MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

ngassabc

Timu yetu ya taifa ya soka,Taifa Stars, imerejea hapo jana kutoka huko nchini Ivory Coast ambako ilikwenda kushiriki mashindano ya CHAN (Africa Nations Championships)ambayo ni kama kombe la Afrika ila kwa wachezaji ambao wanacheza soka ndani ya bara la Afrika pekee bila kuwashirikisha wale wanaosakata kabumbu ughaibuni.Mashindano hayo yanatarajiwa kufikia kilele jumapili ijayo huko Ivory Coast.

Taifa Stars,hawakuambulia kombe ila mashabiki wengi wa soka,ndani na nje ya Tanzania,wanakubaliana kwamba Taifa Stars hivi sasa siyo ya kubeza.Sio tena kile kichwa cha mwendawazimu alichowahi kukizungumzia Rais mstaafu,Ally Hassan Mwinyi.

Miongoni mwa wachezaji ambao Tanzania hivi sasa inajivunia ni kijana mdogo Mrisho Ngassa(pichani).Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza,Khalfan Ngassa,alizaliwa tarehe 5 mwezi wa May mwaka 1989.Bao la ushindi alilolifunga huko nchini Ivory Coast dhidi ya wenyeji Ivory Coast limeelezewa kuwa mojawapo ya mabao bora kabisa ya mashindano hayo.

Je nini kifanyike ili kuendeleza vipaji kama cha Ngassa na wachezaji wengine wengi nchini Tanzania?Kumbuka kwamba mpaka hivi leo,Tanzania bado haijatokea kupata au kutoa mchezaji ambaye akatamba hususani katika ligi kubwa za soka ulimwenguni kama ile ya Premier ya Uingereza au Seria A ya Italy au La Liga ya Spain kama ambavyo mataifa mengine(mengi ya Afrika Magharibi) yamekuwa yakifanya.

Halafu kuna mjadala ambao mwenzetu Issa Michuzi ameuanzisha.Ni kuhusu hatma ya kocha wa Taifa Stars,Mbrazil Maximo.Swali la msingi ni;Je mkataba wa Maximo usitishwe au apewe mkataba mpya.Unaweza kusoma na kuchangia mjadala huo muhimu kwa maendeleo ya soka nchini Tanzania kwa kubonyeza hapa.

BC inafanya juhudi za kumpata Ngassa kwa mahojiano rasmi.Stay tuned.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

8 Responses to “NGASSA:A NEW HOPE?”

  1. Comment by mr degree on March 5th, 2009 12:24 am

    ANADAI ANA MIAKA 19 LAKINI ANA MTOTO WA MIAKA 5,KWA HESABU ZA HARAKA HARAKA ALIPATA MTOTO AKIWA PRIMARY SCHOOL KITU AMBACHO SI CHA KWELI. HATUWEZI KUPATA PROFFESSION WA UKWELI KWA KUDANGANYA UMRI, ANY WAY KUHUSU SOKA YAKE SI HABA MBIO ANAZO!

  2. Comment by JOHN CENA on March 5th, 2009 2:36 am

    Mrisho Ngassa ni kifaa kitarajiwa ila sasa kwa uswahili wa BONGO FITNA FOOTBOLI angalia mdogo wangu usije ukaishia kuandikwa kwenye magazeti ya bongo tuu ambayo wakina WENGER,BENITEZ,BABU FERGIE hawayasomi jaribu kuwaangalia sana hao mawakala ambao ofisi za zipo KARIAKOO wanasema wanatafuta team ulaya……….!!!!
    BUT KEEP IT UP UTATOKA TUU.TUPO PAMOJA

  3. Comment by Mickey Jones Amos - Denmark on March 5th, 2009 8:58 am

    Nitasubiri mpaka BC itakapopata nafasi ya mazunmgumzo na kipaji Ngassa mwenyewe atupe mawazo yake ya uchezaji wa “kibinafsi” na “Kiumoja” kama Taifa Stars wanaoelewana katika kuleta matokeo mazuri ya ushindi wa mashindano yote.

    Wachezaji vipaji binafsi wamekuja na kutoweka bila ya kuiletea Taifa Stars ushindi wa kimataifa kwa muda mrefu uliyopita,lakini itakuwa vizuri kusikia maelezo tofauti binafsi ya kipaji-Ngassa.

