
Ni wazi kwamba yapo mambo mengi sana(tena sana) ambayo wanaume wanaweza kujifunza kutoka kwa Rais wa Marekani,Barack H.Obama.Ni mengi kiasi kwamba tukianza kuyaorodhesha hapa sidhani kama patatosha.
Lakini kama wasemavyo wenzetu wa magharibi,Behind Every Successful Man, There is A Woman. Kwa upande wa Obama yupo Michelle.Hilo sidhani kama lina ubishi.Swali ambalo limejikita kichwani ni je,Michelle Obama anatoa mafunzo gani muhimu kwa wanandoa na zaidi wanawake?
Picha ya Michelle unayoiona hapo juu ndio picha yake rasmi (official potrait) kama ilivyotolewa na ikulu ya Marekani hapo majuzi.Picha kwa hisani ya White House/Joyce N.Boghosian.
Feedback / Comments
35 Responses to “MICHELLE OBAMA:ANATUFUNZA NINI WANAJAMII?”
Leave a Reply


Hapa kweli umetupatia BC.Majuzi watu walilalamika kwamba wanataka mada muhimu naona umewapatia.Nikiwa kama mwanamke nadhani Michelle ananifundisha kwanza uvumilivu na pili kumpatia mwenzangu sapoti.Kama Michelle asingekuwa muelewa wakati jamaa akikesha kwenye vikao huko vya kupanga jinsi ya kugombea useneti na baadaye uraisi ingekuwaje unafikiri.Tuvumiliane,tupendane.
wow!! Nimependa sana huyu First Lady alivyo simple….wacha bwaana!!…
Veronica (hapo juu nakuunga mkono…)….ILA sometimes wanawake wengi wanakwazika na TABIA TATA za waume zao….definately Michelle anamuelewa Obama,…(na hapa nasisistiza kuwa OBAMA amekuwa MUWAZI kwa mkewe….akisema nipo nafanya campaign ni kweli yupo hukooo kwenye campaigns na sivinginevyo….SASA kweli MIchelle atashindwa KUTOA FULL SUPPOrt….atatoa zaidi ya full support….HAPO NNDIO RAHA YA NDOA NA PENZI INAPOLALA.
…MSAIDIE MWENZIO KUKUAMINI……
…THEN life BECOMES SO SIMPLE….AND ENJOYABLE TO BOTH PARTIES….
nAWAKILISHA……BANG BANG BANG…!!!!!
BC,
Kuna mambo mengi sana mtu unatakiwa kijufunza toka kwa Michelle.Moja watu wasidhanie maisha ni lelemama.Ukisoma bio ya Michelle ni msomi aliyebobea, na alikua mentor wa Obama kazini…ktk ofisi moja ya sheria.
Kitu kingine, wanaume tusikurupe kuoa tu kwa kuangalia shepu, umaarufu wa mtu nk.Kikubwa ni kuangalia utu wa utu, uwezo, tabia.Hapo ndipo unaona genetics (chromosome) za baba na mama 23/23 zinaleta watoto bora pia akina Sasha na Malia.
Kama mdau wa hapo juu, Da Veronica alivyodokeza khs uvumilivu…ukiachilia maisha ya kisiasa, je wasichana wangapi na waume zao wapo tayari kuvumiliana katika kipindi cha mpito??
MAKULILO Jr,
http://www.makulilo.blogspot.com
wote nyie mnatuzengua tu….michele alimpa sapoti obama lakini hatujui ndani wanaishiji..kwani mbona mkapa na anna,Mkapa alivyogomea uraisi Anna alimpa support??lakini penzi lilikuwa hakuna..acheni uzushi bwaana ..michele michle na obama nao ndo wale walt tu..
hata Clinton na mkewe walikuwa wanaonekana couples wa kuigwa mpaka pale malaya walipoamua kuuza ishu zake ndo watu wakafunguka masikio! na hao inawezekana ndo hivyohivyo ila wanaficha makucha tuu kupitia siasa. kwanza nikimuangalia macho yake huyo michele namuona kama mjanjamjanja hivi sijui kama braza haibiwi hapo!
Veronica na Mwanamke wa shoka nawaunga mikono na miguu jamani huyu mama kwangu mimi ni role model wangu kabisa,very simple woman,mrembo wa nguvu aisee!
