapoandika tutataka waandike yote waliyofanya wakiwa madarakani mazuri na mabaya. Kwa mfano: Mzee Mwinyi ajumuishe sera zake za biashara huria(ruksa) na kasha za mkewe na dhahabu na mambo ya kasha kama ile ya Roliondo. Raisi mkapa ni vema azungumzie jitihada zake za kufufua uchumu, na wakati huo huo aweke wazi jinsi alivyofanya biashara akiwa ikulu na mradi wa makaa ya mawe wa Kiwila. Waziri mkuu mstaafu Ndugu E. Lowasa naye atuelezee jitihada zake za kuongeza mashule Tanzania na ugoro wake wa Richmond.
    Ninavyosema hivyo nina maana watuelezee historia zao kiunaga ubaga bila kuficha jambo ktk vitabu hivyo. Hatutaki wajisifie tuuuuu! wakati Taifa la Tanzania wamelihujumu pia.

  3. Comment by Simon Kitururu on March 1st, 2009 1:22 pm

    Hongera Mzee Kawawa

  4. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on March 1st, 2009 2:06 pm

    ….tehe tehe tehe…!!….anga kaanga mbuyu….lol…

  5. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on March 1st, 2009 2:13 pm

    ….wala sintotoa hata senti tano ninunue vitabu vya akina Mwinyi, Mkapa, Lowasa, na etc etc….

    …..bora nipeleke vijisenti vyangu vikasaidie kunywesha na kulisha watoto yatima popote pale walipo hapo Bongo…kuna nyumba nyiingi za mayatima zinahitaji msaada.

    …na kamwe sio nINUNUE vitabu vya hao mizuka….no sorry…!!!!!!!!!!!…will be a waste of money and for heavens sake where do i get the time to read such nasty and cooked up stories….!!!!!!!!…..Fed up of this. Thats my bottom line.

  6. Comment by Mattylda on March 2nd, 2009 1:10 am

    FUNIKA KIKOMBE???gues what i mean??utani umo jamani teh teh teh teh Halima unakumbuka hiyo????
    Hongera Mzee Kawawa wetu jamani,hakika wewe ulikuwa muadilifu haswaaaaaa Mungu azidi kukulinda na kukupa maisha marefu zaidi!

    Heh he hee tukisema kila mtu aandike kitabu namuonea huruma Lowasa na mkapa, sijui wataandika nini maana ni mara mie Rais wetu anaweza andika mengi mno hata ujio wa Bush Tz lol!sikwambii Maximo akipewa hiyo chance hahahahha anaweza ua band maana taifa stars toka aje ishazifunga timu kibao sina rekodi kamili pls Blackmanen kaka nisaidie kwa hili!

  7. Comment by DUNDA GALDEN on March 2nd, 2009 2:31 am

    NAUNGANA NA WALE WOTE WANAMPONGEZA HUYU MZEE WETU.KIZAZI KIJACHO KINAHITAJI KUSOMA NA KUJIFUNZA YALE MAZURI NA KIHISTORIA WALIYO ITENDEA TANZANIA NA SI VIBAYA KUSOMA MABAYA NA KUJENGA PALIPO NA HITILAFU

  8. Comment by Mzee wa ££££ za kutosha on March 2nd, 2009 5:11 am

    Hi mwanamke wa shoka wazo lako ni zuri, kwani ujue, kutokana na matendo ya ukiukwaji wa uongozi bora yanayofanywa na viongozi wengine, yanawafanya viongozi wengine kuonekana ufanyaji kazi wao ni mbovu,

    Ni vizuri kama unawazo hilo kutoa msaada kwa mlengwa moja kwa moja unakuwa na uhakika %100 umesaidia jamii.

    poa ndo maoni yangu hayo kwaleo,
    pamoja sana

  9. Comment by Mickey Jones Amos - Denmark on March 2nd, 2009 10:16 am

    HONGERA MZEE KAWAWA-SIMBA WA VITA.

    Tunakushukuru kwa kazi kubwa uliyoifanya
    kulitumikia “TAIFA” kwa uongozi bora katika upande wa “kuvumiliana” na “kuheshimu” dini zote nchini,tatizo ambalo nchi zingine zinakosa uvumbuzi na hata kupoteza maisha ya wengi.
    Sijabahatika kusoma kitabu kipya kilichozinduliwa na rais mh.Kikwete lakini nategemea kutakuwepo maelezo machache kuhusu
    kazi kubwa uliyoifanya kuweka “misingi” ya “kuvumiliana” na “kuheshimiana” katika madhehebu ya dini katika Taifa letu.

    mickey@mail-online.dk
    Copenhagen

  10. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on March 2nd, 2009 10:42 am

    Oyaa Mzee wa ££££…wazo lako ni poa na nimelipokea…Asante kwa kunijenga….lol

  11. Comment by sambona on March 2nd, 2009 3:26 pm

    Mwandishi wa habari ya utangulizi para 2 ametumia neno lazima kawawa kupongezwa kwa kuandika kitabu chake. sijui wadau kama kweli ni lazima au amekosea lugha. ni sahihi kumpongeza kawawa lakini haiwezi kuwa lazima kwa yeoyote kufanya hivyo. mawazo yangu.

  12. Comment by mr degree on March 3rd, 2009 1:22 am

    natamani kusema lakini naogopa laana!

  13. Comment by manray on March 4th, 2009 6:48 am

    The more you read the more the skills it became so tanzanians work up to build the culture reading to increase the number of literate people. gud day

Leave a Reply