anna_tibaijukabc

Miongoni mwa wanawake ambao ni nyota,mfano wa kuigwa na ambao Tanzania inajivunia kuwa nao ni Prof.Anna Tibaijuka. Ni miongoni mwa wale wanawake ambao DaMija huwaitwa “Wanawake wa Shoka”.

Pamoja na hayo,hivi karibuni ulimwengu ulishuhudia cheo alichokuwa akikishikilia pale UN-Habitat yenye makao yake makuu jijini Nairobi-Kenya kikiota mbawa katika mazingira ambao wengi hawajaelewa wala kukubaliana nayo.Miongoni mwa wasiokubaliana na “kushushwa cheo’ kwa Prof.Tibaijuka ni wafanyakazi wenzake.

Je ni kwanini Ban Ki Moon amemshusha cheo mama Anna Tibaijuka wakati hata hivyo mkataba wake ulikuwa unaelekea ukingoni(2010)? Je kuna harufu ya ufisadi? Soma zaidi kwa kubonyeza hapa na kisha tizama taarifa ya habari hapo chini kisha uwe muamuzi.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Feedback / Comments

12 Responses to “TIBAIJUKA NA MKASA WA KAZI”

  1. Comment by sisterTZ on March 17th, 2009 2:28 pm

    heeeee kumbe UN pia kuna politics jamani..kwa kweli Ban Kin Moon aleze ukweli wa kumtoa huyo kwenye cheo..maana she was the first female ever to head an UN mission kama sikosei..kwa mim binafsi nimesikitika mno

  2. Comment by MAKULILO Jr on March 17th, 2009 3:01 pm

    POLE TIBAIJUKA

    Ukisoma kwa makini link ya east africa standard hiyo ambayo mmeweka hapo juu na kusikiliza taarifa hiyo ya habari, kuna mambo yafuatayo ninayaona.

    Kwa kabisa utendaji wa Anna Tibaijuka ni mzuri kama ulivyooneshwa ktk gazeti hilo.Na mpaka watu wanaamua kuandika barua ya wazi kwa Ban Kin-Moon kutoa maoni endelevu kuhusu changes hizo ni jambo la ku-prove utendaji huo.

    Mimi nachopinga ktk changes hiyo ni kuona huyo Steiner ambaye anachukua nafasi ya Tibaijuka wakati akiendelea kushika ubosi wa UNEP. Kama Moon akisema kuwa ni suala la rotation, ambayo ni sababu ya msingi, basi Tibaijuka angekwenda kule kuwa bosi ya UNEP naye au ktk agency nyingine ya UN.Kitendo cha Steiner kuendelea kushikilia nafasi mbili kwa wakati mmoja ndio zinaongeza zengwe hapo.

    Napingana na hoja ya Rhoda Atana ambaye ni The President of the UN Nairobi Staff Union ambaye hoja yake kubwa kupingwa ni GENDER, kwakua Tibaijuka ni mwanamke, na kulikua na mwanamke mmoja tu Tibaijuka kushika cheo hicho.Hoja ya kusema ni mwanamke ndio iwe sababu ya kupinga binafsi nakubali kutofautiana kihoja na Rhoda Atana.Tibaijuka wakati anateuliwa na Koffi Annani hakuteuliwa kwa kuwa ni mwanamke.Asha Rose Migiro kuteuliwa ktk nafasi ya katibu msaidizi wa UN hajateuliwa kwa huruma eti ni mwanamke.Kuchaguliwa kwa Angela Mackel huko Ujerumani si kwakua ni mwanamke.Obama kumteua Hilary Clinton kuwa Secretary of State sio kwakuwa ni mwanamke., na wengine wengi.Hao wote wana sifa nzuri kielimu, na utendaji wao ni makini sana.Ujengaji wao hoja, utekelezaji wao mambo, ufanisi ktk kazi zao zimewafikisha hapo.Hivyo ondoa hoja za uruma ktk ulimwengu huu shindani.

    Kwa hiyo dada Rhoda Atana, unataka kuniambia wewe kushika hicho cheo cha President of the UN Nairobi Staff Union umechaguliwa/teuliwa kwa kuwa ni mwanamke ili kuleta uwiano wa wanawake na wanaume UN Nairobi au ni uwezo wako?Naomba utofautishe haki sawa kati ya wanawake na wanaume, na upendeleo.Haki sawa haina maana upendeleo.Kunaweza kuwepo sababu zingine ambazo unatakiwa kusimamia ktk kujenga hoja kuhusu Tibaijuka kuwepo ktk nafasi yake kama ulivyokiri kuwa uwepo wake uliongeza morali, ufanisi nk, na sio msisitizo wako wote ni uanauke wake.

    Suala lingine la msingi, watu wa Kenya nawakubali sana ktk mambo kama haya ya haki kudai.Ingekuwa ni Tanzania mkenya ndio kashushwa cheo, tungekuwa kimya,au hata angekuwa ni mtanzania kashushwa cheo, lakini ofisi yake ipo hapo Tanzania pia wagtu wangekuwa kimya.Ila wenzetu Kenya wanaweka hoja, wanasimamia hoja na si nguvu tu.