Kwakweli anaonekana ni mama mwenye msimamo na anaupendo sana na familia yake,kama ulivosema mwanamke wa shoka hawa waume zetu tuwajenge vp sasa watuamini?hapo ndipo pagumu!
kwenu kina baba/kaka kila fanikio la mwanaume nyuma yake yupo mama/dada habari ndo hiyo!!!!!!!wabishi utawasikia tu ngoja nione.
Anatufundisha kuwa wake wa marais au….
wadau hapo juu na MAKULILO Jr nawaunga mkono..Mimi binafsi nimejifunza mambo kadhaa kutoka kwa Michelle Obama. Kwanza kabisa nimejifunza kuwa mwanamke wa karne hii lazima asome (you can be everything you want to be if you decided to study) 2. Uvumilivu 3. kumsupport mwenzio (hapa pia hata kama wewe ni mume na mke ana position nzuri ni vema kumsupport) ktk masuala ya maendeleo 4. malezi bora ya watoto (maana ktk interview moja Michelle alisema watoto wake lazima watandike vitanda vyao wenyewe na wasaidie ku clean up there rooms) 4. Confidence maana juzi nilimuona anavyoingia senate kusikiliza hotuba ya mume wake jamani mama kaingia na ma-confidence 5.style za nguo she has good taste..Namtakia Michelle kila la kheri katika safari yake ndefu mungu amsaidie….
MAKULILO Jr, hapo juu umeibua hoja moja muhimu sana kuhusu issue ya uvumilivu umeuliza. JE WASICHANA WANGAPI WAPO TAYARI KUWAVUMILIA WAUME ZAO KATIKA KIPINDI CHA MPITO? Unajua ndugu yangu we are all not perfect ila nachoweza kusema mimi wanawake wengi ni wavumilivu sana…of course sio wote but asilimia kubwa..ila sasa kinachoboa ni kwamba mtu unamvumilia mume wako watika labda hana kazi au ndio hivyo tena kasimamishwa kazini ect..basi unajitaidi na kazi yako kulisha familia na kusomesha watoto unajinyima kweli kweli..ila sasa siku mume ndio karudishwa kazini au kapata kazi mpya..wee mbona pesa yake hauioni tena (anaenda kuigawa either BAR au kwa nyumba ndogo na hajali familia yake)…sasa ndugu zanguni ktk mazingira kama haya uvumilivu na upendo utakuwepo kweli??..maana hapa tusiongelee akina mama tu na wanaume nao mara nyingi hawana uvumilivu kabisa… hili ni wazo ambalo ni true story
mimi nimejifunza ktk kwa Michelle kwamba uvumilivu na upendo wa familia. Vile vile wadau mimi nadhani mume ni muhimu kuweka familia yake mbele ili kuipa familia confidence..maana Obama yeye ndio anawasomea watoto wake Bed time stories (kwa hapa bongo wadau mie mume wangu anawahadithia watoto wetu hadithi za sungura na panya)…na kuwa baba ni kuonyesha mapenzi kwa watoto na mama yao na sio kuleta pesa tu nyumbani..
Da!!! Nimeamini ndugu zangu kuwa katika kila penye mafanikio kuna mwanamke .Nakuahidi mume wangu Robart nitafanya kama Michelle Obama.
Big up sana Obama.
Hongera sana kwa website ya nguvu inavutia sana imetengenezwa kitaalam na ni kweli Michell ametufundisha mengi.
Lakini ningependa kubadilisha usemi siku hizi sio BEHIND EVERY SUCCESSFUL MAN THERE IS A WOMAN ila ni BESIDE EVERY SUCCESSFUL MAN THERE IS A MAN kwasababu siku hizi wanawake na wanaume ni equal partners in development
Kwa mtazamo wangu Michelle ananifundisha 1.Upendo kwake mwenyewe kwa maana ya kujipenda,upendo kwa mume, familia na jamii nzima kwa ujumla. Usipojipenda mwenyewe je waweza kumpenda mwingine?
2. Uvumilivu kwa maana kuwa mumewe mara kwa mara alikuwa akirudi amechoka na mara nyingi ukichoka huwezi kumpa mwenza wako unyumba. Na kuna baadhi ya sisi wanawake hilo ni kosa la jinai. Utanuna na kumsimanga mumeo ooh sasa siasa ndio imekuwa mkeo sio!