    Copenhagen

  4. Comment by Mzee wa ££££ za kutosha on March 5th, 2009 10:08 am

    hahahaha Ebwana Mr Degree unanichekesha sana, kumbe prof footballer anatakiwa kwanza kuwa mkweli? ujue umri kweli uku Utaborani wachezaji wakali wanamiaka kuanzia 19 – 24, sasa naona kijana nae anasema mule mule , lakini mi namkubali sana, sema tu anatakiwa kuwa makini kwani bongo matapeli wengi, watamlia buku! buku zake wakimdanganya wanamtaftia timu Ulaya, kumbe changa la macho.
    Kazana sana kijana, siri ya mafanikio ni KUKAZANA.

  5. Comment by mchizi on March 5th, 2009 12:48 pm

    Sasa wewe Mr degree ,cha kushangaza nini hapo? mbona hushangai yule ‘mtoto’ wa uingereza aliyepata mtoto akiwa na miaka 13 au kwa vile ni mzungu.

  6. Comment by MAKULILO Jr on March 5th, 2009 9:39 pm

    Ngassa kusema kweli anajituma sana, na uwezo anao tu mzuri.Juhudi tu asilewe sifa za kibongo, akomae barani ulaya atacheza tu.

    Huwa napingana na watu wengi ambao kila kukicha wanasema oohh wachezaji wa bongo maumbo yao ni madogo mfano ni Ngassa, na wengineo.Mpira sio maumbo wandugu, kama ni maumbo, akina Mwaikimba wapo wapi??Si Maximo alimchukua kwa kuangalia umbo eti litatisha, nani alitishika sasa??Mbona akina Messi, Pato, Flamini, Fabregas, Rafael, Robinho nk maumbo yao madogo??Akili, juhudi na uwezo vinamuwezesha mtu kuwa bora.Ngassa komaa utapata tu chance ya kucheza ulaya.

    Mafanikio mema
    MAKULILO Jr,
    West Virginia, Marekani
    http://www.makulilo.blogspot.com

  7. Comment by Mickey Jones Amos - Denmark on March 6th, 2009 6:58 am

    Nakubaliana na mtazamo wa mchangiaji MAKULILO JR.

    Naheshimu ingawaje sikubaliani na mtazamo
    wa “Prof.degree”.

    kwa uchezaji wa nchi za huku hauitaji “Umbo au kitambi”anatakiwa kutumia kipaji chake cha kuzaliwa na kuhitimu zaidi mafunzo ya walimu wake.

    Umri wake si kikwazo pia kama kipo sawa au hakipo sawa kinachoangaliwz ni “makaratasi” yake ya kuzaliwa yaliyopitishwa katika
    ngazi zote zinazohusika.

    Muhimu kuwepo na ushirikiano wa Taifa Stars kama wachezaji wanaoelewana kwa umoja katika michezo yote badala ya kuendelea na mawazo yetu ya kizamni kuangalia “kipaji-kifaa” kama kipo zaidi kuliko wengine,hayo yatafuatia baada ya Taifa Stars kuleta matokeo ya umoja.

    Vipaji(vifaa) vyetu binafsi wakiwa wachezaji wa kulipwa wataonyesha “ufundi wa kibinafsi” kwa sasa tunataka “TIMU YA TAIFA STARS” kuleta matokeo ya kimataifa katika kipindi cha miaka mitno ijayo.

    mickey@mail-online.dk
    Copenhagen

  8. Comment by Mgugule on March 6th, 2009 10:11 am

    Mimi nashanga kwa wale wanaomjadiri huyu Mr Degree a.k.a (Mr,hater) kwani yeye kashajiweka Opposite kwa lolote lile rinalo hitaji kuchangiwa.

    Watu kama Mr Degree wapo wengi kwa mtazamo wangu inapendeza kuwepo mtu kama huyo humu kwenye midahalo kwani ameweza kuwasugua vichwa vya wadau wengi na haswa wa BC.

    Nilikuwa nikifuatiria kwa karibu hoja za wadau wengi pamoja na za huyu digrii hoja nyingine zina kuwa za msingi kweli na nyingine kichefuchefu kama hii alioitoa hapo juu duh.hii inaonyesha jinsi arivyo hater,

    kama swala ni mtoto Degree wewe hiyo haikuhusu.
    kama swala Umri hiyo sikazi yako ukitazama hata kwenye vilabu vikubwa vya huko nje wachezaji wengi wameghushi umri wao na bado wanasukuma ngozi vizuri sana na hii yote ni kutafuta maslahi nadhani hili unalifahamu vilivyo ila kwa vile wewe ni kati ya wale Wazee wa haters. Usikonde mwana Peace.

Leave a Reply