    Tusubirie mstakabali, ila sidhani kama Tibaijuka anaweza kurudishwa ktk cheo hicho, labda anaweza kupelekwa ktk UN Agency nyingine kuwa bosi huko kupitia hoja ya Ban Moon ya Rotation of senior officers.Maana akimrudisha ni ku-prove failure ktk uongozi.Na atakuwa anaongozwa kwa matishio.

    Nawasilisha hoja
    MAKULILO Jr,
    http://www.makulilo.blogspot.com

  3. Comment by EDDY on March 17th, 2009 7:11 pm

    MAKULILO UNAONEKANA MWEPESI WA KUKUBALI HOJA ZA KIJANJA HAPO KUNA MKONO WA SERIKALI YA KENYA KAMA HUNA HABARI SOMA VIZURI NA SIKILIZA VIZURI? KILICHOMO NDANI YA AKILI ZA WATU NI KWA NINI TANZANIA IWE NA WATU WAWILI WAKUBWA KATIKA UN? SASA NANI AWE SADAKA? BASI WAKAONA HUYU AWE, KWANI ASINGEMTOA ASHA KWA VILE YEYE NDO ALIMTEUWA. HAPO NI ROHO YA KOROSHO TU YA KWA NINI WA TZ WAWILI???/

  4. Comment by IsaackJr on March 18th, 2009 5:39 am

    Ni jambo ambalo la kusikitisha kwa kupoteza nafasi kubwa ambayo ilikuwa inashikiliwa na mama wa shoka tena kutoka Tanzania,i think Ba-ki moon should come with the reasonable reasons for his decision.

  5. Comment by Mwanamke wa Shoka (UK) on March 18th, 2009 9:33 am

    mhhh!!…hii imenisikitisha saana…Anyway, Prof. Tibaijuka keep it on…you have been a shining star…and u will continue to be…

  6. Comment by Tito on March 18th, 2009 11:37 am

    My opinion: This is sad knowing that huyu dada ni mtanzania na alikuwa ana present Tanzania, na watanzania tunampa heshima na kujivunia. The way I understand the clip above, inasemekana kuwa kulikuwa na wizi wa mamilioni ya pesa in her watch. Sasa jamani hata kama ni mtanzania na tunampenda lazima tuwajibike na tusema ukweli, kama kweli hizo pesa zimepotea lazima atolewe hicho cheo. wakati mwengine tujaribu kuangalia undani wa vitu kabla hatuja play part of victimization. sio kila wakati sisi tuu ndio tunaonewa. That’s my opinion, but still respect her and wish her the best.

  7. Comment by Bingo on March 19th, 2009 3:06 am

    I feel pity for what happened to you Anna and never should you loose hope. I strongly believe that before you were born God himself had choosen and equiped you with tools you need to successifully chage people’s lives positively. Just know that, that is part and parcel of life, there is always ups and downs, just stand up dust yourself off and keep going, keep the faith and focus towards the original goal set forth by yourself, the sky is your limit baby.

  8. Comment by Othman Michuzi on March 19th, 2009 4:46 am

    kwa kweli hapa inawezekana kabisa kukawa na mkono wa mtu,maana haiwezekani akashushwa cheo ghafla namna hii na wakati kabakiza mwaka mmoja tu katika hicho kitengo chake.

  9. Comment by kuluchu on March 20th, 2009 11:02 pm

    MAMA ILA TANZANIA NDO KUNA MAKAZI MABOVU SANA.PLIZ KEEP YOUR EYE NYUMBANI JAPO KWA KUWAPA HATA USHAURI.MAGUFULI ALIJITAHIDI WAKAMUONDOA WAKAMTUPA KWNY KITOWEO.HUKO NAKO BADO ANAENDELEA KU-SHINE.HEBU MAMA TOA KAMCHANGO JAPO KA MAWAZO MIKOA MIKUBWA KAMA DAR ARUSHA MWANZA NA MBEYA JAPO KUWE NA MAKAZI BORA TUKUONE MCHANGO WAKO NYUMBANI MAMA.SAMAHANI KAMA NIMEKUSUMBUA WAKATI HUU WA MAJONZI.ILA BADO TUPO NAWE KWA SALA

  10. Comment by Bakananuka on March 23rd, 2009 7:20 am

    UFISADI UNAWEZEKANA.MFANO MDOGO NI PALE ALIPO LAZIMISHA KUWEKA MRADI WA MAJI WILANI MWAKE NA KUACHA WILAYA ZENYE MATATIZO MAKUBWA MAKUBWA YA MAJI MKOANI KAGERA.VIGEZO HAVIKUZINGATIWA

  11. Comment by sisterTZ on March 23rd, 2009 10:52 am

    KAKA TITO msimamo wako nauunga mkono. Hata mimi nimesikia kwamba kuna pesa vimepotea ndio maana ameshushwa cheo..ila who knows nani kaweka mkona wake hapo. BAn Ki Moon inabidi afanye uchunguzi zaidi

  12. Comment by Mama ethan on April 11th, 2009 4:02 pm

    Hiyo ni chuki binafsi kumwondoa tibaijuka ktk hyo nafac nakumuweka huyo mdhungu.u knw wat men m nafkiri hata majirani ze2 hawafurahishwi na cc kushine ktk anga zakimataifa so inawezekana nawao wamechangia kwa kuunganisha fitna zao.lakini co ishu kwe2 cz uwezo 2nao.keep it up mama tibaijuka 2po pamoja.

Leave a Reply