Amani. Muonekano wao tu unaonyesha ni watu wenye AMANI. Haijalishi mikwaruzano ya hapa na pale kwani hakuna ndoa isiyo na mikwaruzano. Inategemea ni kiasi gani mna deal na mikwaruzano yenu. Maana baadhi yetu wanawake hatuwezi kuvumilia makwazo ukasubiri muda muafaka na mahali muafaka pa kuongelea matatizo. Yawezekana baadhi yetu tunapayuka mbele za watoto,majirani na jamii kwa ujumla.
SHE IS MY ROLE MODEL
BC kwanza big up sana hizi ndo mada tunazohitaji. Kwanza kabisa uyo bi mkubwa apo juu ucpme, ni mvumilivu, anaejua shida za watu, mwenye upendo na ni mtu aliyeona mbali na kitu cha mwisho ni bonge la msomi alafu yuko simple kiasi kwamba uwezi amini, we angalia tu iyo picha au hata katika historia yake, nafasi kama hiyo ingekuwa kama ndio wale, wake za jamaa zetu apo bongo duh, hiyo migold na mitanzanite, na mi silver yote angevaa yeye lakini, the world 1st lady aka, neckless yake nyeupe na gauni jeusi tosha raha mustarehe. Haya jamani ndo hivyo wenye elimu yao ya kutosha na nafasi za maana umu duniani wako simple, lakini tunaotoka kwenye maisha ya kuunga unga na kupigana mizinga ya buku buku tunataka maisha ya matawi ya juu wakati, jamii inataabika, somo tosha ilo.
Bc Big up endelea kutuletea ishu za maana.
one love an all the best
Mr degree issue ya Clinton hiyo achana nayo kabisa kaka yangu usiiguse kabisaaaaa. Hillary Clinton i am sure issue ilimboa sana lakini watalaam wa Siasa walimwambia yeye atulie tu ajifanye ana msupport mume wake ktk swala hilo zima,kama kweli anataka kugombea uraisi 2008..basi mama Clinton (very smart) akasikiliza ushauri wa wataalam wa Siasa, akatulia tuli,hakuomba divorce wala nini..na sasa si mnaona mwenyewe uraisi kakosa ila position ya juu ktk Serikali amepewa.. we we acha kabisa siasa..Hillary Clinton ni lawyer bwana na she exactly knew what she wanted years ahead na siajabu alikuwa najua kwamba huyo mumewe ni f$ska..ila sasa ikabidi for the sake of her own career akae kimya, sasa hivi si mnaona wenyewe?? Ameula ile mbaya well done…vile vile Mr. Degree jana nilikuwa nasoma interview ya Michelle ktk gazeti fulani ambayo alisema kwamba marriage yake yeye na Obama is like any other marriage (it is not perfect at all) but she said,they are both working on it everyday..so inaonekana ni watu wa kawaida ambao they have the same problems like ours ktk ndoa yao…kwa taarifa tu…
kilonda A, wewe dada umenichekesha jamani yaani umeamua kabisa kumwambia ROBART utamfanyia kama Michelle Obama, my respect to you…keep it up ila na yeye sasa akukumbuke jamani maana hawa wanaume hawa..akipata pesa familia anasahau..
WA WOTE ndugu yangu kuwa rahisi sio kama mtu ndio hana matatizo..sisi sote ni binaadam we are not perfect so hayo ya mama mkapa sawa labda ni kweli but that is life ndugu yangu..and it happens to all of us maybe ya kwetu hauyajui bec we are not famous..
Wewe Mr Degree mbona mshamba sana..eti Michelle Obama anaonekana mjanjamja…wewe ndio wale wanaume wakiona mwanamke mzuri tu wanasema muhuni. Maana hiyo ndio tafsiri ya mesg yako hapo juu acha ushamba sawa?? Michelle Obama ni mzuri sana,ni msomi wa hali ya juu, watoto wazuri, mume mzuri na ni RAIS basi we mwenzetu kabarikiwa jamani tumtakie kheri…Mr.Degree acha wivu ehhhhhh
PJ kuna true story pia kuwa mke alimkimbia mumewe baada ya kupoteza kazi. Tena akawa kiruka njia kabisa. Kwakuwa MWENYEZI MUNGU si Athumani, maisha ya mumewe yalikuja kubadirika ghafla na kunyooka tena. Yule mwanamke baada ya kuona sasa mambo safi akajaribu kujirudisha tena kwa mwanaume aliyemkimbia.
….True story nyingine, mwanamke alimkimbia mumewe kwakuwa hakupenda watoto aliowakuta kwa mumewe(kitu ambacho aliwekewa bayana toka awali. Baadae akang`ang`ania watoto aliozaa na mumewe tena mahakamani. Ni kweli alipatiwa watoto na pesa za poshi akawa anapata kila mwezi. Lakini watoto walipoanza kufikia muda wa kusoma shule ya sekondali (za kulipia) aliwarudisha mbio kwa baba yao.
…..True story nyingine,mwanaume kajitolea kumsomesha mkewe kwa kamshahara kake kadogo alikonako kwa muda wote wa masomo. Baada ya yule mwanamke kuhitimu masomo na kupata kazi nzuri, akamuancha mumewe tena kwa dharau na kebei kwa kumwambia eti “nimejaribu kukupenda ktk maisha yangu yote tangu tulipokutana, lakini nimeshindwa!…hivyo basi, naona bora tuachane….
TJ, swala la mke bora ama mke bora, ni bahati na Baraka toka kwa mungu. Wanawake wanaopenda wanaume kwa ajili ya kufaidika aidha kiuchumi na kimaslahi ni wengi sana ukilinganisha na wanaume.
HUO UNABAKI KUWA NI UKWELI TJ
Usemi usemao kuwa katika kila penye mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke sikubaliani nao kwa 100% Kuna watu kibao tu wana mafanikio makubwa ktk maisha yao bila kumhusisha mwanamke hata chembe. Tena bado hawajachumbia wala kuoa.
jamani hii imenikuna saaana….nafurahia saana stakeholders wanavyoijadili hiii…..
….na ni katika KUDUMISHA MAISHA YA FAMILIA ambayo ni uti wa mgongo wa maendeleo ya kijamiii…..
….dereva nyoosha mguu…konda angalia vichwa…..hado Posta mwisho….lol
Hii mada ni nzuri sana. Kwa kweli mimi naamini Michele amechangia sana mafanikio ya familia yake. kama alivyosema veronica uvumilivu ni muhimu kwa mwanamke, lakini kuna uvumilivu na ujinga. wanawake lazima tutofautishe hayo. Haya kina baba mbona siwaoni humu, inabidi na ninyi mtuambie Obama amewafundisha nini, sio BC kutumbia kuwa kuna mengi saana hayasemeki, yasemeni tujifunze wote kwa pamoja.
Duh Wabongo ukiwapa mada kidogo tu ya kuizungumzia balaa. Hiyo msg #19 kifungu (TJ),ndiyo mwisho wa yote naifagilia sana hiyo message yaani ni full point, zilizobaki ni hadithi za kina (Abunuasi)tu.kila mmoja anajitahidi kumuelezea Michelle. na Hillary Clinton mpaka zinaboa haa! kama mlikuwa(class mates)wenu acheni uwongo.
Hata mwaka bado hajamaliza mshaza kumjadili Michelle Obama.kabla ya hapo mlijuwa alikuwa na tabia gani? hiyo ni siasa lazima abadilike elimu si kigezo tosha chakumkubali mtu kitabia kama elimu hata George bush pia anayo. tumpe mda kwaza aonyeshe uwezo wake na haswa haswa barani Africa kuna matatizo lukuki kwa upande wa kina mama na watoto Msitoe misifa hovyo sifa ina hadhi yake jamani sio kiunafki ilmradi nichangie BC.
Ukisema Ooo.. Mwanamke mwezetu Wapo Viongozi wa kike hapa Tanzania ambao pia ni mifano bora kabisa ya kuigwa hata kwenye familia zao kama hao BC akiwatoa nitamwaga misifa itategemea na mtu atakaye tajwa na sio kicheche.
Tobaaa msinitoe pua jamani hayo ni maoni tu.
MTANZANIA, you are right kuna true story nyingi kwa kweli ila cha msingi nadhani ni sisi sote kuwe na upendo na familia zetu…
Katika gazeti la kingereza la the guardian nimesoma article ya “the aging presidents” sikukumbuki mwandishi lakini ni article inayo muhusu mr president wetu-Kikwete anavyoonekana sasa ukilinganisha na alivyo kuwa kabla ya kuwa rais, kuna mabadiriko ya smile ya kulazimisha huku nyuma ya kichwa yaani katika modulu yake kukiwa kumejaa mambo mengi ya kurekebisha maendeleo, uchumi,na wizi wa fedha za umma kwa maislahi ya inchi yetu.
sasa ninapenda tu kuwaeleza wadau kuwa kufanya au kuwa mwanasiasi ningu munno. Obama alianza akiwa na mwonekano wa kupendeza, kukenua na kujieleza bila kusiota.Alikuwa na maneno mazuri katika flow ya speech zake hasa ile ya kwenye mkutano wa 2004 wakati akimpigia debe kelly ayekuwa akingombea kiti cha urais. Ilikuwa superb. sasa vitu vyote hivyo vimanza kupotea . Anawaza sana na kufanya maamuzi mengi.Hukunja uso wake mara nyingi na hiyo nikawaida.
Hatahivyo naamini michelle obama kwa kutumia umakini wake na wala siyo uzuri kama wengi wanavyo sema hapa,atamusaidia mumewe kufanya vizuri. Kwa ujumla siamini katika uzuri wa mwanamke kama kigezo cha mafanikio ya mume.uzuri ni uzuri tu. I consider uzuri wa sura kama kigezo cha matatizo mengi. Lakini kwa nchi zilizoendelea huwezi kuwa nawasisi wasisi yoyote kuwa na mke mzuru wa sura kama ilivyo kwa inchi zetu za ulimwengu wa tatu. wanaume tunafanyiziana na culture zetu zimetuharibu kwa kutufundisha kuona kawaida para mke au mume anapotaka inje ya ndoa. kwa makabila mengine niajabu kusikia mume hana kimada wa nje,utamaduni duni kweli kweli. Hata hivyo kwa nadharia yangu mimi ” I can only believe in the beauties of my own mother who raised 10 of us and yet stays married for 50 years with her men( my father) for until now. I believe maria and sasha would say the same to their beloved parents.
Dada Missy unapatikana wapi???naona una mawazo chanya mno hiyo ya clinton ni kweli kabisa maza alishauriwa atulize kitenes mzee kaula life inasonga!
Mtanzania maoni yako yananikumbusha mbali sana na hii kitu UVUMULIVU jamani wengi wetu uvumilivu ni EF (f)
NB:MKE/MME MWEMA anatoka kwa MUNGU!
hallo wapenzi wa hii bongo celebrity kama mlivyoona michelle obama ni mwanamke shupavu sana kwa sababu aliweza kumvumilia mumewe alipokuwa anashinda kwenye mikutano ya kuwania urais lakini wangekuwa ni wanawake wengine wenye wivu ingeshakuwa ugomvi mkubwa na kumwambia kwamba ana kimada nje. sasa basi tujifunze kwa hilo wanawake tuamke na kuonesha kuwajali wanaume zenu ndio maendeleo.ni hayo tu jamani.
Senior nakubalina na hoja hapo juu. Ila kitu ambacho ume- high light- kwa kusema: -Wanaume tunafanyiziana na culture zetu zimetuharibu kwa kutufundisha kuona kawaida para mke au mume anapotaka nje ya ndoa…ndio hiyo culture yetu ya kiafrika mtu tangu mdogo esp wanawake wanaambiwa mume kutoka nje ni kawaida. Wadau mimi binafsi hii culture siipendi kabisa (najua wengi hapa watanipinga)..ila kwa kwetu waafrica ni kawaida ila kwa wenzetu wa nchi nyingine wanashangaa sana na sio culture yao eti mume kuwa na kimada..kama hapa Germany mume au mke akigundulika ana kimada result yake ni divorce na hamna discussion wala nini..Sasa kuna siku moja nilikuwa zangu Bongo, tulikuwa tunaangalia TV likaja tangazo la Ukimwi ile ambalo linasema- MTU AWE NA MPENZI MMOJA AMBAE HAJAAMBUKIZWA ILI KUEPUKA UKIMWI. huyu rafiki yangu alishangaa sana (kiswahili anajua) akaniambia mbona kuwa na mpenzi mmoja ndio inavyotakiwa hili tangazo ndio linawambia watu wawe na mpenzi mmoja..yaani wadau ilibidi nimueleza kwamba huku Africa mare nyingi watu wengi esp wanaume wana wanawake wengi ndio maana hilo tangazo limetengenezwe mpaka anaondoka alishangaa sana..ndio Africa yetu hiyo
Huyu mama anawafundisha kina mama kuacha umbea na kuringia madaraka au mali au umaarufu wa waume zao na badala yake kufanya kazi kwa bidii na kuacha mawazo ya wizi na ufisadi. Kwa umaarufu aliyonao OBAMA angekuwa kwenye nchi zetu hizi masikini huyu mama angekuwa amesheni vito vya gharama kubwa mwili mzima
Watanzania wenzangu wanaBC,
Nimeyafuatilia kwa umakini mkubwa sana, maoni yenu kuhusu mwanamama “Michelle Obama”, na nimegundua mambo mengi sana ambayo yawezekana hata ninyi watoa maoni hamkujua kuwa hamuyajui.
Hali hiyo ya kutoelewa, itaendelea kuwa hivyo kwa wengi wenu, hata baada ya mada hii kuisha hapa.
Michelle Obama wala Barack Obama, hawana lolote jipya la kutufanya kujifunza kutoka kwao. Kutokana na utofauti wetu na wao ulivyo.
Lakini kwa maoni ya wengi nilivyoyaona, na hasa wanawake. Mtu mwenye wadhifa, anayetoka nchi zilizonona kama Ulaya na USA, anayeletwa hapa BC au mahali popote panapokuwa na nafasi kama hii, ya watu kutoa maoni yao, kila mtu anasema kile anachokitamani rohoni. Akijiweka sawa na watu hao.
Kutokana na utafiti wangu wa maoni usiokuwa rasmi, nimegundua kuwa, wanawake wa Kitanzania wengi sana, wana ndoto zao kubwa sana za maisha mazuri, kama wanavyoishi ma-celebrities wa Ulaya na USA. Lakini sio kama Ma-celebrities wa Kibongo.
BC walituletea “Celebrity” wa Kitanzania – Mh. Sofia Simba. Nilitegemea kuona maoni mazuri na yenye mawazo ya kuendeleza kutoka kwa wanawake. Maana maoni yao yangegusa zaidi maisha halisi ya wanawake wa Kitanzania katika ukombozi wa maisha yao.
Lakini kwa bahati mbaya sikukutana na maoni yanayoweza kumwendeleza mtu kimawazo wala kimaisha.
Wengi ya watoa maoni walimwandama Mh. Sofia Simba kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na maneno yenye mwelekeo wa kumdhalilisha. Tunao macelebrities wengi sana, Mama Salma Kikwete, Maria Nyerere, Getrude Mongela, Dr Asha-Rose Migiro, Generali Madawili nk.
Je, Watanzania na wanaBC wenzangu! Kwanini tunathamini zaidi vitu vya watu wengine na kuvidharau vya kwetu? Je, mawazo haya ya kufugwa tumeyatoa wapi?
Kwa kweli ninaumia sana rohoni mwangu, ninapoona hali kama hii kwa ndugu zangu wa damu kushabikia na kuyatamani maisha ya watu wa juu na kujidharau wenyewe. Tamaa ya maendeleo ni nzuri kama haichanganyiki na chuki au kujidhalilisha utu wako mwenyewe.
It’s Great To Be Black=Blackmannen
BLackmann wazo lako si baya BC wekeni Celebries wa kibongo hapa tuwajadili (ila tafuteni picha zao halisi)…ila mimi binafsi nadhani it is also ok to discuss celebreties ambao sio watanzania…
Hiyo picha ukiiangalia tu- kitu cha kwanza unachokiona ni fitness! Wanawake wetu wa kibongo mmeng’anana na machips kuku na mahenkeni kila mkichuna mabuzi badala ya kwenda gym, matokeo yake mnazeeka kabla ya siku zenu, bao moja tu ulimi nje!
Kana-Ka-Nsungu mdau, umenichekesha eti bao moja tu ulimi nje…unajua wanawake wengi bongo hawafanyi mazoezi na wanatembea taratibu kwa sababu ya unene…na ukifanya mazoezi watu wanakushangaa kweli kweli maana ndugu yangu unene si ndio wanaume wa kiafrica wanapenda jamani? mimi mama yangu alipata stroke sasa Dr. akamwambia inabidi afanye mazoez ya kutembea 5km ect basi yeye akitoka kazini anashushwa victoria na anatembea mpaka sinza..majirani walimshangaa mpaka siku hizi wamemzoe na kumuita ´mama mazoezi´. jamani tufanye mazoezi siku hizi bongo pressure zipo nyingi
Kana-Ka-Nsungu upo ulaya nini.. bongo wanake wengi mazoezi ni sumu (si unajua tena wengi ni wanene wanaogopa kukonda, sasa wapungua mabuzi watapata wapi)… kula chips kuku, chips mayai na kumywa Bia za offer..